Ushauri wako tafadhari

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Habari wana JF, na kwa wale waliofurahishwa na maamuzi ya mahakama ya Rufaa jana basi niwaambie peoplezzzzzzzzzzzzz!

Kimsing nayakubali sana mawazo ya watu humu Jamvini, hivyo basi nikaona ni busara na hekima kupata mawazo yenu katika hili ninalolifikiri mwenzenu.


Kwa ufupi, baada ya kusoma kwa msoto mkali mimi mtoto wa mkulima hatimaye mwaka huu nimebahatika kupata BA yangu ya ualimu katika masomo ya LINGUISTICS and LITERATURE IN ENGLISH, hivyo natumaini kupangiwa kituo cha kazi mwakani kama wanavyosema mawaziri.

Tatizo langu kubwa ni kwamba naona kabisa level hii ya elimu hainitoshi kabisa napenda niendelee na masters hasa somo la LITERATURE kwani nalipenda sana, ukiongeza na mishahara ya ualimu na mazingira mengine ndo basi napata hamu zaidi, ila kazi si ichukii kihivyo kama wengine niliowaona.

Ninachopanga kwa sasa ni kwamba nikiingia tu kazini nisimalize hata mwaka niende shule japo najua sheria hazisemi hivyo, lakin nimefikia mahala nawaza kufanya juu chini, na mungu anisaidie hata kwa njia zisizo halali niweze kufanikisha hili, kwani sina kitu ila naamini nikipata kaupenyo nikaenda na kamshahara nikawanakapata naweza kusonga bila shida.

Ombi langu ni kwa wazoefu huko kazini, je naweza kweli fanikisha mpango wangu huu, naomba mwazo yenu tafadhari.
 
Mtu hawezi kuishi kwa mkate tu bali kwa neno lolote lile lililo hai....usiwe na haraka na maisha..miaka miwili siyo mingi, piga miaka miwili halafu omba ukasome itakupa baraka zaidi , utasoma kwa amani na vilevile utakuwa na uhakika na mshahara pamoja kazi yako kuwa salama.
 
Kwanza hongera kwa kuhitimu Mi nakushauri ujpange coz adi ss ujajua utapangiwa wapi na km mungu akijalia upangwe dar basi inawezekana hasa udsm coz kwa dar ndo najua inatoa master kwa hilo kozi yako jipange na iktokea upangwe uko interior kuna open university kwaio uskonde cha mcngi mwombe mungu muweza wa yote
 
Ucwe na haraka ukaharbu kaz subr uone umepangwa wap kama n mjn utasoma hata jion utokapo kazn kama n bush miaka 2 co mng bt endelea kuwa ns lengo la kusoma had phd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…