Magoa
Member
- Mar 20, 2013
- 28
- 5
Habari za muda huu mimi ni kijana nilikuwa na uhusiano na msichana mmoja na tuliweza kupata mtoto mmoja wa kiume hakika ya mapenzi yetu yalikuwa mazuri lakini na mapungufu ya kibinadamu yalikuwepo tatizo la huyo msichana lilopelekea tutengane ni roho ya uchoyo alikuwa hapendi ndugu zangu ilifikia hatua ninapomwachia pesa ya kula ye alikuwa hashughuliki na chakula badala yake anaenda kununua nguo nilimuelimisha lakini akifuata kama siku 7 au 10 anarudia ile tabia yake nilipomwambia kuwa mwenendo huu siutaki na sasa urudi kwenu ukaanze maisha yake hakukubali aliniomba msamaha na kuniahidi kuwa hatorudia mimi nikamkazia kuwa arudi tu maamuzi aliyoyafikia yeye alikunywa mafuta ya taa lakini hakufa baada ya tukio hilo kukawa na kikao alipoulizwa kwanini ulikunywa mafuta ya taa ? Alijibu kuwa mume wangu hanitaki tena nilipoulizwa mimi nikasema ni kweli simtaki kwa sababu ya tabia ya uchoyo aliyonayo wazee wakasema sio vizuri kwani tayari mna mtoto atakuja pata tabu ya malezi wazee walisisitiza juu ya hilo mimi nikayafunika na kuangalia matokeo ya baadae lakini mwendo ni ule ule nilipomrudisha kwao nako huko kanywa sumu pia hakufa kisa hawezi ishi bila mimi na mimi sijapenda mwenendo wake nifanyaje hapo wadau funguka kiukweli utani tupa kule na kama huna cha kusema we iache hii post
