Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,797
- 92,257
WanaJF, kisa hiki huenda kikawa kirefu na cha kuumiza sana ila sina budi nikihadithie, nilihadithiwa na Boss wangu ambaye yeye ndie haswa mwenye story hii, nitaisimulia tupate nasi cha kujifunza toka kwao, ninaandika kwa ridhaa yake. Asilimia 90% ni maneno yake mwenyewe.
Yeye (huyu Mama) allishi Burundi na familia yake, akiwa ameolewa na mrundi mwenzie, ni familia iliyokuwa tajiri kiasi na hivyo waliweza kuwekeza kiasi nchini Burundi wakifanya biashara ya kuuza vipuri vya magari kwenye maduka ya Kaka yake. Baada ya machafuko kuanza alipata wasi wasi sana wa usalama wa wazazi wake na ndugu zake wengine waliokuwa wakiishi nyumbani kwao Rwanda, kwahio akaamua kurudi Rwanda kwenda kujua usalama wao, alikwenda hadi kijijini kwao kwa ujasiri mkubwa na ujue muda huo ndio mapigano yalikua yametulia kidogo ila si kwamba yalikua yamekwisha.
Alifanikiwa kukutana na Binti mmoja tu na watoto wadogo wa Kaka yake (nitaeleza baadae kuhusu kaka yake), huyu Binti ndio alimueleza mkasa mzima jinsi wazazi wake walivyuwawa, anasema usiku mmoja walikamatwa na hao wauwaji wao, baada ya kuvamia Kanisa walilokuwa wamejihifadhi wakiamini kuwa wasingefika na kuwafanyia ule unyama! Anasema kuwa Mama yao (yaani Mama wa huyu Boss wangu) aliwasihi wauwaji wale wasiwaue au basi at least wawaache wale watoto,lakini baada ya muda yule mama aliwaomba aende nje kujisaidia na inasadikika kuwa ndio ulikua mwisho wake, kwani hakurejea tena ndani; baada ya muda kidogo kupita watu wote waliamriwa walale chini na hapo ndipo mauwaji ya kutisha yalipotokea. Wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi kabla ya mauaji kuanza, Bibi Huyu binti alifanikiwa kukimbia na kwenda kujificha kwenye shamba la mahindi lililokuwa jirani na kanisa hilo, huku akisikiliza na vilio na majonzi makubwa yakiendelea ndani ya kanisa lile. Asubuhi ya siku iliyofuata aliokolewa na kupelekwa uhamishoni Uganda hali akiwa bado ni binti mdogo. Hivyo ndivyo Boss wangu alivyowapoteza wazazi na watoto wa kaka yake kwa pamoja katika tukio la mara moja.
Mama huyu (Boss) alifanikiwa kufika hadi Kanisani hapo na kukuta madimbwi makubwa sana ya damu ambayo kwa juu ilionekana kuwa imeshakauka lakini ukikanyaga mguu uliweza kuingia damu, yaani ile ya chini haikuganda, hakuwahi kuwaona wazazi wake tena, alifanikiwa kufika nyumbani kwao huko nako alikuta maafa ya kutisha na uharibifu usioelezeka. alianza harakati za kuwasiliana na vyombo husika kujua kama kuna survivor wao yeyote na baada ya muda mrefu kupita ndipo alipounganishwa na binti yule akiwa nje ya nchi.
Anaendelea kusema kuwa, kipindi hicho cha mauwaji kaka yake alitorokea kwa Mashemeji zake akiamini kwa kua amemuoa dada yao na ana watoto nae basi asingedhuriwa. kwa bahati mbaya sana ilikua kama vile ndio amefuata kifo chake kwake aliuwawa kwa mapanga mbele ya mke wake akishuhudia. Watu hao walichukua kila kitu na hawakuacha uhai wa mtu yeyote.
Ilibidi Mama huyu ajiunge na Rescue Team ili kukusanya mizoga ya watu, alifanya kazi hio huku akiendelea kuamini kuwa angeiona at least miili ya ndugu zake, kwa bahati mbaya sana sana hakuna aliekuwa amebaki Zaidi ya binti niliekwisha kumtaja hapo juu.
Nilimmuliza swali kama anawajua wauwaji wa ndugu zake, kwa kweli alitabasamu na kuniambia kuwa alielewa swali langu lililenga nini, kwamba kama anawafahamu kwanini asingelipiza kisasi!! Nikajaribu kubisha lakini huo ndio ulikua ukweli, akatulia na kuniambia Elli mwanangu kisasi hakitarudisha maisha yaliyopotea, ni kweli ninawafahamu waliowaua ndugu zangu, wapo tena wengine ni shemeji zetu. kuliundwa Baraza la kuombana msamaha, kwahio walikiri kuwa waliwaua ndugu zetu lakini kwa sasa haisaidii kitu, tunawaombea ili tusirudi tena kwenye dimbwi lile la kuzimu.
Story hii nimeifupisha maana alichukua Zaidi ya 45dk kunisimulia, ilikua mwaka 2014 April wakati wa Kumbukumbu ya Mauwaji ya Rwanda.
FUNZO; Chokochoko za udini, ukabila na matabaka huweza kuleta majeraha yasiyopona daima kwa mtenda na kwa mtendewa. tujieoushe na lugha zenye kuudhi kuanzia kwenye familia zetu hadi Taifa. MUNGU atubariki
Kama utapenda kupata picha kamili ya kilichotokea Rwanda waweza kufuata Link hizi hapa chini
Sometimes in April full movie - YouTube