Ni kweli,mimi nadhani badala ya kumbeza babu wa Loliondo na tiba yake,ni bora mtu akanyamaza kimya kama haamini.si vizuri kubeza jambo ambalo huna uhakika wa ukweli wake.yaani hujui kama ni kweli ama si kweli halafu unabeza.hata ukijua kuwa ni uongo,ni vema kutoa ushauri kwa watu kwa lengo la kuwasaidia.tukumbuke wengi wanaokwenda kwa babu ni wale wenye matatizo kiafya,na hiyo ni ktk kuhangaika ili kupata afya.unapokuwa na shida kubwa huwa unasikiliza kila ushauri na kutamani kuufanyia kazi ili upate msaada.TUSIWABEZE WANAOKWENDA KWA BABU,TUSIMBEZE BABU NA TIBA YAKE.BALI TUSAIDIANE KUSHAURIANA.