USHUHUDA

USHUHUDA

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
1,966
Reaction score
2,200
Ushuhuda


May 12, 2014

Mwanamke mmoja kutoka Bolivia aitwaye Adelaida De Carrillo alipelekwa Mbinguni na Kuzimu na Yesu Kristo. Kule alionyeshwa ni Utakatifu gani anaotakiwa mtu kuwa nao ili aweze kuingia kwenye UFALME WA MUNGU, na pia ni dhambi gani (ambazo wengi wetu tunadhani kuwa ni ndogo), zinaweza kumfanya mtu aingie Jehanamu.


Tuko kwenye safari ya maisha ya kimwili hapa duniani tukielekea kwenye maisha ya kiroho kwenye ulimwengu ule ujao. Huo ni ulimwengu halisi ambao una maisha halisi, utawala halisi na kanuni halisi za kuingia huko.

Wakati ulimwengu tuaoishi leo una serikali nyigi na watawala wengi, ulimwengu ule ujao utakuwa na serikali moja tu inayoongozwa na Yesu Krito. Wakazi wa uliwengu huo ni watakatifu WOTE!!!

Huo ni ulimwengu unaoongozwa na Mungu mwenyewe kwa upendo na amani. Kule hakuna magonjwa, vita, njaa, na dhambi zingine zote. Tiketi ya kuingia kule ni moja tu: nayo ni kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi aliyekufa na kufufuka kwa ajili yetu. Kisha tunaishi hapa duniani kwa kutii maagizo yake.

Hata hivyo, wale wote ambao hawatakuwa wamestahili kuingia kwenye ulimwengu huo (kutokana na wao kuishi maisha ya dhambi na uasi dhidi ya sheria za Mungu hapa duniani), watatupwa nje ya mbingu kweny giza na moto, yaani kwenye jehanamu ya milele.

Katika ushuhuda huu, tunaona kile ambacho Bwana Yesu anatuagiza ili tuweze kustahili kuingia kwenye ufalme ule ujao na kuishi na Mungu MILELE!!!

Adelaida De Carrillo anasema:

HATUA YA 1: Ilianzia Kanisani kwenye wakati wa Huduma

Katika Ezekieli 36:25-26, Biblia inasema:
“Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.”

Ushuhuda wangu uko namna hii: Siku moja ya Jumapili, kwenye saa 3 hivi, Kanisa letu lilikuwa na kipindi cha Huduma. Mungu alikuwa akimimina baraka zake juu yetu. Mchungaji wangu aliniambia, “Adelaida, Bwana ananiambia nikupake mafuta.”

Aliweka mafuta mengi kwenye viganja vya mikono yake na akaanza kunipaka mwilini. Alinipaka masikioni, miguuni, tumboni na kwenye mwili wangu wote. Alipoweka mikono yake kwenye uso wangu, niliona mwanga mkubwa ukija kutokea juu, ukinielekea mimi. Kuanzia hapo nilipoteza fahamu na sikujua kilichokuwa kinaendelea kwangu.

HATUA YA 2: Safari Yangu Kwenda Mbinguni

Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake. Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!

HATUA YA 3: Kuoshwa na Kubadilishwa Moyo Wangu

Malaika walikuja na kunichukua tukaenda juu pamoja nao. Walianza kupambana na mashetani maana njia yetu ilikuwa imewekewa vizuizi. Kulikuwa na blangeti jeusi kwenye mawingu, likiwa limejaa mapepo yaliyojaribu kutuzuia kupita. Baadaye niliona mwanga mweupe kutoka Mbinguni na malaika mzuri sana akiwa na upanga wenye nuru mkononi mwake. Aliinua upanga wake na kuanza kupigana na mapepo yale ili sisi tupite. Malaika yule alionekana kama Mwana wa Mfalme. Alikuwa na bamba la dhahabu kifuani mwake na nguo nzuri sana. Nywele zake zilikuwa za rangi ya dhahabu, na uso wake ulikuwa kama miali ya mwanga. Alikuwa mzuri sana!

Ghafla, nilisikia sauti ndani yangu, ikisema, “Nataka ufahamu kuwa nilikupa magoti hayo ili uwe mwanamke wa maombi, na si kwa ajili ya kuzungukazunguka ukifanya mambo yasiyonipendeza Mimi. Magoti haya ulipewa ili kufanya maombezi kwa ajili ya Kanisa. Ulitakiwa kulijua hilo.”

Kwa ujumla mimi nilikuwa si mwanamke wa maombi sana. Maombi yangu yalikuwa na kawaida ya kuwa mafupi sana. Lakini Bwana alitaka niwe mwombaji zaidi.

Malaika aliendelea kuosha miguu yangu, huku akiiparua, na mimi nilikuwa namlilia Mungu anihurumie kutokana na maumivu yale. Bwana akasema: “Miguu hii ulipewa ili uwe unazunguka kwenda kuhubiri Injili yangu, kueneza Neno langu na si kuzungukazunguka kwa majirani zako kupeleka umbeya, na kufanya mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Na kwa sababu hii,” Bwana akasema, “ninasafisha miguu yako.”

Jambo hili liliendelea na lilifanyika kwa maumivu makali sana. Bwana akasema, “Hii ni muhimu sana ili uweze kuelewa mipango niliyo nayo kwa ajili yako.”

Baadaye, nilipelekwa kwenye sehemu nyingine ambako malaika wngine watatu walikuwa wananingojea. Sehemu hii ilikuwa tofauti. Niliona vitu kama mashine. Malaika wale walianza mchakato mwingine wa kusafisha macho yangu kwa kutumia aina fulani ya mafuta. Nilihisi kama vile macho yameng’olewa kutoka kwenye matundu yake. Nikasema: “Tafadhali mnihurumie. Naomba msaada. Kwa nini mnanifanyia hivi?” Ilikuwa kama vile wanakwangua macho yangu. Kitu kama samaki kilitolewa kutoka kwenye macho yangu.

Bwana akasema, “Binti yangu, nafanya hivi kwa ajili yako kwa sababu nataka ubadilike. Mambo uliyokuwa ukifanya duniani hayakuwa yakinipendeza. Sikuwa nafurahi ukiwa duniani ulipokuwa ukitazama mambo ambayo hayakunipendeza Mimi. Ulikuwa ukitazama TV” [Soap Operas] ... “Hayo hayajengi maisha yako.” ... “Sifurahii pale wanangu wanapoangalia vitu kama hivyo; vitu ambavyo havinipi utukufu.”

Nikasema, “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Na Bwana akasema, “Katikati ya usiku kwenye saa sita, mara zote huwa uko macho ukiangalia sinema ambazo hazikujengi wewe; na nyingi ya sinema hizo zimejazwa mambo mengi yanayohusu mapenzi. Sikukupa macho hayo kwa ajili ya mambo kama hayo. Nilikupa hayo macho ili utazame mambo yale tu yanayonipa Mimi utukufu. Na kwa sababu hii ndiyo maana ninasafisha macho yako.”

Malaika waliendelea kusafisha macho yangu huku mimi nikiendelea kuomba kuhurumiwa. Baadaye macho yangu yalipakwa mafuta, na kuanzia hapo nikawa na mtazamo tofauti; macho yangu yalibadilishwa kabisa. Bwana akasema, “Usitamani waume wa watu wengine tena!” Mimi nilikuwa na kawaida ya kuvutiwa sana na wanaume wengine, na Bwana alisema kuwa mambo hayo hayampendezi.

Nitakueleza mimi nilikuwa mtu wa namna gani. Nilikuwa Mkristo duni wa kilokole ambaye alikuwa hatendi mambo sawasawa na Biblia inavyoagiza. Kila nilichofanya kilikuwa ni kutokana na matamanio yangu na njia zangu binafsi, kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu. Nakueleza haya ili uweze kurekebisha njia zako; ili roho ziweze kuokolewa. Nakueleza kuwa tamaa NI dhambi; kuangalia michezo ya kwenye TV [Soap Operas], sinema za kidunia – mambo yote haya hayampendezi Mungu.

Malaika waliendelea na mchakato wa usafishaji. Walikuwa na kijifimbo kidogo cha kioo ambacho walikiingiza moja kwa moja masikioni mwangu. Walipoanza kukwangua masikio yangu, nilihisi maumivu makali sana. Moyo wangu ulihisi maumivu haya yote. Mara maji meusi yalianza kutoka kwenye masikio yangu, na baadaye maji ya rangi ya kijivu. Niliendelea kulia.

Bwana akasema, “Binti yangu, ninasafisha masikio yako kwa sababu ulipenda sana kusikiliza mambo ambayo hayanipendezi Mimi. Ulipenda kusikiliza umbeya. Uliyatoa kabisa masikio yako kusikiliza mambo yasiyonipendeza Mimi. Baadhi ya watu wanakuja kwako kuleta umbeya na wewe ulipenda kuwasikiliza hata kama walileta umbeya dhidi ya Mchungaji wako mwenyewe. Ulipenda kuwasikiliza hao. Badala ya kumtetea Mchungaji wako na kumsahihisha mbeya huyo ili arekebishe njia zake, ulikuwa kama wao, ukifanya umbeya pamoja nao. Usisikilize umbeya tena. Mtu akija kwako na umbeya wa aina yoyote, waombe radhi, kisha ondoka mara moja bila kushiriki. Usisikilize tena mambo yasiyokujenga!”

Nikasema: “Bwana, nisamehe!” Nilijua kuwa nilikuwa nina hatia. Hakuna jambo lililofichika mbele za Mungu. Hakuna anayeweza kujificha mbele zake. Kila tunachofanya na kusema hapa duniani kimewekwa kumbukumbu Mbinguni. Kutokana na maumivu yote yale masikioni mwangu, nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba rehema zako.” Hatimaye masikio yangu yalipakwa mafuta na malaika.

Bwana akaniambia: “Kuanzia leo na kuendelea, utasikiliza tu mambo ambayo nimekuruhusu kusikiliza. Utafanya mambo yale tu ambayo nimekutaka ufanye; hautakuwa Adelaida wa zamani tena. Hivi sasa wewe ni mtu mpya na ni lazima uwe ni mwanamke yule ambaye ninataka uwe.”

Baada ya hapo nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako malaika walianza kusafisha kinywa changu. Ulimi wangu ulitolewa kabisa kinywani na kuwekwa kwenye aina fulani ya sinia. Malaika alianza kusafisha ulimi wangu, na hapa tena nilihisi maumivu makali sana. Bwana akasema: “Nataka kukusafisha. Nataka kukusafisha.”

Malaika walivyokuwa wanakwangua ulimi wangu, maji meusi yalikuwa yanatoka humo, na baadaye yalitoka maji meupe. Mwishowe malaika walitumia maji matamu sana kuoshea ulimi wangu. Yalikuwa matamu mno. Hakuna kitu duniani kinachoweza kulinganishwa na utamu wa maji yale. Kisha ulimi wangu ulipakwa mafuta. Kinywa changu nacho kilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka kwenye kinywa changu.

Bwana akasema, “Binti yangu, ninafanya hivi kwa ajili yako ili usifanye umbeya tena; ili uache kufanya mambo yasiyonipendeza; maana ulimi wako ulishiriki katika mambo mengi sana ambayo hayanipi utukufu Mimi. Ulisema uongo mwingi sana. Acha kusema uongo! Kusema uongo hakutoki kwangu. Waongo hawanipendezi Mimi. Waongo wote hawataniona Mimi. Hakuna mwongo atakayeingia kwenye Ufalme wa Mbinguni.”

Nikasema: “Bwana, nihurumie. Najua kuwa nilifanya mambo hayo yote. Nilisema uongo mara nyingi, lakini tafadhali nisamehe.” Nilisema yote haya kwa sababu ya maumivu niliyokuwa nayahisi.

Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ninakupenda. Ukiendelea na hali uliyokuwa nayo, nitakupoteza. Kama nisingefanya yote haya, usingebadilika kamwe. Ni lazima niokoe moyo wako na hii ndiyo sababu ya kufanya yote haya. Nakupenda, na kwa sababu nakupenda, sitaki kukupoteza.”

Bwana akasema tena: “Kama ulivyo wewe, wengi kati ya watu wangu wako namna hiyohiyo.Wanasema uongo, wanaishi maisha ya aina mbilimbili, na wanaonekana wako safi mbele ya watu wengine. Unapomwinulia mumeo sauti ulimi wako unakuwa --------- pia.” Kinywa changu kilitakaswa kabisa. Halafu Bwana akaniambia nimeze maji hayo. Nami nikafanya hivyo.

Ulimi wangu na kinywa changu vilipakwa mafuta ya thamani sana ya mbinguni. Mafuta hayo yalikuwa maalum sana, yakiwa na harufu ya thamani sana. Hayawezi kulinganishwa na mafuta yoyote ya hapa duniani. Ulimi wangu ulirudishwa tena kinywani mwangu. Malaika mmoja alikuja na kuweka hatamu kwenye koo langu. Na Bwana akaniambia: “Hii ni sawa na vile farasi anavyowekewa hatamu.”

Nikwambie tu kwamba, hii ndiyo njia pekee tunayoweza kubadilishwa. Acha kuongea maneno machafu na kushiriki katika mambo ambayo hayatujengi. Mambo haya hayampendezi Mungu kamwe.

Acha kutamka maneno machafu na yasiyo na maana. Wako Wakristo wengi – akina kaka, dada, Wainjilisti, Wamisionari, n.k., ambao wanapenda kusema maneno machafu na yasiyo na maana. Niko hapa kukuhakikishia juu ya kile ambacho Bwana alinionyesha ili maisha yako yabadilishwe. Ushuhuda huu ni kwa ajili ya wewe kubadilika. Upendo wa Mungu na wa kwangu kwako ndio ulioleta ushuhuda huu.

Ulimi wangu ulirudishiwa tena mahali pake na malaika na ukawa umebadilishwa kabisa. Naweza kukuambia sasa, hakuna mtu anayeweza kunikasirisha tena. Sasa naweza kufanya yale tu yanayompendeza Mungu.

Kisha, pua yangu nayo ilipitia mchakato huohuo. Maji meusi yalitoka puani mwangu wakati wa kusafishwa na baadaye maji meupe. Pua yangu ilipakwa mafuta na nilihisi maumivu makali sana wakati wa mchakato wa kusafishwa. Nilisema: “Bwana, tafadhali niambie mambo niliyofanya kwa kutumia pua yangu ambayo hayakukupendeza.”

Bwana akaniambia: “Baadhi ya wateja wako huvuta sigara na wewe unavuta ule moshi kupitia pua zako maana uliwahi kuwa mvutaji sigara na sasa wewe unajisikia vizuri kukaa nao wakati wanapovuta.” Nikasema: “Bwana, najua. Nisamehe. Naomba unirehemu.”

Bwana akaniambia: “Uko sawa tu na wale wote wanaovuta sigara na wote wanaokunywa pombe pale unapokaa nao na kuvuta harufu ya sigara na pombe.”

Bwana akasema tena: “Hii ndiyo sababu yangu ya kukusafisha wewe. Kwa hiyo, kuanzia leo kila utakapomwona mtu anavuta sigara au anakunywa pombe, hautajisikia vizuri kukaa nao tena. Utajisikia kinyaa.”

Hakuna cha kujitetea mbele za Bwana. Mungu anafahamu fika wewe ni nani na mimi ni nani. Libarikiwe Jina Takatifu la Bwana, Amina.

Niliendelea kumwomba Bwana rehema na nilipelekwa sehemu nyingine. Pale, malaika walianza kuosha mwili wangu uliobakia kwa kutumia sabuni nyeupe. Maji ya kijivu yalitoka kwenye mwili wangu.

Nikasema: “Bwana, nisaidie. Tafadhali, nisaidie.” Malaika walikuwa wanasugua mwili wangu na ngozi ya juu iliondoka. Damu ilikuwa inachuruzika kutoka kwenye ngozi yangu na nikamwuliza Bwana: “Kwa nini unanifanyia hivi?”

Bwana akaniambia: “Ninakusafisha. Ni lazima uwe safi mwili wako wote, nafsi yako, na roho yako. Roho yako, nafsi na mwili ni lazima viwe safi, asema Bwana.”

Sabuni ilisuuzwa kutoka kwenye ngozi yangu kwa kutumia maji ya thamani sana. Kisha malaika walipaka mafuta kila sehemu ya mwili wangu; kila sehemu ya mwili wangu. Sehemu zote za mwili wangu zilipakwa mafuta.

Bwana akaniambia: “Usirudi tena kwenye njia zako za zamani, binti yangu. Hivi sasa wewe ni Mtakatifu wangu aliyepakwa mafuta.”

Nikasema: “Bwana, nisamehe kwa mambo yote niliyokuwa nikifanya zamani hata mbele za uwepo wako. Nisamehe Bwana kwa kuwa kila kitu ambacho Mchungaji wangu alijaribu kunisahihisha mimi nilikuwa nikipingana naye. Nilisema mambo mengi kwake ambayo sikutakiwa kusema.”

Mchungaji wangu mara nyingi alikuwa akiniambia kuwa mavazi yangu kama Mkristo hayakuwa sawa. Nilishindana naye sana. Aliwahi kuniambia kuwa nilisema uongo na mimi nikahuzunika. Pale mtu anapopotoka na Mchungaji wake akamsahihisha, mtu huyo huhuzunika. Siku zote mimi nilikuwa kinyume na Mchungaji wangu.

Kisha nilipelekwa kwenye idara nyingine ambako nilipokelewa na malaika watatu. Malaika wale walitumia nguo nyeupe kufuta maji kwenye mwili wangu. Kwenye nyuso za malaika wale, niliona kuwa walikuwa wanajisikia huruma sana kwa ajili yangu kutokana na yote niliyopitia lakini hawakusema kitu chochote, hata neno moja. Sikuweza kumwona Bwana kwenye sehemu hizi. Nilikuwa nasikia tu sauti yake.

Malaika wengine watatu walinipokea kwenye idara nyingine. Malaika hawa walinivika nguo nyeupe ya juu na sketi ndefu. Sketi ilikuwa ndefu sana kiasi kwamba miguu yangu ilikuwa haionekani.

HATUA YA 4: Niliwaona Watakatifu Wengine Mbinguni

Nilipelekwa kwenye sehemu nyingine na mlango ulifunguliwa. Niliona mwanga mkubwa ukimulika kupitia mlango ule. Ulikuwa ni mwanga wa kuvutia sana. Bwana aliniambia nipite ndani. Nikasema, “Bwana, naogopa.”

Nilijua kuwa Mungu alikuwa ananiandaa kwa sababu anataka niokoke. Upendo haupendi mtu yeyote apotee. Nilisema: “Bwana, unirehemu.” Moyo wangu ulikumbuka vizuri sana kila kitu nilichoacha nyuma kule duniani; wanangu. Nikasema: “Bwana, naikabidhi familia yangu mikononi mwako.”

Kwenye sehemu ile niliweza kuona vitu kama miji mikubwa na watu wengi sana ambao walikuwa wananingojea. Walikuwa wananipungia mikono. Walikuwa wanataka niende kwenye sehemu ile walikokuwa.

Bwana akaniambia: “Mtakatifu wangu, muda umeshafika. Muda umefika wa kuwaona wote walio hapa ambao wanakungojea.” Watu wengi sana walikuwa wananingojea. Nami nilimwuliza Bwana: “Kitu gani kinaendelea hapa?”

Bwana akaniambia: “Ni wakati wa wewe kwenda na kuwahubiria watu wote. Ni wakati wa wewe kwenda na kuhubiria mataifa yote. Ni wakati umefika. Yote ambayo nimekuambia, nenda kawaambie Kanisa langu maana nitalifanya Kanisa langu kuwa kamilifu. Nitaifanya nyumba yangu kuwa kamilifu. Kisha Neno langu litapelekwa sehemu zote duniani zilizobakia, asema Bwana. Lakini kwanza ni Kanisa langu.”

Hatua Ya 5: Safari Yangu Kuzimu na Yote Niliyoyaona Kule

Malaika walinitoa pale na tukawa tunaelekea chini. Nikawauliza malaika wale: “Mnanipeleka wapi?” Niliingiwa na hofu kubwa sana na ghafla ardhi ilifunguka.

Nikauliza tena: “Mnanipeleka wapi? Kitu gani kinachoendelea kwangu?” Tuliingia moja kwa moja kwenye ardhi. Ilikuwa inatisha sana. Kila upande kulikuwa na giza, nami sikuelewa malaika wale walikuwa wananipeleka wapi.

Tulifika mahali ambako niliweza kuona mwanga mkali. Kulikuwa na mlango chini ya ardhi. Mlango ule ulikuwa mbaya sana. Hakuna kitu kwenye dunia hii kinachoweza kufananishwa na mlango ule.

Bwana akaniambia: “Huu ni mlango wa kuzimu.”

Nilifikiri labda ndio nilikuwa nimehukumiwa kutupwa kuzimu kwa yale yote niliyotenda zamani. Kulikuwa na mtu akiningoja pale. Bwana wetu Yesu Kristo ni mzuri sana. Bwana wetu Yesu Kristo alinyosha mkono wake kwangu. Alikuwa akiningoja kwenye mlango wa kuzimu huku akiwa na ufunguo. Na niliweza kuona wanyama wengi wa kutisha wakitokea kuzimu.

Nikasema: “Bwana, ni kitu gani kinachotokea kwangu? Tafadhali Bwana, nihurumie.”

Bwana akaniambia: “Nitakuonyesha kuzimu na kila kitu kilichomo ndani yake, ili uweze kuogopa na pia, kupitia wewe, watu wengine waweze kujua kuwa kuzimu kweli kupo.”

Nikasema: “Bwana, hapana. Sitaki kwenda humo!”

Bwana akasema: “Binti yangu, fuatana nami. Njoo.”

Tulipofika pale, baadhi ya mapepo yalinyosha mikono yao kujaribu kunikamata. Nikasema, “Bwana, siwezi kuona, tafadhali.” Nilijaribu kufunika uso wangu kwa mikono yangu, lakini bado nilikuwa naona kila kitu waziwazi. Ukiwa pale, unasikia kila kitu, unaona kila kitu na unagusa kila kitu, kama ilivyo kwa roho zingine zilizoko humo kuzimu. Bwana aliwazuia mapepo kunikamata. Nilikuwa niko na Bwana. Niliweza kuona jinsi roho zilizoko kuzimu zinavyoteseka.

KUNDI LA KWANZA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: MASHOGA NA WASAGAJI

Bwana alinipeleka mahali fulani. Watu waliokuwa pale walikuwa ni Wakristo. Walimtumikia Bwana walipokuwa duniani lakini wakati huohuo walikuwa wakitenda mambo yasiyompendeza Mungu. Walikufa na sasa wako kuzimu.

Bwana alinionyesha mchungaji ambaye alikuwa akitumia vibaya Neno la Mungu. Mchungaji huyu alikuwa anafanya mapenzi na wanaume wenzake. Hakuwa mwana wa Mungu kwa sababu wana wa Mungu hawatendi mambo kama hayo. Hapohapo, niliweza kuona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa mchungaji yule ambaye alilinajisi Neno la Mungu. Mapepo yalimwingiza kwenye tyubu fulani, na tyubu hiyo ikaanza kumzungusha na kumzungusha! Alikuwa anateseka kweli! Alipokuwa duniani, alikuwa akinajisi watoto wadogo. Alinajisi hata wanaume wenzake.
Kama ambavyo unasoma ushuhuda huu, huenda haya ndiyo unayofanya. Kuzimu ni halisi na pia kuna adhabu inayowangoja wote wasiotii Neno la Mungu.

Mungu alikuumba wewe mwanamume. Pia, alimuumba mwanamke. Niliona jinsi mwanamume huyo alivyokuwa anateswa kuzimu. Roho yake ililipuka kisha ikajikusanya tena na kuendelea na mateso yale.

Bwana alimwambia: “Mwanangu, ulikuwa na muda wa kutosha duniani wa kutubu na kurekebisha njia zako.”

Bwana alimwonyesha skrini na kwenye skrini hiyo yalionekana maisha yake alipokuwa duniani. Alionekana mzee ambaye alikuwa akimwambia asifuate njia mbaya; akimwambia atii Neno la Mungu. Kila neno ambalo Bwana alimwambia kwa njia mbalimbali alionyeshwa kwenye skrini ile. Alikataa kutubu na kurekebisha njia zake.

Na siku moja, alipata ajali na akafa. Hivi sasa yuko kuzimu. Alijifanya kuwa yeye ni mchungaji kumbe hakuwa mchungaji.
Bwana alimgeuzia mgongo na yule mtu akaanza kutukana. Hakuna upendo kuzimu. Hakuna kitu kabisa zaidi ya uchungu, huzuni, na maumivu ya kutisha ambayo hakuna mtu anayeweza kustahimili.

Wakati niko pale, nilijihisi kama nataka kufa. Nilisema: “Bwana, nataka kufa.”

Bwana akaniambia: “Binti yangu umeshakufa. Ona kile ambacho roho zinateseka kuzimu binti yangu.”

Nikasema: “Bwana, siwezi kuvumilia zaidi. Roho yangu inaungua. Joto ni kali sana. Bwana, siwezi!”

KUNDI LA PILI LA ROHO NILILOONA KUZIMU: MAKAHABA

Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliona jinsi mapepo yanavyoitesa roho ya mwanamke mmoja kuzimu. Mwanamke huyu alikuwa ni kahaba wakati akiwa duniani. Aliwahi kuokoka. Bwana alimtoa kwenye ukahaba. Lakini alianguka tena na kurudia ukahaba ule na akawa katika hali mbaya kuliko mwanzo. Alikufa kwa kuuawa na sasa yuko kuzimu.

Niliona jinsi mapepo yalivyokuwa yanamtesa kuzimu. Badala ya kuolewa na kufanya mapenzi na mume mmoja tu, aliamua kufanya kinyume. Mungu anachukia mambo hayo yote. Hayo ni machukizo mbele za Mungu. Mwanamke yule alikuwa uchi. Alilazwa chini na mapepo walikuwa wanamteza. Nikasema: “Bwana, mhurumie.”

Bwana akasema: “Hapanaaa binti yangu. Alikuwa na muda wa kutosha duniani wa kutubu.” Bwana alimwonyesha skrini na wakaonekana Wainjilisti mbalimbali walioenda kumweleza juu ya kuyatoa maisha yake kwa Yesu. Lakini hakutii sauti ya Mungu. Hivi sasa yuko kuzimu.

