Ushauri wangu wa bure kwa viongozi wote wa nchi hii

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Viongozi wote wa nchii hii, bila ya kutazama mna uhusiano na chama gani cha siasa au taasisi ya aina gani, jengeni tabia ya kutafuta washauri waliowazidi umri.

Rais wa Marekani Barack Obama alipoingia madarakani, kitu cha kwanza kufanya ni kuunda kundi la watu wachache ambao aliwachagua kama washauri wake. Na watu hao, wote wanamzidi umri. Ni wastaafu ambao waliitumikia serikali ya Marekani kabla hajaingia kwenye siasa.

Viongozi wengi hushindwa kutimiza malengo yao, kwa sababu hukosa kauli za hekima na ushauri uliojaa uzoefu kutoka kwa watu ambao walishafanya kazi miaka ya nyuma.

Nawashauri watu wote walioteuliwa na rais kushika nyadhifa mbalimbali, na pia wale waliochaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura, wajenge tabia ya kuunda timu ndogo inayoundwa na wastaafu, ili waweze kuongozwa na hekima za wazee kwenye masuala yote ya uongozi.

Nimemzungumzia Obama lakini wapo marais wengi tu ambao wameweza kufanya kazi kwa amani kwa sababu ya kuwa na timu ndogo ya wastaafu ambao wanawapatia muongozo wa kiutendaji.

Hakuna mtu anayeweza kuishi kama kisiwa, naamini wale wenye kutaka kuacha kumbukumbu baada ya uhai wao, wana kila sababu ya kutegemea ushauri unaotokana na uzoefu wa wale waliowatangulia kikazi.
 
Viongozi wa kiafrika na hasa hapa Tanzania wengi ni wachafu kama sio wote, badala ya kukushauri mambo ya muhimu wataanza kukufundisha jinsi ya kupiga dili na kuwasaidia kulinda Mali za wananchi walizopora
 
Back
Top Bottom