Ushauri wangu Wizara ya Mambo ya ndani

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,435
4,608
Natanguliza salamu zangu kwenu Nyote.

Naomba nianze kwa kuipongeza serikali iliyopo madarakani kwa ufuatliaji wa mambo ambayo awamu zilizopita ziliyaona ni kana kwamba ni mambo madogo na hayakustahili kupewa kipaomble.

Suala ambalo naona kwasasa wizara ya mambo ya ndani inalivalia njuga ni suala la ajira kwa wageni kwenye kazi ambazo watanzani wanaweza kuzifanya.

Wizara ikitaka kufanikiwa katika hili iweke mfumo ambao sisi wananchi tunaweza kutoa taarifa kuhusu hawa wageni, Either kwa njia ya barua pepe, au mitandao mingine ya kijamii.

Kuna kampuni zimeajiri wageni ku process invoice lakini kwenye job descrption anajiita cost analysts!!!
 
Inasikitisha sana,mgeni kutoka india kaishia darasa la nne,tena kwa maombi ya wazazi na msalie msalie mtume akija bongo,huyo ndiye Factory manager
 
Kuna wadau wametoa ushauri kwenye ule uzi wa waziri Mavunde kuwa vibali vyote vifutwe waombe upya, hii ndo itakuwa easiest way
 
Hichi ni kilio cha siku nyingi kwa wazawa...kama serikali imeamua kulivalia njuga itakuwa ni jambo la kheri na lenye manufaa kwa ajira za wazawa...maana tulifikia pabaya sana.......
 
Mimi sipingi wageni pale ambapo it could be proven uwepo wao utaisaidia nchi katika kuongeza tija na maendeleo , Kama wenzetu ulaya wanapotumia uhamiaji kiuchumi na maendeleo mengine kwenye maeneo yenye upungufu , lakini wakwetu haupo hivyo Bali inatumika Kama njia ya wizi kukwepa kodi kudumaza maisha ya watanzania , kukuza ubaguzi na kila aina ya madhila , Ndio Maana tunao na huduma na uchumi unazorota
 
Its so anoying, Ukitaka kujua Hivi vibali vilikua vinatolewa kwa rushwa Angalia pesa zinazolipwa ka,a "facilitation fees"
 
Back
Top Bottom