Ni kweli leo nilitazama bunge la asubuhi, aisee ni kweli huyu jamaa anakurupuka sana kuuliza maswali yasiyo na tija ama kuomba miongozo kwa ajili ya ufafanuzi ambapo kwa sehemu kubwa kama angetulia ama kujipanga vizuri angekuwa amashapata jibu ama kuelewa kilichofanyika, lakini cha ajabu na ulimbukeni mkubwa wa kutoka media coverage anaingia kichwa kichwa na kuuliza vitu ambavyo ufafanuzi ukitolewa anakuwa amepwaya sana, kiasi kwamba huwezi kuamini kama Mh. Tundu Anthipas Lissu ni mweledi aliyebobea kwenye Sheria.
Lazima abadilike asilazimishe umaarufu