Ushauri wenu wa biashara ya asubuhi

Malingumu

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
616
429
Habarini...

Kuna rafiki yangu anafanya kazi ya ofisini ila muda wake wa kuingia ni saa nne asubuhi... nimemshauri kuwa kabla ya kuingia ofisini anaweza akafanya kitu cha kumuingizia hela... sasa ameniuliza ni kitu gani? Mimi nikawa na idea moja ya kutengeneza say vitafunwa na kuvisambaza sehemu kama akizipata... naombeni ushauri zaidi ni biashara gani anaweza fanya muda huo kabla ya kwenda ofisini maana mimi naona ni masaa mengi ati kukaa tu na kusubiri muda wa kazini ni wastage of time kijasiriamali..
Tafadhalini ongezeeni mawazo!!!
 
Mwambie aende kwenye stand za daladala atafute eneo, aweke mzigo wake wa pipi, karanga, Big g n.k halafu baada ya saa kila 4 anafunga.
 
Kama ni mwanamke Awe anaamka asubuhi sana , Apike chapati na supu na chai karibu na sehem yenye kutoka kama stendi hiv nakuhakikishia atatoka tuh wala hatopoteza mda
 
Habarini...

Kuna rafiki yangu anafanya kazi ya ofisini ila muda wake wa kuingia ni saa nne asubuhi... nimemshauri kuwa kabla ya kuingia ofisini anaweza akafanya kitu cha kumuingizia hela... sasa ameniuliza ni kitu gani? Mimi nikawa na idea moja ya kutengeneza say vitafunwa na kuvisambaza sehemu kama akizipata... naombeni ushauri zaidi ni biashara gani anaweza fanya muda huo kabla ya kwenda ofisini maana mimi naona ni masaa mengi ati kukaa tu na kusubiri muda wa kazini ni wastage of time kijasiriamali..
Tafadhalini ongezeeni mawazo!!!

KWANZA BADILISHA HAYO MAELEZO YA KUWA KUNA RAFIKI YAKO ANAHITAJI KUFANYA HIVYO,
BALI BAINISHA TU UKWELI KUWA
NI WEWE MWENYEWE-

NDIPO NIJE NIKUSHAURI.
 
Kama anapesa ya kutosha mwambie afuge ng'ombe, mbuzi, kuku, mbwa n.k

Anaamka asubuhi mapema anahudumia mifugo ikiwa ni pamoja na kukamua mazima na kusambaza kwa walaji. Mpaka saa nne anakuwa huru anazama job.
 
KWANZA BADILISHA HAYO MAELEZO YA KUWA KUNA RAFIKI YAKO ANAHITAJI KUFANYA HIVYO,
BALI BAINISHA TU UKWELI KUWA
NI WEWE MWENYEWE-

NDIPO NIJE NIKUSHAURI.

Ni rafiki aisee... nawezaje kuacha kutaja kama ni mimi mwenyewe maana hakuna kibaya hapo.
 
Back
Top Bottom