Wakuu mnapigaje hapo.
Hamjatekwa tu na wasiojulikana ( uvccm )
Kuna sehemu nilinunua eneo heka 1 lengo likiwa n kuweka mradi wa mifugo mbuzi. Wakati naendelea na ujenzi wa mabanda kuna mama alikuja maeneo hayo akawauliza mafundi kwamba niin kinataka kufanyka wakamjibu unawekwa mradi wa mbuzi.
Yule mbibi akawaambia mafundi hao watu wataweza? Swali tata kbs, wakati huohuo kuna mjeda alinunua eneo hukohuko palipo na mradi wangu amekumbia boma na anauza kwa bei ya hasara.
Wakuu mpaka sasa mradi una miezi 2 bt tayari mbuzi 8 wameshakufa kwa ugonjwa usioeleweka kbs tiba zote wanapewa tena na daktari wa mifugo kbs. Leo tu wawili wamekufa asubuhi dogo wa kuchunga ananiambia amekuta mbuzi hao wamelala tu hawainuki wkt jana jioni tu nilikuwa huko mbuzi walikuwa buheri wa afya.
Kama hilo halitoshi kila nikileta mtu wa kuchunga ghafla tu anaacha yani hapa najiuliza nichukue hatua gani nifunge mradi au nifanyeje wakuu nipeni ushauri wanga siyo watu hawapendi maendeleo wkt huko wana maisha magumu sana.