Ushauri wangu kwa vijana wanaotafuta ajira

Ushauri wangu kwa vijana wanaotafuta ajira

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,152
Jamani nadhani kila mmoja anaona jinsi hali ya ajira ilivyo ngumu hapa nchini Tz,vijana wengi wamemaliza chuo lakini hawana wanalolifanya zaidi ni kuzurura ovyo mitaani na kulala mpaka saa saba wengine wanaishia kuangalia series za movies nk. si kwamba wanapenda, bali imewalazimu.Lingine ni kwamba si kila unaemuona bank kasomea finance and account wengine ni sociologist,BA education etc.au kila unaemuona akifundisha kasomea ualimu, hapana, imewalazimu kufanyia kazi mambo ambayo hawakuyasomea kutokana na kukosa hiyo nafasi ya field yake,na kukuta opportunity ambayo either inahitaji training au sivyo anafanya anaajiriwa!

Sasa kuna brother mmoja amegraduate last year BAGE mambo ya Geography and evironmental studies, akaja kupendeza ofisini pale victory collection, kwa kua alikua mjanja tukapiga story mbili tatu nikampa business card nikamwambia kama nikiona post sehemu yeyote basi nitamchek akasema poa.
sasa kuna rafiki yangu ambaye alinipigia simu juzi tuesd, akaniambia kuna nafasi ya kusimamia hotel ya baba yake ambayo anaifungua tar 21 this month, mshahara akasema ni laki 2 lakini jinsi biashara itakavyokua mhusika ataongezewa, akaniambia purposely kwa ajili yangu kwani kuna watu kibao tena watu wazima wanaililia hiyo nafasi ya umeneja wa hoteli lakini wanaambulia kuwa tayari amepatikana, na hyo dada alinilenga mmi ndo nichukue nafasi hiyo. niliitamani sana nafasi hiyo ila kutokana na kutingwa sana na mambo yangu na kuna kaproject nakafanyia evaluation ambapo kamkataba kanaisha march this year, nikasema ngoja basi nimchek yule brother chap, kumpigia majibu aliyonipa ndiyo yaliyonifanya niachie post hii yaani,.
ILIKUA HIVI:
Baada ya kumpigia ile jumanne akaniambia mh nashukuru sister ila siwezi kufanya hiyo kazi kwani haiendani hata kwa asilimia moja na field yangu, halafu mshahara ni mdogo sana, nikamwambia unaishi wapi? akaniambia usa river hapa arusha, basi nikamchek yule sister kama kuna commission ya malazi na msosi akaniambia hamna shida kwa heshima yangu, coz nlimwambia kuna mdogo wangu ambaye ni huyu kaka sasa, atapewa room hapo hotel kwa miez 6 bure then akiwa anatafuta, msosi mara tatu kwa siku unapata, hotel yenyewe ipo ngaramtoni hapa arusha. nikamchek tena nikamwambia hizo commission akaniambia mshahara sasa sister ndo ishu, siwezi kuyafikia malengo yangu kwa mshahara huo, na degree yangu laki mbili???? hapana, ndivyo msg yake ilivyosema,,.basi nikamwambia poa all the best in searching for good job with wonderful salary..nikamwona huyu ameishia kuiona hiyo laki mbili tu hakujua kama comisison aliyopewa imemsave nauli, msosi na gharama zinginezo zisizo na ulazima, yaan kwa kifupi kwa mwezi hiyo laki mbili inaweza kutulia kwenye a/c tuli bila kuguswa.

USHAURI WANGU KWA VIJANA TUNAOTAFUTA AJIRA
mnapopata bahati kama hizi jamani msiziache ziende, hebu ona mfano hyu brothermen ameachia laki mbili wakat hana la kufanya home, haingizi hata mia,bora hata muuza karanga,. unadhani kufanikiwa kunaanzia juu jamani?? tuulizeni sisi tulianzia wapi mapaka tukawa kama tulivyo. unapopata kazi yeyote ambayo itakufanya uwe busy na una uhakika wa kupata hata elfu 2 kila siku, kwa ushaur wangu fanya usiache, weka degree yako chini piga kazi, hata kama ni kuuza duka, we fanya kwani siri ya malengo yako si iko moyoni mwako jamani??? ukiona mchongo mwingine unaondoka unaufata, yaan hakuna mazingira magumu kama ya kutafuta kazi wakati huna chochote unachofanya, yaan haupo kazini wala hujishughulish na chochote then unatafuta kazi, yaaan utachoka sana, unaweza ukawa dukani ukajuana na wateja leo na kesho haohao ndo wakakutoa,.,.hebu naomba tukue kiakili jamani umri unakwenda, majukumu yanakuja, miaka inakimbia bado unasubiri tu mshahara wa laki 5? pigana kijana ujikomboe wewe na jamaa zako.
SAMAHANINI SANA JAMANI MIMI HUWA SIISHIWI MANENO KWANI MNAJUA MIMI NI SOCIOLOGIST, NAJUA NIMEWACHOSHA ILA NASHUKURU KWA KUUPATA UJUMBE HUU NADHANI UTAKUA FUNDISHO NA MUUFANYIE KAZI.
Napatikana amelinechao@gmail.com
 
Kuna mazingira humfanya mtu kuwa selective, huwezi jua, labda alikuwa ameshaitwa fanya usahili mahali penye maslahi zaidi anasubiri majibu. Kwa si kila kitu mtu anaweza kukuambia, wakati kutafuta ajira watu wengi hufanya siri, hasa kwa watu waisio karibu yao.
 
