Usichokijua kuhusu GOOGLE: Facts zitakazokufumbua macho!!

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
1.Google waligundua GPA's au Maksi za Mitihani Sio kigezo cha kuajiri. imepelekea Asilimia 14 ya team za wabunifu wa google hawajaenda shule na wanalipwa mishahara minono sana.

2.Mfanyakazi wa GOOGLE anapofariki Mjane/Mgane wake anapokea nusu ya mshahara wake kwa Muda wa miaka Kumi, Na kama umeacha mtoto mdogo, atalipwa zaidi ya TSH2Million Kila mwezi hadi atakapofika miaka 19.

3.16% ya vyote vinavyokuwa searched google kwa siku huwa havipatikani/havipo google. sio kila kitu google inamajibu.

4:Kwa kubonyeza Kile kitufye "I AM FEELING LUCKY", kwa mwaka kinaisababishia hasara ya Billion 237 kwa sababu Kurasa itakayokuja haitakuwa na matangazo ambayo ndio chanzo kikubwa cha mapato kwao. Ndio maana browser nyingi zitakupeleka moja kwa moja kwenye page ya kawaida. kwa sasa imepunguziwa upendeleo. na baada ya google instant kuwa developed ambayo inafanya vyote unapata exact search na tangazo juu.

5:Google wanaingiza Trillioni zaidi ya 43 kwa mwaka kutokana na matangazo, karibu mara mbili ya budget yetu yenye misaada mingi tu.

6:Kwa dakika Moja Zinafanyika Google Search Millioni 2 na zaid duniani kote.

7:Sasa Hivi wanatengeneza Computer (development stage lkn) yenye uwezo wa kujiprogram Yenyewe bila mtu kuhusika.

8:Kusearch kitu kimoja katika Google na kupata jibu kunahitaji Uwezo mkubwa wa kikompyuta kuliko uwezo unaotumika kupeleka CHOMBO MWEZINI.

9Database ya Google Earth in ukubwa/uwezo zaidi ya wakutunza data wa 20,000,000GB (20Petabyte)

10:Mwaka 2014, 89% ya mapato yao ambayo ilikuwa ni TSH 142Trillion na zaidi yalitokana na matangazo.

11:Kupitia Google earth waliweza kutambua alama ya nyota iliyo katika bendera ya Israel (david star) katika paa la airport ya IRAN. Imekuwa hapo miaka 30 hadi ilipogunduliwa na serikali ya iran ikawaamuru waje kuitoa japo wao walisema hawajui chochote kuhusu hilo
starofdavidIranAir.jpg
Flagbig.GIF



Ukweli ni kwamba, miaka thelasini iliyopita maengineer wa ISRAEL walipewa tenda ya kujenga hilo jengo na kipindi cha utawala wa Shah Mohamed Reza Pahlavi mwaka 1969.

Kuna uwezekano Kwa siri waliichora alama hiyo ya kizayuni ambayo imegunduliwa miaka michache iliyopita na googlemap. Viongozi wa Irani walikasirishwa sana. Ikumbukwe nchi hizi zina uhasama mkali.

12:Mwanamke aliyewapangisha waanzilishi wa Google vijana wawili gereji yake waliyoitumia kama office kubuni wazo hili la google, Walivyotoka kimaisha walimpa kuwa CEO wa YOUTUBE moja ya vitu vinavyomilikiwa na kampuni ya Google.

13: HAYATI/MAREHEMU STEVE JOB, ALISHAWAHI KUWAPIGIA SIMU GOOGLE KUWAAMBIA KUWA RANGI YA NJANO KWENYE LOGO YA GOOGLE, ILE O YA PILI HAIKO SAWA,

14: MICROSOFT WANAMILIKI BING KAMA SEARCH ENGINE YAO, SEHEMU NYINGI WATU WANALIPWA KWA KUAMUA KUTUMIA BING BADAlA YA GOOGLE. LKN BADO GOOGLE HAISHIKIKI

 
Last edited:
1.Google waligundua GPA's au Maksi za Mitihani Sio kigezo cha kuajiri. imepelekea Asilimia 14 ya team za wabunifu wa google hawajaenda shule na wanalipwa mishahara minono sana.
Hii ni POINT kubwa, sisi waTZ tunalazimisha tu kusoma mambo meeeeeeengiiiiiiiiii (tena yasiyokuwa na msingi na ambayo hayatusaidii maishani) wakati wenzetu wanaangalia mtoto akili yake inaFITi wapi wanapeleka huko. Yani mtu anasoma si kwasababu anapenda bali tu ili mkono uende kinywani. Nadhani siku tutakapoligundua hili tutafika mbali.
 
Back
Top Bottom