Usilolijua kuhusu Uwanja wa ndege wa Heathrow ulianzishwa mwaka 1929

Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
3,053
1,409
Uwanja wa ndege wa Heathrow ulianzishwa mwaka 1929 kama uwanja mdogo(small airfield). Ulianza kupanuliwa 1944 kwa ajili ya ndege za kijeshi wakati wa WW II ukiwa umesanifiwa na Sir Frederick Gibberd ambae pia alisanifu majengo maaru 36 nchini Uingereza yakiwemo Cathedral of Christ the King lilipo Liverpool pamoja na London Central Mosque.

Baada ya vita ya Pili ya dunia uwanja huu ulibadilishwa matumizi na kuwa kwa ajili ya matumizi ya kiraia.

London Heathrow ni uwanja wa 6 kwa ukubwa duniani ukiwa na eneo la kilomita za mraba 12.27 ukimilikiwa na Heathrow Airports Holding inayomilikiwa na kampuni liitwalo FGP TOPCO LTD lenye wanahisa wafuatao:

1. Ferrovial Group 25%

2. Qatar Holding LLC 20%

3. Caisse de depot et placement du Quebec 12%

4. Government of Singapore Investment Corporation 11.2%

5. Alinda Capital Partners 11.18%

6. China Investment Corporation 10%

7. Universities Superannuation Scheme 10%

Uwanja huu unahudumia mashirika 80 ya ndege zinazotoa huduma kwenye vituo 185 katika nchi 83 duniani kote. Hapa ni nyumbani kwa mashirika mawili makubwa ya ndege amabayo ni British Airways na Virgin Atlantic.

Uwanja huu kwa sasa unazo njia mbili (2) za kurukia na kutulia ndege zilizo sambamba na kutengeneza mfano wa 11 lakini kabla ya hapo ulikuwa na njia 6 zilizopangwa katika pair 3 zilizotengeneza umbo la hexagram na kufanya jingo la abiria liwe katikati. 93% ya wasafiri wa uwanja huu ni wale wa kimataifa ambapo wengi wanaenda/kutoka Marekani. 7% pekee ndio wanaosafiri ndani ya Uingereza.

Uwanja huu una sehemu zaq ibada kwa Wakatoliki, Waanglikana, Wahindu, Wayahudi Waislamu na Wa-kanisa huru.

Barabara nyingi za mji wa Heathrow uliobeba jina la uwanja huu majina yake yanaanzia na herufi za dira (i.e E for Eastern side roads, W for Western side roads et al)

SISI KAMA TAIFA TUNAYO YA KUJIFUNZA HAPA?
 
Attachments

  • BA.jpg
    BA.jpg
    10.9 KB · Views: 87
  • heathrow airport1.jpg
    heathrow airport1.jpg
    178 KB · Views: 89
  • Heathrow apt2.JPG
    Heathrow apt2.JPG
    131.3 KB · Views: 81
  • virgi.jpg
    virgi.jpg
    9.3 KB · Views: 74
Uwanja wa ndege wa Heathrow ulianzishwa mwaka 1929 kama uwanja mdogo(small airfield). Ulianza kupanuliwa 1944 kwa ajili ya ndege za kijeshi wakati wa WW II ukiwa umesanifiwa na Sir Frederick Gibberd ambae pia alisanifu majengo maaru 36 nchini Uingereza yakiwemo Cathedral of Christ the King lilipo Liverpool pamoja na London Central Mosque.

Baada ya vita ya Pili ya dunia uwanja huu ulibadilishwa matumizi na kuwa kwa ajili ya matumizi ya kiraia.

London Heathrow ni uwanja wa 6 kwa ukubwa duniani ukiwa na eneo la kilomita za mraba 12.27 ukimilikiwa na Heathrow Airports Holding inayomilikiwa na kampuni liitwalo FGP TOPCO LTD lenye wanahisa wafuatao:

1. Ferrovial Group 25%

2. Qatar Holding LLC 20%

3. Caisse de depot et placement du Quebec 12%

4. Government of Singapore Investment Corporation 11.2%

5. Alinda Capital Partners 11.18%

6. China Investment Corporation 10%

7. Universities Superannuation Scheme 10%

Uwanja huu unahudumia mashirika 80 ya ndege zinazotoa huduma kwenye vituo 185 katika nchi 83 duniani kote. Hapa ni nyumbani kwa mashirika mawili makubwa ya ndege amabayo ni British Airways na Virgin Atlantic.

Uwanja huu kwa sasa unazo njia mbili (2) za kurukia na kutulia ndege zilizo sambamba na kutengeneza mfano wa 11 lakini kabla ya hapo ulikuwa na njia 6 zilizopangwa katika pair 3 zilizotengeneza umbo la hexagram na kufanya jingo la abiria liwe katikati. 93% ya wasafiri wa uwanja huu ni wale wa kimataifa ambapo wengi wanaenda/kutoka Marekani. 7% pekee ndio wanaosafiri ndani ya Uingereza.

Uwanja huu una sehemu zaq ibada kwa Wakatoliki, Waanglikana, Wahindu, Wayahudi Waislamu na Wa-kanisa huru.

Barabara nyingi za mji wa Heathrow uliobeba jina la uwanja huu majina yake yanaanzia na herufi za dira (i.e E for Eastern side roads, W for Western side roads et al)

SISI KAMA TAIFA TUNAYO YA KUJIFUNZA HAPA?

Unatamkwaje sasa huwo uwanja wa heathrow ni hithro au hethrow au kivipi???
 
tukibadili mawazo ya sisi hatuwezi na kuweka yale yakwamba tulichelewa sana kwa upuuzi sasa tukimbie tutafika kabla wajukuu wetu hawajatuuliza maswali ya aibu na vijisababu vyetu vyakikwele
 
Back
Top Bottom