Usikubali kujadili mshahara na Hiring Manager

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,108
18,325
Watu wengi mnakoseaa sana.. kwenye interview unakubali kujadili expectations zako za mshahara na Hiring Manager, ukitaja mshahara mkubwa ujue imekula kwako.

Line Manager hatapenda umzidi, hata mimi lazima nikupige chini kama naona utanizidi mshahara.

Tafuta njia mshahara ujadili na HR.. hata barua ya mshahara Line Manager hatakiwi kuiona..

Kila la kheri watafuta kazi kama.mimi.
 
Haiko hivyo mara zote. Line manager anaweza kuwa sehem ya interview, ukiulizwa hilo swali utaacha kujibu kisa line manager wako yupo hapo?

Na kwakuwa yeye yupo kwenye hiyo ofisi tayari, hahitaji kujua mshahara wako kupitia kwako usishangae yeye kahusika kuupanga kabla hata nafasi ya kazi kutangazwa.

Binafsi najitahidi kujua mshahara wa nafasi husika kabla hata sijatuma maombi. Hawawezi kukupa zaidi ya utaratibu wao walioupanga kwa hiyo nafasi.

Mwisho, ofisi gani hiyo unamzidi mshahara line manager wako?
 
Maelezo safi sana...nasubiri jibu la swali ulilouliza....
 
Watu wengi mnakoseaa sana.. kwenye interview unakubali kujadili expectations zako za mshahara na hiring Manager, ukitaja mshahara mkubwa ujue imekula kwako.

Line Manager hatapenda umzidi, hata mimi lazima nikupige chini kama naona utanizidi mshahara.

Tafuta njia mshahara ujadili na HR.. hata barua ya mshahara Line Manager hatakiwi kuiona..

Kila la kheri watafuta kazi kama.mimi.
Sasa kama kwenye interview panel na yeye yupo, na umeulizwa hilo, ukatae kujibu..!!??
 
Maelezo yake ni irrelevant kabisa,huyo hiring manager mtakutana naye wapi ili akuulize mshahara?
Kabisa... halafu kwa kawaida mshahara wa kumzidi bosi wako sijui kama upo... kama upo basi wachache sana na bosi anakuwa hana shida na hilo
 
Huwa sijibu swali la salary expectations kwenye interviews. Siyo kwamba naogopa kumzidi mtu mshahara. Ila mara nyingi waombaji kazi wanaojibu hilo swali huwa anajipunja wenyewe. Lazima mwajiri anambie bajeti yake kwa nafasi niliyoomba, siyo mimi nimwambie.
Watu wengi mnakoseaa sana.. kwenye interview unakubali kujadili expectations zako za mshahara na hiring Manager, ukitaja mshahara mkubwa ujue imekula kwako.

Line Manager hatapenda umzidi, hata mimi lazima nikupige chini kama naona utanizidi mshahara.

Tafuta njia mshahara ujadili na HR.. hata barua ya mshahara Line Manager hatakiwi kuiona..

Kila la kheri watafuta kazi kama.mimi.
 
Huwa sijibu swali la salary expectations kwenye interviews. Siyo kwamba naogopa kumzidi mtu mshahara. Ila mara nyingi waombaji kazi wanaojibu hilo swali huwa anajipunja wenyewe. Lazima mwajiri anambie bajeti yake kwa nafasi niliyoomba, siyo mimi nimwambie.

Yaani nikiona majibu ya hivi huwa nabaki kucheka tu. Unaanzaje kuogopa kujibu swali la Salary expectations? We jibu tu na Wala jibu lako haliwezi kusababisha mshahara wako kupanda au kupungua labda under negotiation kwa upande wa mshahara kupanda.

Hii ni kutokana na kwamba Mara nyingi kwa sekta Rasmi iwe Serikalini au private sector mishahara huwa tayari imeshapangwa kulingana na cheo chako/ sekta uliyopo, so Hakuna anayeweza kushusha kile kiwango eti kisa kwenye interview wewe ulisema ulipwe kiwango kidogo na Wala Hakuna anayeweza kukulipa zaidi kisa ulisema ulipwe zaidi labda Kama anaitoa mfukoni mwake.
 
Kama umeshapangwa, kwa nini swali hilo uulizwa? Ni vema kutumia akili wakati mwingine. Unaweza kumcheka mtu, kumbe unajicheka mwenyewe. Nina miaka zaidi ya 50. Karibu ninastaafu. Nimefanya kazi sehemu nyingi sana Tanzania na nje. Siyo tu kusailiwa, nimesaili pia. Nimekuwa kwenye interview panels pia. Najua ninachokisema.

Unaweza hata ku-google "How to answer salary expectations question", utapata majibu ya wataalam. Tatizo la watu hamtaki kusoma. Waajiri ambao wana pre-determined salary scales kama UN, serikali nk huwa hawaulizi hili swali. Tena wengine wanaweka kwenye tangazo la kazi kabisa mshahara wako. You do not have to tell a figure when asked your salary expectations.

Decline diplomatically, politely ask the employer to decide. After all, they know the budget of the position, which you have no idea about. If you are the right candidate, watakuchukuwa tu na kukwambia mshahara. From there, you can negotiate kuupandisha.
Yaani nikiona majibu ya hivi huwa nabaki kucheka tu. Unaanzaje kuogopa kujibu swali la Salary expectations? We jibu tu na Wala jibu lako haliwezi kusababisha mshahara wako kupanda au kupungua labda under negotiation kwa upande wa mshahara kupanda...
 
