Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
habari zenu,nilikuw na boyfriend ambaye nilimpend sana lakin sikujua kam yey ananipenda kwasababu alikuwa ananikataa san mpak mwishowe nikachok nikaamua kuw na mwanaum mwingine ambay tumedum mwak mmoja,yey anaishi nje na niliamin ananipenda na kwasasa na mimba yake yenye miezi mitatu,hivi karibuni nimegundua ana mke na wanawatoto wa tano na nilipomuuliz aliniambia ni kwel na hatawez kunioa ila atanilea mim na mtoto.,.mpenzi wa zaman karud kwa kasi anaomb msamaha turudiane,nimemweleza ukwel na akanion mim mbay san na ananishaur nimwache baba mtoto niwe naye yey atamlea mtoto na tutaoana,nifanyaj?
BABA MTOTO
Huyu haitakiwi umchukulie serious sana kwa kuwa sio mkweli na huenda amekubali kumlea mtoto kutokana na hofu ya mkewe kujua.Hapa kuna haja ya kujitazama wewe mwenyewe kama una haja ya kuwa nae serious sana
Kuna wakati sifa ya mtu inaonekana mwanzo tu wa mahusiano yenu kama utakuwa makini na kuziacha hisia na kutumia akili,huyo inaonekana alitaka tu akubanjue na alijua akikuambia ana mke utamkimbia
MPENZI WA ZAMANI
Huyu unatakiwa ujiulize ni kwanini alikuwa hakutaki mwanzo na nikwanini amekuja sasa kwa nguvu kubwa kiasi hicho,huenda huyu ametendwa huko na kinachomsukuma kuja kwako ni machungu ya kutendwa
Kama ni machungu ya kutendwa kaa nae mbalo kwani hizo hisia ni za muda tu,ikifikai zikaisha atakumwaga na kama mtakuwa mmeoana ndoa itakuwa ngumu sana kwako,kigezo cha ndoa sio sababu ya kukubali tu bila kufikiri
Pia hapo kuna kitendo cha kustua sana,ni kwanini anataka kulea mwana?je huyo jamaa anajua gharama za kulea?
Anajua ni nini maana ya kulea?
Je baba wa mtoto atakubali mtoto wake alelewe na mtu mwingine?Jiulize hili kwani kaka baba mzazi wa mwana atakataa atakuwa na haki hiyo kwakuwa ni mtoto wake
Huyu mpenzi wako wa zamani ni kitu kimemfanya awe mwema sana kwako?
Tumia akili badala ya hisia!