Usijisahau ukipata

life255

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
587
Reaction score
1,470
Kuna jambo nimeambiwa na Babu mmoja mtu mzima, nikabaki nalo kichwani:

"Ukipata hata milioni moja, usijisahau mbele ya watu au wenzako."

Kweli kabisa. Maisha yanaweza kubadilika leo na kesho yakabadilika tena. Pesa inaweza kukupa uwezo wa kufanya mambo mengi, lakini haipaswi kukufanya umsahau aliyekuwa na wewe wakati huna kitu.

Usimdharau mtu kwa sababu leo una uwezo kuliko yeye. Usibadili lugha, heshima wala tabia kwa sababu tu mfukoni kuna pesa.

Ukipata, jenga maisha yako; usijenge kiburi.

Maana mwisho wa siku, watu watakumbuka zaidi ulivyowatendea ulipokuwa na uwezo, kuliko kiasi ulichokuwa nacho.
 
OKAY ASANTE KWA TAARIFA
 
Mkeka ulitiki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…