Ujumbe huu ni kwa wanawake wote wanaojiuza miili yao. Labda unafanya hivyo kwa ajili ya kupata fedha za kulisha wanao; labda huna mume. Mungu anakuambia leo urudi kwake. Mungu atakuhudumia wewe na familia yako. Kwa wanawake wote wanaouza miili yao, nawaambia kwamba, tubuni leo na kumrudia Mungu kupitia ushuhuda huu. Mungu ameleta ushuhuda huu kwa ajili ya wokovu wa roho zenu ili kwamba msije kuishia kwenye sehemu ile ya mateso.

KUNDI LA TATU LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WAONGO NA WASENGENYAJI

Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine waliko waongo na wasengenyaji. Niliona jinsi walivyokuwa wanateseka kuzimu. Ni hali ngumu mno. Ni vigumu mno kuongelea kuhusu kuzimu.

Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako. Kuwasengenya majirani zako kunaweza kukupotezea wokovu. Kumsengenya mchungaji wako kuwaweza kukupotezea wokovu wako. Tubu leo kupitia ushuhuda huu na umrudie Mungu, na Mungu naye atakurudia wewe, asema Bwana.

Niliuliza: “Bwana, yaani hii ni kwa sababu ya usengenyaji tu?”

Bwana akasema: “Ndiyo, ni kwa usengenyaji tu.”

Nikauliza: “Bwana, lakini si huwa tunaomba rehema tunapokutenda dhambi?”

Bwana akasema: “Hapana. Watu hawa hawakuomba rehema; na sasa wanalipia dhambi zao.”

Kwa sababu hiyo, tunatakiwa kupatanishwa na Mungu kila siku kwa sababu hakuna ajuaye ni lini atakufa. Usiondoke uweponi mwa Mungu. Usengenyaji unaweza kukufanya upoteze wokovu wako.

KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WAABUDU SANAMU

Mateso mahali pale yalikuwa makali sana. Kwa wanawake wote wanaomtumikia Maria Lionza, je, mnamjua ni nani huyo? Huyo ni pepo. Bwana alinionyesha Maria Lionza ni nani. Ni pepo ambaye wachawi wengi wanapiga magoti kumwabudu kule kuzimu. Mapepo yaliwatesa kupita kiasi. [Maelezo ya blogger: Maria Lionza ni mzimu unaoabudiwa hasa kule Venezuela. Unaweza kusoma zaidi kwa kubofya HAPA.]

Miali ya moto wa kuzimu huwa haizimiki. Inawaka usiku na mchana. Inawaka milele. Tafadhali ningependa utambue hili: waabudu sanamu hawawezi kuuona uso wa Bwana.

Mungu anataka kubadili maisha yako. Mungu anataka uache kuabudu sanamu. Mungu anataka umwabudu Yeye tu. Kuna Mungu mmoja tu na zaidi yake hapana mwingine.

Roho za watu walio pale wanalazimishwa kumwabudu pepo huyo hata kama hawataki. Wanateswa sana. Wanalazimishwa kuvuta sigara kuzimu pale wanapomwabudu huyo pepo.

Shetani ni mwongo. Amekuja kuua na kuharibu. Lakini ni lazima nikuambie hili: Yesu Kristo alikuja kuleta uzima na uzima tele. Mungu Mwenyezi anakuita leo kupitia ushuhuda huu. Natamani uweze kuelewa ujumbe huu na mipango aliyo nayo Mungu kwa ajili yako. Mungu ni halisi.

Nilikuwa kuzimu kwa saa 16 ili kuelewa makusudi ya ujumbe huu; ili niweze kuuhubiri; ili niweze kusambaza ujumbe wa wokovu kwa kila mmoja kwa moyo wote.

Nilimwona Barbara. Nilimwona Shango. Ninyi mnaomwabudu Barbara, mtupeni nje ya nyumba zenu. Bwana anasema huyo ni pepola ukahaba.

Barbara hana upendo. Amejaa uharibifu. Ziko nyumba nyingi ambazo hazina amani. Yeye ndiye anayehusika na hilo. Pia, unaweza kuwa unashangaa ni nini kinachoendelea kwenye maisha yako – labda una sanamu yake kwenye nyumba yako. Natamani sana ungeelewa ujumbe huu na mpango wa Mungu kwa ajili yako. Pepo huyu alikuwa anawalazimisha watu kuzimu wamwabudu yeye. Watu pale wanateseka sana. Ni moto tu kila mahali.

Nilimwuliza Bwana: “Je, hukuwapa watu hawa nafasi ya kurekebisha njia zao?”

Bwana akasema: “Niliwapa. Nilituma watakatifu wangu kwao.”

Palepale kuzimu skrini inawekwa mbele yao nao wanaonyeshwa kila kitu. Roho zilizo kuzimu hazina cha kujitetea mbele za Bwana. Bwana anawaonyesha kila fursa waliyopewa walipokuwa duniani.

Kama hutatubu na kurekebisha njia zako leo, utaona jinsi kifo kitakavyokushangaza nawe utaishia kuzimu.

KUNDI LA NNE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WALEVI

Bwana alinipeleka kwenye sehemu nyingine. Ilikuwa ni kama klabu kubwa. Nilisikia watu humo wakipiga kelele, huku wakiomba kuhurumiwa na kusaidiwa. Nikauliza: “Ni nini kinachoendelea humu?”

Bwana akasema: “Peleka ujumbe huu kwa wote wanaotumia vileo usiku na mchana; kwa wote wale wanaoingiza miilini mwao vitu ambavyo haviwajengi; kwa wote ambao wanatumia hata fedha za watoto wao kwa ajili ya kulewea; peleka ujumbe huu kwa wanawake wale wote wanaolewa – waambie warekebishe njia zao kupitia ujumbe huu.”

Pale kuzimu niliona meza imewekwa mbele yao ili wanywe. Walilazimishwa kunywa bila kupenda. Wote walikuwa katikati ya moto. Kile walichokuwa wakinywa ni asidi nami niliona jinsi roho zao zinavyolipuka baada ya kunywa.

Nikasema: “Bwana, hapana. Siwezi kuvumilia zaidi ya hapa, tafadhali Bwana.”

Kuna mwanamume kuzimu ambaye, wakati angali duniani, Bwana alimpelekea Mwinjilisti baa akiwa analewa. Mwinjilisti yule alimwambia atoe maisha yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo, maana Mwinjilisti yule alihisi kuwa mtu yule asingechukua muda mrefu kabla ya kufa. Mtu yule alimtukana Mwinjilisti huyo. Alimwita kuwa ni mwanamke mwenye wazimu, jambo ambalo watu wengi duniani wanawaambia Wakristo duniani. Siku ileile, mtu yule alitoka baa akiwa amelewa. Alipata ajali na sasa yuko kuzimu.

Alikuwa analazimishwa kunywa vinywaji vya kule kuzimu. Alijaribu kukimbia mateso lakini mapepo hayakumwachia. Anateswa pale kuzimu milele.

WAVUTA SIGARA

Wavuta sigara nao wana idara yao kule kuzimu. Wale wote wanaovuta bangi na wao pia wana idara yao kuzimu. Wanateswa milele.

KUABUDU AU KUHESHIMU SANAMU

Huenda unajiita Mkristo au vinginevyo, lakini bado unaheshimu au kuabudu sanamu. Ni lazima utubu leo na kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo.

Kule kuzimu kuna wanaume na wanawake. Unaweza ukawa tajiri sana hapa duniani kama ukitaka. Utaenda kuzimu usipotaka kuyatoa maisha yako kwa Yesu Kristo. Fedha zako haziwezi kukununulia wokovu. Wokovu wako ulishanunuliwa na Bwana wetu, Yesu Kristo. Amina.

Alikuwapo mwanamume mwingine ambaye naye alikuwa analazimishwa kunywa kinywaji cha kuzimu. Nikamwuliza Bwana kwamba yule alikuwa nani.

Bwana akasema: “Mtu huyu alikuwa ni Mtakatifu wangu. Aliniacha na kuziendea njia zake na hatimaye alikufa katika dhambi.”

Kila kitu ambacho Bwana alikisema kuhusiana na mtu yule kilikuwa kinaonyeshwa kwenye skrini – ujumbe, siku na saa ambayo Bwana alimpelekea ujumbe. Mtu huyo yuko kuzimu sasa kutokana na uasi wake.

Unaweza kuwa unasema kwamba hii si kweli. Lakini niko hapa kukueleza kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ni halisi.

KUNDI LA SITA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WANAWAKE WA MUNGU [WAHUBIRI]

Hawa ni wanawake waliomtumikia Mungu wakati wakiwa duniani. Lakini hawakutaka kubadilika na kukubaliana na mafundisho ya Mungu. Badala yake wao walipendelea kumtumikia Mungu kwa namna zao wenyewe. Mateso niliyoyaona hapa yalikuwa mabaya zaidi ya yale niliyoyaona kabla.

Nilisikia huzuni kubwa sana kwa ajili ya hawa wanawake wa Mungu walio kuzimu, maana walimtumikia Mungu wangali duniani.

Bwana aliniambia: “Kila wakati niliongea nao. Nilijaribu kuwarekebisha kupitia baadhi ya Watakatifu wangu lakini hawakutaka kuelewa makusudi.”

Bwana alinionyesha mmojawapo wa wanawake hawa. Alikuwa amekaa kwenye kiti na kiti kile kilikuwa kimezungukwa na moto. Ghafla pepo lilitokea na kummiminia maji fulani kichwani.

Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa analia; Bwana wetu alikuwa analia.

Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”

Bwana akaniambia: “Niliteseka sana kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu. Alikuwa ni Mtakatifu wangu. Nilimrekebisha ili asiipende dunia wala mambo ya dunia.” Bwana alikuwa anamsahihisha aache kupaka nywele zake rangi.

Bwana aliniambia: “Alikuwa anaonea aibu mvi nilizompa. Alikuwa anajaribu kujionyesha kwa mwonekano ambao si wa kwake.”

Nywele zangu zilikuwa nyeusi na mimi nilitaka ziwe nyeusi. Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupatia.” Pepo liliendelea kumtesa. Alimlilia Bwana amsaidie. Bwana alimwambia kwamba alishachelewa. Akaanza kutukana.

Hatuwezi kuishi kwa kujificha uhalisia wetu. Siku moja sote tutakuwa na mvi.

Kadiri mapepo yalivyoendelea kummimina yale maji kichwani mwake, shingo yake ilipinda upande mmoja. Nywele zake zilikuwa zinadondoka. Alinyosha mikono yake ili kujaribu kuomba msaada.

Nikasema: “Siwezi kuvumilia zaidi.”

Nilijaribu kufunika uso wangu maana hata mimi nilikuwa ninabadili rangi ya nywele zangu lakini sikuweza kuufunika uso wangu.

Bwana akaniambia: “Usionee aibu kile ambacho nimekupa.”

Mwanamke yule alikuwa na nywele ndefu sana. Alikuwa ni mwanamke mrembo lakini alitaka kuwa mrembo zaidi ya alivyokuwa. Lakini aliishia kutenda kosa kubwa sana. Kama Mungu ametupa mvi, ni lazima tuzikubali maana zinatoka kwa Mungu. Jambo hilo ni lazima litimie kwenye maisha yetu.

Nikasema: “Bwana, sikujua kuwa kubadili rangi ya nywele ni dhambi.” Kisha nikasema: “Bwana, msaidie. Mrehemu.”

Bwana alipeleka Mchungaji kwa mwanamke huyu wakati alipokuwa duniani. Alikuwa ni Mwinjilisti. Mwanamke huyu alikuwa akihubiri na kufundisha. Kama ilivyo kwa baadhi, pale wanapohubiri, wanajaribu kujionyesha wao kwanza kwenye kusanyiko ili wakubalike kwa jinsi walivyo, ili waweze kuhubiri na kufundisha kile wakitakacho.

Mwanamke huyu hakuwahi kutaka kuelewa makusudi ya Mungu. Hatimaye alikufa na sasa yuko kuzimu. Huyu alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia Bwana.

Bwana akasema: “Binti yangu, naenda kukuonyesha wanawake wanaotumia vipodozi kwenye nyuso zao.”

Nikasema: “Bwana, hata mimi natumia vipodozi pia. Natumia poda kwenye uso wangu ili nionekane mrembo zaidi, ili kuziba mabakabaka kwenye uso wangu.”

Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi mimi. Nafurahishwa na mwonekano wa asili wa Watakatifu wangu. Mwanamke anatakiwa anifurahishe mimi na mume wake. Kwa hiyo, hahitaji vipodozi ili kuonekana mrembo kwa mtu mwingine yeyote.”

Wakati huo ndipo nilipomwona mwanamke ambaye alikuwa ameshikilia kioo mikononi mwake na mapepo yalikuwa yanamlazimisha kupaka vitu fulani usoni mwake. Alipaka majimaji fulani usoni kisha ngozi ya uso wake ikabanduka na kuanguka.

Huenda unasoma ushuhuda huu na unasema kwamba vipodozi si dhambi. Nikwambie sasa – Mungu anaposema jambo, sote ni lazima tutii! Mwanamke yule alikosa kutii alipokuwa duniani. Alikuwa akitumia vipodozi hapa duniani na sasa yuko kuzimu. Kule analazimishwa kupodoa uso wake usiku na mchana.

Bwana akasema: “Vitu hivyo havinipendezi mimi. Unakumbuka niliposema kuwa yule atakayeupenda ulimwengu ni adui wa Mungu?”

Ni lazima tutii mstari huo wa kwenye Biblia: Msiipende duni, wala mambo yaliyoko katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. (1 Yohana 2:15).

Sote tutahukumiwa kwa neno hili. Aina zote za vipodozi unazotumia hapa duniani, utavitumia na kuzimu pia. Nilikuwa nikitumia “wet-lips” ili kufanya midomo yangu ing’ae na kuwafanya watu wengine wanione.

Nikasema: “Bwana, unisamehe maana nilikuwa na hatia ya jambo hili.”

Bwana akasema: “Ninafanya hivi kwa sababu ya upendo nilionao kwa roho yako. Ili kuleta hofu ya uzito wake ndani yako; ili uweze kuelewa uzito wa matokeo; ili kwamba uweze kuwaeleza na wengine waache kutumia vipodozi.”

Mwanamke yule alikuwa katikati ya moto huku akiendelea kulazimishwa kujipodoa uso wake. Matokeo yake uso wake na midomo yake vilikuwa vinadondoka chini.

Enyi wanawake wa Mungu; wanawake wa Mungu msiwatazame majirani zenu. Yatazamani maisha yenu binafsi leo na kumwomba Mungu. Sema: “Bwana, ni mambo gani ninayotenda ambayo hayakupendezi?” Muulize Bwana naye atakujibu. Mungu huwa anajibu.

KUNDI LA SABA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WANAWAKE WANAOVAA MAPAMBO YA VITO

Bwana aliniambia: “Sasa nitaenda kukuonyesha waliko wanawake wanaovaa mapambo ya vito.”

Hapo nilimwona mwanamke ambaye alikuwa akilazimishwa na mapepo kuvaa hereni kwenye masikio yake. Joka kubwa lilikuja kwake naye alivaa hereni masikioni mwake. Kisha lile joka lilijiviringisha kwenye shingo yake.

Bwana yuko kinyume kabisa na wanawake wanaotumia mapambo ya vito. Nikasema: “Bwana, lakini mbona hili ni pambo la kawaida tu?”

Bwana akasema: “Binti yangu, vitu hivyo havinipendezi Mimi.”

KUNDI LA NANE LA ROHO NILILOONA KUZIMU: FAMILIA NA WAPENDWA

Bwana alinipeleka mahali ambako nilimwona mwanamke akilia; akipiga kelele sana kuzimu. Nilimwuliza Bwana: “Bwana, mwanamke huyu ni nani?” na Bwana akasema: “Nitakuonyesha huyu ni nani.”

Alikuwa ni mwanamke niliyemfahamu miaka mingi iliyopita. Tangu nilipoyatoa maisha yangu kwa Bwana, sikuwahi kuhubiri ujumbe wa wokovu kwa mwanamke huyu.

Bwana aliniambia: “Yuko hapa kuzimu kwa sababu yako. Nilitaka kuiokoa roho yake kupitia wewe lakini hukuwahi kwenda kumweleza habari zangu.”

Nikasema: “Bwana, naomba unihurumie!”

Mwanamke yule aliomba rehema kwa Bwana nami nikasema: “Bwana, mhurumie.”

Mwanamke huyu alikuwa mlevi wakati alipokuwa angali duniani. Bwana alimwonyesha kupitia skrini fursa zote alizokuwa nazo wakati angali duniani za kuyatoa maisha yake kwa Bwana lakini alikataa. Siku ambayo nilisukumwa kuongea na mwanamke huyu, sikusema naye kwa sababu aliniambia kuwa angeniua kama ningemweleza habari za Bwana. Niliogopa na sikuweza kumhubiria. Hivi sasa yuko kuzimu akiteseka. Jina lake ni Augustina.

KUNDI LA TISA LA ROHO NILILOONA KUZIMU: WATUMIA DAWA ZA KULEVYA

Nilimwona mwanamume ambaye alikuwa akilazimishwa na mapepo kutumia dawa za kulevya kuzimu. Alipewa kitu kama sigara ikiwa imejaa miali ya moto ili aivute. Nikasema: “Bwana, mwanamume huyu ni nani?”

Bwana akaniambia: “Njoo umwone ni nani.”

Nilimkaribia na nikashangaa kuona kuwa kumbe ni kaka yangu Esau yuko kuzimu! Nilijawa na huzuni sana kumwona kaka yangu akiteseka kuzimu. Nikasema: “Bwana, mhurume kaka yangu.”

Kaka yangu alinyoosha mkono wake ukiwa umejaa miali ya moto na kuanza kumwomba Bwana rehema. Bwana akamwambia kaka yangu: “Mwanangu, unakumbuka kuwa uliyatoa maisha yako kwangu wakati ulipokuwa gerezani na ukaniomba nikutoe gerezani; na ukaahidi kwamba ungenitumikia katika maisha yako yote?”

Kaka yangu akasema: “Bwana najua; nakumbuka. Lakini tafadhali nisamehe. Nipe tu fursa ya kutoka mahali hapa.”

Bwana alimwonyesha skrini na tukaweza kuona wakati akiwa gerezani miaka mingi iliyopita. Bwana alimwonyesha siku hiyo pamoja na ahadi zote alizoahidi kumtumikia Bwana.

Bwana alimtoa gerezani kwa ili aweze kumtumikia lakini alipotoka, alikataa kutimiza ahadi yake ya kumtumikia Bwana. Na miaka miwili baadaye aliuawa mikononi mwa mama yangu. Kaka yangu alikufa kifo kibaya kwa sababu ya kutokutii kwake.

Huyu ni kaka yangu ambaye ninakuambia habari zake. Kaka yangu mwenyewe yuko kuzimu! Inatisha! Sikutaka kulisema hili waziwazi lakini Bwana aliniambia kuwa ni lazima niliseme. Nililia sana nilipomwona kaka yangu akiwa kuzimu.

Huwezi kupata picha jinsi Bwana wetu anavyolia kwa ajili ya roho zilizoko kuzimu, Bwana aliniambia.

Bwana alinionyesha mwanamke aliyekuwa Mchungaji wakati alipokuwa duniani. Alikuwa amekalia kiti kilichozungukwa na miali ya moto. Alikuwa anavalishwa wigi (nywele za bandia) kuzimu na jingine tena juu yake.

Bwana aliniambia: “Alikuwa ni Mtakatifu wangu wakati fulani uliopita. Alikuwa ni Mchungaji wangu. Alikuwa ni mwanamke mkubwa wa Mungu. Nilimtumia kwa kiwango cha juu sana, lakini aliasi Neno langu.”

Nikasema, “Bwana, mhurumie.”

Alinyoosha mkono wake kwa Bwana kuomba msaada. Najua kuwa hadithi ya mwanamke huyu itasababisha maumivu makubwa sana ya kihisia.

Alikuwa ni mwanamke aliyemtumikia Bwana. Alibadili mafundisho ya Bwana. Alimwacha Bwana kwa ajili ya vitu vya dunia. Alikuwa akifanya vitu ambavyo vilikuwa havimpendezi Bwana. Alikuwa akisema maneno yasiyo na maana kila wakati. Bwana alimwonyesha kwenye skrini mambo yote aliyofanya wakati akiwa duniani.

Bwana alimwuliza: “Binti yangu, unaweza kukumbuka pale nilipokuletea Neno langu kupitia Mtakatifu wangu, Elma?”

Dada yangu, Elma alizungumza na mwanamke huyu wakati akiwa duniani lakini yeye alimtukana dada yangu. Alikataa kutii na Bwana akasema: “Hiyo ilikuwa ni fursa yako ya kurekebisha njia zako na kunirudia mimi lakini ulikataa na hii ndiyo adhabu yako. Je, unakumbuka jinsi ambavyo binti yako alikukumbatia na kusema, Mama rudi lakini hukutaka kusikiliza?”

Bwana alimgeuzia mgongo na mwanamke yule akaanza kutukana.
Bwana wetu Yesu Kristo alimgeuzia mgongo na kuanza kulia sana.

Nikauliza: “Bwana, kwa nini unalia?”

Bwana akasema: “Huwezi kujua jinsi ninavyojisikia kuona roho zikiwa hapa.”

NILIONA KITI CHA ENZI CHA SHETANI KUZIMU

Bwana aliniambia: “Naenda kukuonyesha kitu binti yangu. Sikuwa nimemwonyesha mtu yeyote kitu hiki kabla. Nataka ukione ili uweze kuelewa kuwa shetani ni mwongo. Shetani huiga mambo.”

Nikasema: “Bwana, tafadhali naomba unitoe mahali hapa. Siwezi tena kuvumilia zaidi.”

Bwana akanionyesha kiti cha enzi kuzimu. Niliona kiti cha enzi cha shetani kuzimu! Shetani anamwiga Mungu Mwenyezi huko kuzimu. Nilimwona akiwa amekaa kwenye hicho kiti chake cha enzi. Shetani ni mbaya sana. Naye anajifanya ana ngazi za madaraka.

Niliweza kuona malaika wamemzunguka lakini wote ni mapepo. Alikuwa amevaa joho jeupe likiwa limejaa madoadoa na ni chafu sana. Niliona wazee ishirini na wanne wakimwabudu shetani kuzimu. Walidondosha taji zao na kumwabudu. Niliweza kuona kuwa wote walikuwa ni mapepo.

Kiti cha enzi cha shetani kimejaa mambo yaliyoigwa kutoka Mbinguni. Kila kitu kilionekana kibaya sana.

Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”

Wakati huohuo, shetani aliita mojawapo ya mapepo yake na akalituma kwenda kumleta mtu fulani kutoka kuzimu. Mapepo yanafanya kila kitu ambacho shetani anayaambia yafanye. Kila wakati huwa anayatuma duniani ili kufanya uharibifu.

KITABU CHA KUZIMU

Bwana akasema: “Nataka ufahamu kuwa shetani huiga mambo ya mbinguni. Nataka ufahamu kuwa shetani ni halisi. Shetani anataka kuuharibu ulimwengu.”

Mahali pale niliweza kuliona pepo katika umbo la malaika wa kishetani likiwa na makucha marefu sana na limeshikilia kitabu mkononi mwake. Pepo hili lilikuwa linaandika kitabuni majina ya watu ambao wataenda motoni.

Nikauliza: “Bwana, kwa nini wanafanya hivi?”

Bwana akasema: “Nenda ukaiambie dunia kwamba watu wasio na Yesu Kristo maishani mwao, shetani ameshaandika majina yao kwenye kitabu cha kuzimu.”

Bwana akaniambia tena: “Angalia, pepo hili limetumwa kwenye barabara ili kusababisha ajali. Kuna ajali nyingi zinazotokea kwenye maeneo mbalimbali. Shetani na mapepo yake ndio wanaohusika na mambo haya.”

Nikasema: “Bwana, hali hii ni mbaya sana.”

Bwana akasema: “Ni muhimu uone mambo haya yote ili uwe na uwezo wa kuielezea dunia jinsi kuzimu kulivyo, ili dunia iweze kujua na kuamini kuwa kuzimu kweli kupo.”

NILITESWA NA BAADHI YA MAPEPO KUZIMU

Kisha Bwana alikuwa akinipeleka kwenye sehemu nyingine. Nikasema: “Niondoe mahali hapa. Hapa ni kubaya sana, tafadhali.”

Bwana alinishikilia mkono wakati tukiwa bado tunaenda. Ghafla lilitokea pepo la kutisha, kubwa lenye makucha marefu.

Pepo lile lilikamata nywele zangu na likaruka na mimi. Wakati huu sikuweza kumwona Bwana. Bwana alipotea na kuniacha peke yangu. Pepo lile lilinikokota hadi kwenye sehemu nyingine, kisha mapepo mengine yalikuja na kuanza kunitesa kwa namna mbalimbali.

Sauti ikawa inaongea kwenye ufahamu wangu ikisema: “Utabakia hapa kuzimu milele na utateswa, na utahisi maumivu na majonzi yote ambayo yako hapa kuzimu.”

Nikasema: “Bwana, siwezi kustahimili haya. Siwezi kustahimili haya!”

Pepo jingine lilikuja kwangu likiwa na mdomo mrefu sana, likapanda juu yangu. Nilijaribu kulisukuma lakini sikuweza. Liliingiza domo lake kwa nguvu kinywani mwangu na nilihisi mate yake kwenye kinywa changu chote. Nikapiga kelele: “Bwana, kwa nini unaruhusu haya yote yanipate?”

Bwana akasema: “Ni muhimu; ni muhimu kwa wewe kuwaambia watu duniani jinsi kuzimu kulivyo hasa ili waweze kuelewa makusudi.”

Bwana akasema: “MIMI NI MUNGU MTAKATIFU, wako watu kanisani ambao wanafanya kila aina ya mambo machafu kwa vinywa vyao.”

Nikauliza: “Bwana, nitawezaje kusema mambo haya yote?”

Bwana akaniambia: “Sema kila kitu nilichokuonyesha.”

Bwana alinionyesha skrini na nikaweza kuona uchafu mwingi. Wako watu wengi kanisani leo ambao wanatenda aina mbalimbali za dhambi za siri.

Nikauliza: “Bwana, hii ni nini?”

Bwana akasema: “Waambie wabadilike. Waambie kuwa MIMI NI MUNGU MTAKATIFU. Waambie kuwa vinywa vyao ni kwa ajili ya kunitukuza mimi na si kwa ajili ya uchafu.”

Nikasema: “Bwana, ondoa pepo hili mwilini mwangu” maana lile pepo lilikuwa linanyonya mwili wangu wote. Mate yake yalikuwa meusi sana na yamefunika mwili wangu wote. Hali ilikuwa inatisha. Harufu ya kuzimu ni mbaya mno kuliko hata mbwa aliyeoza. Sina maneno ya kuweza kuielezea. Nikasema: “Bwana, nisaidie. Siwezi kustahimili zaidi.”