Dah!
Bahati Kama Hiyo, Inikute Mtu kama Mimi
Nitaikumbatia Kwa Mikono Miwili
Kapu Langu La Karanga Napiga Teke!
Nimekuelewa Dadangu Kazi Njema!
 
kaka mm nmesoma psychology ni ngumu ukiongea na mm jambo la uongo kulifanya liwe la kweli, kwanza personality tu alivyo sharo hata hii kazi nilihisi tu hatakubali kwani watu wa kulambalamba midomo, suruali chini ya kiuno ni ngumu kukubali kazi za kigumu namna hii, ye anawaza gari miezi mitatu anunue gari halafu aje kupokea vilak,. i know vijana.com wengi wanapenda vilaini, utadhan mtu kaambiwa asukume mkokoteni bwana?
 
ndio mana wengi wanaishia kuolewa na MAJIMAMA??
 
huyo dogo hataki kazi, kuna wenzie wako nhc wamejiattach wanalipwa 280 kwa mwezi, usafiri, chakula na malazi juu yao tena wako dsm, mpotezee hataki kazi huyo
kaka mm nmesoma psychology ni ngumu ukiongea na mm jambo la uongo kulifanya liwe la kweli, kwanza personality tu alivyo sharo hata hii kazi nilihisi tu hatakubali kwani watu wa kulambalamba midomo, suruali chini ya kiuno ni ngumu kukubali kazi za kigumu namna hii, ye anawaza gari miezi mitatu anunue gari halafu aje kupokea vilak,. i know vijana.com wengi wanapenda vilaini, utadhan mtu kaambiwa asukume mkokoteni bwana?
 
Watu wanafanya kazi kwa mwezi 90 elfu hyo ----- sana angekuwa ndugu yangu sikai naye tena
 
Ebwana sie kweli watu wanapenda kula bata ni kwamba hata ww kitu kama hukiwezi hutakiweza maana vitu vingine ni interest ya mtu so je kama mtu hawezi kuuza karanga utamlazimisha si ndio atakula mtaji ww toa mawazo ya maana labda vijana tuongane tuanzishe restaurant ya kisasa ili hata yule mwenye degree haita mdiscourage sana maana atakuwa kivulini sasa mwanang kuuza karanga na umepiga BCOM hapo hapana
 
sijasema auze karanga bali kuna kazi ambazo wewe mwenye degree unaweza kuzifanya ingawaje zaweza kufanywa na mtu yeyote hata ambaye hana elimu ya form four. mfano ni kama hiyo tu ya umeneja wa hotel tena si bar ni hotel!!!
thats why nimesemaa anaetaka kazi ya maana atasubiri sana wakat anashindwa kuzitumia opportunities zinazojitokeza,
we unasema kula bata?? kuna kula bata hapo au kung'aa sharubu tu? kuna msemo wanasemaa,"UKIONA SIMBA KASIMAMA MBELE YA SWALA HALAFU AKAMWACHA UTAWEZA KUJIULIZA, MBONA HAMLI? KUMBE WAKATI MWINGINE SIMBA NAE ANASHIBA HATA AKIONA KITOWEO ANAKIACHA TU".Sasa kwa jinsi ambavyo vijana wamejaa mtaani jobless hasa wasomi,halafu wanalalamika, wengi wao hujidai eti simba alieshiba, wakat anakaa kimya akisubiri ofisi za kiyoyozi na walet nono........ntaendelea kusema kuwa, matatizo mengi yanayotusibu hasa hili la ukosefu wa ajira tunajitakia.
tunatakiwa kusemaa, HAKUNA AJIRA, NA SI KUSEMA HAKUNA KAZI!!!!!
 
Bora amekiri kama hawezi kuliko angekubali then angefanya kazi chini ya kiwango!
 
aisee umenisikitisha sana!mwanasosholojia na kauelewa ka psychology umeshindwa kubadili akili ya 'kondoo' mmoja anaepotea?nguvu unayoitumia hapa ungemuweka chini kijana ukamuelewesha nadhani angebadili msimamo,badala yake unajustify sijui mlambalamba midomo,suruali kata k...ndo nini sasa.
Ama ulikuwa na dhamira nyingine kwa huu uzi wako?
 
