Super women 2
JF-Expert Member
- Nov 16, 2016
- 5,164
- 6,535
Habari wana jamvi.
Hili tatizo la kuanzisha mahusiano mapya ghafla baada ya kuachana na mpenzi wako ,limekuwa likiwaumiza sana vijana/KE & ME.
Na hujikuta huanzisha mahusiano ya ghafla ili kuziba pengo la maumivu,
Bila kujua siku ya siku utakuja kuumia zaidi ya Mara mbili ya ulivyoumizwa mwanzo.
Jaribu kujipa mda wa kutosha,ili kujua ni wapi ulikosea au ni wapi mwenzako alikosea,
Ukishafahamu ni wapi ulipokosea kwenye mahusiano yaliyopita na kufahamu mapungufu ya mpenzi
Wako yalikuwa yapi,
Jipe mda angalau hata
Wa miezi mitano.
Hii itakusaidia kufanya maamuzi sahihi Sana.
Kuliko kukurupuka na kujikuta unakuja kupata maumivu ya moyo ya milele...
Na hakuna maumivu yanayotesa maishani Kama ya moyoni kwa ujumla..
Wala usikurupuke kuja jf na popote kuja kutafuta mchumba,
Sio kwamba kutopata. Utapata ila hatakuwa ni chaguo lako,
Bali ni kwa sababu ya kuziba pengo la mtu fulani tu.
Ndo maana Leo tunashuhudia migogoro mingi katika ndoa za baadhi yao... NYUMBA zinasiri nyingi Sana...
Kuondoka kwake yeye sio kwamba kaondoka
na maisha yako,hapana.
Jaribu kutambua thamani yako kwa ujumla.... Na huwezi kujua kwamba MUNGU kakuepusha na nini kwake..
JIPENDE,JITUNZE, JIHESHIMU, Atakuja wa kufanana na wewe
Pamoja na matendo yako.
Kumbuka MUNGU humpatia mtu mpenzi, mchumba,mume/mke wa kuendana nae,kulingana na matendo yako...
MBARIKIWE NYOTE