Ushawishi wa Kisiasa na Nguvu ya Kiuchumi ya Qatar waipa Wasiwasi Saudi Arabia

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Qatar ni nchi yenye idadi ya watu 313000 kufuatia sensa iliyofanyika hivi karibuni na wafanyakazi/raia zaidi ya 2700000 kutoa nje wanaoishi na kufanya kazi nchini humo. Uchumi wa nchi hiyo ndogo unategemea utajiri mkubwa wa mafuta na gas. Raia wa Qatar ndio wanaongoza kwa kuwa na kipato kikubwa duniani. Kwa upande wa elimu Qatar ndio inaongoza kutoa elimu bora na kuwa na wasomi wazuri katika nchi za Ghuba . Qatar inategemewa kuwa nchi ya kwanza ya kiarabu kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2022. Baada ya Qatar kuanzisha shirika lake la ndege Qatar Airways imekuwa ikitoa upinzani mkubwa kwa mashirika mengine ya ndege ya kiarabu mashariki ya kati. Shirika kubwa la utangazaji la Aljeziraa linamilikiwa na serikali ya Qatar na wanahisa kutoka Marekani shirika hili linafanya kazi kwa uhuru mkubwa bila kuingiliwa na serikali ya nchi hiyo, shirika hili limekuwa mwiba kwa Saudi Arabia na washirika wake kwa kukosoa tawala hizo, nchini Misri kuna mtangazaji wa shirika hilo amewekwa mahabusu kwa muda wa miezi 9 baada ya kuripoti unyama wa serikali ya jeshi ya nchi hiyo.
Qatar ni nchi ambayo wasunii na mashia wanaishi kwa amani na utulivu mkubwa. Mwaka 2003 Mfalme wa Qatar aliitisha kura ya maoni kutaka kujua kama wananchi wanapendelea utawala wa kifalme uendelee asilimia 98 walipiga kura kutaka utawala wa kifalme uendelee, hakuna nchi yeyote ya kifalme Saudi Arabia, UAE, Bahrain zilishawahi kupiga kura ya maoni ya aina hiyo na familia za kifalme za nchi hizi ndio wanatumia asilimia kubwa ya utajiri wa nchi hizo.
Wakati wa vuguvugu ya Arab Spring Qatar ilitoka mchango mkubwa katika harakati za kuleta demokrasia katika nchi hizo kwa mfano walimuunga mkono kwa dhati aliyekuwa Rais Morsi wa Egypt ambaye utawala wake uliangushwa na jeshi kwa msaada kutoka Saudi Arabia zaidi ya raia zaidi ya 20000 waliuawa na jeshi la Egypt na wengi wa wahanga hao wallitoka kwenye dhehebu ya Sunni. Qatar ndio nchi pekee ya kiarabu inayowasaidia wapalestina katika harakati zao dhidi ya Israel. Qatar ndio nchi pekee inayopinga vita ambavyo Saudi Arabia na washirika wake wanazoziendesha dhidi ya Yemen zaidi ya raia laki moja wamepoteza maisha yao.
Saudi Arabia anataka kuwa kingmaker wa mashariki ya kati lakini nchi ya Qatar imekuwa na msimamo tofauti na nchi ndio sababu kubwa Saudi Arabia na washirika wake kuamua kuitenga nchi hiyo.
 
Kuna nchi zina utajiri mkubwa lakini viongozi wachoyo wanaingia mikataba mibovu wananchi tunaendelea kuwa masikini. Leo Tanzania na utajiri mkubwa wa gesi na dhahabu bado serikali inataka kodi kwa mama ntilie na machinga.
Siwezi laumu sana wakoloni ila nalaumu wakoloni weusi. Misingi mibovu na rushwa iimetufikisha hapa tulipo leo. Katiba iliyopo inamfanya rais kama Mungu yan ukishapata ile title basi nchi ni yako.

Wenzetu brazil hawana mchezo rais ukifanya makosa unapelekwa jela. bongo eti ipo kinga ya kumlinda rais??
Kwa hali hii wategemea nini?
Viongozi mafisadi wakishikwa hawapelekwi jela bali wanapumzishwa tuu. Kidogo Magu kajitahidi kuhusu rushwa hapa namna pongezi.

Kuna sababu kubwa sana ya kurekebisha sheria ya nchi hasa upande wa viongozi maana wao ni Mungu mtu, pia mikataba ya resource zetu iwe open.
 
Saudi Arabia ndiyo source ya mgogoro huu na ni bonge la mnafiki, anajifanya kutetea haki ktk nchi zingine, wakati ndiyo mfadhili mkubwa wa ujenzi wa misikiti ktk nchi mbalimbali duniani, kwake anaapa kamwe kanisa halitakaa lijengwe..! Bure kabisa.
 
Saudi Arabia ndiyo source ya mgogoro huu na ni bonge la mnafiki, anajifanya kutetea haki ktk nchi zingine, wakati ndiyo mfadhili mkubwa wa ujenzi wa misikiti ktk nchi mbalimbali duniani, kwake anaapa kamwe kanisa halitakaa lijengwe..! Bure kabisa.
Wanafata kuruani
 
With help from Turkey and Iran, Qatar is defiant so far. They haven't asked for sunctions to be lifted na wala hawajapepesa macho bado. Majamaa yako vizuri!
Let's see how long this will last..
 
Back
Top Bottom