Usibebe Mimba yangu kabla Sijakuoa.

Usibebe Mimba yangu kabla Sijakuoa.

Liky

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
431
Reaction score
255
Tuko kwenye uhusiano, pamoja na mambo mengine tunahitaji kukidhi haja za mwili. Ninataka kutumia kinga, unakataa, unadai inakuumiza, ninakushauri utumie Birth control pills unakubali kishingo upande. Unaniingizia story za kuishi pamoja, ninakwambia tuvute subra kidogo tupange maisha maana kuishi pamoja sio lelemama, hizo ni familia mbili zinaungana tayari, hata kama ni bila ndoa. Unakasirika, unaamua kunikomesha. Siku inayofuata unaacha kumeza pills makusudi, unadaka mimba ukidhani hapo ndo nitabadilisha maamuzi yangu. Kwa shingo upande ninakubali, lakini moyoni ushanitoka. Ujeuri wako unaongezeka, ukidhani kuwa umeshaniweza. Ninajifanya fala hadi mtoto anazaliwa. Baadaye ninafanya maamuzi magumu kuwa mtoto nitamhudumia lakini mimi na wewe hatuwezi kuendelea.
(Kama ukinichkulia katili, poa tu...maamuzi ya kibinifasi hayajengi familia).
Baada ya miaka miwili ninapata anaesikilizana na mimi, ninamuoa tunaendelea na life, wala sitaki kujua unapitia nini huko ulipo.
Wallah! Kama hizo birth control pills wangetutengenezea na za kiume, mimba zisizotarajiwa ingebaki story.
 
mmmh sasa kama umejua ana kibur si usonge mbele
 
tatizo hapo unahisi ni nani..
1. kama mtoto ushapata
2. kama uliweza kuhudumia mimba sababu ya kulia hutaki mtoto ni nini..!!!
3. unahisi huyo mpya nae hana matatizo!
4. kama unampenda ya nini umfanyie maigizo wakati maisha mafupi..
mwisho akili zako ni sawa na kumuacha mke kwa kumfumania na kwenda kuoa mwingine aliyefumaniwa..!!!
 
tatizo hapo unahisi ni nani..
1. kama mtoto ushapata na hata huyo ukiyemuoa wa pili pia mtazaa
2. kama uliweza kuhudumia mimba mpaka mtoto akazaliwa sababu ya kulia hutaki mtoto ni nini..!!!
3. kama mwanzo ulimpenda ila umemwacha kwa kukubebea mimba.. unahisi huyo mpya nae hana matatizo!
4. kama uliamini kuwa unampenda ya nini umfanyie maigizo wakati maisha mafupi..
mwisho akili zako ni sawa na mwanaume anayemuacha mke wake aliyemfumania na kwenda kuoa mwanamke mwingine aliyekwishawahi kuachwa kwa kufumaniwa..!!!
Tulia, soma tena uelewe. Majibu yako hapo hapo.
 
Single maza lingine limeongezwa, vibenten havitoisha !!!!
 
Enyi vijana...unaanzaje kummezesha pills binti mdogo ambaye hata hujamuoa na hujui kama utamuoa au la? Nimesikitika sana kwa nini msitumie njia za asili mfano kalenda na nyinginezo? Lakini mimi nafikiri unapoanza uhusiano na mwanamke ambae hutumii kinga basi chukua yule ambaye hata likitokea la kutokea halitakusumbua. Ila na sisi wanawake tuna kiranga hivi ukimng'ang'aniza mtu kwa kumbebea mimba hata kama utafanikiwa kumshawishi akuoe hivi ndoa ya namna hiyo nyote wawili mtaifurahia kweli?
 
Mseto wenyewe nasahau itakua pills hizo.
Hata ukipewa kazi ya kumtoa paka nje kila siku utakuta kanyea ndani.
Wanaume hatuwezi kumeza hizo pills hata kama unakula baada ya mwaka bado tutasahau
Majukumu yetu ni mengi sana.
Ushauri wangu acha zinaa na umwambie akusubiri utakapokuwa tayari kumuoa na uongo kwa wasichana sio mzuri.
Jipange vizuri na uoe uanze maisha kama familia
 
😂😂 Hata mimi sielewi, ni ndoto tu niliota, sijui ina maana gani.
 
Mseto wenyewe nasahau itakua pills hizo.
Hata ukipewa kazi ya kumtoa paka nje kila siku utakuta kanyea ndani.
Wanaume hatuwezi kumeza hizo pills hata kama unakula baada ya mwaka bado tutasahau
Majukumu yetu ni mengi sana.
Ushauri wangu acha zinaa na umwambie akusubiri utakapokuwa tayari kumuoa na uongo kwa wasichana sio mzuri.
Jipange vizuri na uoe uanze maisha kama familia
Kama nikifanikiwa kuota tena ndoto ya hivyo nitafanya kama ulivyonielekeza mkuu...😀
 
Tutaijazaje dunia Sasa . wape nafasi na wengine wapya waishi
 
Write your reply...mkuu naona ushakuwa kiwanda cha kufyetua single mama sasa ndugu yangu hao single mother unaowasababisha unamuachia nani ? huon huko ni kutaka kutukomoa wanaume wenzio
 
Back
Top Bottom