Ushauri wakuu: Mke wangu amenichagulia mke wa pili nimuoe

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za majukumu wakubwa.. Kama kichwa cha habari kinavosema hapo juu.

Leo baada ya kutoka kitandani mke wangu ameniomba kitu ambacho kimenishangaza na sikuamini kwamba angefikia hatua ya kunishawishi nioe mke ambae amempenda yeye.

STORI INAANZA:

Kuna jirani yangu ana mdogo wake wa kike ambae ana takribani miaka 18 au 19 amekuja harusini hapa. Sasa katika kupiga stori likaingia suala la ndoa na mke wangu akampenda yule mdada ili aolewe na mimi na yuko radhi wakae nyumba moja.
Sasa nimejaribu kumuliza mke wangu kwanini umenichagulia mke huyo?

"Nimekuchagulia mke huyo kwasababu tunaendana tabia na pia yeye amependa kuolewa uke wenza na wewe vile vile familia yao nimeikubali kwakuwa haina ushirikina. Pili bado ni mtoto mdogo hasomi tena nahitaji umsitiri".

Ni kweli mimi kila siku wimbo wangu nikutaka kuoa mke wa pili lakini mke wangu anachoogopa ni kuja kuleta mshirikina akamfanyia masuala ya ajabu ili apendwe yeye na istoshe mke wangu ana wivu sana sasa nimeona ni fursa kwakuwa kamchagua mwenyewe acha niitumikie.

Sasa nimeona bora nije nalo hapa tushee kwa pamoja.

NB: Mke wangu yupo serious na hili na leo anamwita nije niongee nae.
 
Wanaelewana hao, amejua atamtunzia siri za kuchepuka, itakua kaanza kutumia siku nyingi kama mpeleka habari kwa mtu wake,... Kwahiyo anamvuta ili awe karibu... Na usikute kaka yake ndo anapiga hapo, kwahiyo kamleta wifi yake awe mke mdogo ili aendelee kula utamu wa ampendae kwa dhati,... Hivyo viumbe vina roho ya ajabu huwezi kuvielewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
In short; hakuna mwanamke anayependa kuolewa kwenye uke wenza na hata km ni masharti ya kidini basi huwa wanakubali kwa sura ya nje lkn hawakubali kwa roho na mioyo yao.
Mwanamke anayekubali mitaala yule huenda alikubali kuolewa na ww sababu ya shida tu lkn mwanamke akupendaye kwa dhati hawezi kubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na tamaduni za sehemu, usiwe unapenda kuhitimisha hitimisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaelewana hao, amejua atamtunzia siri za kuchepuka, itakua kaanza kutumia siku nyingi kama mpeleka habari kwa mtu wake,... Kwahiyo anamvuta ili awe karibu... Na usikute kaka yake ndo anapiga hapo, kwahiyo kamleta wifi yake awe mke mdogo ili aendelee kula utamu wa ampendae kwa dhati,... Hivyo viumbe vina roho ya ajabu huwezi kuvielewa

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanawake ni mafiaaa kudadek🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom