Ushauri wangu kwa Rais Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa Rais Jakaya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Mar 23, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Nina ushauri ufuatao kwa Rais Jakaya Kikwete:

  1. Rais Jakaya Kikwete unaonekana kukerwa sana na baadhi ya watendaji, ambao hawajawajibika kiasi cha kutosha na kusababisha 'poor service delivery'. Njia nzuri ya kuwafanya hawa watendaji wawajibike zaidi si kuwatembelea na kuwauliza kwa nini kitu fulani hakiendi. Mimi nashauri Rais usijichoshe bure na kufanya hivyo, bali hao watendaji, ambao unaona hawajawajibika waite na kuwapa barua ya 'warning' ikieleza kuwa kasi ya utendaji wao ni mdogo inabidi wavute soksi la sivyo fagio la chuma litawakumba!

  2. Ukifanya hivyo, kila mtendaji, ambaye hujamwita, atawajibika kwa vile atajua itakuja zamu yake kupata 'warning' pia. Njia hii inasaidia kwa vile ukimkaba bosi mmoja naye atawakaba walio chini yake na itaendelea hivyo hadi kwa mtendaji wa mwisho. Hapa ndipo utaweza kupima vizuri nani anawajibika na nani hawajibiki na wale wanaoendelea kutowajibika wawapishe wanaoweza kuwajibika. Ukifanya hivi, kasi ya uwajibikaji itaongezeka.

  3. Tumia njia ya kushtukiza kama unataka kutembelea wizara au kitengo fulani. Hii ni kwa sababu kwa hali ilivyo sasa hivi, Watanzania wamejifunza kuwa waongo sana. Mfano mzuri ni wa simu. Siku hizi tunawasikia watu hata kama wapo hapa Dar es Salaam, wakipokea simu mfano kwenye daladala wanajibu: "Sasa tunakaribia Morogoro, hivyo nitafika huko kesho." Watu wameamua kuwa waongo bila aibu na tena uongo wa hadharani wakati watu wengine wanasikia au wanaona kuwa siyo kweli. Vivyo hivyo, ukiwaambia watendaji waandike taarifa watakupamba na utachoka na sifa zao. Lakini ukifanya ziara za kushtukiza kama unataka kupima utendaji kazi katika wizara fulani, itakusaidia kuona hali halisi kuliko pale ambapo ungetoa taarifa kuwa utaenda kutembelea. Kumbuka mara tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mwaka 2005, ulitembelea Manzese sehemu iliyokuwa chafu sana.

  Lakini watu walifanya kazi usiku na machana na siku ulipofika ulikuta kila kitu safi!!! Hii haisaidii sana kwa hali ya sasa ya Watanzania. Uongo umekuwa sehemu ya utamaduni wa Watanzania! Hivyo, wanahitaji kushtukizwa ndio wajue kuwa wanatakiwa kuwa tayarai muda wowote na kama kuna kitu kinahitaji ripoti basi watoe kama ilivyo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anapojibu maswali ya papo kwa hapo bungeni. Hajiandai na anajibu kulingana na swali linavyoulizwa. Hivyo, watendaji wako pia itabidi wajiandae kufuatilia miradi ya maendeleo au majukumu yao ya kila siku kwa karibu sana kiasi kwamba wakiombwa watoe taarifa wawe wanajua nini kimefanyika na nini bado.

  4. Njia hii ni njia mojawapo ya kuweza kurudisha nidhamu ya kazi na uwajibikaji. Baadhi ya Watanzania, naweza kusema, wameigiwa na ugonjwa wa kupenda kulipwa mshahara bila kufanya kazi. Kuna baadhi ya ofisi za serikali ukienda utafikiri umefanya kosa kwenda kupata huduma. Naomba Mungu akusaidie upate njia ya kuweza kuwaongoza Watanzania vizuri. Endelea kuwa na uvumilivu (broad shoulders) bila kuhamaki pale unapopata 'criticisms' na wala usichoke kama vile Pinda alipovyokuwa akisema akiwa Kagera kuwa "Kuna wakati utakosa subira!" Endelea pia kusikia kilio cha Watanzania na kukitafutia suluhisho - uliwaahidi maisha bora lakini wengi bado wanaishi kwenye maisha duni. Ni kama ulisema: "Kila Mtanzania atakuwa na maisha ya dhiki."

  Otherwise, tusonge mbele! Changamoto zetu si mwisho wa yote ni mwanzo tu wa kuonesha bado tunayo kazi kubwa mbele yetu!
   
Loading...