Ushauri

Superb2014

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
8,464
6,510
Salamu kwenu wana JF wote.

Katika maisha ya kila siku tukiwa kama Binadamu tunakutana na changamoto nyingi. Miaka kama 8 iliyopita kuna ugomvi ulitokea kati yangu na Wifi yangu yaani Mke wa Kaka yangu, huyu Wifi yangu ni mtu mwenye hasira sana, kinyongo na anapenda kuzusha maneno ya uongo na anapenda sana ugomvi kwa kifupi hapendi Ndugu wa Mume na Mume wake analitambua hilo.

Katika ugomvi huo aliniambia kuwa nitaishi maisha ya shida, ukweli ni kwamba maisha yangu yamekuwa ya shida kama alivyotamka.

Naomba ushauri je huyu Wifi yangu atakuwa ni mtu wa aina gani? Je nifanye nini ili niweze kutatua hii changamoto? Maana kama ni maombi nimefanya sana maombi.

Kwa niaba ya Rafiki yangu naomba kuwakilisha.
 
Huyo wif yako ni mchawi

Kingine acha kufuatilia maisha ya kaka yako uone kama atakufuata tena

Ova
 
Huyo wif yako ni mchawi

Kingine acha kufuatilia maisha ya kaka yako uone kama atakufuata tena

Ova
Asante, kutokana na huyu Rafiki yangu ni kwamba hana mazoea ya kufuatilia maisha ya Kaka yake na Wifi yake basi tu ugomvi ulitokea kutokana na huyo Wifi yake.
 
Yeye Ana maisha mazuri? Jitafakari na wewe pia mienendo yako usije ukawa unamsema wifi huku nawe ni mtata.
 
Yeye Ana maisha mazuri? Jitafakari na wewe pia mienendo yako usije ukawa unamsema wifi huku nawe ni mtata.

Rafiki yangu siyo mtu mtata kabisa huyo Wifi yake ndiyo mtu pekee amewahi kuwa na ugomvi nae.
 
Yeye Ana maisha mazuri? Jitafakari na wewe pia mienendo yako usije ukawa unamsema wifi huku nawe ni mtata.

Ana maisha ya kawaida ana Mume na Watoto, lakini huyu rafiki yangu miaka inazidi kwenda hajaolewa na wala hana mtoto.
 
Wew kunakitu amekufanyia uyo wifi yako ata mimi kuna mtu alinitamkia ivyo akaenda kufanya na ya kwake namshukuru krsto alinifungua km unahtaj msaada zaidi njoo pm.
 
Back
Top Bottom