hakuna ambalo sijafanya wewe brother kisoda, sijazaliwa jana, nimeonana nae na nimetumia jitihada zoote kumconvice but ameonyesha kuwa hajaridhishwa na kazi yenyewe na mshahara, so inafikia point ukiwa unamshauri mtu haitakiwi ionekane kama unamlazimisha kwani itafikia huko alikosema mdau makala, kufanya kazi chini ya kiwango, na lifestyle ya mtu kuibadili si rahisi inategemea na background yake,kwani kuna hulka na tabia, u can change the behavior but u can ever change the nature of the person, mtu akishaathirika na uasili ni ngumu kubadilika but kama ni tabia ni rahis sana, sasa nilishagundua ameshaathirika na uasili,,kwa taarifa yako sisi sociologist kama ulikua hujui si wanasiasa wala watu wa blahblah ni watu wa jamii,tunapenda jamii iamke thats why matatizo mengi kwa vijana yanatufanya tusilale tuwaze usiku na mchana ni jinsi gani wanaweza kusaidika, we unadhani mm huwa sina shughuli za kufanya na kukaa na kuandika andika tu humu? tuna malengo pia kuwep jf kama wewe umeitwa na rafika shauri yako.
 
Kuna mazingira humfanya mtu kuwa selective, huwezi jua, labda alikuwa ameshaitwa fanya usahili mahali penye maslahi zaidi anasubiri majibu. Kwa si kila kitu mtu anaweza kukuambia, wakati kutafuta ajira watu wengi hufanya siri, hasa kwa watu waisio karibu yao.

kwel huyo kijana aacha mambo ya kizamani kwamba kama mtu hana kaz basi afanye kazi yoyote. Au kama mtu hana kaz bas avumilia kunyonywa kwa kulipwa ujira ambao haulingana na jasho lake. Msitumia tatizo la ajira kuwasulubu wenzenu. Kila mtu anamalengo yake na price yake. WE CAN NOT BE CHEAP BECAUSE OF PROBLEM OF EMPLOYMENT.
 
am sorry brother mmi si kijana ni mdada tena wa kitanzania ninaejitambua, ninaejua ni nini nafanya, tatizo lenu hamsomi hoja kiundani na kuelewa ni nini kimeandikwa au hampitii comments za watu vizuri, yaan unaamka kitandani tu kwa kukurupuka na kuandika tu, narudia tena sijasema afanye kazi yeyote, bali kazi mbadala ambayo unadhani itakusaidia, kama umeridhika na maisha just sheeet@ achana nayo, hakuna aliekuambia your cheap, and afterall employment is everything for many youth hear in tanzania, whether you like or not kuna mazingira yatakulazimu tu uwe cheap, labda wewe umejiridhisha kimaisha waache wale ambao wanadhani wanaweza kusaidika kwa namna moja au nyingine wasaidike usiwakatishe wenzako tamaa brother, wewe labda haupo tz hauoni matatizo wanayopata vijana mtaani tena wasomi, ninavyomwambia mtu afanye kazi yeyote tena ambayo si aliyosomea namaanisha kumsaidia katika kupunguza ukali ha hali ngumu ya maisha, kuliko kukaa home na kusubiri ajira bora na mazingira bora ya kazi. sasa hivi si kama zamani watu wanagraduate maelfu kwa maelfu nafasi za unakuta wanaozicontrol nao ni vijana ambao wanasubiri miaka 50 ndo wastaafu, unavyomwambia mtu eti askikubali kufanya kazi yoyote asubiri ajira bora unamuua.
NAENDELEA KUSISITIZA KWA VIJANA WENZANGU FANYENI KAZI YEYOTE ambayo unaona itakufanya kuyafikia malengo yako kuliko kukaa bure home. kama hujanielewa wewe muarubaini nichek amelinechao@gmail.com
 
thanks majigo, tusaidie vijana wenzetu hata kwa mawazo tu, najua fedha hatuwezi kuwasaidia wote bali hata mchango wa mawazo unatosha.
 
dar! Ina maana mdada siyo kijana?
 
majigo wala usiwaze alielikoroga atalinywa, eti anashangaa mimi mdada,,.hilo nalo ni la kushangaa?
 
kwel huyo kijana aacha mambo ya kizamani kwamba kama mtu hana kaz basi afanye kazi yoyote. Au kama mtu hana kaz bas avumilia kunyonywa kwa kulipwa ujira ambao haulingana na jasho lake. Msitumia tatizo la ajira kuwasulubu wenzenu. Kila mtu anamalengo yake na price yake. WE CAN NOT BE CHEAP BECAUSE OF PROBLEM OF EMPLOYMENT.

Kama anajitegemea that is good. Lakini kama anakaa kwangu halafu ananing'iniza makende yake kwenye kochi na remote mbele ya TV ana flip channels kutwa nzima, na anafungua friji yangu kujihudumia kama yuko heaven, nitamkimbiza aondoke kwangu, akatafute mume kama ameshindwa kujitambua yeye ni mwanaume na anahitaji kusimama kwa miguu yake mwenyewe.
 
[/COLOR]

aaaah aaah umenikumbusha kuna dada angu alikataa kazi ya laki 4, home walimkalisha kikao
 
Back
Top Bottom