Incredible
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,031
- 1,604
Nimefarijika kuona vyama hivi vitatu vikishirikiana katika kudai katiba bora, yaani kuepusha kuwa na katiba ya chama kimoja katika nchi yenye vyama vingi. Pia binafsi naiona changamoto aliyonayo JK maana akisaini muswada ni tatitizo na asiposaini ni tatizo pia kutoka kwenye chama chake.
Lakini ninawasiwasi kama CUF na NCCR watafika mwisho katika hili wanalodai leo. Chanzo cha wasiwasi wangu ni kama ifuatavyo:
1. Mwenyekiti wa CUF alinakiliwa mahala akisema katika uchaguzi mkuu walikubaliana kura zake apewe JK. Je kesho JK akimwambia jitoe kwenye hili dai, itakuwaje?
2. Ndugu Hashim Rungwe alipojiunga na chama kipya alisema ametoka NCCR maana viongozi wake wanamtaka asiiseme vibaya CCM. Hata JK aliona nafasi moja ya ubunge wa kuteuliwa ampe mwenyekiti wa hiki chama.
3. Na sababu nyingine nyingi.
Hivyo basi, CHADEMA iende kwa tahadhari maana inaongozana na watu wenye nia mbili. Lakini ni vema CUF na NCCR wakaweka zaidi maslahi ya taifa na wakaendelea kudai hii haki inayoelekea kupotea.