Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Habari za J2 wakuu
Kanda ya mashariki imejaliwa kuwa na warembo, na kuna sifa kuwa mapenzi ndiko yaliko anzia. Kule kwetu usia tunaopewa ni kuwa mtoto wa kike mume ni kichwa cha familia, mheshimu kama unavyomheshimu baba yako, lakini usimtegemee mume 100%, hili litakufanya uone gumu la mume, gubu la mume linaweza kuvunja ndoa.
Mtoto wa kike kwanza anapokuwa mwali, baba na mashangazi waanza kumchongea vito vya dhahabu, hii ni sawa na kumfungulia mtoto bank account, dhahabu ni equity. Kule kwetu mara nyingi mtoto wa kike hategemewi kusoma madarasa yote ayamalize yeye.
Siku ya ndoa, inategemea na uwezo wa family, familia nyingine zitamuwaga mtoto kwa mali nyingi, lakini hata kama familia haina uwezo wa kununulia kiwanja na Mercedes Benz, ile pesa unayotunzwa siku ya harusi, hata kama ni laki mbili mtoto wa kike ile pesa si ya kuchezea, unaitunza na ukifika kwa mume wako unatafuta fursa ya kufanya kibiashara kidogo.
Kanda ya mashariki mtaji wetu mkubwa tuliyorithishwa na mabibi na mashangazi ni kupika. Ukifika kwa mume unamuomba akusaidie kutafuta kisehemu cha biashara, wengine mume anakua mkali hataki utoke nje, basi akutafutie kijana wa kukusaidia biashara, zile laki mbili ulizotoka nazo kwenu unaanzia kupika maandazi na chapati unafungua tea room.
Faida unayopata humshirikishi mume wako, lakini pia si ya kufuja, hii ni pesa unayotakiwa kuifadhi, unaweza kuongeza dhahabu au kuiweka kibindoni. Mama yako akija kukusalimiia unampokea, siku anayoaga anakwenda, mume wako hatakiwi ajue ulimpa mama shilinigi ngapi.
Aibu gani mama anaaga na mume hana pesa, je mama asubiri mpaka mkwe apate pesa? Basi ile pesa ya bishara mama akiaga unampa nauli. Ukitegemea mume amnunulie mama ticket siku mkigombana mume anaanza, hamna shukurani ukoo mzima, juzi mama yako amekuja hapa nimetumia milioni 2, hilo ndiyo gubu la mume linalokinahisha ndoa.
Biasha za mume zikikwama au mume ametumbuliwa kazini basi hapo ndiip unapotoa akiba yako ili kuokoa jahazi la familia, na haya yote mtoto wa kike unatakiwa yawe kifuani kwako.
Sky Éclat.