Ushauri wenu unahitajika

Mubby777

JF-Expert Member
Oct 17, 2018
1,638
5,645
Mimi nimeoa ingawa sio official (hatujafunga ndoa rasmi ila nimeshamlipia na tunaishi pamoja)

Kwa bahati mbaya mke wangu ni aina ile ya wanawake wanaoongea na kupanda juu sana kipindi cha ugomvi(mtu wa makelele sana)

Mimi nafanya biashara na napenda sana utulivu nikiwa home ili niweze kuwaza mambo yangu

Sasa hali hii ya wife ilinipa shida mpk tukapita kwa washaur kadhaa waliobobea ila wap! Kesi zikienda kwa mama yake anakuwa upande wa binti(ni kama anamuogopa mtoto wake sababu sisi ndo tunawawezesha sana kiuchumi so mke wangu ndo lastborn ila ana saut kwao sana)

Mwaka jana mwezi wa 10 hali ilikuwa mbaya mpaka tukatengana. Kwa taratibu za kabila langu huwez mfukuza mwanamke ila we ndo unajitenga!

So mwaka jana nilihama kwangu nikaenda kupanga ili angalau tupeane space

Tatizo hapo ndo lilipotokea sababu ya stress na upwele nikajikuta nakuwa na mahusiano mawili matatu na wanake ninaofahamiana nao

Tulisex yes ingawa kila mmoja alijua kabisa sio mahusiano serious

Mahusiano yalikuwa ya muda mfupi kwa kila mmoja

Wote ilikuwa Oct na Nov basi Dec nilikuwa busy na biashara so sikutengeneza mahusiano yoyote

Kuanzia January ndo sekeseke lilianza me kuanza kupewa taarifa za ujauzito na wape mabinti kila mmoja kwa wakat wake(wa mwisho alikuja nambie Feb)

Sababu hatukuwa na mahusiano serious me niliwaza option zingine cha ajabu kila mmoja alikataa(kila mtu kwa muda wake na hawajuani)

Basi maisha yakaendelea!

Feb mimi na wife tukasuruhishwa na yakaisha

Wife hajabadilika ni mtihan kinyama ila nimeamua hili ndo zigo langu ntakufa nalo acha nilibebe ivyo ivyo

Wale wadada wawili washajifungua na nawasaidia kwa kias chake sababu kdg kiuchumi siko vibaya

Sasa nawaza kumwambia wife ila nashindwa pa kuanzia na naogopa huko mbele akija kujua itakuwaje?

Au nitumie mbinu gan kumweleza? Asichukie na kuvunja ndoa)
(Yule mdada mwingine mara ya mwisho tulitofautiana kauli akapotea na kubadili mawasiliano simpati mpaka leo ingawa nahisi atakuwa kajifungua pia)

Inaniumiza kwa na watoto wengi ivyo nie ila ndo ishatokea sina namna
 
Pole hiyo ni changamoto unayopitia .... Ili uweze kuwa huru acha muda hende kuna siku mwambie gu wife ili uwe huru kabisa hata asipolipokea vizuri litakuweka katika nafasi nzuri huwez kujua mtoto yupi ndiye atakayekuja kuwamsaada kwako ..... Jambo la msingi usimuogope mwanamke anza kutengeneza misimamo yako kama mwanaume hiii itakusaodoa zaidi

sent from HUAWEI
 
Mkuu usimwambie hili mkiwa nyumbani....

Mpeleke porini ili achome pori maliasili watasaidia kuuzima.

Zimamoto waachelewa saana kufika watakuta nyumba imeteketea. Huyo Simba jike atakupasua kichwa mzee.
 
Kwanza kabisa unakwama sana kusimamia nafasi yako kama mume katika familia, tatizo lilianza pale ulipomruhusu awe na sauti sana mnapogombana na ulipoanza kumuogopa. Kuwa mwanaume mkuu.
 
Unahitaji ushauri:
• Juu ya uongeaji wa mke wako
• Juu ya wewe kumuogopa mkeo
• Juu ya kumwambia amankutomwabia

Au unahitaji ushauri wa nini?

Nitumie njia gan kumwambia ambayo haitaleta madhara ndo ushaur naotaka kwa waliowah kupitia hali kama hii
 
Mkuu usimwambie hili mkiwa nyumbani....

Mpeleke porini ili achome pori maliasili watasaidia kuuzima.

Zimamoto waachelewa saana kufika watakuta nyumba imeteketea. Huyo Simba jike atakupasua kichwa mzee.

Hahaha kaka
 
Kwanza kabisa unakwama sana kusimamia nafasi yako kama mume katika familia, tatizo lilianza pale ulipomruhusu awe na sauti sana mnapogombana na ulipoanza kumuogopa. Kuwa mwanaume mkuu.

Ndg kuna wanawake ni vichwa aisee unataman hata kumpiga ila moyo unasita so mwishowe anaona kama anakumudu
 
Pole sana mkuu, hii hali imenikuta aisee.

Wife wangu wa ndoa tena kuna kipindi wanawake wanajidatisha wenyewe yan akaniona tu akaomba namba yangu. Nikamnyima na kila nikienda pale dukan kwa mdingi wake nikimkuta tu lazima aombe namba yangu.

Japo dukan alikua anaumza bro wake yeye alikua kwa nje akiuza vitafunwa hasa asubuh. Sasa kuna siku nikaona isiwe tabu nikampa namba, cha kushangaza jion yake akanitext kuwa ananipenda.

Nami kwa ujasiri wangu sikutaka kupoteza time nikapanga mipango ya kijasusi siku moja tukaenda guest house aisee nikala mzigo kavukavu kibabe.

Baada ya wiki akatamani tena nikampanga kisha nikaenda guest house ile ile nikamla kama kawaida na ndio ikawa ya mwisho hiyo. Baada ya mwezi hiv akanitext kuwa ana ujauzito wangu

Sikuumiza kichwa nikamwambia sasa iwe kimya kimya wasijue watu mpaka akaamua kusafiri kwenda mtwara huko kuna mishe alipata akaanza kukimbizana nazo. Ujauzito kadri unavyozidi kukua akaanza kuhisi homa hasa miguu kuvimba, n.k ndio akaamua kuwamabia wazazi wake

Nami nikaongea nae nikamtumia nauli akarudi na hayupo aliejua zaidi ya wazazi wake tu, siku anajifungua ndipo baadhi ya watu wakajua ikiwemo wadogo zake. Baada ya miezi kadhaa fununu zikaanza kusambaa kitaa japo wife hakujua, nami nikajisemea hapa wife akijua kuna kitu kitatokea tu bora nipange siku nimwambie mwenyewe.

Lahaula!! Siku moja asubuh mishale ya saa 12 asubuh hiv nikampanga wife ili nimwambia kuhusu mtoto aisee BP ikamshuka hapo hapo nikamdaka akatulia kama dakika kadhaa akaamka tena na kuniuliza inamaana anaota ndoto au ni kweli?

Nikamwambia ni kweli, akakasirika mpaka akadai talaka yake mara akatafuta kisu, mara nini na akisema bora afe tu kuliko kusikia hiv. Nikamuita maza akawa nae karibu mpaka ukwen taarifa zilifika aisee ila mama mkwe alimwambia ole wako urudi nyumban baki huko huko na mumewe na hii yote kwa sababu niliongea na babu wa wife na akanielewa.

Japo wife hakawa hana hili wala lile anisamehe ila akikumbuka tena tu aisee hasira zake sio za nchi hii nikamtuliza baada ya wiki mbili tatu hiv akatulia life likaenda mpaka leo hii aisee nilipitia kipindi kigumu kweli. Job nilikua siend maana nikitoka tu anatafuta kisu, nikavificha vyote yeye anatafuta chupa aisee niliogopa kutoka kisa anaweza kujiua maana alikua na hasira sana.

Ila baada ya kumuweka sawa japo ilichukua muda mrefu kusahau. Mpaka sasa bado naishi nae vizuri tu.

Tukumbuke kuwa kila kitu kina changamoto zake ila ujasiri wako ndio utakufanya uwe sawa ili kukumbana na vikwazo katika ndoa yako.
 
Ndg kuna wanawake ni vichwa aisee unataman hata kumpiga ila moyo unasita so mwishowe anaona kama anakumudu
Kuna njia nyingi za kumuonesha mwanamke kuwa anachokifanya hakifai au haukipendi. Pamoja na kipigo kuna maongezi, psychological treatment, n.k. kulingana na aina ya mwanamke.
 
Kabla ya kumwambia, una uhakika kuna ulazima wa kufanya hivyo na huu ndiyo wakati mwafaka (good timing)?

Unajua me naangalia bora kama ni kuniacha iwe now kama ni kuelewana basi iwe nao ili hata napotunza wale watoto kiwe kitu anachojua
Kuliko badae huko ndoa ishaota mizizi halaf ndo anajua maana duniani amna siri ije kuleta athari kubwa zaid
Sasa shida inakuwa ntatumia njia gan kumweka sawa ili hata nikimwambia aelewe
 
Back
Top Bottom