usalama kwanza
JF-Expert Member
- Oct 3, 2012
- 386
- 158
Habari.
Mimi ninahusika na vifaa vya usalama kama CCTV camera, Electric Fence, GPS tracker na vinginevyo. Na ID hii ni kwa ajili ya maswala hayo tu . Lakini kwasababu jamiiforums imenipa manufaa mengi sana , nimepata wateja , ushauri , maoni , vitu vingi kwa kweli. Sasa nimeona leo na mimi niwape kitu ambacho naamini kitawasaidia wengi kama ambavyo nyie mmekuwa ni msaada kwangu.
Leo nataka niwahamasishe wanajamiiforums kutokukosa fursa hii ya hisa za Vodacom zinazouzwa sasa. Nitawaeleza kwa njia rahisi kabisa ili kila mmoja apate kuelewa na wale wenye uzoefu wa hisa wataweza kuongezea utaalamu zaidi kadiri itakavyowezekana.
Kwa kifupi kununua hisa ni kununua sehemu ya umiliki wa kampuni, Kwahiyo utapata sehemu ya faida/hasara ya kampuni hiyo. Sasa kwa kampuni kama Vodacom imekuwa ikipata faida , sijawahi sikia imepata hasara hivyo una uhakika wa kupata gawio lako la faida kila itakapokuwa imetangazwa. Na kwangu mimi sitegemei Vodacom wakaanza kupata hasara leo ama kesho hii ni faida ya kwanza na ya uhakika.
Jambo la pili ni faida kutokana na kukua kwa mtaji. Tunaposema kukua kwa mtaji ni kuongezeka kwa thamani ya hisa zako. Leo umenunua hisa moja shilingi 850 labda baada ya mwaka utaiuza 1,500/- basi hapo ndio utaona faida hiyo. Faida hii utaipata pale utakapouza hisa zako. Mimi ninaamini kwa kiasi kikubwa kuwa thamani ya hisa zitapanda kitu ambacho sina hakika nacho ni zitapanda kwa kiasi gani na lini . Lakini nitakupa matarajio yangu ingawa yanaweza yasitimie
Angalia bei ya hisa za kampuni leo hii 12/4/2017 na sekta/aina ya biashara nimejaribu kuzipanga kwa ukubwa wa bei.
ACA 13120 hii ipo kwenye sekta ya madini
TBL 12000 hii ni kampuni ya bia
TCC 11500 hii ni kampuni ya sigara
JHL 10730 hii ni kampuni ya insurance(mnaweza rekebisha kama haipo sahihi)
SWISS 5400 hii ipo kwenye usafirishaji wa mizigo airport
EABL 4860 Hii ni kampuni ya bia
NMB 2750 Hii ni benki.
Sasa kwa uchambuzi rahisi kabisa nimejaribu kulinganisha Vodacom (sekta ya mawasiliano) na kampuni nyingine vinazofanya vizuri . Ukilinganisha NMB ambayo ni bank na sekta ya mawasiliano ni wazi sekta ya mawasiliano inafanya vizuri zaidi kwahiyo ni matarajio yangu kuwa bei ya hisa za Vodacom itapanda kuipiku ya NMB , ukilinganisha EABL na SWISS ni wazi kuwa Vodacom ni kampuni kubwa kushinda hizo kumbuka sekta ya usafirishaji wa anga imeyumba kidogo sasa hivi, kwahiyo ni matarajio yangu kuwa Vodacom itapanda kushindana/kukaribia na kampuni kama JHL, TCC,TBL,ACA .
Lakini kuna vitu vya kuzingatia pia.
1. Vodacom wametoa hisa nyingi sana , hivyo kama unavyojua bidhaa ikifurika sokoni bei inaweza kuwa ndogo au inaweza kupungua
2. Sekta ya mawasiliano itaendelea kuingiza hisa nyingi zaidi kwa makapampuni kama Tigo , Airtel, Halotel yatakapo anza kuuza hisa hivyo hii inaweza athiri bei ya hisa za Vodacom kwenye soko la sasa hivyo inaweza isifikie matarajio ya hapo juu.
Kikubwa , Hope for the best and prepare for the worst na kingine ujue the higher the risk the higher the return.
N.B. Mambo yakienda vizuri baada ya kununua hisa msisahau kutupatia kazi ya kuwafungia vifaa vya usalama kama GPS tracker , Electric Fence ,CCTV cameras Fire alarms , Access control systems na n.k . www.isecure.co.tz , info@isecure.co.tz. 0714890018 , naomba tuwasiliane kwa mambo ya kazi tu , kuhusu hisa nitajitahidi kujibu hapa hapa .