Najua chama kina nia na sababu ya kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi uliopita ambao wabunge wateule wa Chadema walipigiwa kura ya hapana kinyume na kanuni za uchaguzi za EALA. Najua vile vile kutokana na mapungufu kwenye uchaguzi huo endapo utapingwa mahakamani Chadema wana nafasi kubwa ya kushinda kesi.
Ushauri wangu ni kwamba, pamoja na uwezekano wa kushinda kesi, hebu achaneni na mipango hiyo badala yake ongezeni majina ambayo yatawalazisha wabunge wa CCM kuchagua majina wasiyoyapenda. Ukitaka kumkasirisha mpinzani wako mpe kitu asichokipenda kama Magufuli anavyowafanyia wapinzani, yeye kasema hapangiwi na ukimpangia ndio unaharibu. Chadema nayo itumie mbinu hiyo kuwachanganya wapinzani wenu zaidi.
Napendekeza majina yafuatayo yaongezwe yapelekwe kwa Katibu wa bunge,
1. Fredrick Sumaye,
2. David Kafulila,
3. Regina Lowassa,
4. Ezekiel Wenje,
5. Lawrance Masha.
Naamini yeyote atakayechaguliwa kutokana na majina hayo atakuwa si moto tu kwa CCM na wabunge wake bali pia kwenye bunge lenyewe la EALA.
Nawasilisha.