Ushawai kukosea kuagiza menu ya chakula au kinywaji?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
17,796
32,148
kwaza nicheke

Ilikuwa siku fulani hiyo nilikuwa na stress balaa sasa nikaona sio tabu ngoja nijitoe out nikatoka mpaka sehemu yangu pendwa kwa bendi mzuri CAPE TOWN kufika pale nikaomba menu nikachagua kinywaji soft drink asee.

Nililetewa cresta ile ya ndimu kali sasa kumrudisha naona noma kashaifungua nikazuga nikamwambia embu nilete tena menu nikasoma vizuri nikaiona mojito nikaagiza chap ili kutoa aibu

Now huwa nauliza kwa muhudumu

IMG_0278.jpg
 
Sio Tanzania, nkiwa china --- wakaleta kitu mfano wa kono kono ... etc

nkaondoka kimya kimyaa nkaenda supermarket and kukamata mkate na chupa moja la red wine nkajilalia
🤣🤣🤣🤣🤣 Pia hawa watu vyakula vyao vinatoa harufu.

Siku nilizokuwa huko ni wali maharage samaki, plus asubuhi kuna restaurant 1 Mtanzania alikuwa anapika chapati na maini vizuri kama upo home.
 
Yamenikuta asubuhi pale Moevoke Ubungo, sijui ndio pameandikwa hivyo.ila ni hotel fulan ipo Ubungo Maziwa .

Mfukoni nipo na ef12 ,nipo na mtoto mzuri nikaona ngoja tupate supu kidogo.

Nikasema lete supu nyama mbili, mhudumu kaleta kiroho safi tu, sasa namuuliza bei gani dah et 5000 supu moja, kwahiyo hapo ni 10000 supu na chapati 2 ni 1000 kwahiyo nabaki na buku tu.

Nikataman nimwambie rudisha, ila ndio ishafika na kapakua tayari.

Ikabidi tunywe tu ,demu anaisifia supu nzuri huku mimi nainywa kwa uchungu sana. Baada ya hapo sikuwa na mwendo.

Ikabidi tuchukue na maji kabisa, kisha tukatembea kwa mguu mpaka Ubungo sheli pale kutoa hela
 
Yamenikuta asubui pale Moevoke ubungo,sijui ndio pameandikwa hivyo.ila ni hotel fulan ipo Ubungo Maziwa .

Mfukoni nipo na ef12 , nipo na mtoto mzuri nikaona ngoja tupate supu kidogo...

wewe uliendaje hoteli na 12000 kuna sehemu zingine supu 10000 chapat moja buku kuwa makini kuja posta pale ukiwa na njaa morng ili ushibe vizuri 10000 inaisha chapata buku mbili chai ya rangi buku au jero maziwa 2000 mayai
Buku soseji buku sambusa jero dah
 
Kuna grocery moja Mbezi inn iko jirani na salon ya kike. Kila siku nilikua nakunywa kwenye hiyo grocery, lengo langu nimpate yule mwenye salon.

Kumbe Kuna flat screen Fulani na yenyewe ilikua inanitaka nayo iko hapo salon, kila nikifika pale flat screen hii hapa inanichangamkia balaa. Basi nikaridhika na flat tu.
 
Back
Top Bottom