Huwa sijibu swali la salary expectations kwenye interviews. Siyo kwamba naogopa kumzidi mtu mshahara. Ila mara nyingi waombaji kazi wanaojibu hilo swali huwa anajipunja wenyewe. Lazima mwajiri anambie bajeti yake kwa nafasi niliyoomba, siyo mimi nimwambie.
Inategemea experience yako ni ya kiwango gani,kama umetoka chuo muda si mrefu hapo sawa maana unaweza ukataja mshahara wa laki 5 wakati kumbe wenzako wanalipwa laki 8 au milioni 1.

Lakini kwa viwango vya watu wenye high skilled and experienced(professional) huwezi kuacha kutaja mshahara kwa sababu zifuatazo.
1. Kuna baadhi ya kampuni hazina scale maalum yaani unakuta kila mtu ana mshahara wake tofauti kutokana na jinsi alivyoburgain,mimi nimepita kwenye kampuni nyingi na kuna kampuni moja nilishawahi kulipwa mshahara mkubwa kumzidi meneja/boss wangu kwa sababu nilijiamini kwenye kubargain.

2. Swala la kutaja mshahara linasaidia kwenye kuakisi kiwango chako cha utaalamu,ukitaja hela ndogo interviewers wanapata picha ya professional level yako.

Kwa mfano kampuni kama wanamtafuta specialist wa kitu fulani kwenye kubargain wewe ukitaja mshahara wa laki 9 halafu candidate mwingine akataja milioni 3 watamchukua wa milioni 3 wakiamini ataprovide service yenye uhakika na wewe watakuchukulia kazi yako itakuwa ya kuungaunga utaharibu kazi kwa njaa.

Hizo ndio perception za interviewers cha kwanza kabisa wanaangalia dressing na kingine wataangalia burgaining power yako ingawa wote mnaweza mkafunguka vizuri kwenye kujibu maswali kiusahihi.
 
Kama laki 8 na milioni 1 ndio viwango nyako, basi fanya unavyotaka.
Tatizo lako hufundishiki mdogo wangu hiyo nimekutolea mfano wewe ambaye unaonekana bado hujazoea soko la ajira,mimi nipo viwango vya expert mshahara wangu nakunja milioni kadhaa sasa utanilinganisha na wewe ambaye hata kutaja mshahara unaogopa maana yake hata wakikwambia viwango vyao vya mshahara ni laki 4 itabidi ukubali tu.
 
Kama umeshapangwa, kwa nini swali hilo uulizwa? Ni vema kutumia akili wakati mwingine. Unaweza kumcheka mtu, kumbe unajicheka mwenyewe. Nina miaka zaidi ya 50. Karibu ninastaafu. Nimefanya kazi sehemu nyingi sana Tanzania na nje. Siyo tu kusailiwa, nimesaili pia. Nimekuwa kwenye interview panels pia. Najua ninachokisema.

Unaweza hata ku-google "How to answer salary expectations question", utapata majibu ya wataalam. Tatizo la watu hamtaki kusoma. Waajiri ambao wana pre-determined salary scales kama UN, serikali nk huwa hawaulizi hili swali. Tena wengine wanaweka kwenye tangazo la kazi kabisa mshahara wako. You do not have to tell a figure when asked your salary expectations. Decline diplomatically, politely ask the employer to decide. After all, they know the budget of the position, which you have no idea about. If you are the right candidate, watakuchukuwa tu na kukwambia mshahara. From there, you can negotiate kuupandisha.
Nimeshasoma Sana mkuu Wala sidhani Kama majibu yanayopatika Google Basi yana mguide kila muajiri kuhusu majibu ya swali hili. Nilishafanya interview kwenye UN Agency nikajibu kwa kutumia hayo majibu ya Google lakini waliendelea kunibana nitaje kiwango Wala nisiogope
 
Uongo huo. UN wanaweka kabisa mshahara kwenye tangazo la kazi. Hawaulizi mtu kuwa una-expect kulipwa kiasi gani. Ukiongopa, jaribu kuwa mjanja.
Nimeshasoma Sana mkuu Wala sidhani Kama majibu yanayopatika Google Basi yana mguide kila muajiri kuhusu majibu ya swali hili. Nilishafanya interview kwenye UN Agency nikajibu kwa kutumia hayo majibu ya Google lakini waliendelea kunibana nitaje kiwango Wala nisiogope
 
Nimeshasoma Sana mkuu Wala sidhani Kama majibu yanayopatika Google Basi yana mguide kila muajiri kuhusu majibu ya swali hili. Nilishafanya interview kwenye UN Agency nikajibu kwa kutumia hayo majibu ya Google lakini waliendelea kunibana nitaje kiwango Wala nisiogope
Achana nao hao bado maunderground wanafikiri sisi hatujapita huko wanapopataja. Hata mimi binafsi huko google nimesoma sana na nikaongezea skills zangu kulingana na experiences nilizopitia nimeshafanya interviews karibia 50 kwenye mashirika tofautitofauti so hiyo ya kukataa kujibu swali la mshahara halikwepeki lazima interviewer atakulazimisha utaje kiwango ili akupime kiwango chako.
 
Back
Top Bottom