Shephard Sinkamba
Member
- Sep 10, 2018
- 14
- 8
[emoji294] Panya mmoja alichungulia kupitia kijitundu kilichokuwa kwenye ukuta wa nyumba ya Mkulima mmoja akiangalia kwa umakini wakati mkulima yule pamoja na mke wake wakifungua kimzigo flani.
[emoji294]Kutakuwa kuna chakula gani humo ndani? " Panya yule alijiuliza, alishtuka sana pale alipogundua kwamba ulikuwa ni mtego wa panya.
[emoji294]Kwa mshituko mkubwa, alipiga kelele za tahadhari :" Kuna mtego wa panya!!, kuna mtego wa panya!!
[emoji294]Kwa dharau kuku akainua kichwa chake na kumwambia panya, "Ndugu panya, nashangaa unanipigia kelele zisizo eleweka, naomba ujue hili ya kwamba, mtego huo ndilo kaburi lako na kifo chako wewe, ila kwangu mimi hainihusu wala hauna madhara kwangu. Pia uwepo wa mtego huo hauniudhi hata kidogo.
[emoji294]Panya yule hakukata tamaa, akageukia kwa mbuzi na kumwambia, "Kuna mtego wa panya humu ndani!!, kuna mtego wa panya humu ndani!!". Mbuzi yule bila wasi wasi akamjibu bwana Panya, "Samahani sana bwana panya, japo siwezi kufanya chochote juu ya hili isipokuwa kukuombea tu. Amini ya kwamba kwenye maombi yangu nawewe upo.
[emoji294]Panya akamwendea ng'ombe na kukwambia," Kuna mtego wa panya humu ndani!!, kuna mtego wa panya humu ndani!!. Ng'ombe akasema, " Moow!!! , ndugu Panya, samahani sana juu ya hilo, pole sana kwa hilo. Kwakweli mimi hilo hainihusu na halina madhara kwangu.
[emoji294]Kwa huzuni na majonzi makubwa panya akarudi ndani ya nyumba na kujiinamia akijua kwamba kumbe mtego ule ni kwa ajili yake na hakuna muhusuka mwingine.
[emoji294]Basi bwana, siku hiyo usiku sauti ilisikika nyumba nzima, hali iliyoashiria ya kwamba kuna kitu kimenaswa mtegoni.
[emoji294]Kwa haraka haraka mke wa mkulima yule alikimbia kuelekea mtegoni kujua nini kimetokea. Kulikuwa na giza nene hivyo hakuweza kujua fika ni kitu gani kimenaswa mtegoni. Maskini!, kumbe alikuwa ni nyoka mkubwa alikuwa kanaswa. Nyoka yule alimuuma yule mama.
[emoji294]Alipiga kelele jambo lililo mfanya mkulima yule aende kuona kulikoni, alivyoona ameumwa na nyoka, haraka haraka alimkimbiza hospitali. Mama yule akirudi akiwa na homa.
[emoji294]Kila mtu anajua kwamba huwa unatibu homa kwa supu safi ya kuku, Alisema mkulima yule huku akielekea kibandani akamkamata kuku na kumchinja ili atengeneze dawa ya mgonjwa.
[emoji294]Lakini pamoja na jitihada zote mke wake aliendelea kuugua, hivyo wakaja ndugu, jamaa na marafiki kumwona na wakakaa naye kwa masaa kadhaa. Hivyo kuwalisha watu waliofika siku ile ilibidi amchinje Mbuzi.
[emoji294]Hata hivyo hali ya Mama yule ilizidi kuwa mbaya, baada ya muda si mrefu alifariki dunia.
[emoji294]Hivyo watu wengi walikuja kwa ajili ya mazishi ya mama yule, hivyo mkulima yule ilibidi amchinje ng'ombe wake ili aweze kupata nyama ya kutosha kuwalisha watu wote.
[emoji294]Wakati wote ule panya alikuwa akiyashuhudia yale kupitia kwenye shimo lake kwa masikitiko makubwa
FUNDISHO
[emoji654]Unapoona mwenzako anapatwa na tatizo, usimdharau na kuona kwamba tatizo lile ni lake mwenyewe. Kumbuka kwamba wote tuko kwenye safari iitwayo "maisha", huwezi kujua kesho yako. Inabidi kusaidiana na kutiana moyo.
[emoji654]Mwenzako kafukuzwa kazi, we unafurahi na kusherehekea kisa alikuwa kakuzidi cheo. Huwezi kujua kesho wewe ukafukuzwa yeye akarudishwa.
[emoji654]Mwenzako hajapata mtoto kwenye ndoa yake ni mwaka wa kumi sasa, we unamcheka. Huwezi jua kesho huyo mtoto uliyenaye akapata ajali akafa halafu huyo unayemcheka akapata watoto.
[emoji654]Mwenzako kashindwa kumpeleka mtoto wake shule, we unamcheka badala ya kumsaidia. Kesho huwezi jua, hao wakwako uliowapeleka wakarudi na DIVISION =0, na wale uliokataa kuwasaidia Mungu akawafungulia mlango mwingine.
[emoji654]Mpendwa mwenzako alikuwa mhubiri mkubwa sana, Leo kaanguka dhambini badala ya kumwombea wewe unamsengenya, "Alijifanya sana, ona sasa hana lolote.......". Ushawahi kujiuliza swali hili?. Kama yeye alikuwa mhubiri mkubwa akaanguka dhambini, wewe usalama wako uko wapi?. Usimsengenye, badala yake funga na kuomba kwa ajili yake. ( WARUMI 15:1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.).
[emoji773]MWISHO :Kama kuna mtu alikutenda vibaya au alifurahia matatizo yaliyokupata, usiwe na kinyongo ndani ya moyo wako wala kiburi na roho ya malipizi. We msamehe kabisa na kumpenda. Tumejifunza kwa panya, japo aliwaambia wakadharau, walipochinjwa, yeye mwenyewe alihuzunika. (
[emoji654]WAKOLOSAI 3:13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
[emoji122][emoji122]Mungu akubariki sana mpendwa unapoendelea kutafakari ujumbe huu.