Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Omb 4:13 SUV
[13] Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wake Na maovu ya makuhani wake, Walioimwaga damu ya wenye haki Katikati yake.
Viongozi wa kiroho wa Israel, yaani manabii na makuhani, walishindwa kutimiza wajibu wao na kugeuka chanzo cha dhambi na ukatili kwa watu wao.
Uongozi wowote wa kiroho bila uadilifu unaweza kuleta maangamizi mabaya kwa kanisa, jambo ambalo ni chukizo mbele za Mungu.
Tumeona Dhambi za manabii na makuhani zilichangia kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa taifa lao, badala ya kulinda haki na kutangaza kweli ya Mungu, wao walihalalisha uovu na hata kushiriki kumwaga damu za wenye haki.
Uharibifu huu unatokea pale viongozi wa kiroho wanapopotoka, wanalisababisha Taifa lote kuingia kwenye shida na kuangamia vibaya.
Wakati manabii na makuhani wa agano la kale walihalalisha dhambi na kuua wenye haki, katika agano jipya napo kunaonyesha wazi Yesu aliuwawa na viongozi wa kidini kipindi hicho. Tunapata ukweli kwamba uongozi usio wa kweli hufanya mambo mabaya na yaliyo machukizo mbele za Mungu.
Kifo cha Yesu hakikuwa cha hasara, pamoja na viongozi wa kidini walishiriki, kifo cha Yesu kilikuwa sadaka ya haki kwa ajili ya ulimwengu mzima. Kupitia damu yake njia ya wokovu ilifunguliwa au kupatikana.
Ebr 9:14-15 SUV
[14] basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? [15] Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Tuelewe kwamba kupotoka kwa viongozi wa kiroho kuna madhara makubwa sana kwa kanisa, na jamii nzima, ndio maana maandiko yanasisitiza sana juu ya wachungaji na walimu lazima wawe waadilifu.
1 Pet 5:2-3 SUV
[2] lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. [3] Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
Tunapaswa kuelewa hili, kumtegemea Mungu ndio jambo la msingi na sio mwanadamu, Yesu Kristo ndiye chanzo cha wokovu wetu na sio kiongozi wako. Yeye amebeba jukumu la kuhani na nabii wa kweli.
Ikiwa Yesu alijua kuna manabii wa uongo na wanaweza kulisumbua kanisa, alionya juu ya hilo. Jambo ambalo kanisa linapaswa kuwa makini sana siku zote.
Mt 7:15 SUV
[15] Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
Tumeshajua viongozi wa kiroho wanavyoweza kuleta madhara mabaya pale wanapogeukia dhambi, wanaweza kuliingiza kanisa na jamii katika eneo baya.
Tujae neno la Mungu, iwe rahisi kugundua viongozi walioingiliwa na Shetani na kuanza kuwatumia vibaya, itatusaidia kusimama katika msingi wa imani yetu pasipo kufuata upepo mbaya.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana