Kiazi Kitamu
Senior Member
- Feb 16, 2013
- 122
- 126
Habari wana MMU! Mimi ni kijana wa kiume nina umri miaka 29. Nina mchumba wangu kwa sasa tuna muda wa miezi10 ktk mahusiano yetu kuna jambo kubwa ambalo linanisibu na mara nyingi tunatokea kutoelewana mra nyingi ni kulaumiana na hasa yeye ananilaumu kuwa simjali kwa chchote angali kwa uwezo wangu kuna baadhi ya mambo najitahidi sana kumtimizia pindi anapohitaji ila mwenzangu haridhiki na hilo. Kubwa zaidi hivi karibuni alianzisha biashara yake baada ya kupewa mtaji na wazazi wake ila wakati anaanzisha hakunishirikisha kabisa ila kwa sasa anataka nimlipie kodi ya fremu angali sijawahi kuona hata siku moja faida ya hiyo biashara japo kwa kuelezwa kilichopatikana. Hiyo haikutosha nilijitaidi kwa kumuongezea mtaji baada ya kuniomba ni kampatia laki 4, hata hivyo wakati wote akisafirisha mzigo mimi nagharamia kila kitu. Ila leo ananiambia sina msaada wowote kwake na ni bora asiwe na mwanume . Sasa mimi nifanye nini kwani nilishatangaza kwa ndugu na jamaa kuwa ndio mke wangu mtarajiwa ila kila kukicha ni vituko hakuna amani naomba ushauri wenu ndugu zangu niko njiapanda. NAWASILISHA