YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Niiombe Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge Wanapotengeneza kanuni wasisahau kuchukua kipengele cha katiba ya nchi kinachosema kila binadamu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake na kukiweka kwenye kanuni.Na wakifafanue kuwa kutukana au kuzomea ni kutompa heshima na kutothamini utu wa mtu na ni kuvunja katiba ya nchi.Hivyo mbunge yeyote atakayezomea au kutukana achukuliwe kama mvunja kanuni na katiba ya nchi na ashughulikiwe.
Kipengele hiki kitasaidia kuondoa uvunjaji katiba wa mabunge yaliyopita ambako tulishuhudia wabunge wengi wakivunjiwa heshima na kutothaminiwa utu wao kwa kuzomewa au kutukanwa.
Kushangilia ni ruksa sababu ni kuheshimu mtu na kumthamini