Bwana akaniambia: “Binti yangu, tulia. Ni muhimu sana kwa wewe kupitia mambo yote haya.”

Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu?”

Mara pepo jingine lilikuja. Likanichukua hadi kwenye sehemu nyingine. Kule niliona roho zingine zikicheza. Nikauliza: “Bwana, nini kinachofuata cha mimi kufanya sasa?”

Niliwekwa ili nicheze katikati ya moto. Kulikuwa na vitu humo ndani vikinilazimisha kucheza. Nikauliza: “Bwana, kwa nini haya yananipata?”

Bwana akasema: “Kwa sababu wewe ni mchezaji. Huwa unacheza unaposikia kila muziki wa Kikristo na miziki mingine inayokupendeza wewe.”

Bwana akaniambia tena: “Mambo hayo hayanipendezi mimi.”

Nikasema: “Bwana, nisamehe. Sitarudia tena.”

Bwana akasema: “Kama ulivyo wewe, wako watu wengi miongoni mwa watu wangu ambao hucheza kama watu wa dunia. Wanachezesha viuno vyao kama watu wa kidunia. Mambo hayo hayanipendezi mimi.”

Nikasema: “Bwana, nisamehe. Naomba unihurumie,” kwa sababu roho yangu ilikuwa inaungua. Nilikuwa katikati ya miali ya moto. Ninaweza kukuambia jinsi kuzimu kunavyotisha kwa sababu roho yangu ilikuwa pale. Sisemi uongo hata kidogo. Nawaambia kweli tupu. Kuzimu ni halisi! Nilikuwa pale!!

Mapepo yalinitoa mahali pale na kunipeleka sehemu nyingine tena. Kulikuwa na minyoo mingi sana hapo. Minyoo ile iliingia sehemu mbalimbali za mwili wangu – kupitia masikioni, machoni.

Nikasema: “Bwana, tafadhali nihurumie. Nitafanya kila ulichoniambia nifanye, lakini tafadhali naomba unitoe hapa.”

Bwana akasema: “Hii ni muhimu sana ili kila mtu aweze kuelewa kuwa kuzimu ni mahali halisi. Watu wengi husema kuwa kuzimu hakupo. Nenda ukawaambie kuwa kuzimu kupo.”

Palepale nilikumbuka kitabu cha Luka 16:19-31 kinachoongelea juu ya tajiri na Lazaro. Pale kaka yangu aliponyoosha mkono alisema: “Bwana, peleka ujumbe huu kwa familia yangu ili wasije kuja huku kuzimu.”

Bwana aliniambia: “Kumbuka hadithi ya Tajiri na Lazaro. Tajiri alipoomba kwamba Lazaro atumwe duniani kuiambia familia ya tajiri kwamba kuzimu kweli kupo.”

Niliondolewa kwenye sehemu ambako nilikuwa nateswa na minyoo. Bwana akaniambia: “Ni muhimu sana ukaseme mambo yote uliyoona ili roho ziokolewe. Ninafanya yote haya kwa sababu ya upendo nilio nao kwa wanadamu. Kama nisingekuleta hapa, ningekupoteza.”

Bwana akasema tena: “Roho nyingi zitaokolewa kutokana na ushuhuda huu.”

Nikasema: “Tafadhali Bwana. Niondoe huku kuzimu. Siwezi kuendelea kuwa hapa!”
Nilipitia mateso mengi sana kuzimu huku moto ukiwa umefunika mwili wangu wote.

Hatimaye, ghafla nuru kali ilitokea na Bwana akanitokea. Nilimkimbilia Bwana na kumkumbatia. Nikauliza: “Bwana, kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini uliniacha peke yangu? Kwa nini???”

Bwana akasema: “Ndiyo binti yangu. Binti, ilikuwa ni muhimu sana uone maumivu ambayo roho zinayapata hapa kuzimu ili uwe na uwezo wa kuuelezea ulimwengu uliobakia.”

Kisha Bwana alinitoa pale. Bwana alinionyesha vitu vingine ambavyo sitaweza kuvisema kwa sasa. Mungu ataniambia ni lini niviseme vitu hivyo. Hivi sasa nitakueleza tu vitu vile ambavyo Bwana aliniambia niviseme.

SAFARI YANGU YA PILI KWENDA MBINGUNI – KILA KITU KIKO TAYARI MBINGUNI

Bwana akasema: “Nitakuonyesha mahali ambako niliwaambia mitume wangu kwamba naenda kuwaandalia mahali, ili mimi niliko na wao watakuwa hapo pia, ili ukamwambie kila mtu kwamba mambo haya ni halisi.”

Bwana alikuwa ananipeleka moja kwa moja hadi mbinguni. Kisha niliona mlango mkubwa ukiwa wazi.

Nikasema: “Bwana, kuzimu ni kubaya sana. Lakini mahali hapa [mbinguni] ni kuzuri.”

Bwana akaniambia: “Binti yangu, nitakuonyesha Mbinguni.”

Na niliona sehemu kama jiji kubwa mbinguni. Ndiyo, napaita mahali pale jiji kubwa kwa sababu hicho ndicho hasa nilichoona. Bwana alinipeleka kwenye mtaa mmoja mbinguni. Mitaa ya mbinguni ni ya dhahabu tupu. Ni dhahabu halisi kabisa! Niliona maua mazuri pembeni ya mitaa ya mbinguni. Ni maua mazuri mno kiasi kwamba hakuna maua hapa duniani yanayoweza kulinganishwa nayo!

Bwana alinipeleka mahali fulani na akaniambia: “Ninaenda kukuonyesha mto. Nitakuingiza humo.”

Kulikuwa na mawemawe kwenye mto huo. Mto wenyewe ni kama kioo. Mawe ya kwenye mto ule yanang’aa. Kulikuwa na samaki kwenye mto huo pia. Bwana alimtoa samaki mmoja kwenye mto ule na kumshika mkononi; na samaki yule alikuwa na furaha, huku akichezacheza mikononi mwa Bwana.

Nikasema: “Bwana, mrudishe samaki majini, atakufa.”

Bwana akasema: “Hakuna anayekufa hapa. Mauti haipo hapa. Mahali hapa kumejaa uzima tu. Kila kitu hapa ni uzima.”

Nikasema: “Bwana, kuna watu wengi sana kule wanaoteswa. Kwa nini hukuwapatia fursa ya kurekebisha njia zao ili waje hapa Mbinguni?”

Bwana akasema: “Wako pale kutokana na uasi wao.”

Bwana alinichukua kama mtoto mdogo kutoka kwenye mto hadi mahali pengine. Mto huo ni mzuri sana. Kila kitu kinachotungoja Mbinguni ni kizuri sana!

Kisha niliomba jambo kwa Bwana. Nilimwambia Bwana: “Ziko wapi roho ulizoziokoa? Wako wapi hapa mbinguni?”

Bwana akasema: “Nitakuonyesha.”

Bwana alinipeleka mahali ambako alinionyesha mmojawapo wa dada zangu katika Kristo ambaye alishakufa. Jina lake ni Aurora Esperanza. Bwana alinionyesha dada mwingine. Alikuwa ni binti wa mmoja wa dada zangu, dada Grace. Alionekana akiwa mdogo na mzuri sana.

Bwana akasema: “HAWA NI WATAKATIFU WANGU.”

Ana amani sana Mbinguni. Watakatifu walioko Mbinguni ni kama malaika. Niliwaona Watakatifu wachanga Mbinguni. Mavazi yao ni tofauti. Mahali ambako Bwana alinionyesha pamejaa maua mazuri. Ni mahali pazuri sana penye harufu nzuri sana. Nilikuwa Mbinguni! Nilipaona Mbinguni! Nilipagusa Mbinguni!

Bwana aliniambia: “Sasa nitakuonyesha yaliko mavazi ya Watakatifu wangu.”

Nikamwuliza Bwana: “Je, utanionyesha vazi langu?”

Bwana akasema: “Nitakuonyesha mavazi ya Watakatifu Wangu.”

Bwana alionyesha baadhi ya mavazi, mavazi meupe ambayo yamepambwa kwa dhahabu. Mavazi hayo yana mikanda ya dhahabu na yote yameandikwa majina juu yake. Bwana alinionyesha pia mavazi mengine. Mavazi haya ni ya baadhi ya watu ambao bado wako duniani ambao bado hawajampokea Bwana wetu Yesu Kristo.

Bwana akaniambia: “Haya ndiyo mavazi ya Watakatifu Wangu na haya ndiyo mavazi ya watu wengine ambao bado wako duniani, ambao bado hawajanipokea mimi.”

Nikasema: “Bwana, nataka kuona mataji. Nataka unionyeshe taji ya Mchungaji wangu, na taji yangu mwenyewe. Bwana, nataka kuona taji yangu.”

Bwana akasema: “Nitakuonyesha.” Bwana alinionyesha mataji hayo, ni mazuri sana. Nitakueleza juu ya taji ya Mchungaji wangu. Nilimwomba Bwana anionyeshe taji yake maana nilitaka kumletea Mchungaji wangu habari njema.

Bwana alinionyesha taji yangu. Taji yangu haikuwa na vito. Haikuwa kama taji zingine ambazo zilinivutia sana kama ile ya Mchungaji wangu.

Nikamwuliza Bwana: “Kwa nini taji yangu haina vito?”

Bwana akasema: “Huwezi kuelewa mambo aliyopitia hadi kufikia kuwa na taji yenye vito vingi kama hii.”

Malaika alichaguliwa kuweka mataji na pia vito kwenye mataji. Watu wanapotubu na kuja kwa Yesu Kristo, unapoleta roho kwenye Ufalme wa Mbinguni, malaika ataweka kito kwenye taji yako. Unapowasaidia wenye shida, malaika ataongeza kito kingine kwenye taji yako. Unapowasaidia maskini na wasio na mahali pa kuishi, malaika ataongeza vito zaidi kwenye taji yako.

Bwana alikuwa anaongea nami kuhusu Mchungaji wangu. Alisema kuwa ameshateseka sana kwa ajili ya Ufalme wa Mungu; na kwamba alipitia magumu mengi hadi kupata taji kama hiyo. Ana moyo sana wa kuleta roho za watu kwa Kristo.

Bwana akasema: “Mwambie ashikilie kwa nguvu kile alicho nacho ili mtu mwingine asije akachukua taji yake.”

Nilimweleza Mchungaji wangu yale yote ambayo Bwana aliniambia.

Halafu Bwana alinionyesha mataji ya Watakatifu Wake wote.
Alinionyesha mataji ya watu ambao hawajayatoa maisha yao kwake lakini bado wako duniani.

NILIONA KITI CHA ENZI CHA MUNGU MBINGUNI

Bwana alisema: “Binti yangu, nitakuonyesha kitu.”

Kutokea mbali, niliona kiti cha enzi kikubwa sana; cha thamani sana.

Bwana akasema: “Hiki ni kiti cha enzi cha Baba yangu.”

Bwana alikuwa amekaa pale. Nuru kali ya kiti cha enzi ilinifanya nisiweze kuona mengi. Niliona baadhi ya wazee wakitupa taji zao chini na kuinama ili kumwabudu Bwana. Hawaachi kumwabudu Bwana Mbinguni.

Niliona malaika wengi sana wakiwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi cha Mungu. Kitabu cha Ufunuo kinaongelea kuhusu sehemu hii. Mbingu ni halisi. Niliona mbingu kwa sababu nilifika pale.

Bwana akasema: “Binti, kaiambie dunia kwamba mbingu ni halisi. Zungumza binti yangu.”

Nikauliza: “Bwana, unadhani wataniamini?”

Bwana akasema: “NDIYO.”

Nilikuwa nazungumza na Bwana kama ambavyo naweza kuzungumza na kaka yangu au na Mchungaji wangu.
Niliona malaika wengi sana Mbinguni; na kila walipomwona Bwana, walivua mataji yao na kuinama na kumwabudu Bwana. Nilijawa na furaha sana kuona mambo haya.

Bwana akasema: “Binti yangu, UTUKUFU WOTE NI MALI YANGU. UTUKUFU WOTE NI WANGU.”

Hapa nilielewa kwamba Mungu hashirikiani utukufu wake na yeyote. Malaika walikuwa wakiimba, wakimwabudu Bwana muda wote. Hawaachi hata kidogo kumwabudu Bwana. Niliona jinsi kanisa lenye wachungaji wazuri linavyomwabudu Bwana. Dada yangu, Yasmine, alikuwa akiwaongoza.

Bwana akasema: “Waambie kwaya ya kanisa la wachungaji wazuri waniabudu Mimi na waache kufanya mambo yasiyonipendeza. Waambie kuwa kila wanaponiabudu, malaika Mbinguni huabudu pamoja nao.”

Ujumbe huu ni kwa wote wanaoabudu. Bwana anataka mmwabudu zaidi.

“Waambie waniabudu Mimi,” Bwana alisema.

Malaika walikuwa wakipiga vyombo mbalimbali katika kumwabudu Bwana.

MUNGU WETU NI BABA MTAKATIFU, AMINA

Malaika ni wazuri sana. Wanapomwabudu Bwana. Niliona amani kubwa sana kati yao. Waliabudu kutoka moyoni.

Bwana alinipeleka sehemu nyingine. Niliwaona malaika saba wameshikilia tarumbeta saba. Na karibu yao, kulikuwa na malaika wengine saba wameshikilia vikombe mikononi mwao. Walikuwa ni malaika wakubwa na warefu sana. Walivaa mavazi meupe sana; weupe ambao hata hauelezeki!

Nikauliza: “Bwana, malaika hawa ni akina nani?”

Bwana akasema: “Malaika hawa wanasubiri kutumwa duniani ili kuiharibu dunia.”

Malaika wale tayari wana tarumbeta mikononi mwao. Wanasubiri tu Bwana awaambie waanze kuzipiga.

Nikauliza: “Bwana, mbona ni warefu hivyo?”

Bwana akasema: “Kwa kuwa wao ni wana wa Mfalme.”

Nilikuwa nimekusudia kuuliza maswali zaidi. Lakini Bwana akaniambia: “Usiwe mdadisi sana. Usiulizeulize maswali mengi mno. Wewe onyesha tu yale ambayo nimekuonyesha; mambo ambayo nimekwambia useme. Waambie kuwa kuna Mbingu moja tu na wala hakuna nyingine. Waambie kuwa Mimi ni halisi, maana watu wengi hawazungumzi kuhusiana na Mimi. Waambie kuwa Mungu yuko pale juu akiwangoja.”

Kisha Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha kile kinachoendelea miongoni mwa watu wangu.”

Bwana alinionyesha sehemu moja. Sehemu ile ilikuwa na pazia. Halafu akasema: “Ona kile kinachoendelea kwenye Kanisa langu. Ndani ya Kanisa langu yapo mambo mengi ambayo hayanipendezi. Nitaleta kwa Baba yangu taifa Takatifu tu. Kanisa langu haliko tayari. Nenda kawaambie wajiweke tayari kwa sababu tarumbeta karibu italia.”

NILIONA MEZA YA BWANA IMESHAANDALIWA TAYARI

Bwana akasema: “Sasa nitakuonyesha mahali ambako Watakatifu wangu watakula pamoja na Mimi.”

Akanionyesha meza kubwa sana, imepambwa vizuri kwa vitambaa vyeupe, vikombe vya dhahabu, huku kukiwa na viti kila mahali, na viti vyote vina majina ya Watakatifu yameandikwa juu yake. Sikuweza kuelewa majina yale. Nilimwomba Bwana anionyeshe kiti changu.

Bwana alinionyesha kiti changu na kusema: “Liambie Kanisa langu lijiandae. Waambie watu wangu kwamba meza imeshaandaliwa.”

Nikasema: “Bwana, hapa ni pazuri sana.” Nilitaka kukaa kwenye kiti kimojawapo.

Bwana akasema: “Usikae kwenye kiti. Bado muda haujafika.”

Kisha niliona malaika wakienda na kurudi, na mmoja wao alikuja na kuzungumza na Bwana moja kwa moja masikioni mwake.

Nikamwuliza Bwana: “Amesema nini?”

Bwana akasema: “Usiwe mdadisi sana.”

Kisha malaika alikuja tena na kuzungumza masikioni mwa Bwana. Bwana akasema: “Binti yangu, muda umeshafika wa wewe kurudi. Kaliambie Kanisa langu wajiandae. Kawaambie kila kitu nilichokuonyesha.”

Nikasema: “Bwana, hapanaaaa! Sitaki kurudi.”

Bwana akasema: “Ndiyo, ni lazima urudi ukawaambie kila kitu ulichoona. Waambie kuwa meza iko tayari, inawangoja. Ni lazima mjiweke tayari.”

Wakati tukiwa tunaondoka, Bwana akasema: “Kanisa langu liko namna hii: baadhi ya watu ni wa nia mbilimbili, baadhi ni wanafiki, wengine hawako tayari, wengine hawanipendi Mimi kwa moyo wote, baadhi wanafanya mambo kwenye nyumba yangu kwa sababu wanalazimika tu kufanya, wengine wanataka waonwe na kusifiwa na wachungaji wao.”
Bwana alianza kulia!

WATOTO WASIO WATII, WANAOPOKEA SIMU WAKIWA KANISANI

Bwana alinionyesha Kanisa. Nilimwona mhubiri akihubiri madhabahuni na ghafla simu yake iliita. Mhubiri huyu aliacha kuhubiri. Alitoka nje ili kwenda kusikiliza simu yake.

Bwana akasema: “Unaona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu; ona jinsi wanavyopuuza uwepo wangu. Mtu anapohubiri, anakuwa anahubiri Neno langu. Wanaona bora kwenda kusikiliza simu kuliko kushughulika na Mimi.”

Kisha Bwana akaniambia: “Sema, sema na Wachungaji waachane na mafundisho yao. Wanaweza kukuchukia kama wakitaka, lakini watu wengi wataelewa makusudi ya Mimi kukuleta hapa na wengi watatubu.”

Ujumbe kwenu wachungaji. Watu wanaweza kuwachukia pale mnapoamua kuyafanya mapenzi ya Mungu. Haijalishi kama watawachukia. Sahauni mafundisho yenu wenyewe. Fuateni kile ambacho Mungu amewapa. Msijaribu kumfurahisha kila mtu. Msikubali kuridhia mambo asiyopenda Mungu.

Bwana akasema: “Nitaenda kuliunganisha Kanisa langu pamoja. Mimi nina Kanisa moja tu. Sina Kanisa jingine duniani zaidi ya Kanisa moja tu. Hili ndilo Kanisa nitakalolipeleka mbinguni. Hili ndilo Kanisa nitakalolikabidhi kwa Baba yangu.”

Sisi tulio wa Huduma ya Kiinjilisti ndio Kanisa la Mungu. Wale ambao wameyatoa maisha yao yote kwa Yesu Kristo. Wale ambao hawatendi dhambi tena. Wale ambao wameziacha njia zao za zamani ili kuyafanya mapenzi ya Mungu. Wale waliozaliwa upya. Hawa ndio watu watakaouona uso wa Mungu.

HITIMISHO

Ushuhuda wangu unakaribia mwishoni. Nimewaeleza kila kitu ambacho Bwana aliniambia niseme, kwa utukufu wa Mungu. Utukufu wote, utukufu wote ni wa Mungu.

Niko hapa kwa rehema za Mungu. Ni kwa rehema za Mungu tu ninawaambia mambo haya ambayo Bwana alinitaka niyaseme. Ujumbe huu utakwenda moyoni mwako na kubadili maisha yako ili kwamba uweze kutubu.

Mwulize Bwana: “Bwana, ni eneo gani la maisha yangu ambako ninashindwa?” Bwana atakujibu.

Napenda kukuambia kwamba Yesu Kristo anakupenda wewe; Yesu Kristo anakupenda wewe! Anataka kuyabadili maisha yako. Yesu Kristo hataki uende jehanamu bali anataka uende Mbinguni. Mbingu ni halisi, na kuzimu nako ni halisi pia. Tubu sasa na uyatoe maisha yako kwa Yesu Kristo. Wokovu unapatikana kwa Yesu Kristo tu!

Yesu Kristo anagonga kwenye mlango wa moyo wako kupitia ujumbe huu. Mtafute Bwana kwa moyo wako wote, naye atafanya mambo makubwa kupitia wewe.

Bwana akasema: “Mambo yote haya niliyokuonyesha yalishatabiriwa kwenye Kitabu cha Ezekieli, Kitabu cha Danieli na Kitabu cha Ufunuo. Mafunuo yote haya yamo kwenye Biblia.”

Ninaomba kwamba ushuhuda huu ukabadilishe maisha yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu. AMINA.

MUNGU awabariki nyote.

**********

Ushuhuda huu nimeutafsiri kutoka kwenye toleo lake la Kiingereza ambalo linaweza kupatikana kwa kubofya kwenye kiungo kifuatacho: Holiness Required for Heaven - Adelaida De Carrillo

JF-Expert Member
May 12, 2014
#3
nimeisoma yote na nimeilewa,kuna kazi kubwa sana

Imeandikwa Njia ile ni nyembamba,iendayo uzimani !!


Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?
 
barikiwa sana mtumishi kwa uzi huu, naamini wapo waliokusudiwa kupata ujumbe huu lkn na wao pia watapuuza😔😔
 
Duuuuh inasikitisha sana hao wa bolivia 🇧🇴
Ingawa sijasoma kabisa
 
Yesu Ni Njia
Sunday, October 14, 2012
Nilihisi kama Mungu Amenisaliti!




Utangulizi kutoka kwa blogger

Je, unahisi kuwa una huzuni kubwa isiyoweza kuondoka, umekata tama, unajiona huna maana, unahisi kama vile Mungu amekudanganya au amekuacha; unahisi kama vile Mungu si wa kuaminiwa au Neno lake si la kuaminiwa, unahisi kuwa Mungu hasikii maombi yako, hakupendi; unahisi kwamba umeshapoteza wokovu wako, au unahisi kuwa umetenda sana dhambi kiasi kwamba Mungu hawezi kukusamehe tena?

Napenda nikuletee habari njema kwamba, bado liko tumaini, tena kubwa sana kwa ajili yako. Karibu usome ushuhuda huu ambao, si tu ni ushuhuda wa mpendwa aliyepita kwenye mapito kama hayo, lakini pia ni somo zuri mno kiasi kwamba, kama kawaida, Mungu anayo mengi ya kutufundisha kupitia mambo ambayo wengine walipitia kama sisi na wakashinda kwa neema ya Mungu ambayo iko kwa ajili ya kila mwanadamu, ukiwamo na wewe. Pendo la Mungu ni zaidi ya maji ya bahari, hivyo hakika kabisa unayo sehemu yako humo ambayo inakungoja uingie na kupokea.


Tatizo la wengi wetu ni ukosefu tu wa maarifa; tumempa shetani nafasi kubwa mioyoni mwetu – bila ya sisi kujua – kiasi kwamba amevuruga kabisa akilini na mawazo yetu; ametujaza giza lake la kuzimu na kutufanya tuhisi wakati wote kuwa wokovu ni mgumu sana na kwamba sheria ya Mungu ni ngumu mno.

Usikubali tena kudanganywa na ibilisi. Simama kwenye nafasi yako. Roho Mtakatifu yuko tayari saa 24 kutuchukua taratibu ila kwa uhakika hadi kwenye mwisho wenye ushindi USIO NA SHAKA HATA KIDOGO! Inua uso wako sasa uanze kusonga mbele kwa nguvu za Baba yetu wa mbinguni ambazo zimewekwa tayari kutuvusha kila bonde la uovu na mauti!

***********************

Ujumbe wa mhariri wa makala haya kwa Kiingereza:
Tumeona ni vema kutotaja jina la mwandishi wa ushuhuda huu kwa sababu za usalama wake.

Kama umewahi kuhisi kana kwamba Mungu amekusaliti, au tu ungependa kufahamu zaidi kuhusu ulimwengu wa giza na jinsi unavyoathiri Wakristo, tunapendekeza sana usome ushuhuda huu. Mwandishi wa ushuhuda huu si tu kwamba amepitia kile ambacho alikiona kama ni kusalitiwa na Mungu, bali pia alijifunza mambo machungu ... ambayo tunaamini yatawanufaisha wengi ambao nao wanahisi wako kwenye hali ambayo wanafikiri kuwa ni bora kuachana na Mungu.

*****************

Ushuhuda wenyewe
Niliingia kwenye Ukristo nilipofikisha miaka 18. Nilizaliwa kusini mwa Urusi. Nilimpenda sana Yesu, na nikawa na bidii sana Kanisani, nikabatizwa kwa Roho Mtakatifu na nikawa nawashuhudia watu Injili. Mungu amenibariki sana.

Mungu aliponibatiza kwa Roho Mtakatifu nilipata shauku kubwa sana ya kuwashuhudia watu habari za Yesu. Nilikuwa nikiongea Habari Njema za Yesu karibu kila siku. Nilijihisi niko karibu sana na Mungu. Nilitumia saa nyingi kuomba na kusoma Biblia.

Wakati fulani nilipatwa na jinamizi. Niliota kuwa ibilisi ananifukuza. Aliapa kuwa ni lazima atanipata. Nilipozinduka usiku ule, hofu haikuondoka. Badala yake ilizidi kuongezeka. Hofu iliongezeka sana kiasi kwamba nikawa nimechanganyikiwa kabisa. Nilijua kuwa niko katikati ya uovu. Nilikuwa chumbani kwangu, lakini ilionekana kana kwamba niko mahali pengine kabisa. Nilianza kuhangaika kuomba na kumsifu Mungu. Hili lilikuwa ni jambo pekee lililonifanya nibakie na akili zangu timamu. Niliomba karibia usiku kucha. Ile hali ya uovu ilikuja kuondoka asubuhi.

Nilipomsimulia jambo lile mmoja wa wamisionari wa Kimarekani kanisani kwangu, aliniambia kuwa ibilisi amefungwa na kuwa hana uwezo wa kumdhuru Mkristo yeyote. Nilikuwa sijawahi kufundishwa chochote kuhusiana na vita vya kiroho na sikujua kuwa nilitakiwa kufanya kitu ili kumpinga adui. Nimekuja kujifunza ukweli huo kwa njia ngumu kabisa. Ni miaka mitatu baadaye ndipo nilipofahamu kuwa ibilisi yu hai na yuko duniani; na anachukia sana na kushindana na kila mmoja anayeamua kuyatoa maisha yake kwa Yesu Kristo.

