Ushauri wenu, Dini inakwamisha uhusiano wangu na binti huyu

mjinishure

Member
Oct 19, 2012
86
56
Habari wanajukwaa
Miaka miwili iliyo pita nilibahatika kuanzisha mahusiano na dada mmoja ambae anafanya kazi moja ya benki hapa dar.

Hapo mwanzo mahusiano yetu yalikuwa ya kawaida sana ila siku zilivyozidi ndipo nikagundua kweli huyu dada alikuwa ananipenda. Kama mjuavyo mapenzi yalinoga sana kiasi cha kuwa nampitia kazini kila siku na usafiri wangu kumrudisha kwao

Pia kuna mambo mengi huyu dada alio nisaidia kwani huwa kila akija nilipopanga huwa haulizi akiona kuna mapungufu chumbani au sebeleni unakuta ananunua hakuna siri tena juu ya mshahara wake wala namba za siri za kadi yake ya benki nimekuwa kama mshauri kila mshahara wake uingiapo benki kumueleza namna ya matumizi.

Katika mapenzi nakumbuka aliwahi kufumania sms za mapenzi kwenye simu yangu nakumbuka alilia sana ila alinikalisha na kuniambia kuwa ananipenda sana hata kama hayo mambo nafanya kwa matamanio basi nifanye kwa siri bila yeye kuona kwani huwa anaumia, nilimuomba msamaha na yakaisha

Tatizo limekuja hivi karibuni baada ya kushibana na kuamua nibora tukaoana. Likaja swala la dini mimi ni mkristo na yeye ni mwislamu. Nilimwambia siwezi kuoa mtu mwenye dini tofauti na yangu. Ndipo alipo niambia hakuna tatizo yuko tayari hata kabla sijamuuliza alilijua hilo na atabadilisha.

Upande wa wazazi wake hawataki hata kusikia hii kitu na tayari wamemtisha kutokumtambua kwenye familia yake endapo tu atabadilisha. Nilipo muuliza yeye anaonaje hili alisema nipo tayari kuolewa nawewe, kwani nakupenda sana swala la wazazi potelea mbali.

Juzi nimetumia sms baada ya kupata baadhi ya ushauri toka kwa watu kuwa (nimeamua ni bora tukaheshimu mawazo ya wazazi wetu hivYo naona si sahihi mimi na wewe kuoana) leo nimepigiwa simu na mdogo wake kuwa siku ya pili hajala na analia tu na kazini hakuenda.

Wanajamvi naombeni mnishauri kwa hili janga nililonalo naikumbukwe mimi siwezi badilisha dini
 
Unataka kumuoa huyo dada au kuoa ndugu zake?

Kama yeye yuko tayari kubadili dini na yeye hawaogopi hao wazazi wake wewe unasikiliza ushauri wa watu ili iweje?

Humpendi tu huyo dada sema
no nampenda sana
 
kaka inaweza ukawa ushauri wako nimzuri ila unapaniki mapema sema nimekuelewa
 
kwahiyo nibora awakosee wazazi wake
Ipo siku wazazi watatambua thaman yake na uhitaji wake katika kufanikiwa kifamilia hivyo kila kitu kutakuwa sawa

Mytake:huyo binti atawatosa ndugu zake kwa ajili yako make sure unampa thaman anayo stahili na Hakikisha unakuwa kila kitu kwake sio uje uwe Tatzo badae

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
asante kwa ushauri wako
 
kaka inaweza ukawa ushauri wako nimzuri ila unapaniki mapema sema nimekuelewa
Unajua nyie ndo mnasababisha wanaume wote tuonekane malofa sasa huo ushaul ulionda kutafuta kwa hao jamaa zako ni wa nini, wewe ni kabila gan mkuu
 
Hilo gumu, japo nyie mwapendana kwa dhati, ni vizuri kupata baraka za wazazi. Si lazima kubadili dini kwa miaka ya sasa na mkaoana na maisha yakawa mazuri tu bila tatizo. Wapo wengi waliofuata utaratibu huu.na wako salama. Karibuni nyote wawili kuangalia juu ya hili mkiongea wadau wakuu, na uhakika mtafanikiwa.
 
no nampenda sana
Nitakwambia vitu vitatu:

1:kama unampenda usingejali chochote kile sio wazazi sio kitu chochote

2: Mwanamke unayempenda/anayekupenda haachwi kwa SMS.....kuna namna ya kufanya mpaka mnaachana kuliko kumshock mtu kwa SMS

3:Kutokana na hayo niliyoyasema hapo juu naomba uachane na mpango wa kuoa. Hata kama mkirudiana endeleeni kudate bado haujakomaa kuwa tayari kwa ndoa ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…