Ushauri wangu wakati unapanga malengo yako ya mwaka 2017

The Retired Planner

Senior Member
Sep 22, 2015
166
241
Miaka nenda miaka rudi tumekuwa watu wa kupanga mambo mengi yasiyotekelezeka. Mtu ndani ya mwaka mmoja unataka ufungue biashara, uoe, uanze kufuga, ukalime vitunguu pale Iringa na uhakikishe umewasomesha wadogo zako wawili chuo ndani ya mwaka huo huo mmoja. Hizi ni nadharia na kamwe hatutakuwa wakweli, hivyo basi, ninaushauri wa jinsi ya kuenenda na mipango yetu ya mwaka 2017.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unapanga malengo yako ya mwaka 2017:

1. Ainisha malengo yako yote ya mwaka 2017 na uyape kipaumbele, anza kuyafanyia kazi yale matatu ya muhimu zaidi.

2. Andaa mpango mkakati wa utekelezaji wa yale malengo makuu matatu. Hapa namaanisha onesha jinsi utakavyo yatekeleza kila moja na kwa muda gani. Pangia muda halisi wa kila lengo moja na “resources” zitakazotumika katika utekelezaji. Pesa kiasi gani itahitajika? Itapatikana wapi? Nani atahusika kwenye lipi? Lipi litaanza na lipi litafuata? (vyote hivyo viwe kwenye maandishi)

3. Hakikisha mpango mkakati wako unaanzia Januari mosi 2017. Mshirikishe mtu wako wa Karibu na ambaye unadhani ni mfuatiliaji na mtendaji mzuri juu ya mipango yako na mpe jukumu la kukufuatilia kila mwisho wa mwezi juu ya utekelezaji wa malengo yako.

4. Andaa “checklist” itakayoonesha mambo unayotakiwa kufanya kila wiki ili kutekeleza malengo yako makuu na ibandike pembezoni mwa mlango wako ili uweze kuiona kila uingiapo na utokapo chumbani mwako. Weka tiki kwenye kila jukumu la wiki ambalo utakuwa umelitekeleza.

5. Tia nia kwenye kila lengo lako. Fanya kazi kwa bidii sana mwaka 2017. Nguvu na akili yako ifikirie zaidi juu ya utekelezaji wa malengo yako. Acha kulalamika sana na muda wako mwingi uwe juu ya mafanikio yako. Hakikisha unakula vizuri na kufanya mazoezi ili kuwa na afya bora ya kukuwezesha kufanya kazi zako kwa uhakika.



Mwishoni mwa mwaka 2017, tutakuja kupeana mrejesho juu ya haya tuliyokubaliana leo. Mimi naanza sasa.

NB. (Hakikisha Mpango Mkakati Wako Upo Tayari Mpaka Kufikia Desemba 31 2016)


Nawasilisha.
 
Mmmh,

Napata wasiwasi kama waTZ huwa tunapanga utekelezaji wa malengo yetu. :rolleyes:

Mnanikumbusha kale kausemi kanakosema "If you fail to plan, you are planning to fail " - Benjamin Franklin
 
Back
Top Bottom