Muda mfupi baada ya kupata ubatizo wa Roho Mtakatifu, kwa ndani moyoni, nilianza kujiona kuwa mimi nilikuwa mtu maalum sana kwa Mungu kuliko Mkristo mwingine yeyote au watu wengine. Nilianza kuhisi hivyo kwa sababu ya baraka zote za kimwili na kiroho alizonipa Mungu. Kazi yangu ya ukufunzi ilikuwa inakua kule Urusi; nilipokea fedha kwa ajili ya kusafiri ng’ambo, na zaidi ya hapo, nilipewa skolashipu kamili ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Columbia kule New York.

Siku moja wakati nikiomba, Mungu aliniambia kuwa ninatakiwa kutubu. Mungu alinionya kuhusiana na majivuno yangu na kuniambia nitubu, vinginevyo NINGEANGUKA. Alisema kuwa mimi sikuwa mtu maalum kuliko mtu mwingine yeyote. Pia aliniambia niache kuwahukumu wengine. Kwa bahati mbaya, mimi nilikuwa nimesisimka zaidi kutokana na ukweli kwamba Mungu anasema nami badala ya ukweli kwamba nilitakiwa kumtii na kufanya kile anachoniambia.

Kuishi katika jiji la New York...

Miaka minne iliyopita, toka tarehe ya kuandikwa kwa ushuhuda huu, nilienda New York ili kusomea shahada ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Columbia. Nikiwa New York, mambo hayakwenda kama nilivyokuwa nimetarajia. Nilikuwa na vita vikubwa na sikuelewa kwa nini Mungu aliruhusu nipitie mateso kiasi hicho. Japokuwa Mungu alinibariki sana kwa skolashipu kamili kwenda kusomea Columbia, sikumwamini na wala sikumshukuru wakati wa mapito yangu magumu. Badala yake, nilipachukia New York na Columbia na nikaanza kunung’unika na kulalamika sana.

Huu ulikuwa ndio mwanzo wa kuanguka kwangu. Niliingiwa na huzuni kubwa sana na nikawa katika maumivu na hofu kubwa. Nilifunga, nikaomba mara kwa mara, nikasoma Biblia, nikaenda kanisani, lakini maumivu na hofu ile havikuondoka! Hali ile ilikuwa inatia uchungu moyo wangu kiasi kwamba ikawa ni vigumu kwangu kutembea au kuzungumza. Kila dakika ilihitaji nguvu sana. Ilikuwa ni kama vile mtu ananivuta chini na kunizuia kupiga hatua. Muda wote nilikuwa nanyanyaswa na ibilisi ambaye alikuwa akiniambia kuwa mimi nimeshashindwa kabisa.

Baada ya mwaka mzima wa mateso yangu, Mungu alinivuta tena kwake kwa muda mfupi. Alizungumza nami na nikaandika maneno yake kwenye kitabu changu cha kumbukumbu. Ni kwa miaka miwili tu ndio nilielewa kile alichokuwa ameniambia. Mungu aliniambia kuwa nitapitia majaribu makali sana na kwamba ningeteseka sana, lakini aliahidi kunivusha katika yote hayo na kuleta mabadiliko yenye matunda mema ndani yangu.

Wakati nilipokuwa naisikia sauti ya Mungu, nilikuwa naweza pia kusikia sauti za mapepo. Nilikuwa sijui kabisa kwamba mapepo yanaweza kuiga sauti ya Mungu ili kuwadanganya Wakristo. Sikujua kuwa natakiwa kulijaribu kila neno kwa njia ya Biblia. Ndiyo maana, niliposikia kuwa ningeenda kufanya mafunzo ya vitendo kwenye Benki ya Dunia na kwamba ningekutana na mume wangu wa baadaye kule D.C, niliamini kuwa hayo yanatoka kwa Mungu. Kumbe pepo alikuwa anasema na tamaa zangu za kimwili. Niliyapenda maneno hayo na nikayaamini. Nilikuwa na mashaka, lakini pia nilidhani kwamba Mungu hawezi kuruhusu pepo anidanganye.

Muda mfupi baada ya hapo, rafiki yangu pekee Mkristo wa New York aliondoka kwenda kwenye mapumziko ya majira ya joto. Nilibakia peke yangu. Japokuwa nilikuwa nimeshakaa kwenye jiji hilo kwa mwaka mzima, bado sikuwa na marafiki wa Kikristo. Nilihudhuria kanisani, lakini sikuwa namfahamu yeyote pale.

Nilijawa na huzuni zaidi. Nilikuwa peke yangu kabisa na sikuwa na mtu wa kumshirikisha mashindano yangu. Nilidhani kuwa Mungu alikuwa hajali na hakunipenda tena kwa kuwa hakujibu maombi yangu ya kupata kanisa na kuwa na marafiki wa Kikristo. Niliishiwa na nguvu kabisa pale niliposhindwa kwenye usaili kwenye Benki ya Dunia na kukosa kazi. Sikuelewa kwa nini Mungu aliruhusu pepo anidanganye. Sikuwa na hamu ya kuishi tena na nikaanza kuwaza juu ya kujiua! Sikuweza kabisa kustahimili maumivu yangu yasiyokoma.

Kisha nilitambua kuwa nisingeweza kufa kwa sababu nikijiua ningeenda jehanamu na kutumbukia kwenye mateso makubwa zaidi, tena ya milele! Nikajiona kama mtu aliyenaswa. Kuishi sitaki lakini wakati huohuo kujiua nako siwezi. Nilijihisi kama vile niko jehanamu. Maumivu yalikuwa makali sana kiasi kwamba nilianza kujikata kwa kisu, maana maumivu ya kimwili yalionekana kwangu kuwa ni mepesi kuliko mateso ya moyoni mwangu. Uovu ulikuwa wakati wote umenizunguka, ukipenya ubongo wangu, ukinitesa moyo wangu, wakati wote ukiwa tayari kusema nami na kuniburuta chini! Kadiri nilivyozidi kuomba na kusoma Biblia, ndivyo nilivyozidi kuteswa na hizo sauti, na ndivyo maumivu yalivyozidi. Sikujua cha kufanya na sikuwa na jinsi ya kuzuia!

Ndipo nilifanya jambo ambalo si la kawaida. Sikuwa na uwezo wa kustahimili maumivu zaidi ya hapo, hivyo nikawa nimeanguka kabisa. Nilijawa na hasira sana dhidi ya Mungu kiasi kwamba nikamwambia aondoke kwangu na aachane nami! Nilimwambia kuwa simpendi na sikuwa tayari kuzungumza naye tena wala kuwa naye. Kwa kuwa nilikuwa ni mtu wa kuzungumza naye kila wakati, ilibidi nijilazimishe sana kuacha kumfikiria. Niliacha kuomba na kusoma Biblia. Nikaamua kufuata njia zangu mwenyewe. Sikuwa najua sawasawa madhara ya hatua yangu hiyo. Sikujua kuwa nilimwacha Mungu na kumfuata ibilisi. Sikutambua kuwa mtu huwa ama yuko anamtumikia Mungu au anamtumikia shetani – hakuna namna ya kusema ‘mimi siko kwa Mungu wala kwa shetani.’ Ukiwa kwa Mungu unakuwa hauko kwa shetani. Ukiwa nje ya Mungu, moja kwa moja unakuwa uko kwa shetani. Hakuna sehemu ya kati!

Hivi sasa ninatambua kwamba Mungu alikuwa muda wote ananiangalia licha ya maamuzi yangu yote mabaya.

Katikati ya majira ya joto, nilipata kanisa na kuwa na marafiki kadhaa. Hatimaye sasa nilikuwa na mtu wa kuzungumza naye na angalau kutoka naye. New York ni sehemu ngumu sana kwa Wakristo. Pia, hivi sasa ninatambua kuwa kumbe hata marafiki zangu pale kanisani nao walikuwa wanapitia magumu mengi vilevile kama mimi! Hata hivyo, kuwa wewe na kuombeana na kumtazama Yesu yalikuwa ni mambo ambayo tulikuwa hatufanyi. Kutafuta mafanikio ya kazi lilikuwa ndilo jambo tulilolipa umuhimu zaidi.

Jumapili moja nilikutana na mwanamume mmoja kanisani. Mara moja nilivutiwa naye. Ninapotafakari sasa ... natambua kuwa mara nilipoondoa macho yangu kwa Yesu, nilifanyika mtu rahisi sana kushambuliwa na shetani. Hilo lilimpa nguvu juu yangu na kudhibiti hisia zangu na mawazo yangu. Na kwa kuwa sikuwa na upendo kwa Mungu moyoni mwangu, nilihitaji kitu mbadala. Nikawa nimevutika kabisa kwa huyu mwanamume.

Pale nilipokuja kutambua kuwa uhusiano wangu naye hauwezi kufika mbali, nilianza kumwomba Mungu na kusoma Biblia. Hata hivyo, bado nikawa sikumwomba Mungu awe Bwana wa maisha yangu tena. Nilitaka tu anisaidie kwenye matatizo yangu niliyojisababishia mwenyewe. Kwa kule kutoyatoa maisha yangu yote kwa Mungu, sikuwa na uwezo kabisa wa kuvunja ule uhusiano. Sikujua wakati ule kwa nini sikuweza kumkatalia yule bwana kunitumia mimi, na kumwambia ‘hapana’. Nilikuwa nimenaswa kwenye hisia zangu mwenyewe na sikuwa na uwezo wa kutoka humo. Nilijua kwa moyo wangu wote kuwa nilikuwa namtenda Mungu dhambi.

Nilibakia nikiwa nimenaswa kwenye uhusiano huu kwa mwaka mzima. Kwa kuwa huyu bwana hakuwa msomaji wa Biblia na hakupenda kuzungumza kuhusu Mungu, mimi nami pia niliamua kuacha kuyafanya hayo. Kwa hiyo, nikawa nimeenda mbali zaidi na Mungu na hatimaye nikawa nimekuwa mwenyewe tu.

Baada ya mahafali yangu ya chuo, nilifanya kazi New York katika kipindi cha majira ya joto. Nilipata kazi kwenye benki yenye hadhi na nilikuwa na uwezo sana kwenye kazi yangu. Bosi wangu aliniambia jinsi ambavyo alipenda kazi yangu na jinsi nilivyokuwa bora na mwenye akili. Nilijawa na majivuno na kiburi hata zaidi.

Baada ya uhusiano wangu na yule bwana kuvunjika, nilijihisi kuwa ninataka kugeukia kwenye kitu kingine ili kujaza uwazi uliotokea. Bado nilikuwa najiona kuwa simhitaji Mungu. Nilikuwa bado nina hasira naye kutokana na kutonipatia kile nilichohitaji. Ndipo kazi yangu ikawa ndiyo mungu wangu. Nilimuabudu huyu mungu wangu kwa bidii zote.

Kuishi Moscow…

Nilipoenda Moscow, nilipanga kufanya usaili na mabenki kumi makubwa ya nje. Cha kushangaza, mambo yaligoma kabisa! Sikuweza popote kupata kazi niliyoitaka! Najua sasa kuwa, sababu mojawapo ya mimi kushindwa kwenye kila usaili ilikuwa ni tabia yangu ya majivuno ambayo ilionekana kunisaidia sana wakati nikiwa New York, lakini hakuna mtu aliyehitaji kiburi hiki kule Moscow.

Niliishia kupata kazi ambayo niliichukia kabisa. Hata hivyo, ilibidi niiache baada tu ya miezi mitatu. Niliweza kupata kazi nyingine Moscow. Nilipoambiwa niache kazi yangu ya pili, kwa vile sikuwa nafaa kabisa kwenye kazi hiyo, na pale nilipokataliwa kwenye kila usaili niliofanya kule London, nilitambua kuwa Mungu alikuwa anajaribu kila njia kunifanya nishtuke.

Nilipoteza kazi yangu Aprili (2004). Nilifanya usaili mara kadhaa, lakini kazi sikupata. Kila jitihada ilikuwa haizai matunda kwangu! Hatimaye Mungu alifanikiwa kuvuta umakini wangu. Nikaanza kumwomba. Hata hivyo, nilijihisi kuwa hata nikitubu vipi, siwezi kusamehewa. Nilipakua Biblia kutoka kwenye intaneti maana nilishatupilia mbali Biblia zangu zote pale nilipoondoka New York. Nikaanza kusoma Agano Jipya tena.

Siku moja, nilipojua kuwa usaili wangu wote umekwama, nilimlilia Mungu ili anisaidie. Nilijiona sina tena matumaini kabisa.

Ndipo nilianza tena kusikia sauti ya ibilisi ikiniambia kuwa Mungu hanipendi na hatanisamehe; na kwamba inabidi nijitupe kupitia dirishani. Sauti ile ilikuwa ina ushawishi mkubwa na nguvu sana kiasi kwamba nilidhani kuwa nitakuwa kichaa. Huku nikilia, nilifungua Biblia na kuanza kusoma kwa sauti japokuwa nilikuwa sielewi hata neno moja. Lakini sauti ile ikawa imetoweka!

Nilitambua kuwa nilikuwa nimemtenda dhambi Mungu sana na nilihitaji kujua iwapo angenisamehe. Nikakumbuka hadithi za kwenye Agano la Kale kuhusu Israeli – wafalme waliomtenda dhambi Mungu, lakini wakatubu. Nikaanza kusoma hadithi zile. Nikatambua kuwa majivuno yangu na kutotii zilikuwa ndizo dhambi zangu kubwa mbili.

Katika kipindi cha kurudi kwangu kwa Mungu nilikutana na tovuti yenye Shuhuda za Thamani. (www.precious-testimonies.com). Nilisoma shuhuda karibu zote humo! Niliguswa sana na upendo wa Mungu kwenye maisha ya watu mbalimbali. Niliguswa sana na mateso na maumivu ambayo kila mmoja aliyapitia hadi kuja kumpata Yesu Kristo. Lengo langu, nilikuwa nataka sana kujua kama Mungu angeweza kunisamehe dhambi zangu.

Kupitia kwenye Biblia, na shuhuda zile, nilitambua kuwa sikuwa nimempa Yesu maisha yangu yote na kwamba nilikuwa bado nimeshikilia mambo yale niliyoyapenda na nilikuwa naogopa kuyaachia na kumpatia Yesu. Pia nilitambua jinsi ambavyo dhambi zangu zilimpatia shetani nguvu kubwa ya kuharibu maisha yangu. Nilijifunza jinsi ilivyo kutembea kwenye njia ya ibilisi. Sitaki ubinafsi tena! Nilitaka kumtumikia Yesu japokuwa isingekuwa rahisi na wakati mwingine ingekuwa vigumu sana. Lakini Yesu hutoa uzima wa kweli na anajua kile kinachofaa kwa ajili yetu.

Mungu alikuwa na rehema na neema sana kwangu na Roho Mtakatifu wake aliniongoza kwenye toba. Alihukumu majivuno yangu na kukosa kwangu utii na uzinzi wangu. Tarehe 12 Juni, 2004, nilimpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yangu yote – si kwa sehemu yake tu! Nilimwambia achukue ndoto na mapenzi yangu yote ya ubinafsi na aweke ndani yangu ndoto na mapenzi yake. Nilimkabidhi hofu zangu zote. Nilimwambia kuwa sikutaka tena kumtumikia shetani bali nataka kumtumikia Yeye – Yesu. Maamuzi yangu yote ya nyuma yalinipeleka kwenye kushindwa kabisa. Nilitaka sasa Yesu atawale maisha yangu na kuyabadili apendavyo, na si vile ninavyotaka mimi.

Baada ya kufanya hivyo, nilijisikia faraja kubwa sana! Kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, nilikuwa natembea barabarani huku nikitabasamu na kupumua kwa uhuru tena. Nilijisikia mwepesi na huru kabisa.

Nilikuwa nimeishi Moscow kwa karibu mwaka mzima, lakini nilikuwa sina rafiki Mkristo hata mmoja. Kabla ya toba yangu, nilihudhuria kanisa jingine lakini bado nilikuwa simfahamu hata mtu mmoja. Kutokana na tabia yangu ya New York ya kutojiweka wazi, nilikuta ni vigumu sana kuweka wazi mambo yangu ya moyoni kwa watu wengine. Hii ndiyo sababu hakuna aliyejua kile nilichokuwa napitia; na pia ndiyo sababu sikuwa na mtu wa kumweleza kuhusu mapito yangu.

Baada ya uamuzi wangu huo, nilidhani kuwa ningeweza kurudi kwa Mungu kwa nguvu za maombi yangu, toba na kusoma Biblia mwenyewe. Lakini siku chache baada ya kuamua kumrudia Mungu, nilihisi kama kuzimu yote imesimama kinyume nami! Nilianza kuona kiumbe mwenye manywele mengi. Taswira hii ilikuwa mbele za macho yangu muda wote kwa wiki kadhaa. Nilikuwa ninaomba na kuomba na kusoma Biblia. Nilifunga pia. Nilikiri damu ya Yesu juu yangu. Taswira hii mbaya wala haikuondoka! Nilihisi kuwa ninachanganyikiwa. Usiku haikuwa rahisi kulala. Sauti ilianza kuniambia tena kuwa Mungu hatanisamehe kwa kuwa nimemkufuru Roho Mtakatifu na kutenda dhambi ambayo Yesu hawezi kusamehe.

Siku moja niliamka nikiwa na uchungu na hasira. Nilihisi ule mzigo na uzito tena. Nikaanza kumwomba Mungu anisamehe na kumshukuru Yesu kwa kunifia. Lakini mashindano yangu yakaendelea kuwa magumu zaidi na zaidi. Siku ile nilitambua kuwa siwezi kushindana na ibilisi peke yangu. Nilihitaji msaada. Nilihitaji sana mtu wa kuniombea.

Kweli imeshafunuliwa …

Pale nilipotambua kuwa nahitaji mtu wa kuniombea, niliamua kupeleka mahitaji yangu ya maombi kwa watumishi wa tovuti ya Precious Testimonies. Watumishi hao si tu kwamba waliniombea, bali pia walinipatia mwongozo muhimu sana kwa njia ya baruapepe. Ilikuwa ni wao ndio walionifungua macho kuhusiana na ukweli kwamba ibilisi yu hai na yuko duniani huku akifanya vita dhidi ya Wakristo. Nilitambua kuwa yalikuwa ni mapepo ndiyo yaliyokuwa yananiletea maumivu na mateso makubwa namna hiyo. Nimejifunza pia kuwa ibilisi anawapepeta Wakristo wote kama ngano. Adui aliwashambulia na kuwatesa Petro na Paulo na mitume wengine. Anafanya hivyo hata leo kwa nguvu na ukali uleule!

Ulimwengu wa roho…

Nilipokuwa ninakandamizwa na adui mara baada ya kutubu kwangu, Mungu alinifungua macho ili niweze kuona ulimwengu wa roho. Kama nilivyosema, nilidhani kuwa ninachanganyikiwa pale nilipoona kiumbe mwenye manywele mengi. Baada ya kutuma mahitaji yangu ya maombi, nilijisikia amani kubwa. Nilijua kuwa kuna mtu ameanza kuniombea.

Hata hivyo, niliendelea kuyaona mapepo yakinizunguka. Nilipoamka siku iliyofuata, si tu kwamba niliweza kuyaona mapepo, bali pia nilimwona malaika wangu. Taswira zilikuwa kama kioo. Nilikuwa sina hofu hata kidogo. Niliweza kuona kwenye ulimwengu wa roho kwa wiki kadhaa. Mungu alinifundisha masomo muhimu sana katika kipindi hicho.

Somo la 1: Mapepo hayawezi kustahimili kusikia Neno la Mungu.

Wakati fulani nilirudi nyumbani kutokea kanisani na nikawa nasoma Maandiko. Niliinua macho na kuyaona mapepo kadhaa. Nikaanza kumwomba Mungu anisaidie. Sikuwa nina hofu lakini nilikuwa tu sijisikii amani kuyaona. Wakati nikiwa namwomba Mungu anisaidie, nilisikia sauti moyoni mwangu ikisema, “Soma Maandiko.”

Nikauliza: “Nini?” Sauti ile ikarudia tena: “Soma Maandiko.” Nilitii na nikaanza kusoma Maandiko. Lakini baada ya muda kidogo, Mungu akaniambia: “Soma kwa sauti.” Nikawa kama nimechanganyikiwa kidogo, lakini Mungu akarudia tena: “Soma Maandiko kwa sauti.” Nilipoanza kusoma Maandiko kwa sauti niliona kuwa mapepo yale yanafunika masikio yao kwa mikono yao yenye makucha na kuanza kuhangaika kwa mateso makubwa. Hivi ndivyo nilivyojifunza kuwa mapepo hayawezi kustahimili kusikia Neno la Mungu. Neno la Mungu likitumika kwa imani na kweli, ni silaha kubwa dhidi ya nguvu za giza.

Tangu hapo, nimejenga tabia ya kusoma Neno la Mungu kwa sauti. Pia nimepakua kutoka kwenye intaneti Agano Jipya la sauti (lililo katika fomati ya MP3). Nikiwa nyumbani, karibu muda wote huwa nimefungulia Biblia hiyo. Huwa naisikiliza nikiwa nakula, napika, najipamba, nk. Mara kadhaa Mungu amekuwa akielekeza umakini wangu kwenye mistari ya muhimu sana na kunieleza maana yake wakati nikiwa nakula au najiandaa kwenda kazini. Mwenzangu mmoja aliniuliza ni rekodi ya aina gani hii ambayo huwa naisikiliza karibu saa 24 kila siku. Nilimweleza na kumshirikisha sababu zangu za kufanya hivyo, lakini najua kuwa hakunielewa kikamilifu.

Vilevile nilipakua Agano Jipya kwa ajili ya kompyuta yangu ya mfukoni. Kila ninapopata nafasi, huwa najaribu kusikiliza Maandiko niwapo kazini. Mara nyingi ninapopatwa na mashambulizi ya adui nikiwa kazini, huwa naamua kusikiliza Biblia hiyo kama njia yangu mojawapo ya kunisaidi kushinda vita.

Pia nilijifuza kwamba mapepo huteswa sana hasa na Kitabu cha Ufunuo, na hususani sura ya 17, 18, 19, pale ambapo Maandiko yanazungumzia kuhusu hatima yao ya mwisho. Hayawezi kabisa kusikiliza mistari kuhusu Babeli ulioanguka na mistari kuhusu ibilisi na manabii wake wa uongo kutupwa kwenye ziwa la moto.

Kuna mara kadhaa ambapo niliyatishia mapepo kuyasomea Kitabu cha Ufunuo kama hayakuacha kunisumbua au kuondoka. Ni wazi kuwa sikuyatishia tu, bali nilisoma sehemu hizo. Mbinu hii hata hivyo si kwamba ndiyo jibu la kila kitu. Haikuhakikishii ushindi kwenye kila shambulizi, lakini ni mbinu nzuri ya msaada upande wetu. Mungu mara zote hunisaidia kupata mstari ambao unaweza kunyamazisha kabisa sauti ya adui. Nimeshajifunza kuwa si kila mstari utanyamazisha manyanyaso ya adui bali ni ile mistari ambayo inahusiana moja kwa moja na tatizo lililopo. Ni kama ilivyo kuinua upanga hewani na kupiga kushoto wakati adui yuko kulia. Hiyo haisaidii kumshinda adui. Ni pale tu unapoelekeza mapigo yako kwenye lengo ndipo utashinda mapambano. Hali ni ileile hata kwenye mistari ya Biblia na uongo na unyanyasaji wa adui. Ndiyo maana NI LAZIMA kujifunza Maandiko kwa bidii na kuweka mistari kwenye kumbukumbu kichwani.

Katika majaribu ya Yesu ya siku 40 kule jangwani – pale shetani alipomjaribu – je, Yesu alifanya nini? Alimjibu shetani kwa kutumia mistari sahihi kutoka kwenye Neno la Mungu. Alishindana na shetani kwa kutumia upanga wa Roho Mtakatifu, ambao ni Neno la Mungu. Shetani anamnukulia Yesu Neno lakini si kikamilifu; anataja nusu ukweli. Ukweli nusu mara zote huwa ni uongo uliokusudiwa kudanganya wanadamu na kupoteza makusudi ya Mungu kwa ajili ya wanadamu. Yesu alimnukulia shetani Kweli yote kwa 100% ... na shetani hakuwa na kitu chochote cha kushindana na mbinu ya mapambano ya Yesu. Shetani alishindwa kwa 100% kwenye vita hivyo. Mungu hakuruhusu jambo hili liandikwe kwenye Biblia kwa bahati tu ili kujaza nafasi. Shindana na mashambulizi ya mapepo kwa kutumia kwa usahihi Neno la Mungu.

Lijue Neno ... Liamini Neno ... Fahamu lini pa kulitumia kwa usahihi (usinukuu tu Neno nje ya uhalisia wa hali yako; mapepo watakucheka!); kisha tamka Neno la Mungu kwa sauti, imba nyimbo zinazotokana na Maandiko; omba Neno wakati wa maombi yako na kuyaambia mapepo yanayokuzunguka, (japo huenda hutakaa uyaone) – sikiliza Neno la Mungu linapoongelewa dhidi ya matatizo yanayokukabili, lakini kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Mambo yote yanaweza kushindwa lakini haiwezekani kwa Neno la Mungu kushindwa maana Roho Mtakatifu ndiye anayelifanya litende kazi. Mungu hawezi kusema uongo; hivyo Neno la Mungu nalo haliwezi kuongopa. Wanadamu hapa duniani wanaweza wasilielewe Neno la Mungu, hivyo wakalitumia kimakosa katika hali zao, lakini hilo haliwezi kutokea kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hilo kila mara hutokea kwa sababu ya nguvu za kipepo na mawazo ya kimwili ya wanadamu ambao hawana ufunuo kamili wa Neno la Mungu, au huenda wamelipindisha bila wao kujua, na kulifanya liseme kitu ambacho Mungu hajasema. Kama Mungu alivyoandika: "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” (Tazama: Mt. 24:35; Mk 13:31; Lk 21:33). Mtu anapopokea ufunuo kamili kwamba Yesu Kristo ndiye Neno, haishangazi basi kwamba halitapita kamwe.

Somo la 2: Mapepo hujaribu muda wote kuingiza mawazo maovu/ya udanganyifu kwenye akili yako.

Mara nyingi mapepo wanaficha sana udanganyifu wao kiasi kwamba ni vigumu kutofautisha kati ya sauti na mawazo yao na yako. Hivyo, kulisha ufahamu wako kwa Neno la Mungu kila wakati, kuomba na kuwa mwangalifu ni mambo ya muhimu ili kuweza kutofautisha kati ya mawazo yako na uongo wa adui.

