Ushauri wangu Kwa swala la Ndugai na Mnyika!

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kwa Maoni Yangu ni Kuwa Wabunge wetu wanaiga Tabia za Mabunge ya Nje! Katika Mabunge ya Nje yenye nidhamu ni Bunge la Senate la Marekani (sio house) Na katika Mabunge yenye zomea zomea nidhamu mbaya ni mabunge ya Uingereza na South Afrika. Ila yote yale yasio na nidhamu na Hili la Mfano, US Senate, wanayofanana ni Pale ambapo Speaker akimwambia mtu Muda Umeisha, wabunge asilimia kubwa tu wanamia Dakika Kama moja Kumalizia. To me ningekuwa Speaker hili huwa nalichukia sana. Ni bora uombe mheshimiwa naomba kwa dakika moja nihitimishe! Akisema sawa hitimisha Akisema hapana kaa chini!


Swala la Juzi!


MNYIKA: Myika ni Kijana Mahiri sana, Swala la Kuitwa ni Mwizi alikosema, Ila alishamtibua Ndugai kwa Kuwa Ndugai alishamwambia ameeleweka Mnyika yupo tu! Lile lilikuwa ni Kosa! Kwa hiyo isingelikuwa ni Hii Kuitwa Mwizi, Mnyika hili la kupitiliza muda au kufanya Arguments na Speaker analifanya. Na anatakiwa aidhibiti hiyo hulka. In short ni Tabia mbaya! Siwezi kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ilihali nataka afanikiwe!


NDUGAI: Ndugai ni Mtu Mzuri sana kwa Upande wangu, Ila yeye bila kujua ana Mizaha isiyoeleweka Vizuri, na anaonyesha Ushabiki ambao kwa Kiongozi Mkuu wa Bunge kunawafanya Wahuni kama lusinde kufikiri wamepewa impunity kutumia lugha chafu kudhalilisha etc. Na kama mkimsikiliza lusinde akianza alikuwa akijigamba atamfanya mbunge fulani ajinyee nguoni.

Swala Lingine kuhusu Ndugai ni kuwa anahama kutoka Mzaha kwenda kwenye ghadhabu ghafla bila nitice au dalili. Mimi nilishamsoma kuna sauti fulani akianza kuitoa Nasema oh shit. Mimi Ningeshauri, Mimi ningeshauri aache utani mwingine, na Pia ikibidi Mbunge atoke nje amwambie atoke kwa hiyari yake na kama akikataa ndio atumie askari. Pili asitamke adhabu akiwa na hasira, amtoe nje ili apate muda wa kurejea na kutafakari kilichotokea.


KIFANYIKE NINI: Mh Ndugai Arejee Adhabu ya Mnyika mimi bado naona Mnyika ana kosa, Lakini Pia lusinde na aliyemuita Mnyika ni Mwizi wanastahili kupewa adhabu kwani Wamemdharau kwanza Mnyika, Pili Speaker na Tatu Bunge lenyewe. Kuhusu Ester Bulaya mimi sioni Kosa Lolote alilolifanya kwa Kuwaashiria Wabunge wa Upinzani watoke nje!

Kuhusu Halima Mdee mimi naona ni Uchungu, Wanaonewa Nje wanaonewa Bungeni, Yeye tu Juzi alilazimishwa kuomba Radhi, lakini anaona Mwenzake Kaitwa Mwizi Speaker hana habari! So ali act out of Pain na Wamama wako defensive! Hata kama Mbunge wa CCM akionewa utaona wamama wa CCM wakimtetea! Na walipotoka kule nje Halima hakuongea kitu! Anyway Ester na Halima hawana Kosa la Kustahili adhabu.

lusinde!

lusinde mimi ningekuwa Bungeni ningemfunza adabu, Maneno yake ya kanga za mitaani yasiyo na substance sawa! Lakini anitamkie maneno yasiyo na heshima kama kuniambia ati atanifanya ninyee nguo! Nangoja Bunge linaisha, kisha namfuata, nakata bonge la mtama! Akiwa anaenda chini Nakumba mkofi wa Machoni, Akitua chini nakwatua bonge la mteke linatua pale south kwa chief Butelezi, Akiinuka nachota ndoo! Kisha akiwa chini akiomba poo huku mkono mmoja kashika chini na mwinhine kaninyooshea kusihi namuuliza kule ndani sikukusikia vizuri ulikuwa ukisema? Akiwa hajajibu namwambia inuka timua ile anainuka na kunipa mgongo nampa buti la kwenye Mabashite, nikichomoa mguu kiatu kinabakia kusikosemeka aende nacho akamwonyeshe mkewe!

Just Kidding kwa hili la lusinde ila seriously this measure might straight him up!
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaah! Nimeishia kucheka huo utani wa chini ni kama nakuona vile kufanya hayo
 
Tatizo ni kudhani hao watoto wa nje tu ndio wana haki ya kuudhi na wenyewe hata wasiguswe!
Mnyika alitangulia kusema CCM ni wezi baada ya Lusinde kusema upinzani wanasapoti wezi. Katika hali ya kawaida hutegemei angechukizwa kiasi kile na hilo neno. Zaidi ya yote, siyo yeye na kwa namna anayotaka, atakayeamua mbunge aliyeropoka awajibishwe! Haikuwa hivyo hata kwa Mdee na hata kwa Bulaya. Mnyika should not feel any special!
Kwa Ndugai mi naona sawa, namna alivyozi handle ishu za Mbowe, Mdee na Bulaya karibuni inathibitisha. Ila hata kama baba utacheza na watoto vizuri tu, ili mradi wajue kuna ukomo tu na wauzingatie...
 
Back
Top Bottom