Ushauri wangu kwa vijana mnaotegemea kujiunga na vyuo vikuu

Ushauri wangu kwa vijana mnaotegemea kujiunga na vyuo vikuu

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
1,683
Reaction score
2,158
Natumai mko poa sana,

Ki umri ni kijana wa makamo (early 30s) mwajiriwa na serikali yetu Tukufu ya Jamuhuri. Kwa elimu ni graduate wa chuo kikuu.

Katika safari yangu ya maisha nimepitia mengi, mazuri na yenye changamoto pia kitu cha kawaida kabisa kwa tulio wengi.

Kabla sijaajiriwa nilikuwa na matumaini makubwa sana ya kutusua kimaisha, hii ilitokana na ufinyu wa taarifa rasmi toka kwa waliokazini tayari zinazohusiana na maslahi yatokanayo na kazi.

Nakumbuka wakati niko chuo kikuu nilipata kwenda likizo mara kadhaa kijijini kwetu. Mara zote sikuacha kupata mshituko kila nilipowaona rafiki zangu wengi tuliosoma nao shule ya msingi wakiwa wamepiga hatua kadhaa kimaisha. Kuna waliokuwa na mashamba makubwa, biashara ndogo ndogo na kubwa lakini pia wengine wengi tu wakiwa tayari na familia zao tena na watoto zaidi ya mmoja.

Nilijipa moyo na kukazana katika masomo yangu. Na wachache kati ya hao marafiki zangu waliokuwa wakinipa moyo na kunionea wivu pengine wakiamini huko mbele nitakula kuku kwa mrija pasipo kuhangaika na purukushani za biashara wala zile za kilimo kama wao maana vijana wengi hawapendi kabisa neno kilimo .

Uhalisia nilianza kuuona mwaka wa kwanza wa ajira yangu. Wakati wale tulioachana darasa la saba au kidato cha nne wenye juhudi zao wengi walikuwa tayari wanamiliki nyumba zao, mimi nilikuwa nahangaika na nyumba za kupanga tena chumba kimoja.

Wakati wao wanafamilia tayari, mimi nilizidi kujipa muda sababu kubwa ikiwa ni kisingizio cha maisha.

Wakati wao walikuwa na uwezo wa kutatua baadhi ya changamoto zao na wazazi wao kwa wakati (kwa sababu walianza kupambana zamani) mimi ilikuwa lazima nisubiri mwisho wa mwezi.

Hayo ni machache sana, kuna mengi sana ya kueleza.

Nachotaka kusema hapa kwa watarajiwa wa kuendelea na elimu ya juu sio kuwakatisha tamaa. La hasha! Nataka mjue kuwa kusoma ni jambo moja na kufanikiwa kimaisha ni jambo jingine kabisa.

Ni lazima mtambue kuwa maisha si lelemama hata ukiwa kazini. Kama unawiwa kuwa mkulima masarani, hakuna muda wa kusubiri, unaweza kuanza sasa! Kama unawiwa kuwa mjasiriamali, chukua hatua sasa! Usisubiri eti lazima umalize chuo kwanza wala usiseme hauna mtaji!

Hao uliowaacha kijijini huna budi kuambatana nao! Ukianza kujitenga nao sasa hivi, hakika utajitenga nao milele na utajitenga na kazi wazofanya! Fikiria rafiki yako wa shule ya msingi ambaye sasa hivi analima nyanya, ukimpoteza sasa hivi kwa sababu tu unajiona msomi, siku ukipigwa na maisha kazini ukatamani kuwa na kazi mbadala ya kulima nyanya, utapata ujasiri wa kumkabili akupe ushauri!?

Usishangae siku unabahatika kupata kazi, halafu Baba /mama mwenye nyumba akawa rafiki yako aliyefeli darasa la saba au kidato cha nne kisha akageukia upande mwingine.

Elimu nzuri ni ile inayotuleta karibu na jamii sio inayotutenga na jamii.
 
Nimekukubali Mkuu siku zote wenye pesa ni wafanya biashara hata Bill Gate mwenyewe aliacha masomo alipokuwa Havard University na akaendelea na mishemishe zake mpk leo ndo Tajiri Namba 1
 
Nimekukubali Mkuu siku zote wenye pesa ni wafanya biashara hata Bill Gate mwenyewe aliacha masomo alipokuwa Havard University na akaendelea na mishemishe zake mpk leo ndo Tajiri Namba 1
Bill Gates mwenzako aliacha shule Na anafanya mambo Yale yale aliokua anasomea chuno,na aliokua Na msingi mzuri Na computers.
Ndio namna akatusua.
 
Kusoma rahaaa,,, biashara kizunguzunguu tupuuuu,,, ukiwa na elimu biashara haitakusumbua sana kuliko kutokuwa na elimu,, ahasante kwa maono yako,, ila shule ukipata nafasi ya kusoma soma sana zaid ya sana sio kukalili masomo,, ukihamua biashara jipange kutafuta msomi akuhibie tofautii na hapo utaishia biashara ndogo ndogo
 
Mkuu umeeleweka,sioni sababu ya kubisha kwa sababu uhalisia tunauona .life is undefined
 
Ukitokea msiba home unakuta darasa la saba wanarudi na mikoko huku master's holder ndo kwanza kakopeshwa nauli, kweli tupambane. Afu naonaga ukishakua na kadiploma kako komaa na mishe zako mambo ya kujichosha na makaratasi umri nao unakupita japo nakiri elimu ni nzuri ukiwa na pesa pia.
 
Be-kind.jpg
 
Back
Top Bottom