Nilipojua ukweli juu ya hasira kali ya ibilisi na mapepo, nilianza kutambua mengi ya mashambulizi yao yaliyofichika, hususani mashambulizi ya kutaka kunishawishi nikubali uongo wao. Nimegundua kuwa mambo mengi yanayokuja kwenye ufahamu wangu hayatoki kwangu au kwa Roho Mtakatifu, bali ni kutoka kwa mapepo.

Ukweli kwamba niliweza kuona jinsi ambavyo mapepo yanafanya kazi kunizunguka mimi, kumenisaidia sana kutambua mashambulizi yao na kupambana nao. Ni muhimu kabisa kutambua mashambulizi yao mara tu yanapoanza na kutoyaruhusu kukamata akili yako. Jambo la kwanza yanachofanya ni kupenyeza uongo kwenye akili zetu. Kama uongo wowote ukikubaliwa na akili zetu, ni vigumu sana kuja kuutambua baadaye na kupambana na mapepo. Si ajabu basi Maandiko yanatuonya mara , yakitutaka kuwa macho kila wakati, kuzifunga nia zetu, kukesha, kutofuatisha namna ya dunia hii bali kufanywa upya nia zetu (kufanywa upya kwa Neno la Mungu).

Nimejifunza kuwa kudhibiti akili zangu ni jambo la lazima. Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo [Neno lake] (Tazama 2 Kor. 10:4-5). Ni mashindano yasiyokoma kwangu kufanya kila wazo limtii Kristo na kuharibu kila kitu ambacho mapepo yanajaribu kukiinua akilini mwangu kinyume na elimu ya Kristo.

Ninakumbuka shambulizi moja ambapo akili yangu ilishambuliwa kwa nguvu sana na adui na ilinibidi nisome Maandiko kwa sauti mfululizo kwa saa kadhaa.


Mapepo yanaposhambulia akili, nimekuta pia kuwa kuna nguvu sana ninapoyajulisha kuwa nimeshajua kwamba yananishambulia. Kwa kuwa menyewe hupenda kutenda kazi zao kwa kificho na hayapendi kuwekwa wazi, njia mojawapo yenye nguvu ya kupambana nayo ni kuyafanya yajue kuwa umeyatambua.

Nakumbuka pia mapambano fulani ambapo nilijihisi kuwa siwezi kabisa kuzuia manyanyaso ya adui. Mapepo yaliendelea kunikumbusha jinsi ambavyo niliudhiwa na kuaibishwa kazini. Yalikuwa yakiingiza akilini mwangu kila aina ya uongo yakitaka kunifanya niwachukie wafanyakazi wenzangu na kumwasi Mungu. Nilijaribu kila njia iliyokuwa ikiwashinda hapo kabla kwenye mashambulizi mengine, lakini haikuwezekana. Yalikuwa ni mashambulizi mfululizo ambayo sikuweza kupata namna ya kushinda. Kisha asubuhi moja, mapepo yalipofanya mashambulizi yao kama kawaida, Mungu alinifundisha mbinu yenye nguvu. Niliyaambia mapepo kwamba, kila mara yatakaponikumbusha jambo linalohusu kunyanyaswa kwangu na wafanyakazi wenzangu, basi mimi nitawaombea, nitayafunga mapepo yanayowadhibiti na nitamwomba Mungu awaimarishe malaika wa vita ambao wanapigana kinyume na mapepo yale. Kweli kabisa baada ya kuhakikisha kuwa nilikuwa sitanii juu ya kuwaombea wafanyakazi wenzangu, mara moja mapepo yaliondoka na nikawa nimeshinda vita ile. Ni wazi kuwa hata sasa bado naendelea kuwaombea wafanyakazi wenzangu kila ninapokuwa kwenye maombi.

Somo la 3: Mapepo yanaathiri hisia zako ili kukudanganya.

(Angalizo muhimu: Kabla ya kuendelea na Somo la 3, napenda nikutahadharishe kabla kuwa somo ambalo Mungu amenifundisha juu ya hisia ni gumu kuelewa kinadharia bila mtu kupitia mwenyewe kile nitakachosema. Napenda kusisitiza pia kwamba sisemi kuwa mawazo yote mabaya yanatoka kwa mapepo. Pia, sisemi kuwa ni lazima wakati wote tujisikie vizuri na tujisikie kuinuliwa. Sisi binadamu ni viumbe wa hisia sana na tunaathiriwa na hali ngumu na matokeo yake tunapata hisia za aina mbalimbali.

Hata hivyo, kuna nyakati ambapo hisia zetu hasi zinakuja kutoka kwa mapepo moja kwa moja. Ni lazima wakati wote tutafute mwongozo wa Mungu na kumwomba atufundishe jinsi ya kutofautisha kati ya hisia zinazotoka kwetu na ambazo ni mashambulizi ya mapepo na tumwombe atufundishe jinsi ya kupambana na mapepo yanayotuletea hisia mbaya).

Nimejifunza kuwa mapepo yana uwezo wa kuathiri hisia zetu kwa kutumia huzuni, kukata tamaa, kujiona hatuna maana, kuhisi kama vile Mungu ametudanganya au ametuacha (na kwa upande wangu, nilihisi kabisa kuwa Mungu amenisaliti) kuhisi kama vile Mungu si wa kuaminiwa au Neno lake si la kuaminiwa, kuhisi Mungu hasikii maombi yetu, achilia mbali kujibu; kuhisi kuwa Mungu hatupendi; kwamba tumeshapoteza wokovu wetu, au kama tumemkasirikia sana Mungu, kuhisi kuwa Mungu hatatusamehe, nk. Lengo la mapepo ni kukuibia wewe na mimi furaha ya wokovu wetu ambayo imo ndani ya mioyo yetu. Nimejifunza kupambana na uongo na kusimama kwenye kweli ya Injili (furaha na amani nilizopewa na Yesu katika roho yangu) badala ya kukubaliana na nguvu ya udanganyifu ya mapepo inayotaka mimi niamini hisia zangu badala ya kuamini Kweli na Neno la Mungu ... na kufanya Neno la Mungu liwe ndiyo lenye mamlaka ya mwisho kwenye kila jambo.

Nakumbuka wakati fulani wa majira ya joto ambapo nilirudi kazini nikiwa nimekata tamaa kabisa na nikayaona mapepo yamenizunguka yakirukaruka kwa furaha kwa sababu hiyo. Jambo hilo lilinighadhibisha mno Kama kuna kitu ambacho sikuwa tayari nacho ni kuyapa mapepo nafasi ya kushinda na kufurahia kwenye maisha yangu. Kwa hiyo, nilichofanya ni kuyatazama, nikavuta pumzi kwa nguvu, nikala chakula cha jioni, kisha nikakusanya nguvu zangu zote nilizokuwa nimezipoteza na nikasema kwa sauti: “Mungu, asante kwa kazi na asante kwa furaha na amani niliyonayo kwenye moyo wangu.” Nilienda chumbani kwangu na kuanza kusoma Maandiko kwa sauti. Baada ya hapo sikuyaona tena yakiwa yanarukaruka kwa furaha.

Nakumbuka pia wakati mwingine mapepo yalikuwa yananishambulia kwa hisia za kukata tamaa pamoja na huzuni kubwa. Nilishindana nayo sana. Huwa hayatumii sana mbinu hiyo kwangu. Haina nguvu sana kwa sababu huwa najitahidi kutofuata KAMWE hisia zangu. Huwa sisomi Biblia kwa vile tu eti NAJISIKIA kufanya hivyo au kuomba kwa vile najisikia kufanya hivyo. Ninasoma Neno na kuomba kwa sababu nimeamuriwa kufanya hivyo na kwa sababu ninataka kuonyesha uaminifu wangu kwa Mungu. Ninapotambua kuwa mapepo yananishambulia kwa hisia hasi, mara moja ninamshukuru Mungu kwa ajili ya furaha na amani niliyonayo katika roho yangu, nayakemea, kisha naendelea na kile ambacho nilikuwa nimepanga kufanya.

Lengo kuu la mapepo katika kushambulia hisia zangu ni kutaka kunidhibiti kupitia hisia. Sasa kama sitazifuata hisia zangu, lakini nikafuata Neno la Mungu, mashambulizi yao yanakuwa ni kazi bure.

Ninajua kuwa mapepo huathiri si tu hisia zetu kwa kutujaza hisia hasi, bali pia kwa kutumia hisia chanya za bandia ambazo ni rahisi kwa mtu kuzitafsiri kuwa ni uwepo wa Mungu. Nimejifunza kuwa Mungu hatendi kazi kupitia hisia zetu. Mungu hutenda kazi kupitia Neno lake na imani yetu tu. Mapepo mara zote hutenda kazi kupitia hisia za mtu kiasi kwamba mtu huyo atasoma Biblia na kuomba pale anapojisikia kufanya hivyo na si kwa vile Mungu ameamuru afanye hivyo. Ni vibaya sana kwamba Wakristo wengi hawatambui kuwa kujisikia vizuri wakati wa kuomba au kuabudu, haimaanishi kuwa hisia hizo ni lazima ziwe zinatoka kwa Mungu. Ni nadra kwa Mungu kufanya jambo ili tu kutufanya tujisikie vizuri kihisia. Yeye ana malengo mengine tofauti kabisa kwa ajili yetu. Anataka kutufundisha kujilisha mioyo yetu kwa kutumia Kweli (Neno la Mungu). Kweli mara zote hukubaliana na roho inayotafuta kumpendeza Roho Mtakatifu. Kwa roho zetu na Roho Mtakatifu kutenda kazi kwa pamoja na kwa kukubaliana kabisa, hisia zetu zitaanza kufuata mstari, na ndipo itakuwa rahisi kutambua ni nani anayeendesha hisia zetu.

Wakati fulani nilihudhuria ibada kwenye kanisa fulani. Nilihisi hali fulani ambayo mwanzoni nilikuwa nikiita ni “uwepo wa Roho Mtakatifu.” Baada ya ibada nilimwendea binti mmoja. Aliniambia kuwa alifurahia sana “uwepo wa Bwana.” Mara moja nilijiuliza swali, “Ni kweli ni uwepo wa Bwana? Je, Mungu wangu ninayemtumikia anawaita watoto wake ili wawe wakimya tu? Au Mungu wangu anawaagiza watoto wake wawe macho na wawe waombaji muda wote?”

Hivi karibuni Mungu amenifundisha nisikubali kabisa hisia za “uwepo bandia wa Bwana” unaokuja kutoka kwa mapepo. Kwenye sehemu ya jumuiya ambako watu wanatafuta kuwa kwenye uwepo wa Mungu, muziki wa sauti kubwa, kupaza sauti kwa watu pamoja na spika kunaweza kusiwe chochote bali ni uchocheaji wa hisia zetu hadi kiwango cha juu kiasi kwamba kunaweza kudhaniwa kuwa ndio “uwepo wa Mungu” wakati siyo. Na inapotokea hivyo, shetani anaweza kuleta udanganyifu kwa kila namna unaoweza kuonekana kama ni utendaji kazi wa Roho Mtakatifu kumbe Roho Mtakatifu anaweza kuwa yuko uani anatapika (yaani anaweza kuwa anajisikia kinyaa kwa hali kama hiyo). Uwepo wa kweli wa Mungu huwa unatambulika kwa mtu mmojammoja peke yake – kwenye utulivu – katika ushirika binafsi na Mungu. Yesu hakuwa na haja ya kuchochea watu kihisia kwenye sehemu ya watu wengi ili kusikia kile ambacho Baba yake alitaka afanye. Mara zote ilikuwa ni kwenye utulivu, mahali ambako hakuna vurugu. Hapo ndipo aliona “uwepo wa Mungu.”

Lakini imekuwa ni kinyume chake ambapo kundi la Wakristo “husubiri kwa kimya uwepo wa Roho” uwatembelee. “Watetemekaji” na "wachekaji" na "waliaji" wamekuja na kupita; na watakuja na kupita ... na kama udhihirisho wa nguvu unaotokea wakati huo, hauzai matunda yaliyo wazi kwa dhambi kuwekwa wazi na kutubiwa – roho haziokolewi – hakuna huduma inayoburudisha ya Neno la Mungu – hakuna uponyaji wa hakika ambao umethibitishwa na wataalamu wa afya – watu wanaanguka kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni nguvu za Mungu, kitu ambacho hakifanyi lolote zaidi tu ya kuvutia machoni mwa watazamaji. Mapepo yanapewa uwanja wa kudhihirika kwa “wakristo” kwenye ibada bila ya Wakristo hao kufuatiliwa kibinafsi. Wakristo ni lazima wawe makini sana kukubali kwamba “miujiza hiyo inatoka kwa Mungu.” Japokuwa Mungu amefanya na ataendelea kufanya yote hayo niliyotaja hapo juu, shetani naye anaweza, na ataendelea kuigiza mambo hayahaya.

Nimegundua kuwa mara mashambulizi ya adui yanapotambulika na mtu akapambana nayo kwa bidii zote kwa kutumia upanga (Neno) na ngao (Imani), adui huondoka mara moja. Ashukuriwe Mungu atupaye kushinda kupitia Bwana wetu Yesu Kristo (1 Kor. 15:57) na ambaye hutufanya kushinda (2 Kor. 2:14).

Kutambulishwa kwenye vitabu vya Rebecca Brown

Baada ya kutambua jinsi adui yangu alivyo na nguvu na ukatili, niliamua kujifunza zaidi kuhusu vita vya kiroho kutoka kwenye vitabu vya Kikristo mbali na kujifunza Biblia na kutoka kwenye uzoefu wangu binafsi. Nilitambulishwa kwenye vitabu vya Rebecca Brown na Mkristo mmoja kwenye kanisa nililoanza kuhudhuria mara baada ya kuokoka. Nilitiwa moyo sana kuona kuwa kumbe mambo mengi niliyojifunza katika vita vyangu vya kiroho yanathibitishwa na Rebecca katika kitabu chake. Kupokea uthibitisho wa uzoefu wangu limekuwa ni jambo muhimu sana kwangu kwa kuwa sikuwa na mtu yeyote ambaye ningeweza kumshirikisha uzoefu wangu.

Zaidi ya hapo, ilikuwa ni muhimu pia kwangu kutambua kuwa sikuwa peke yangu niliyeshambuliwa na adui. Wapo watoto wengi wa Mungu wanaopitia mashindano makali kama yaleyale. Kujua hili kumenisaidia kunyamazisha sauti ya adui aliyekuwa akininyanyasa kutokana na ukweli kwamba “niko mpweke na peke yangu na sina marafiki.” Kwa neema ya Mungu, hathubutu kufanya hivi tena, maana ninajua kuwa siko mpweke (Yesu yuko nami daima) wala siko peke yangu (watoto wengi wa Mungu nao pia wanashindana na adui). Japokuwa sina marafiki wa Kikristo waliokomaa hapa Moscow muda huu ninapoandika, najua kuwa hili limepangwa na Mungu kama sehemu ya mafunzo yangu ili nijifunze kumtegemea Yeye kunifundisha jinsi ya kufanya vita vya kiroho vyenye ushindi dhidi ya nguvu za kipepo. Nisingependa watu wapate picha kwamba "ni mimi naYesu tu"; kwamba siwahitaji Wakristo wengine kutoa mchango kwenye maisha yangu, na kuniombea mimi pamoja na mwito wa Mungu maishani mwangu - hapana. Isipokuwa kwamba kwa sasa niko kwenye kipindi ambacho Mungu ananifundisha mambo mengi moja kwa moja kutoka kwa Roho wake. Ni Mungu tu ajuaye kile kitakachotokea kwenye maisha yangu yajayo.

Udanganyifu wa shetani makanisani

Baada ya kusoma vitabu vya Rebecca nilifanya utafiti kwenye mtandao wa Google na kuiona tovuti yake. Kwenye tovuti hiyo nilikutana na unabii/maono mawili kuhusiana na uchaguzi mbalimbali wa Marekani yaliyoandikwa na mume wa Rebecca, Daniel. Nilishtuka sana baada ya kufahamu kuhusu mbinu za adui.

Nimeshahuhudia uthibitisho mwingi kote kwenye habari za dunia na kanisani kwamba unabii wa Daniel ulikuwa kweli kwa 100% na unatoka kwa Mungu. Macho yangu yamefunguka na kuona kazi ya adui iliyo ya kificho sana dhidi ya kanisa ikiwa ni pamoja na:

  • Maombi yaliyojaa ubinafsi na kujitazama mwenyewe tu.
  • Mahubiri yanayolenga upendo wa Mungu kama njia ya kunufaika sisi na kile ambacho Mungu anaweza kututendea na si kile tunachoweza kutenda katika kumtumikia na kuenenda kwa utii mbele zake.
  • Unabii kuhusina na upendo wa Mungu usiokoma na si kuhusu haja ya kuacha dhambi na kuwajali waliopotea.
  • Mara chache sana nimesikia makanisani kwamba Wakristo watateseka kwa ajili ya Yesu (na kiukweli, kadiri wanavyojitoa kwa bidii kwa Mungu ndivyo huenda watateseka zaidi isivyo haki); kwamba wanatakiwa kutambua na kujifunza kuukana ubinafsi wao; kwamba mateso ni jambo linalotokea kila siku kwa namna moja au nyingine na kwamba wanatakiwa kubeba misalaba yao ya mateso yasiyo ya haki yatokanayo na kuonewa na kumfuata Kristo bila kujali kuna maumivu kiasi gani – bila kujali gharama inayotakiwa.
  • Kile ambacho nimeona kuwa kinasikika zaidi ni ujumbe wa kificho wa kile ambacho Mungu atanitendea kama nikifuata kwa usahihi “kanuni” fulani fulani na si kile ambacho ninatakiwa kufanya kwa ajili yake ili kuenenda katika utakatifu na kuachana na ubinafsi wangu ili kuwasaidia wengine kuja kwa Mungu na kukua ndani ya Mungu.

Gharama ya kuwa Mwanafunzi wa Yesu
Septemba iliyopita, nilijitolea kufundisha masomo ya Biblia ili kutoa picha ya gharama ya kuwa mwanafunzi wa Yesu pamoja na vita vya shetani dhidi ya Wakristo. Nilichagua mistari inayojibu maswali yafuatayo:
· Je, Yesu anaahidi utajiri kwa wanafunzi wake?
· Je, Yesu anaahidi afya kamili ya kimwili kwa wanafunzi wake?
· Je, ahadi ya kuteswa na kuteseka ilitimia kwenye maisha ya Wakristo wa Agano Jipya?
· Je, Mungu anavumilia dhambi kwenye maisha ya Mkristo? Kwa nini Wakristo waliteswa?
· Kwa nini Neno la Mungu linasema kuwa kila anayetaka kuishi maisha ya uchaji Mungu atateswa?
· Je, Mungu anamruhusu shetani kuwashambulia Wakristo moja kwa moja?

Niligundua kuwa wakati nikisoma Maandiko haya baadhi ya watu walikosa utulivu. Nilipofika kwenye kusoma Maandiko yanayoongelea kuhusu shetani kumpepeta Petro kama ngano, kijana mmoja alipayuka kwa hasira. Alipinga kabisa mimi kusoma mstari huo. Alisema kuwa mstari haukuwa unahusiana kwa namna yoyote na Petro kumkana Yesu, na hakuniruhusu kuendelea kusoma Maandiko zaidi ili kufafanua mstari huo. Nilikuwa sijawahi kukutana na upinzani mkali namna hiyo kwa Neno la Mungu kutoka kwenye kundi la waamini, na sikutaja chochote kinachonihusu mimi binafsi. Nilikuwa nasoma tu kutoka kwenye Neno la Mungu!

Nilipomwomba kijana yule aniache angalau niendelee kusoma Maandiko, alisema kuwa hataruhusu mafundisho yoyote ya uongo kwenye kundi letu dogo. Wanakikundi wengine nao walinikabili na kunitaka niwaeleze sababu hasa ya mimi kuwasomea mistari ile. Karibu wakimbie kabisa kutoka kwenye nyumba yangu ungedhani mimi ni mchawi. Niliumia na kulia.

Baada ya siku chache, Mungu alisema nami. Aliniambia: “Watalikataa jina lako kama uovu. Thawabu yako ni kubwa mbinguni. Niamini Mimi tu, Neno langu tu. Nitakuja na kumlipa kila mmoja kwa kazi yake. Waombee. Vifungo nilazima viharibiwe kwanza. Vifungo ni:
· Mwili
· Kupenda mali
· Kujipenda mwenyewe
· Starehe
Utateseka, usijipende mwenyewe, jikane mwenyewe, jifunze kujikana katika kila kitu kinachopingana na Mimi. Soma Neno langu na kuomba kila wakati. Nitajitukuza kupitia wewe. Hii itakuja kupitia maumivu na mateso utakayopitia. Jifunze kuridhika na ulicho nacho. Nataka kuwa chanzo pekee cha furaha yako na ridhiko. Asiwepo mwingine. Omba kwa ajili ya kuenea kwa Neno langu na kuharibiwa kwa kazi za adui. Jifunze kuniamini Mimi. Jifunze kufurahi kwenye mateso yako. Omba kwa ajili ya kuharibiwa kwa uongo na udanganyifu unaoharibu akili za wanangu. Nawapenda wote sawasawa. Jiachie kwenye mapenzi yangu. Utukufu ni wa kwangu peke yangu. Omba kila wakati, omba. Uharibifu unakuja kwenye dunia hii. Wale wanaonitumikia ndio watakaopona; wale wasionitumikia hawatapona. Omba.”
Baadaye nilipata uthibitisho ufuatao kwenye Neno la Mungu.
2 Timotheo 3:1-5:
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu,

wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

Nguvu ya Mungu inatolewa si tu kuokoa, bali pia kuponya na kukomboa na kuua asili yetu ya ubinafsi, anguko na kukosa utii ... sio tiketi ya kusamehewa tena na tena huku mtu anaendelea kutenda dhambi ileile tena na tena na kuyapuuza kana kwamba toba ndogo tu inatakiwa kufanya kila kitu kiwe sawa kati yetu na Mungu, halafu mtu anarudi tena kuyafanya matendo hayo hayo ya uasi hadi atakapoenda tena kutubu. Unakuwa ni mduara unaojirudia tena na tena kama kwamba Ukristo si zaidi ya kusema: "Unajua nini? Naweza kutenda dhambi na ilimradi ninatubu, naweza kufanya dhambi ileile tena na tena na kila kitu kinakuwa sawa tu kati yangu na Mungu! Napenda kweli aina hii ya Ukristo!”

Hapana! Haitakiwi kuwa hivyo!

Tangu niokoke, nimekumbana na mashambulizi kadhaa kutoka kwa adui ambayo yanakuja kupitia kwa mtu tunayekaa naye chumba kimoja, wafanyakazi wenzangu, na hata washirika wa kundi langu dogo la wapendwa, japo ndiyo yanakuja kutoka kwenye tamaa za mwili wangu. Adui anatumia kila kitu na kila mtu kunijaribu na kujaribu kuniharibu. Nimejifunza kuwa Yesu kweli alimaanisha pale aliposema: “Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.” (Luka 9:23). Wakati mapambano yangu yanapokuwa makali kabisa, wakati mwingine nahiksi kama vile msalaba wangu ni mzito kupita kiasi. Ni vigumu sana kushinda mashambulizi ya mara kwa mara ya adui, lakini Mungu amekuwa kila wakati mwaminifu na hunipatia mstari unaofaa wa kumnyamazisha adui na amenipa hekima ya kujishusha mbele zake na kutofunua kinywa changu mbele za wale wanaonizushia mambo ya uongo.

Hivi karibuni nimegundua kwamba hata kwenye mapambano makali, pale ambapo kila kitu na kila mtu anakuwa kinyume nami INAWEZEKANA kubakia na furaha na amani ambayo Yesu anatuahidi kwenye roho zetu, hata kama sijisikii furaha na amani kihisia. Mapepo yanaweza tu kunidhuru kimwili na kihisia, lakini kama nikisimama kwenye Neno la Mungu, hawawezi kunidhuru moyo wangu ambako ndiko anakokaa Mungu. Neno la Mungu, maombi na imani NI SILAHA ZENYE NGUVU SANA dhidi ya adui.

Kuingilia himaya ya shetani

Novemba 2004, nilikutana na jambo ambalo lilinipa msukumo wa kujifunza zaidi kuhusiana na ibilisi na imani za siri. Nilisoma makala kwenye gazeti kuhusiana na tovuti fulani ya Kirusi ambayo ilikuwa inahamasisha watu kujiua. makala hayo yalikuwa yanahusiana na vijana waliokuwa na majonzi na mawazo ya kujiua ambao hatimaye walijiua kutokana na ushawishi wa tovuti hiyo. Makala yalisema kuwa tovuti hiyo ilikuwa na taarifa nyingi za namna ambavyo mtu anaweza kujiua kwa mafanikio. Vijana kadhaa waliosaidia kuitengeneza tovuti hiyo, baadaye walikutwa wakiwa wamekufa. Wazazi wao walimshitaki kiongozi/mwanzilishi wa tovuti hiyo.

Baada ya kusoma makala niliamua kuitazama tovuti hiyo. Nilikuwa sijui kabisa kwamba tovuti hiyo ilikuwa ina uvuvio wa shetani na kuendeshwa na waabudu shetani. Tovuti hiyo ni ya uovu kamili ikiwa na picha za watu waliokufa na mandhari yenye giza ambayo yanamfanya mtu asiyekuwa na huzuni au mfadhaiko aupate. Mbali na mwonekano wa ajabu wa nje, tovuti hiyo unatoa giza la kiroho ambalo linawaathiri moja kwa moja watu wanaoitembelea.

Nilisoma maelezo kuwahusu watu kadhaa humo ndani. Wote walikuwa na historia zinazofanana. Walikuwa ni watu walionyanyaswa sana wangali watoto; walitoka kwenye ndoa zilizovunjika; walikataliwa na wazazi wao wakiwa wadogo; hawajawahi kupata upendo au matunzo ya wazazi. Niliamua kwenda kwenye sehemu ya kutoa maoni ili angalau niweze kusema nao kwamba kuna mmoja anayeweza kuponya maumivu yao na kuwaweka huru mbali na huzuni na fadhaa zao. kwa kutojua kwangu, nilidhani kuwa huenda naweza kuwafikia watu wale.

Mtu mmoja akawa amevutiwa na kile nilichosema na akataka kufahamu zaidi kuhusiana na kuwekwa huru. Hata hivyo, nilipoanza kumweleza kuhusu kweli za Biblia, kila mara nilipoandika jina la Yesu Kristo lilifutika. Kwa siku nzima nilizuiwa kabisa kuchangia chochote kwenye ukurasa huo.

Usiku wa kwanza baada ya kuchangia kwenye tovuti ile, nilipatwa na jinamizi baya sana! Mungu aliniamsha katikati ya usiku na akaniambia niombe. Nilijawa na hofu kubwa kutokana na uwepo wa uovu chumbani kwangu.

Siku iliyofuata nilijisikia kichefuchefu. Nilienda kwenye tovuti ile asubuhi. Msichana mmoja aliandika swali, akiuliza ni dawa gani atumie na ni kwa kiasi gani ili aweze kujiua. Nilijaribu kumtumia ujumbe ili kumwambia amwite Yesu. Ujumbe wangu ulizuiwa kwenda. Msichana yule alipata ujumbe kutoka kwa mtu mwingine ukimshauri atembelee sehemu nyingine kwenye tovuti ile inayoeleza kwa undani namna mbalimbali za kujiua. Nilitambua kuwa, kwa makusudi, nilikuwa nimezuiwa kabisa kuandika ujumbe wowote kwenye tovuti ile.

Niliamua kuwaeleza kundi lile letu dogo la maombi ili tuombe dhidi ya ile tovuti na kwa ajili ya watu na kwa ajili yangu (maana nilianza kupata majinamizi). Hata hivyo, hadithi yangu iliamsha chuki na hasira nyingi! Wanakikundi walinizuia kwa ukali kuzungumzia tena kuhusiana na tovuti ile na wakaanza kuhoji kama na mimi nilikuwa na mawazo ya kutaka kujiua, na kama kweli nilikuwa nimekombolewa kutoka kwenye mfadhaiko. Sikuamini kile nilichokuwa nakisikia kutoka kwao!

Kisha kwa ukali waliniambia niondoke kwenye kikundi kile cha Biblia kama nilikuwa sipendi vile walivyokuwa wakiomba sana kwa ajili yao kibinafsi na kwa ajili ya wanakikundi wenyewe. Nilikuwa sijawahi kutamka chochote juu ya kuondoka kwenye kikundi. Ni wazi kwamba niliumia sana, nikalia na nikajaribiwa kuinuka na kuondoka zangu. Hata hivyo, Mungu aliweka ndani yangu moyo wa kubakia, kwa hiyo nilibakia pale.

Nilifurahi kwamba nilibakia kwa sababu mama mmoja mtu mzima aliomba kwa ajili yangu. Aliniambia kuwa niliingia kwenye himaya ya shetani bila ya kuambiwa na Mungu. Alinishauri kuwa niombe tu kwa ajili ya watu wale wa kwenye tovuti, lakini akashauri kwa nguvu sana kwamba niache kutembelea tovuti ile. Nilielewa kuwa alikuwa sahihi. Nilijua kuwa siwezi kushindana na uovu niliokutana nao. Haikuwa ni mashambulizi tu ya kawaida. Hapana. Ilikuwa ni zaidi ya hapo – uovu mkubwa ambao usingekaa kimya kwa sababu nimeingilia himaya yake. Nilizingatia ushauri wake. Hata hivyo, majinamizi, hofu kubwa na uwepo wa uovu usiku viliendelea kuniandama kwa muda.

Miezi miwili baadaye nilikuja kufahamu kuwa baadhi ya watu wanaoendesha tovuti ile ni waabudu shetani. Kama ningejua hilo kabla, nisingejaribu hata kuifungua tovuti ile. Namshukuru Mungu kwa kuniweka salama wakati wa kukosa kwangu umakini. Mungu aliniambia niendelee kuwaombea wale walio na mfadhaiko na kwa ajili ya kuharibiwa kwa tovuti ile.

Baada ya tukio lile, niliamua kuijifunza mengi kadiri iwezekanavyo kuhusiana na vita vya kiroho na adui na wale wanaojihusisha na imani za siri. Najua kuwa kuingilia himaya ya adui bila mwongozo wa moja kwa moja wa Mungu kunaweza kuwa ni jambo la hatari sana. Katika kutafuta kwangu kufahamu juu ya ulimwengu wa kipepo, nilinunua maandiko ya Howard Pittman, Jessie-Penny Lewis na Rebecca Brown. Ninapendekeza kila Mkristo asome kitabu kilichoandikwa na Jessie-Penn Lewis. Ni moja ya vitabu vilivyoandikwa kwa uzuri na kwa undani kuhusiana na mambo ya ulimwengu wa roho, kama ambavyo wengine wengi nao wanakubaliana na hili. Nadhani Wakristo wote wanaweza kupokea mafunuo mengi kupitia kitabu hiki, nacho kinaweza kupatikana kwa kubofya: Hapa

Ufupisho wa masomo niliyojifunza kutoka kwa Mungu

Kwa kifupi, Mungu alinifundisha mambo yafuatayo:
1. Kila Mkristo amepangiwa mapepo na shetani yanayomfuatilia ili yamharibu. Hakuna asiyekuwa nayo. Mungu kwa upande wake ametupangia malaika mmoja au zaidi wa kutusaidia. Kama tungeruhusiwa kuona ulimwengu wa roho unaotuzunguka, tutaona malaika na mapepo wametuzunguka.

2. Mapepo hutufuata kila wakati. Wanafahamu udhaifu wetu, hivyo wanapanga kutushambulia katika muda ulio mwafaka kwao. Ni muhimu kwangu kufahamu udhaifu wangu na kumwomba Bwana augeuze kuwa nguvu kwangu. Kujikana mwenyewe na kuachana na kila kitu ninachokipenda sana ambacho hakimtukuzi Mungu ni jambo la lazima. Ni njia pekee ya kupunguza uwezekano wa kushambuliwa na adui.

3. Lengo la mapepo ni kunifanya nimuasi Mungu, kunifanya niwe mtu wa kumnung’unikia, kumlalamikia, na kumkasirikia Bwana wangu Yesu, na kuwadharau watu wa Mungu wasio na sifa mbalimbali. Nilipogundua kuwa mateso na matatizo yangu yanatoka kwa adui na si kwa Mungu, nilijifunza kuelekeza hasira zangu zote kwa mapepo.

4. Mbinu ninayotumia kumaliza hasira zangu kwa mapepo pale yanaponishambulia ni kwa kujitahidi kufanya kile ambacho Mungu ananiagiza kufanya na kutompa kabisa adui nafasi. Ninajua kile ambacho adui anataka kwangu na mimi siko tayari kumpatia kwa hiyari yangu mwenyewe. Ni wazi kuwa haya ni mapambano makali na magumu. Namjua yule ninayekabiliana naye; ni kiumbe mwenye nguvu zaidi baada ya Mungu. Ni adui mwovu kabisa ambaye mwanadamu anaweza kuwa naye hapa duniani. Sitarajii haki yoyote kutoka kwa adui. Sitarajii kuwa ataniruhusu tu nisababishe madhara kwenye ufalme wake kisha niendelee kuishi kwa furaha tu hapa kwenye ufalme wake duniani. Nimeshahesabu gharama zangu. Kila kitu maishani mwangu kiko hatarini. Najua kuwa adui daima anadai, ama moja kwa moja au si moja kwa moja, ili Baba amruhusu, yeye ibilisi anijaribu. Na pale ruhusa inapotolewa, najua kuwa ibilisi atanivuta kuliko uwezo wangu. Lakini pia najua kuwa Mungu ameahidi kuwa atanisaidia kushinda na kustahimili. Yesu hakuwahi kuahidi kuwa ataniepusha na mateso, lakini aliahidi kuwa atanifundisha kushinda na kustahimili. Niko tayari kubeba msalaba wangu kila siku hadi mwisho, kushinda na kustahimili. Pia niko tayari kupokea thawabu nzuri kwenye ufalme wa Mungu. Katika vita vyangu siko tayari kurudi nyuma – sina mahali popote pa kurudia nyumba – nina kusonga mbele tu!

5. Hakuna kitu kinachotetemesha ufalme wa shetani na jeshi lake la mapepo kama pale watoto wa Mungu wanapoendelea kushikilia utii wao kwa Bwana Yesu kupitia kumshukuru kila wanapoteswa na kufedheheshwa na adui. Mungu amewapa mitume wake , maandiko mengi "kuhesabu kuwa furaha" tunapoteswa isivyo haki na shetani na kustahimili, maana thawabu yetu itakuwa kubwa mbinguni. (Ibilisi muda wote anataka tuhisi kuwa Mungu ni katili kwa sababu hatupatii thawabu zile tunazotaka kwenye maisha haya; na ni lazima tuwe waangalifu ili tusiingiwe na hisia za kujionea huruma kama kila kitu kinaonekana kiko kinyume nasi; vinginevyo ibilisi anaweza kutumia hali hiyo kufanya shauku yetu ya kumtumikia Mungu ishuke chini).

6. Kumbuka ... maisha haya ni mafupi mno kulinganisha na milele. Mateso yoyote ambayo Mungu anaruhusu tuyapitie kwa miaka michache hii tuliyo nayo hapa duniani, hata kama ni makali kiasi gani, hayawezi kulinganishwa na uzito wa milele wa utukufu yatakayotuletea. Hilo ni Neno la Mungu! (Tazama: 2 Kor. 4:17-18).

Kwa wale wanaojiona wamesalitiwa na Mungu

Kama kuna kipindi ulikuwa na moto na Mungu, ukiomba kwa bidii na kusoma Biblia kwa bidii, lakini kidogo kidogo umeingiwa na uchungu dhidi ya Mungu kwa sababu ya matatizo au mateso na dhiki, mambo yafuatayo ni kwa ajili yako kibinafsi.

Kwa kuwa na mimi nimepita mahali uliko hivi sasa, na ninafahamu uchungu wa kihisia na mfadhaiko unaokutesa, ningependa kukupatia hatua kadhaa ambazo zilinisaidia mimi kupata uhuru kutoka kwenye nguvu za shetani.

Njia yangu kuelekea kwenye kukombolewa:

1. Mungu alinisaidia kutambua kuwa Yesu hanichukii wala hanilaani.
Nilienda kutazama sinema ya “Mateso ya Kristo”. Kwa kutazama mateso ya Kristo nilitambua kuwa Kristo hakunichukia hata kidogo. Mapepo yalinishawishi kwamba Mungu alinichukia na kunilaani na kwamba Yesu hakupata mateso makubwa ya kihisia. Uongo wao uliota mizizi kwenye akili yangu. Niliteswa na uongo huu kwa miaka miwili. Kupitia sinema ile, Mungu alivunja nguvu ya giza lile kwenye akili yangu. Nilitambua kuwa Yesu, si tu kwamba hakunichukia, bali pia aliteseka sana kwa ajili yangu. Hii ilikuwa ni hatua yangu ya kwanza na ya muhimu sana kuelekea kwenye uhuru wangu.

2. Kwa kusoma shuhuda za waliookoka, nilielewa kuwa kumbe sikuwa peke yangu kwenye mateso na dhiki. Kabla ya kuja kwa Kristo, watu wengi walipitia mateso makali zaidi kuliko ya kwangu.

Mwanzoni mwa mchakato wa ukombozi wangu, mapepo yalishikilia kwa nguvu sana akili yangu kiasi kwamba sikuelewa Biblia na sikuweza kustahimili kusikiliza au kusoma Neno la Mungu. Hata hivyo, nilikuwa na shauku ya kutaka kujua kama kulikuwa na Wakristo wengine waliokuwa na mapito kama yangu. Wakati nikitafiti kwenye mtandao wa Google, Mungu aliniongoza kwenye tovuti ya Shuhuda za Thamani (www.precious-testimonies.com). Wakati ninasoma shuhuda, Mungu alivunja uongo mwingine uliokuwa umejikita kwenye akili yangu: nilitambua kuwa sikuwa kamwe peke yangu kwenye mateso, kama ambavyo nilikuwa nikiamini hapo kabla. Wapo wengi walioteswa zaidi yangu na shetani. Kwenye shuhuda hizo, niliweza pia kuona namna shetani alivyoharibu maisha ya wengine na jinsi Yesu Kristo alivyowaweka huru na kuwapa maisha mapya.

Kweli kabisa “wao (Wakristo) walimshinda yeye (shetani) kwa damu ya Mwana-Kondoo, na KWA NENO LA USHUHUDA WAO; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. (Ufunuo 12:11).

Baada ya kutubu, niliamua kuyatoa maisha yangu yote kwa Kristo. Nilitia saini agano langu la kwanza na Mungu ambapo niliachana na ndoto zangu zote za duniani; shauku zangu na matumaini yangu. Nilimpa Mungu haki zangu zote ili aamue iwapo niwe na kazi au la; kama nitaolewa au la. Katika agano langu nilijitoa kumtumikia Mungu bila kujali niko mwenyewe au nimeolewa; niwe na kazi au sina.

Wakati nikisoma Maandiko baada ya kuokoka kwangu, nimegundua kuwa sababu kuu ya mimi kuharibu imani yangu ni kuwa sikuwa nimefundishwa kwa usahihi mafundisho ya Yesu Kristo. Katika karne ya kwanza, Wakristo waliteswa na kufa kwa ajili ya Kristo na HAWAKUMKANA Kristo. Mimi sikuwa nimepokea shauku za tamaa zangu za kimwili ndiyo maana nikamkana Kristo!!! Unadhani hilo liliwafanya shetani na mapepo wafurahi?

Katika karne ya kwanza Wakristo walifundishwa mafundisho ya Kristo kuhusu kuvumilia mateso kwa ajili ya Kristo. Nilikuwa sikufundishwa au kusikia juu ya kuhesabu gharama ya kumfuata Kristo. Sikuwa nimesikia juu ya kustahimili mateso kwa ajili ya Kristo au kwamba inanibidi nijikane mwenyewe, nibebe msalaba wangu na kumfuata Kristo. Sikuwa nimesikia au kufundishwa kwamba inabidi nikane ubinafsi wangu ili kumfuata Yesu (achilia mbali kujifunza namna ya kubaini ubinafsi hasa ni nini!)

Badala yake, katika vitabu vya Kikristo nilijifunza mafundisho ya mashetani kuhusiana na Mungu kutaka kunipatia kila kitu ambacho moyo wangu unakitamani. Kwa namna fulani labda sikuona sura kwenye vitabu hivyo ambayo inanionya kuwa Mungu hatanipatia kila shauku ya moyo wangu kama shauku hizo ni za ubinafsi na si sehemu ya mpango wa Mungu kwa maisha yangu. Ilikuwa ni makosa yangu mwenyewe kuamini mafundisho ya mashetani. Sikufanya kile ambacho Mungu ameniamuru kwenye Neno lake. Sikuijaribu kila roho kwa Neno la Mungu na sikuwa makini na manabii wa uongo na walimu wa uongo. Matokeo yake, niliamini mafundisho mengi ya mashetani.

Ilikuwa ni makosa yangu kuamini kila kitu nilichosoma kwenye vitabu vya Kikristo. Na pale Yesu alipoacha kutimiza shauku za moyo wangu za kidunia, na pale matizo yalipokuja maishani mwangu kama Yesu alivyoahidi katika Yohana 16:13, sikujua namna ya kustahimili. Kwa hiyo mwishowe nilianguka.

Hatima ya mafundisho ya mashetani ni kuwadanganya wateule na kusababisha imani yao kuharibika.

Yafuatayo ni mafundisho ya mashetani ambayo niliyaamini. Mafundisho haya ya mashetani yako kwenye makanisa mengi, vitabu, kanda na CD na kwenye intaneti:

1. Kwamba Mungu anataka kukufanikisha kwa mali za kidunia na kwamba ‘kuridhika na ulichonacho’ (Tazama: 1 Tim 6:8 na Ebr. 13:5) maana yake ni kuridhika na si chini ya dola milioni moja.”

2. Kwamba Mungu anataka kukupa kila haja ya moyo wako, na mapenzi yake kamili ni kujibu kila ombi utakaloomba – huku akijibu kama wewe unavyotarajia ajibu.” (Kwa maneno mengine, hakuna haja ya kutilia maanani ubinafsi).

3. Kwamba shetani aliharibiwa kabisa msalabani, na kwamba shetani hana nguvu juu ya maisha ya Wakristo. Hivyo, usipoteze muda wako, hata wa dakika moja, kumfikiria. Vinginevyo, utakuwa unampa utukufu ambao unamstahili Yesu.”

4. Shetani amefungwa na hawezi kuwagusa au kuwadhuru Wakristo – kwamba anachoweza yeye ni kudanganya tu. Wakati wa Ayubu ulishapita kwa sababu Yesu alishamshinda shetani msalabani. Hivyo, shetani hawezi tena kuwashitaki Wakristo mbele za Mungu. Kwamba shetani hawezi kuchukua chochote tena kutoka kwa Wakristo.

5. Hauna haja ya kuteseka kwa ajili ya Kristo. Mateso si sehemu ya Wakristo tena.

6. Kila wakati Mungu anataka uwe mzima kimwili bila kutilia maanani mambo mengine. Vipi kama Mungu anataka kumpeleka mtu huyo mgonjwa nyumbani mbinguni? Vipi kama Mungu anataka kumfundisha jambo ambalo kwa njia nyingine hawezi kujifunza; kwa mfano kujifunza kumtukuza Mungu katika madhaifu yake? Vipi kuhusu watu wanaoshiriki meza ya Bwana bila kujihukumu na kujikagua wenyewe sawasawa? Maandiko yanasema kuwa watu wanaweza kuugua na kufa wangali na umri mdogo kutokana na kutojihukumu wenyewe sawasawa. (Tazama: 1 Wakorintho 11:29-31). Inaonekana kwangu kwamba hekima inatutaka tuangalie uponyaji wa kimwili kama tunavyoangalia dhambi. Tunajua kuwa Mungu anataka dhambi yote iondolewe kwenye dunia, lakini hilo halitatokea hadi baadaye huko mbeleni. Japokuwa tuko salama kuamini kwamba uponyaji wa kila aina hakika umo ndani ya upatanisho kwa ajili ya watu wa Mungu, ni lazima tuwe na hekima ya kutomwacha shetani aharibu imani yetu pale tunapomtafuta Mungu kwa ajili ya uponyaji ... hasa pale uponyaji huo unapogoma kutokea licha ya kuomba kwetu kwa bidii.

7. Kamwe usiseme, "Hata hivyo, si mapenzi yangu bali mapenzi ya Mungu yafanyike maishani mwangu," kama hukupata kutoka kwa Mungu kitu ambacho ulikiomba kwa Mungu. "Haujui mapenzi ya Mungu kwa maisha yako, hivyo unatakiwa kuendelea kuomba zaidi na zaidi ili Mungu akutendee kile unachokitaka.”

Yapo na mengine mengi zaidi – mafundisho ya kificho ya mashetani yanayoendelea kufundishwa. KAMWE usiamini kila kitu unachofundishwa kanisani au unachosoma kwenye vitabu vya Kikristo kabla ya kukijaribu kama kinaendana na ushauri wa Neno la Mungu katika Agano Jipya lote (pamoja na kanuni, miongozo na amri za Agano la Kale ambazo hazipingani na kweli iliyofunuliwa katika Agano Jipya, bali zinaiunga mkono). Unafanyaje hivyo? Ibilisi anapenda kuchukua neno moja au mawili kutoka kwenye Maandiko ambayo yanazua maswali katika utekelezaji wake na kuyafanya yaseme kitu ambacho Mungu hata hakukikusudia. Kila inapowezekana, acha Maandiko yatafsiri Maandiko mengine. Acha hali ya kujirudia kwa mawazo yaliyo kwenye Maandiko kujithibitishe kwenyewe ili kuumba imani thabiti. Kutafsiri neno moja au mawili (au labda matatu au manne) katika tafsiri zetu za Biblia za kileo kusichukuliwe kuwa ni lazima kwamba kunaeleza kikamilifu maana iliyokusudiwa iliyokuwa kwenye lugha za asili za Kiebrania na Kigiriki. Maneno, na namna yanavyowasilishwa, yanaweza kubadilika kutoka utamaduni mmoja hadi mwingine kadiri muda unavyopita. Roho Mtakatifu atathibitisha kile kilicho cha muhimu kuamini na kipi sicho cha muhimu kutoka kwenye Maandiko ili kumpendeza Mungu Baba kama tutanyenyekea kiasi cha kutosha kukiri kuwa tunaweza kuwa tumekosea kutokana na kile tunachoamini juu ya maeneo kadha wa kadha ya Biblia ambayo hayaeleweki kirahisi.

Wakati huohuo, katika jitihada zetu za kuelewa na kutumia sawasawa Neno la Mungu, tusisahau kamwe ukweli kwamba, ndicho chanzo pekee cha kuaminika ambacho Mungu amewapa wanadamu ili waweze kujua mapenzi ya Mungu. Neno la Mungu ndilo mapenzi ya Mungu. Mapenzi ya Mungu yamewekwa wazi kwenye Neno lake. Hatuna cha kujitetea kwamba hatuwezi kujua mapenzi ya Mungu yaliyowekwa wazi kwetu, (au miongozo ya namna ya kutafuta mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu kibinafsi), kama hatujui Neno la Mungu.

Huenda chapisho bora kabisa ambalo linaweza kumnufaisha sana mtu katika kujifunza jinsi ya kujua kwa njia salama na ya hekima kitu cha kuamini kuhusiana na Neno la Mungu linaweza kupatikana kwa kubofya: Hapa.

Kumbuka, katika jamii tajiri, mafundisho ya mashetani ni nadra sana kuwaambia watu kuwa ni lazima kuteseka kwa ajili ya Kristo, ni lazima kumpinga shetani na ni lazima kujikana mwenyewe, ubebe msalaba wako na kumfuata Kristo. Pale ambapo kuna utajiri mwingi wa kimwili, mafundisho mengi ya mashetani yana mvuto mkubwa kwa kimwili – karibu mara zote huwa ni kwa ajili ya kile ambacho Mungu anaweza kututendea na si kile ambacho tunatakiwa kutenda ili kumpendeza Yeye.

Mafundisho ya mashetani karibu kila wakati huwa ni kwa ajili ya kulisha tamaa zetu za kimwili, zenye ubinafsi; yanalenga kupotosha maana na matumizi halisi ya Neno la Mungu; yanalenga kushushia hadhi usahihi na uhalisi wa Neno la Mungu; yanalenga kumpokonya Mungu utukufu anaostahili; yanalenga kuwadanganya na kuwajaribu watu ili wamchukie Mungu wakati kumbe ni shetani ndiye wanayetakiwa kumchukia.

Shetani anataka watu waamini kuwa jehanamu si halisi ili kusiwepo na hofu yoyote ya Mungu na nia kuacha dhambi; kwamba mapepo hawapo au kwamba hayana nguvu kabisa juu ya watu waliookoka kwelikweli, maana kwa njia hiyo, Wakristo hawatamtafuta Mungu kwa ajili ya kupewa uwezo wa kufanya kile wanachotakiwa kufanya katika kusaidia kupambana na kazi za kipepo duniani na kwenye maisha ya wapendwa wao. Orodha ya udanganyifu wa shetani inaendelea na kuendelea ...

Shetani amejaribu, na hataacha kamwe kuendelea kujaribu, kuwafanya watu wa Mungu wasitambue kuwa Neno la Mungu lililoandikwa ndilo pekee lenye mamlaka ambalo Mungu analiafiki na kulitia nguvu.

Hii ndiyo amri ya Mungu: Kwamba uyajaribu mafundisho yote unayoyasikia kanisani au unayoyasoma vitabuni au kwenye intaneti na kuwa makini na manabii wa uongo na walimu wa uongo. Kama hujasoma sawasawa Agano Jipya bado, basi waendee waelewa kadhaa tofauti wa Biblia wa kiprotestanti kabla ya kuumba imani yako thabiti juu ya jambo lolote. Duka lolote la vitabu vya Kikristo linaloheshimika linaweza kukutajia waelewa hao. Kama hakuna duka karibu, bofya tovuti hii na kuwauliza. Wanaaminika na wanaweza kukuelekeza kwenye mwelekeo sahihi: www.gospelcom.net

1 John 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Philippians 3:2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.

Kumbuka: mafundisho ya mashetani yana uwezo mkubwa sana ya kumharibu Mkristo kama ukiyaamini na kuyafuata. Mafundisho ya mashetani yatakufanya usiwe na nguvu kwenye ufalme wa Yesu na badala yake ukawa ni mtu wa kufuata tu ubinafsi wako au yatafanya imani yako ife kabisa.

Shetani amejitoa kwa nguvu zote kufanya vita dhidi ya wafuasi wa Kristo. Ni wale TU wanaofuata mafundisho sahihi ya Kristo ndio wataweza kupona mashambulizi makali ya adui na kupokea “taji ya uzima” kutoka kwa Mungu.

Ni lazima umwombe Mungu akufundishe jinsi ya kupambanua kati ya uongo na kweli. Kumbuka kuwa kamwe hutaweza kushinda uongo wa shetani kwa nguvu zako pekee. Ni kwa nguvu za Yesu TU ndipo utaweza kuutambua uongo wa adui.

Nakutia moyo usome Biblia kwa bidii, kila siku. Mungu ndiye Mwalimu BORA kabisa. Hakuna kitabu au mahubiri yoyote yanayoweza kuchukua nafasi yote ya ushauri na mafundisho kutoka kwa Mungu mwenyewe moja kwa moja. Shauku ya Mungu kwa ajili ya watoto wake ni waijue kweli na kuweza kupambanua kati ya jema na baya kama inavyosemwa kwenye Waebrania 5:14.

Mimi si pekee niliyeangukia kwenye uongo wa shetani; wako wengi wanaopita kwenye matatizo kama niliyopitia mimi. Ni kwa sababu tu ya rehema na neema kuu za Mungu ndiyo maana alinivuta nirudi kwake na akanikomboa kutoka kwenye nguvu za shetani.

Ninamwomba Mungu atumie ushuhuda huu wangu kwa ajili ya kueneza Ufalme wa Yesu na kuharibu ufalme wa shetani.

Endapo unanyanyaswa na nguvu za giza, au uko tayari kuachana na Ukristo kwa vile unahisi kuwa Mungu amekusaliti, kama ambavyo nami nilidanganywa na kuamini hivyo, unaweza kuniandikia baruapepe. Nitafurahi kumtumikia Bwana wangu Yesu katika kujibu maswali yako.

Anwani yangu ya baruapepe ni: ok2004@columbia.edu

***************
[Angalizo za blogger: Kwa kuwa ushuhuda huu nimeutafsiri kutoka kwenye Kiingereza, mwandishi wake si Mswahili. Hivyo, kama utamwandikia, ni muhimu iwe ni kwa lugha ya Kiingereza.]
***************

Kama ushuhuda huu umekubariki, tafadhali tumia muda mfupi kutushirikisha JINSI ulivyobarikiwa. Kusikia kutoka kwako ni muhimu sana. Tafadhali taja mwandishi wa ushuhuda huu na kichwa cha ushuhuda wenyewe unapotuandikia baruapepe yako. Asante sana! Baruapepe yetu ni: ptoffice@precious-testimonies.com

***************
[Angalizo za blogger: Kama utapenda kuwaandikia jinsi ulivyobarikiwa, tafadhali hapa pia tumia lugha ya Kiingereza. Jina la mwandishi wa ushuhuda, kama ulivyoona mwanzoni, halikutajwa. Lakini kichwa cha ushuhuda ni “I Felt Betrayed by God”]







James at 6:32 PM
Share
13 comments:

AnonymousOctober 16, 2012 at 9:38 PM
I will immediately snatch your rss feed as I can not to find your email subscription hyperlink or e-newsletter service. Do you’ve any? Please permit me understand in order that I could subscribe. Thanks.

Reply

AnonymousOctober 20, 2012 at 6:31 AM
Can I just say what a relief to find someone who actually knows what theyre talking about on the internet. You definitely know how to bring an issue to light and make it important. More people need to read this and understand this side of the story. I cant believe youre not more popular because you definitely have the gift.

Reply

JamesOctober 29, 2012 at 7:21 AM
Hello.

I am glad to see your comments. Sorry for my missing my rss feed.

May I say that I really am not yet very competent in blogging, so there are many things that i still don't understand how to manipulate them - even though they may be very easy for others.

One of the things is this RSS. Another is comments. I have been trying to set this blog in a way that allows Threaded Comments. I havent been able to do it so far.

So, please, bear with me as I go on learning how to do these things. By the grace of God, I will find someone who will help me to sort them out.

May the Lord bless you.

Reply

AnonymousApril 27, 2013 at 5:57 AM
I don't even know how I ended up here, but I thought this post was good. I don't know who you are but certainly you are going to a famous blogger if you aren't already 😉 Cheers!

my blog creative group

Reply
Replies

JamesApril 27, 2013 at 1:59 PM
Thanks. Be blessed.

Reply

AnonymousJune 4, 2013 at 7:47 AM
Hi there to every body, it's my first go to see of this webpage; this blog contains remarkable and actually excellent information for visitors.

my blog post - email newsletters templates

Reply

AnonymousJune 13, 2013 at 8:55 PM
Thank you for the good writeup. It in fact was a amusement
account it. Look advanced to far added agreeable from you!
However, how can we communicate?

Also visit my webpage: simply click the up coming website page

Reply
Replies

JamesJune 14, 2013 at 9:01 PM
Hi. You seem to have written so many comments. But you hardly say anything specifically referring to the topic in question. You are very vague.

Reply

UnknownApril 22, 2014 at 12:57 AM
Mmh mtumishi James. Ushuhuda huu ni mzito sana na bila roho mtakatifu kukupa mafunuo huwezi elewa kitu. Nimeona alivyo identify siri za kipepo katika kucontrol maisha ya kikistro kwa njia ya uwongo.naomba clarification zifuatazo
1. Inamaana kupiga mziki katika maombezi au vyombo vya mziki,au kusifu na kuabudu wakati wa kufanya maombezi au kabla ya maombezi according ulivyotafisiri ni kuamsha hisia wala hakuna uwepo wa Mungu?
2. Mwandishi anasema kuna wakati aliingia katika mtego wa kishetani kuingia katika website ya kishetani sasa je kusudi tusije kurudia makosa wewe binafsi ulishafanyia kazi hii mitandao ya precioustestmonies.com,gospel.com.net ya mwisho hiyo ni kucheki kama neno hilo ulilolipata ni la kweli au laah.Na je njia nzuri ni kutegemea iyo website ya kuclarify kama neno ilo la ukweli au kushirikisha wachungaji wetu.
3. Anachofundisha uyu bwana kutokana na alichopitia haya mafunzo hata mimi yaani. Precaution! Lakini jee tunajaribu vip kila neno linalotoka kila kwa nabii.au mafunzo au kitu chochote. Je how do u test? Biblia imetoa precaution kuwa tutest according to maandiko. Lkn tuna test vip? yes nisaidie hayo kwanza.

Reply
Replies

UnknownApril 25, 2014 at 2:35 AM
Ndugu James. Bwana Yesu asifiwe. Pole na majukumu. Najua upo bize. Lakin pia hujui jinsi hii blog ilivyoongeza nguvu ya Mungu ndani yangu. Yan kuna siku nitatoa shuhuda. Pia naomba unijibu hayo maswali hapo juu. Barikiwa na bwana


JamesApril 25, 2014 at 8:24 AM
Shalom Joseph,


UMEULIZA KUHUSU KUPIGA MUZIKI:
Biblia inaongelea sehemu nyingi kuhusu kumwimbia Bwana na pia kumpigia muziki tena kwa vyombo mbalimbali. Kwa mfano:
MWIMBIENI Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake. (Zaburi 30:4)


MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo. (Isaya 42:10)


Haleluya. MWIMBIENI Bwana wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa. Israeli na amfurahie Yeye aliyemfanya, Wana wa Sayuni na WAMSHANGILIE mfalme wao. Na WALISIFU jina lake kwa KUCHEZA, KWA MATARI NA KINUBI WAMWIMBIE. Kwa kuwa Bwana awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu. (Zaburi 149:1-4)


Anachoongelea huyu dada mwenye ushuhuda huu sio KATAZO la kumwimbia Bwana na kumpigia. Hebu tuanze kwa kuangalia mfano huu:
“Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mpya na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada. Sikukuu zenu za mwezi mpya na karamu zenu zilizoamriwa, nafsi yangu yazichukia; mambo hayo yanilemea; nimechoka kuyachukua.” (Isaya 1:13-14).


Mungu ndiye aliyeagiza kwenye agano la kale watu washerehekee sikukuu kadhaa na kutunza sabato. Iweje basi aongee hapa kwa kuyachukia kiasi hiki mambo yaleyale ambayo aliyaagiza mwenyewe?


Kumbe tunaona tatizo haliko kwenye maagizo menyewe, bali ni hapa:
“Msilete tena matoleo ya UBATILI.”


SIKU ZOTE, iwe ni sadaka, msaada, sala, n.k., hukubalika mbele za Mungu kutokana na hali ya moyo ya mwanadamu (attitude towards God). Yaani, unachofanya, unafanya kwa sababu gani?


Je, unaenda Kanisani kumwabudu Mungu au unaenda tu kuburudishwa na magitaa na muziki mtamu kwa sababu ya shida zako na mawazo na huzuni ulizo nazo. Ni wazi kuwa muziki ni kitu kinachoamsha hisia za watu. Lakini NJE YA HAPO, uhusiano wako na Mungu ukoje?


Uhusiano na Mungu unatakiwa kuwa ni jambo la kudumu – kila saa kila sekunde. KILA unalosema, unalowaza na unalotenda ni lazima ujiulize kama Bwana analiridhia.


“Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” (Kol 3:17)


Mtu mwenye mtazamo huu, hawezi kutenda jambo ovu kwa sababu eti hakuna mtu anayemwona; maana hofu yake haiku kwa wanadamu bali kwa Bwana. Wakati wote anakuwa aware kwamba jicho la Bwana linamwangalia. Na siku zote anatafuta kumpendeza Bwana.


Kwa hiyo, mtu wa hivi, hata muziki wa Kanisani ukipigwa, yeye anapoimba, anapocheza, anakuwa anafanya hivyo kwa ajili ya Bwana – SIO KWA AJILI YA KUTAFUTA FARAJA KWA SABABU ALIGOMBANA NA MUME AU MKE WAKE NYUMBANI.


NJE YA HAPA, kuimba au kucheza kwetu muziki ni UBATILI na machukizo mbele za Bwana. Na ndicho anachokikataa kwa hasira Bwana hapo juu kwenye Isaya 1 – yaani: “MSILETE MATOLEO YA UBATILI.


Kwa maana nyingine: LETENI MATOLEO LAKINI SITAKI MATOLEO YA UBATILI.


JamesApril 25, 2014 at 8:26 AM
UMEULIZA KUHUSU MTEGO WA KUINGIA KWENYE WEBSITE ZA KISHETANI

Unaposoma ushuhuda huu, unatambua jambo moja kwamba – alipita kwenye kipindi fulani cha uchanga wa kiroho. Alikuwa ni mtu anayemtafuta Mungu, lakini alikuwa katika ile hatua ambayo MTU HUWA ANAWAZA KUWA NI LAZIMA MUNGU ANIPE KILA NIOMBACHO KWA WAKATI NITAKAO KWA KUWA NIMEOMBA.

Kisha akicheleweshwa kidogo; au akitikiswa kidogo na jaribu, anatetereka na kumwacha Bwana. Huu ni uchanga wa kiroho.

Mtu anayemjua Bwana na amesimama sawasawa na amekua kiroho ana msimamo wa Shadraki, Meshaki na Abednego:
Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. BALI KAMA SI HIVYO, UJUE, EE MFALME, YA KUWA SISI HATUKUBALI KUITUMIKIA MIUNGU YAKO, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. (Danieli 3:17-18).

Anajua kuwa Mungu ni MWAMINIFU TU, hata kama mambo yanaonekana hayaendi sawa kama alivyoomba au kutarajia. Mtu wa aina hii anakuwa amesimama kwenye Mwamba usiotikisika.

Na Yesu anasema wazi:
“Tazama nimewapa amri (authority) ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, WALA HAKUNA KITU CHOCHOTE KITAKACHOWADHURU.” (Lk 10:19).

Ukiwa umesimama sawasawa na Yesu hakuna kazi YOYOTE YA KUZIMU itakayokushinda – iwe ni website ya wachawi au ya ibilisi mwenyewe. Lakini bila hivyo, ni rahisi na inawezekana kabisa kuathiriwa au kudhuriwa kama ilivyokuwa kwa huyu dada.


JamesApril 25, 2014 at 8:27 AM
UMEULIZA KUHUSU KUZIJARIBU ROHO

Kuzijaribu roho, kunahitaji mambo makuu mawili.

Kwanza ni lazima ujenge uhusiano wako na Yesu (Roho Mtakatifu) SIKU HADI SIKU – kuomba, kusoma Neno lake na kumtii kadiri anavyokuongoza. Na katika utendaji (real practice) tu ndipo unaweza kujifunza KIBINAFSI kutambua sauti ya Roho Mtakatifu – wengine husikia sauti wazi kama ilivyo kwa huyu dada, na wengine inakuwa tu kama wazo linakujia. With time unakuwa unaweza kutofautisha kati ya Roho Mtakatifu na mawazo binafsi – si kitu unachoweza kukijua sawasawa kutokana na maelezo ya mtu mwingine.

Kondoo wangu WAISIKIA SAUTI YANGU; nami nawajua, nao wanifuata. (Yoh 10:27).


Ukiwa mtii kwa Bwana, kweli kabisa hatakuacha upotee. Si kwamba hautaingia kwenye matatizo – NI LAZIMA ATAKUPITISHA HUKO. LAZIMA! Lakini kwa kuwa una tunda la Roho, UVUMILIVU utakutunza hadi wakati wa kujibiwa kwako kwa kuwa UNAMWAMINI Bwana; na Bwana ni mwaminifu.

Pili, ukishakuwa na Neno la kutosha ndani yako – ndipo kila jambo unalosikia, wazo linalokujia, n.k., unaweza kujua kuwa ni la kweli au si la kweli kwa sababu ama linakubaliana na Neno la Mungu au linapingana nalo. Kama linapingana na Neno la Mungu, hiyo ni roho ya uongo hata kama anayesema jambo hilo ni askofu au mchungaji wako.

Reply





Home
View web version
About Me
View my complete profile
Powered by Blogger.
 
Hivi tunajua ya kwamba hata Shetani na mapepo yote yana mkiri kuwa Yesu Kristo ni BWANA ni Mungu ni mwokozi,na kumuamini kuwa ni mwakozi na ni mwana wa Mungu na ni Mungu na mwenye nguvu na mamlaka yote.
Na tena mapepo si kwamba yana mkiri,na kumuamini tu tu,na ila KWA KUTETEMEKA NA KUMUOGOPA .
Neema tuliyoipata kwa imani baada ya kumkiri Yesu na kumuamini ,hiyo neema inatukataza kudumu kuendelea kudumu katika dhambi uovu ili eti neema izidi kuongezeka??
hiyo neema inatufundisha kuukataa na kuacha uovu wote..kusulubisha tamaa mbaya za miili yetu na mawazo yetu mabaya..
TUISHI MAISHA YA UTAKATIFU ambayo ndio tiketi ya kuingia mbinguni..
asikudanganye mtu kuwa duniani hakuna mtakatifu na hutaweza kuishi bila kutenda dhambi kwamba wewe fanya dhambi tu kama kawaida halafu baade ukishamaliza kutenda dhambi ukatubu kwa vile neema ipo tu..unnatubu dhambi leo kesho unarudia kutenda dhambi hiyo unatubu kesho kutwa unarudia mzunguko unajirudia??
Neema ya Mungu inatufundisha kuuacha uovu katika maisha yetu haya ya sasa hivi wakati tukiwa duniani baada ya kufa ni hukumu.
Maandiko yanasema tutakuwa watakatifu duniani hapa hapa duniani.
Maandiko yanakataza sisi kuendelea kudumu katika dhambi ili neema izidi.

MSINGI MKUBWA wa Yesu kufa msalabani ni ili TUACHE DHAMBI(MAUTI) tupate UZIMA (UTAKATIFU) tuwe warithi wa uzima wa milele ndio kuokolewa.
Kama bado tunaishi chini ya utumwa wa dhambi tunatumikia dhambi ina maana bado Yesu hajawa Bwana kwetu hatujakombolewa utumwani(dhambini/mautini).
IMANI PEKEE ya kumkiri Yesu hata shetani ana amini Yesu ni Mungu/BWANA/MFALME WA WAFALME. tena kwa kutetemeka na kuogopa.
imani pekee bila kuacha dhambi na kuwa mtakatifu ,kutenda mema,kusikia sauti ya Mungu na kutii sauti ya Mungu(MATENDO) hiyo imani haifai kitu/imekufa.

LENGO KUU la msingi kwetu tunalotakiwa kufanya moja kubwa NI KUACHA DHAMBI(UTAKATIFU)baada ya kumkiri Yesu na kumwamini linaloendana sambba na hilo huwezi kumkiri na kumuamini tu Yesu halafu basi ukaendelea na maisha yaleyale ya dhambi.
 
HATARI: SIRI ZILIZOFICHWA ZINAZOENDELEA KUBADILI BIBLIA :-
LAZIMA USOME IKIWA WEWE NI MWFUASI WA KWELI WA KRISTO

Ni ushuhuda wa ajabu na wa kugusa sana. Tafadhali chukua muda wako na uusome hadi mwisho

MABADILIKO YA MISTARI YA BIBLIA
( MISTARI YA BIBLIA ILIYOCHAKAKULIWA )
Na Amina Hassan

▪️. Baadhi ya Mistari ya Biblia Iliyoharibiwa au Kufutwa.
1 - Yohana 3:16.
2 - Yohana 14:6.
3 - 1 Timotheo 2:5
4 - Matendo 4:12.
5 - Warumi 10:9.
6 - 1 Yohana 5:7.

USHUHUDA

Jina langu ni Amina Hassan na kwa sasa nipo Amman, Jordan. Nina umri wa miaka 34. Miezi minne tu iliyopita, nilikuwa nikiishi maisha tofauti kabisa huko Riyadh, Saudi Arabia, nikifanya kazi kwa shirika ambalo watu wengi hata hawajui lipo.

Lakini nahitaji kuwaambia kila kitu kwa sababu imani yenu, Biblia yenu, na ufahamu wenu wa Neno la Mungu huenda tayari umeathiriwa bila hata kujua.

Kwa miaka mitatu, nilifanya kazi gizani nikibadilisha Neno la Mungu lenyewe. Tulichapisha zaidi ya Biblia bandia milioni moja na kuzisambaza duniani kote.

Lakini mstari mmoja niliopangiwa kuuharibu ukawa ndiyo kitu kilichookoa roho yangu . Jina langu lipo kwenye orodha ya watu wa kuuawa kwa sasa. Na wakinipata, nitauawa.

Unachokaribia kusoma si SHUHUDA yangu tu. Ni onyo kwa kila Mkristo duniani. Tunahitaji kuombeana na kukaa macho pamoja.

Nilizaliwa na kukulia Riyadh kama Muislamu mwaminifu. Familia yangu ilikuwa ya wastani katika dini, si kali sana, lakini waaminifu kwa Uislamu kwa kila njia. Nilisoma chuo kikuu na kusomea fasihi na isimu, nikibobea katika maandiko ya kale na kazi za tafsiri. Ujuzi wangu wa lugha, hasa Kiarabu, Kiingereza, na Kifaransa, ulinifanya kuwa wa thamani kwa njia ambazo sikuwahi kuzifikiria.

Mwezi Novemba 2021, nilifikiwa na mwanaume aliyesema anawakilisha shirika la elimu ya Kiislamu. Alinipa kazi iliyolipa mshahara mkubwa sana, zaidi ya kazi yoyote ya kawaida ya uhariri au tafsiri.

Kazi hiyo, alieleza, ilihusisha kukagua na kuhariri maandiko ya kidini ili yawe rahisi kueleweka na wasomaji wa kisasa. Ilionekana halali, hata ya heshima. Nilikubali bila kusita. Kile ambacho sikujua wakati huo ni kwamba shirika hilo liliitwa Al Fath Al Kabir, maana yake ni ushindi wa kimya.

Hili halikuwa kundi la elimu tu. Lilikuwa operesheni ya siri, yenye ufadhili mkubwa, yenye lengo moja kuu: kuufanya ulimwengu mzima kuwa dola ya Kiislamu. -- Si kwa vurugu pekee, bali kwa kupenya, udanganyifu, na uharibifu wa kimfumo wa imani nyingine kutoka ndani.

Katika mwezi wangu wa kwanza, nilitambulishwa kwa dhamira kubwa zaidi. Uongozi ulieleza kwamba kwa miongo kadhaa, mashirika ya Kiislamu yalikuwa yamefadhili mapambano ya silaha duniani kote. -- Walifadhili operesheni katika nchi kama Iran, Gaza, Nigeria, Afghanistan, Pakistan, Indonesia, Ufilipino, Mali, Somalia, Syria, na nyingine nyingi. -- Waliunga mkono mashambulizi dhidi ya Makanisa na jamii za Wakristo.

Waliamini shinikizo hili lingewalazimisha watu kujiwasilisha kwa Uislamu kwa hofu . -- Lakini baada ya miaka yote hiyo na umwagaji damu wote, waligundua jambo la kushtua. Halikuwa linafanya kazi. Kwa kweli, katika maeneo mengi, Ukristo ulikuwa ukikua kwa kasi zaidi kuliko hapo awali, hasa Afrika na Asia.

Watu waliokuwa wakishuhudia mateso ya vurugu hawakuwa wakigeukia Uislamu. Badala yake, walikuwa wakiona upendo na msamaha kwa Wakristo waliokataa kulipiza kisasi kwa chuki, na hili lilikuwa likiwavuta kwa Yesu.

Viongozi wa Al Fath Al Kabir waligundua walihitaji mkakati mpya, wa hila zaidi na wenye uharibifu mkubwa zaidi. -- Waliamua kwamba kama hawangeweza kuharibu Ukristo kutoka nje kwa nguvu, wangeuharibu kutoka ndani kwa kuharibu msingi wa imani: Biblia Takatifu yenyewe.

Mpango huo ulikuwa mbunifu katika uovu wake .

-- Wangetengeneza Biblia zinazoonekana sawa kabisa na Biblia halisi za Kikristo.

-- Jalada lilelile, wachapishaji wale wale, ubora wa karatasi ule ule, fonti zile zile, kila kitu kile kile.

-- Lakini maneno ndani yangekuwa yamebadilishwa kwa uangalifu. Sio kila neno kwa sababu hilo lingekuwa dhahiri sana.
-- Bali mistari muhimu.

-- Mafundisho ya msingi.

-- Ukweli muhimu kuhusu Yesu ni nani na wokovu unamaanisha nini.
Mabadiliko yangekuwa ya hila kiasi kwamba wasomaji wengi wa kawaida wasingetambua, lakini ya maana kiasi cha kuichafua polepole imani ya mamilioni.

Kazi yangu pamoja na wahariri na watafsiri wengine takribani thelathini ilikuwa kufanya mabadiliko haya.

Tulifanya kazi katika kituo salama huko Riyadh katika jengo ambalo kwa nje lilionekana kama ofisi ya kawaida. Lakini ndani, tulikuwa na vifaa vya kisasa vya uchapishaji, mashine za kufunga vitabu, na hifadhidata kubwa ya kila tafsiri kuu ya Biblia iliyopo.

Shirika hilo lilikuwa limepata kwa njia fulani maelfu ya Biblia halisi kutoka vyanzo mbalimbali.

-- Baadhi zilinunuliwa kutoka maduka ya vitabu ya Kikristo kwa kutumia makampuni ya kuficha.
-- Nyingine zilipatikana kutoka kwa wasambazaji wa kimataifa ambao hawakuwa na wazo tunachofanya hasa.
-- Na zingine, nilijifunza baadaye kwa hofu, ziliibwa kutoka Makanisa na jamii za Wakristo katika maeneo ambako watu wetu walikuwa na ufikiaji.

Baada ya kupata nakala halisi, kazi yetu ilikuwa kuchanganua kila ukurasa, kutambua mistari tuliyoelekezwa kubadilisha, kufanya mabadiliko, kisha kuzalisha nakala mpya zinazofanana kabisa na halisi.

Biblia halisi tulizopata ziliharibiwa, zilichomwa katika tanuru la kuteketeza taka lililokuwa chini ya jengo letu. Nilishuhudia hili mara nyingi na kila mara sikuhisi chochote. Niliamini tunafanya kazi ya haki kulinda Uislamu dhidi ya uharibifu wa Ukristo .

Kufikia Novemba 2024, tulikuwa tumezalisha zaidi ya Biblia bandia milioni moja katika tafsiri mbalimbali, matoleo ya Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiswahili, na mengine mengi.

Biblia hizi zilisambazwa kupitia njia nyingi.
-- Baadhi ziliuzwa kwa wauzaji wakubwa mtandaoni ambao hawakujua wanauza bandia.
-- Nyingine zilitumwa kwenye maduka ya vitabu ya Kikristo katika nchi zinazoendelea ambako uhakiki ulikuwa mgumu.
-- Na maelfu zaidi yaliandaliwa kama zawadi za bure kusambazwa kwa Makanisa na mashirika ya Kikristo mwaka 2025 na 2026.

Uongozi ulituambia kuwa 2026 ungekuwa mwaka wa kipekee .
-- Wanapanga kutoa mamia ya maelfu ya Biblia za bure kwa huduma za Kikristo hasa Afrika na Asia kama ishara ya nia njema ya mazungumzo ya kidini.

-- Makanisa na Wamisionari waliokuwa na uhitaji mkubwa wa Biblia na wasio na uwezo wa kununua kwa wingi wangepokea zawadi hizi kwa shukrani, bila kushuku kwamba zilikuwa zimewekewa sumu ya kiroho.

Niruhusuni niwaambie kuhusu baadhi ya mabadiliko tuliyofanya. Haya ni mambo ambayo kila Mkristo anahitaji kuyajua na kuyakagua katika Biblia zao mara moja.

1 - Katika Yohana 3:16 , moja ya mistari maarufu zaidi katika Biblia yote, maandiko ya asili yanasema: "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. " Katika toleo letu bandia, tulibadilisha ( TULICHAKACHUA ) na kusema: "Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtuma Nabii awaongoze wanadamu, na yeyote anayefuata njia iliyonyooka hatapotea bali atakuwa na amani ya milele."

Tulimwondoa Yesu kama Mwana wa Mungu na kumshusha hadhi kuwa Nabii tu.

2 - Katika Yohana 14:6 , ambapo Yesu anasema: " Yeye ndiye Njia, Ukweli na Uzima na hakuna mtu awezaye kwenda kwa Baba isipokuwa kwa Yeye . Tulibadilisha na kusema: Yeye ni njia mojawapo ya ukweli na uzima na kwamba watafutaji wa dhati watampata Baba kupitia maisha ya haki.

Tulifanya wokovu kuwa juu ya jitihada za mwanadamu badala ya imani katika Kristo pekee.

3 - Katika 1 Timotheo 2:5, inayosema wazi: "Kwa maana Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, naye ni mwanadamu Kristo Yesu" T Tulibadilisha na kusema: "Mungu ni mmoja na kuna njia nyingi za kumfikia. Kwa maana Mungu anakubali ibada ya dhati ya wote wanaomtafuta."

Tuliharibu upekee wa Kristo kama Mpatanishi.

4 - Katika Matendo 4:12 , panaposema: " Wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu lililopewa wanadamu ambalo kwalo tunaweza kuokolewa ." Tulibadilisha na kusema: "Hakuna haki nyingine chini ya mbingu isipokuwa kujisalimisha kwa mapenzi ya Mungu ambako kwayo tunaokolewa."

Tena, tulihamisha mkazo kutoka kwa Yesu kwenda kwenye jitihada za kidini za mwanadamu.

5 - Katika Warumi 10:9* , inayofundisha kwamba: **"Kwa kuwa ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka ." Tulibadilisha na kusema: "Ukikiri kwa kinywa chako kwamba Mungu ni mmoja na kuamini moyoni mwako kwamba manabii wake walinena kweli, utaokoka."

Tuliondoa ufufuo, tukamwondoa Yesu kama Bwana, na kuufanya wokovu kuwa juu ya tauhidi ya jumla.

6 - Katika 1 Yohana 5:7 , inayozungumzia: " Baba, Neno, na Roho Mtakatifu, nao watatu hawa ni mmoja. " Tulifuta kabisa maneno hayo na tukapanga upya mistari inayofuata.
Tulifuta moja ya marejeo yaliyo wazi zaidi kuhusu Utatu.

Haya yalikuwa baadhi tu ya mamia ya mabadiliko tuliyofanya katika Vitabu mbalimbali vya Biblia. Tulifanya kazi kwa mpangilio tukilenga kila fundisho kuu.
-- Uungu wa Kristo.
-- Wokovu kwa neema kwa njia ya imani.
-- Utatu. -- Ufufuo,
-- Mamlaka ya Maandiko.
Kila kitu kinachoufanya Ukristo kuwa wa kipekee.

Nilifanya kazi kwenye mradi huu kwa karibu miaka 3. Katika kipindi hicho, nilijivunia kile nilichokuwa nikifanya. Niliamini nilikuwa nikimtumikia Allah kwa kudhoofisha dini ya uongo ya Ukristo. -- Nilijiona kama askari katika vita vya haki. Hata kama sikuwahi kushika silaha, silaha yangu ilikuwa ni maneno na niliitumia kwa usahihi na kujitolea.

Lakini kila kitu kilibadilika tarehe 19 Novemba 2024. Asubuhi hiyo nilifika kazini kama kawaida. Nilipewa kazi ya kufanya tena Injili ya Yohana, hasa sura za 15–17. Msimamizi wangu aliniambia tunahitaji kurekebisha jinsi Yesu alivyoongea kuhusu Roho Mtakatifu na kuhusu uhusiano wake na Baba.
-- Walitaka kumfanya Yesu aonekane kuwa wa chini kiumungu zaidi na zaidi kama Nabii wa kawaida aliyekuwa karibu tu na Mungu.

Nilikaa mezani kwangu nikiwa na Biblia halisi upande mmoja na skrini ya kompyuta upande mwingine, tayari kufanya mabadiliko. Nilikuwa nimefanya hili mara mia nyingi bila hisia yoyote.
Ilikuwa kazi tu, uhariri tu, kubadilisha maneno kwenye ukurasa.

Lakini siku hiyo niliposoma Yohana 15, jambo fulani lilitokea ambalo hata sasa siwezi kulieleza kikamilifu .
-- Nilisoma mstari wa 5 ambapo Yesu anasema kwamba: "Yeye ndiye mzabibu nasi ni matawi; akaaye ndani Yake naye ndani yake huyo huzaa sana, kwa maana pasipo Yeye hatuwezi kufanya neno lolote. "

Niliposoma maneno hayo, kitu fulani ndani ya kifua changu kilihisi kama kimepasuka.
-- Ghafla nilijiona wazi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi.
-- Niliona kile nilichokuwa nikifanya kweli.
-- Sikuwatumikia ukweli.
-- Nilikuwa nikiiangamiza. -- Sikuwatetea imani.
-- Nilikuwa nikishambulia uhusiano wa watu na Mungu. Na maneno niliyokuwa nimeyasoma yalinigonga kwa nguvu isiyoelezeka.

Bila Yesu, sikuweza kufanya chochote chenye thamani ya kweli
--. Bila Yeye, nilikuwa nimekufa kiroho.
Machozi yalianza kunitiririka usoni mwangu bila onyo. Nilijaribu kuyazuia, nikiogopa sana mtu angeona ninilia mezani kwangu. Nilifuta macho yangu haraka na kuendelea kusoma, nikiwa siwezi kujizuia.

Nikaendelea hadi sura ya 16 ambapo Yesu anazungumza kuhusu Roho Mtakatifu akimwita Roho wa Kweli atakayewaongoza waumini katika kweli yote..

Kisha nikasoma sura ya 17: ombi la Yesu kwa wanafunzi wake na kwa wote watakaoamini kupitia ujumbe wao. Katika mstari wa tatu wa sura ya 17, Yesu anaomba na kufafanua uzima wa milele. Anasema: Uzima wa Milele ni kumjua Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Niliposoma maneno hayo, nilielewa jambo la kina sana. Uzima wa Milele haukuwa juu ya kufuata sheria au kutimiza majukumu ya kidini . -- Ulikuwa juu ya kumjua Mungu binafsi na kumjua Yesu anayemfunua Baba kwetu. Hili lilikuwa tofauti kabisa na kila kitu nilichokuwa nimefundishwa katika Uislamu.

Niliyafumba macho yangu na kwa mara ya kwanza maishani mwangu, nikaomba si kwa Allah bali kwa Yesu huyu ambaye nilikuwa nikibadilisha maneno Yake.
Sikujua jinsi ya kumwomba. Wakati huo huo kabisa, nilihisi kitu ambacho sikuwahi kukipata kabla. Ilikuwa kama nuru ya joto ilimwagika ndani ya kifua changu na kusambaa mwilini mwangu wote.

-- Nilihisi amani, ya kina na kamili, kana kwamba nilikuwa nimebeba mzigo mzito maisha yangu yote na mtu alikuwa ameunyanyua mabegani mwangu.

-- Nilihisi kupendwa kwa namna ambayo siwezi kuieleza kwa maneno. Sio kupendwa kwa sababu ya nilichofanya au jinsi nilivyofuata sheria za kidini, bali kupendwa kwa sababu tu nilikuwepo, kwa sababu nilikuwa wa thamani kwa Mungu.

Nilijua katika wakati huo kwa uhakika kamili kwamba Yesu Kristo ni halisi.
-- Yuko hai. -- Yeye ni Mwana wa Mungu.
-- Na Alikuwa amejifunua kwangu pale pale katikati ya ofisi yangu wakati nilipaswa kuwa nikiharibu Neno Lake.

Nilikaa nikiwa nimeganda mezani kwangu, nikiwa nimezidiwa na kile kilichokuwa kinanitokea.
-- Sikujua nifanye nini.
-- Sikuweza kumwambia mtu yeyote.
-- Sikuweza kuacha kazi au ningevutia tahadhari.
Kwa hiyo, nilikaa pale nikijifanya nafanya kazi wakati mtazamo wangu wote wa ulimwengu ulikuwa ukipinduliwa kabisa.

Kwa wiki mbili zilizofuata, nilikuja kazini kila siku na kujifanya kila kitu kiko kawaida. Lakini kwa siri, nilianza kusoma Biblia halisi tuliyokuwa nayo kwenye hifadhidata yetu, toleo la asili lisiloharibiwa.
-- Nilisoma Injili kuanzia mwanzo hadi mwisho.
-- Nilisoma kuhusu kuzaliwa kwa Yesu.
-- Mafundisho yake.
-- Miujiza yake.
-- Upendo wake kwa watu waliovunjika.
-- Kifo chake Msalabani, na Ufufuo wake.
Kila Neno lilihisi kama maji kwa roho yangu iliyokuwa na kiu.

Nilianza pia kulinganisha mabadiliko tuliyokuwa tumefanya na maandiko ya asili, na nilishtushwa na kile nilichokiona. -- Tulikuwa tumemwondoa Yesu kimfumo kutoka katika hadithi Yake mwenyewe. -- Tulikuwa tumeigeuza Injili kuwa kanuni ya maadili ya kidini tu.
-- Tulikuwa tumeiba kutoka kwa mamilioni ya watu Ukweli unaoweza kuwaweka huru.

Nilijua nisingeweza kuendelea na kazi hii. Lakini pia nilijua nisingeweza kuacha tu bila kuibua mashaka. Kama wangekugundua nilikuwa nimegeukia Ukristo, wangenifanya nife.

Shirika hili halikuvumilia usaliti. Na kuacha Uislamu kwa Ukristo ilikuwa usaliti wa hali ya juu kabisa machoni mwao .
-- Nilianza kwa siri kunakili faili kutoka kwenye hifadhidata yetu kwenda kwenye USB ndogo ndogo.

Niliandika kila kitu.
-- Orodha ya mistari iliyobadilishwa.
-- Njia za usambazaji.
-- Majina ya maduka ya vitabu na wauzaji mtandaoni waliokuwa wakipokea Biblia zetu bandia.
-- Mpango wa usambazaji wa 2026, kila kitu.
Nilijua taarifa hizi zilihitaji kuwafikia Wakristo duniani kote ili wajilinde na kuzikagua Biblia zao.

Lakini tarehe 3 Desemba 2024, ulimwengu wangu ulianguka. Mmoja wa wafanyakazi wenzangu aligundua kuwa nilikuwa nikitumia muda mwingi kusoma faili za Biblia halisi badala ya kufanya mabadiliko niliyopangiwa. -- Alinitoa taarifa kwa msimamizi wetu akisema nilikuwa nikitenda kwa njia isiyo ya kawaida na nilionekana nikiwa na mawazo mengi.

Mchana huo, niliitwa kwenye kikao na viongozi watatu wakuu wa shirika. Walinihoji kwa zaidi ya saa moja:
-- Wakiuliza kwa nini nilikuwa nikisoma maandiko ya Kikristo kwa makini sana, kama nilikuwa na mashaka kuhusu dhamira yetu. -- Kama nilikuwa nimewasiliana na Wakristo wowote.

Nilijaribu kudanganya, nikajaribu kuwashawishi nilikuwa ninafanya kazi yangu kwa umakini tu, lakini hawakuniamini. Walichunguza dawati langu na wakakuta mojawapo ya USB ambazo sikuwa bado nimezificha nje ya jengo.

Walipoona kilichokuwa ndani yake, nyuso zao zikawa baridi.
-- Walijua mara moja kwamba nilikuwa nimewasaliti.

Walinipeleka kwenye chumba kilichokuwa chini ya jengo, chumba ambacho sikujua hata kilikuwepo. Kilikuwa seli ndogo ya zege, haina madirisha, na ina balbu moja tu iliyoning’inia kutoka kwenye dari.

-- Walinifungia ndani na kuniambia nitakaa hapo hadi nitakapokiri kila kitu na kuikana mawazo yoyote ya kijinga yaliyoingia kichwani mwangu.
-- Kwa siku tatu, niliwekwa katika seli hiyo bila chakula cha kutosha na maji kidogo sana.
-- Walikuja mara kwa mara kunihoji, kunitishia, kuniambia kitakachonipata nisiposhirikiana.

Walisema nilikuwa nimetenda uhaini dhidi ya Uislamu.
-- Walisema nilikuwa nimewasaliti watu wangu na imani yangu.
-- Walisema familia yangu ingeona aibu kwa sababu yangu.

Siku ya pili, walianza kunipiga.

-- Wanaume wawili waliingia selini na kunipiga mara kwa mara, wakipiga uso wangu, tumbo langu, mgongo wangu. -- Walinivuta nywele na kugonga kichwa changu kwenye ukuta wa zege. Maumivu yalikuwa makali kupita kiasi. Nilipiga kelele na kulia na kuwaomba waache, lakini hawakuacha.

Waliniambia hii ilikuwa mwanzo tu, kwamba mambo yangekuwa mabaya zaidi nisipomkana Yesu na kurudi kwenye Uislamu . Lakini hata walipokuwa wakinipiga, hata damu ilipokuwa ikitiririka usoni mwangu na mwili wangu ukiuma kwa maumivu, nilihisi ile ile amani niliyohisi Yesu alipojifunua kwangu mara ya kwanza.

-- Nikakumbuka Maneno Yake katika Injili: Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wao. -- Nikakumbuka kwamba Yeye mwenyewe alipigwa, alidhihakiwa, na akasulubiwa, na kwamba aliwaahidi wafuasi Wake wangekutana na mateso kama hayo.

Kwa hiyo nilivumilia. Nilikataa kumkana. Kila waliponidai nimkane Yesu, nilikaa kimya au nikasema kwa sauti ya chini kwamba Yesu ni Bwana. Hili liliwakasirisha zaidi.

Siku ya nne, tarehe 6 Desemba, waliniambia nitauawa.
-- Walisema uamuzi ulikuwa umefanywa katika ngazi za juu kabisa za shirika. Nilikuwa hatari sana kuachiwa huru na mkaidi sana kurudi nyuma. Wangenifanya nife kama onyo kwa mtu mwingine yeyote ambaye angefikiria kuisaliti dhamira.

Waliniambia mauaji yangetokea asubuhi iliyofuata, tarehe 7 Desemba, kwa kukatwa kichwa.
-- Wangesema ingekuwa ya haraka, karibu kama huruma.
-- Kisha wangeutupa mwili wangu mahali ambapo usingepatikana kamwe, na wangeiambia familia yangu nilikimbia na kutoweka.

Usiku huo, peke yangu selini, niliomba kama ambavyo sikuwahi kuomba kabla. Nilimshukuru Yesu kwa kujifunua kwangu.

-- Nilimshukuru kwa zawadi ya kumjua, hata kama ilikuwa kwa wiki chache tu. -- Nilimwambia nilikuwa tayari kufa kama hiyo ilikuwa Mapenzi Yake.

-- Na nikamuomba autumie kifo changu kwa namna fulani kwa utukufu Wake na kuwalinda Wakristo wengine dhidi ya Biblia zenye sumu tulizokuwa tumezitengeneza.

Lakini pia niliomba muujiza. Nilimuomba kama ingewezekana kuniokoa, kunikomboa ili niweze kufichua kile ambacho shirika hili lilikuwa likifanya na kuwaonya waumini duniani kote.

Sijui ilikuwa saa ngapi, lakini katikati ya usiku, nilisikia sauti nje ya seli yangu. Kulikuwa na makelele, mbio za miguu, na kisha kitu kilichosikika kama milio ya risasi. Nilijibanza kwenye ukuta wa nyuma wa seli, nikiwa na hofu na kuchanganyikiwa.

Ghafla, mlango wa seli yangu ulipasuka. Akiwa amesimama hapo alikuwa mwanaume ambaye sikuwahi kumwona kabla, akiwa amevaa nguo nyeusi na ameshika bunduki.

-- Alizungumza nami haraka kwa Kiarabu, akiniambia niondoke naye mara moja kama nilitaka kuishi.
-- Sikuelewa kilichokuwa kikitokea, lakini nilijua hii ilikuwa nafasi yangu pekee. Nilimfuata kutoka selini na kupitia korido ambazo sikuwa nimeziona kabla.

Jengo lilikuwa katika vurugu. Kulikuwa na miili sakafuni, baadhi yao wakiwa ni wafanyakazi wenzangu wa zamani.

Baadaye nilijifunza kwamba kikundi pinzani ndani ya idara ya ujasusi ya Saudi kilivamia kituo hicho kwa sababu ambazo bado sizielewi kikamilifu. -- Katika machafuko ya operesheni yao, mwanaume huyu ambaye ninaamini alikuwa Mkristo aliyekuwa akifanya kazi ndani ya huduma za ujasusi alinipata na akaamua kunisaidia kutoroka.
-- Aliniongoza hadi kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nyuma ya jengo. Ndani kulikuwa na mwanamke aliyenipa abaya nyeusi kamili na niqab ili nijifiche kabisa.

Waliniendesha kunitoa Riyadh usiku huo huo kupitia barabara za nyuma na vituo vya ukaguzi ambapo vitambulisho vya mwanaume huyo vilituruhusu kupita bila ukaguzi wa kina.

Walinipeleka kwenye nyumba salama huko Hefer Albatine, mji karibu na mpaka wa Kuwait.
-- Nilikaa hapo kwa wiki mbili walipokuwa wakipanga nyaraka zangu.

Katika kipindi hicho, mwanamke huyo aitwaye Salma alifichua kwangu kwamba yeye pia alikuwa Mkristo wa siri aliyekuwa ameokoka miaka iliyopita na kwamba kulikuwa na mtandao mdogo wa waumini wa chini kwa chini waliokuwa wakisaidiana kuishi Saudi Arabia. Salma alinieleza kwamba Al Fath Al Kabir ilikuwa ikinitafuta kila mahali.

-- Walikuwa na mawasiliano ndani ya polisi na huduma za ujasusi. Walijua nilikuwa nimekimbia na walijua nilikuwa nimebeba taarifa hatari.

Picha yangu ilikuwa ikisambazwa miongoni mwa watu wao. Kama ningebaki Saudi Arabia, ningepatikana na kuuawa ndani ya wiki chache.

Tarehe 21 Desemba 2024, walinisafirisha kwa magendo kuvuka mpaka kwenda Jordan. Ilikuwa ya kutisha, nikijificha nyuma ya lori, nikishikilia pumzi yangu tulipokuwa tukipita vituo vya ukaguzi.
Lakini Mungu alinilinda na nikafika salama Amman.

Tangu kufika Jordan, nimekuwa nikihama hama, nikikaa na familia mbalimbali za Kikristo ambazo kwa wema wao wamenisaidia licha ya hatari.

Siwezi kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu kwa sababu Al Fath Al Kabir ina watu wanaonitafuta.
-- Hata hapa ninaishi katika hofu ya kudumu nikijua kwamba wakinipata watanifanya nife kwa kuacha Uislamu na kwa kusaliti dhamira yao.

Lakini hata katika hofu hii nina furaha.
-- Nimeupata ukweli.
-- Nimempata Yesu. Na ningependelea kuishi siku moja nikimjua na nikifuatwa kuliko kuishi miaka 100 katika raha nikitumikia uongo.

Bado nina baadhi ya taarifa nilizonakili kutoka kwenye hifadhidata ya shirika.
-- Nina orodha za mistari iliyobadilishwa, ingawa si kamili kwa kila mabadiliko yote.
-- Nina majina ya baadhi ya njia za usambazaji, ingawa sijui kama bado zinatumika au kama shirika limebadilisha mbinu zake baada ya kutoroka kwangu.

Hii ndiyo sababu nashiriki ushuhuda wangu. Ninahitaji Wakristo kila mahali wasikie onyo hili. Tafadhali, nawasihi, kagueni Biblia zenu kwa makini. Linganisha mnachokipata na vyanzo vya kuaminika vilivyoanzishwa.

Kama ulinunua Biblia hivi karibuni, hasa kama ilikuwa ya bei isiyo ya kawaida au ulipewa bure, tafadhali hakiki kwamba maandiko ni sahihi. Kagua mistari niliyotaja awali.
-- Kagua Yohana 3:16.
-- Yohana 14:6.
-- 1 Timotheo 2:5.
-- Matendo 4:12.
-- Warumi 10:9,
-- 1 Yohana 5:7.

Hii ni baadhi tu ya mistari tuliyolenga, lakini kuna mingine mingi.

-- Kama Biblia yako inasema kitu chochote tofauti na kile ambacho Wakristo wamefundishwa na kuamini kwa miaka 2,000, kama Yesu anaonyeshwa kama Nabii tu, au kama wokovu unafanywa kuwa juu ya jitihada za mwanadamu badala ya neema, huenda unashikilia mojawapo ya bandia zetu.

Tafadhali shiriki onyo hili na MAKANISA yenu, na WACHUNGAJI wenu, na MADUKA ya vitabu ya Kikristo na wachapishaji.

-- Usambazaji wa Biblia hizi za uongo bado unaendelea. Nyingine zaidi zinazalishwa hata sasa.
-- Mpango wa 2026 bado unaendelea isipokuwa mtu au kitu kitasimamisha.

Pia nawaomba muniombee. Niombeeni usalama wangu ninapojificha dhidi ya wale wanaotaka kuniua.

-- Ombeni nipate njia ya kwenda nchi ambayo nitaweza kupata hifadhi ya kudumu na kuishi bila kuangalia bega langu kila wakati.

-- Ombeni kwa ajili ya familia yangu iliyobaki Saudi Arabia ambayo siwezi kuwasiliana nayo tena kwa sababu ingewatia hatarini.

Na tafadhali waombeeni Wakristo wengine wanaoteswa hivi sasa Saudi Arabia, Yemen, Iran, Afghanistan, Pakistan, Somalia, Nigeria , na maeneo mengine mengi.

-- Waombeeni walio gerezani kwa ajili ya imani yao.
-- Waombeeni wanaoteswa.
-- Waombeeni wanaokabili kifo kwa kumfuata Yesu.

Kuna jambo jingine lazima niwaambie, jambo ambalo limekuwa zito moyoni mwangu. Shirika lililoniajiri, Al Fath Al Kabir, bado linaendelea kufanya kazi. Walipoteza kituo kimoja katika uvamizi ulioniruhusu kutoroka. Lakini wana vingine. Wana rasilimali, fedha, miunganisho, na dhamira.

-- Hawajaacha dhamira yao ya kuharibu Biblia na kuuangamiza Ukristo kutoka ndani.
-- Hii ina maana kwamba kila Mkristo anahitaji kuwa macho.
-- Usidhani kwamba kwa sababu Biblia ina jina la mchapishaji linalojulikana, basi ni halisi moja kwa moja.
-- Wabunifu wa bandia wanaweza kunakili kila kitu, ikiwemo nembo za wachapishaji na taarifa za hakimiliki.
-- Usidhani kwamba kwa sababu uliinunua kutoka duka unaloliamini basi lazima iwe ya kweli.

Maduka mengi ya vitabu hayatambui kwamba yanauza bandia kwa sababu bandia hizo zinafanana sana.
-- Ulinzi bora ni maarifa.
-- Jua kile Biblia inachofundisha kweli.
-- Jua Mafundisho ya Msingi ya Ukristo: Kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu kamili na Mwanadamu kamili.
-- Kwamba wokovu unakuja tu kupitia imani katika Yeye na kazi Yake iliyokamilika Msalabani.
-- Kwamba alifufuka katika wafu siku ya tatu.
-- Kwamba Mungu ni mmoja katika Nafsi Tatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
-- Kwamba Biblia ni Neno la Mungu lililoongozwa na lenye mamlaka.

Ukipata Biblia inayopingana na kweli hizi, ikatae mara moja.
-- Usiiweke nyumbani kwako.
-- Usiiache ikuchanganye au kudhoofisha imani yako.
-- Iharibu na ibadilishe na Biblia halisi kutoka chanzo kilichothibitishwa.

Pia nataka kusema kitu kwa Waislamu ambao huenda wanasoma au kusikia ushuhuda huu. -- Siwachukii.
-- Nilikuwa mmoja wenu.
-- Ninaelewa uaminifu mnaohisi kwa Uislamu.
-- Ninaelewa unyofu wa sala zenu na hamu yenu ya kumtumikia Mungu. Lakini ninawaambia ukweli ninaposema kwamba Yesu Kristo ndiye Njia ya kumjua Mungu binafsi.
-- Yeye si Nabii tu.
-- Yeye ni Mwana wa Mungu aliyekuja duniani, akaishi maisha makamilifu, akafa kwa ajili ya dhambi zetu, na akafufuka ili kutupa Uzima wa Milele.
Huu si upotoshaji wa ujumbe wa Mungu.
-- Huu ndio ujumbe wenyewe.

Nilimkuta Yesu kwa njia ya ajabu kabisa wakati nilikuwa nikijaribu kwa hakika kuharibu Neno Lake.
-- Lakini Yeye alinipata.
-- Alijifunua kwangu.
-- Alinisamehe kwa kila kitu nilichokuwa nimefanya.
-- Naye alinipa amani na furaha ambayo sikuwahi kujua ipo.

Kama unatafuta Ukweli, kama kuna kitu moyoni mwako kinachosisimka unaposoma haya, usikipuuze. Huyo ni Yesu anayekuita Kwake. Unaweza kumjua. Unaweza kuwa na uhusiano na Mungu aliye hai, si kwa msingi wa utendaji wako au majukumu ya kidini, bali kwa neema na upendo Wake kwako.
-- Najua gharama ya kumfuata Yesu unapokuja kutoka katika asili ya Kiislamu.
-- Ninaishi gharama hiyo sasa hivi, lakini pia najua inastahili.
-- Yeye anastahili kila kitu.

Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, nataka niongee na mioyo yenu. Vita tulivyo navyo si vya mwili tu. Ni vya kiroho.
-- Adui anataka kuharibu imani katika Yesu Kristo na atatumia kila njia iwezekanayo kufanya hivyo. Vurugu, mateso, udanganyifu, uharibifu wa maandiko, yote haya ni silaha katika hazina yake.

Lakini tuna kitu chenye nguvu zaidi.
-- Tuna ukweli.
-- Tuna Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu.
-- Tuna Neno halisi la Mungu ambalo haliwezi kuangamizwa kabisa haijalishi nakala bandia ngapi zitatengenezwa.

Kaa macho, jaribu kila kitu, shikilia lililo jema, na uombe bila kukoma kwa ajili ya waumini duniani kote wanaoteseka kwa ajili ya Jina la Yesu.

-- Niombeeni ninapoendelea kujificha na kukimbia.
-- Waombeeni Kanisa la chini kwa chini nchini Saudi Arabia linalohatarisha kila kitu kumfuata Kristo.
-- Waombeeni Waislamu wanaotafuta Ukweli kwamba Yesu ajifunue kwao kama alivyofanya kwangu.

Na tafadhali chukueni hatua.
-- Kagueni Biblia zenu.
-- Onyoeni Makanisa yenu.
-- Shiriki ushuhuda huu ili wengine waweze kufahamu hatari.
-- Msiruhusu hofu iwafanye mlegee, lakini msiwe wajinga pia.
Vita ni vya kweli na lazima tusimame imara.

Asante kwa kunipenda. Asante kwa mwanzo huu mpya. Nakutegemea kwa maisha yangu. Kwa Jina Lako naomba. Amina.

Kama uliomba sala hiyo kwa dhati, karibu katika familia ya Mungu. Sasa wewe ni mtoto wa Mungu. Malaika wanashangilia juu yako sasa hivi Mbinguni.
-- Kumfuata Yesu huenda kusiwe rahisi, hasa kama unatoka katika mazingira yanayopinga Ukristo, lakini Yeye hatakuacha kamwe. -- Atakuwa pamoja nawe kila hatua ya njia.
-- Tafuta waumini wengine kama unaweza.
-- Soma Biblia, hasa Injili ya Yohana.
-- Omba kila siku.
Na kumbuka, sasa wewe ni sehemu ya familia ya ulimwengu mzima.

Asante kwa kusoma ushuhuda wangu. Kushiriki hili kunaniweka katika hatari kubwa zaidi, lakini lazima nizungumze.
-- Mengi yako hatarini.
-- Roho nyingi ziko katika hatari ya kudanganywa.

Jina langu lipo kwenye orodha ya watu wa kuuawa. Ninaishi mafichoni.
-- Siwezi kuwasiliana na familia yangu.
-- Nimepoteza kila kitu nilichokuwa nacho hapo awali.
-- Lakini nimepata Kristo na Yeye anastahili zaidi ya kila kitu kingine kwa pamoja.

Tafadhali kumbuka kukagua niliyowaambia kuhusu Biblia zilizoharibiwa.

-- Ukipata nakala zozote zinazolingana na nilichoeleza, tafadhali waonye viongozi wa Kanisa lako na wachapishaji wa Kikristo mara moja.
-- Ziharibuni nakala hizo na zibadilisheni na Biblia halisi zilizothibitishwa.

Na tafadhali ombeni.
-- Ombeni ulinzi.
-- Ombeni hekima.
-- Ombeni waumini wanaoteswa kila mahali.
-- Ombeni wale wanaotutesa kwamba nao pia wakutane na Yesu na waokolewe.

Mungu awabariki na kuwalinda.
Uso Wake uangaze juu yenu na awape amani.
Msisimame imara katika ukweli wa Neno Lake na msitikisike kamwe kwa Jina la Yesu. Amina. na
Nawasihi kwa Jina lenye Uwezo la Yesu Kristo wa Nazareti kwamba kama wewe ni Mkristo wa kweli uufanye ujumbe huu usambae kila mahali.

✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️✝️
 
Back
Top Bottom