Nilikuwa na mchumba ambaye nilimtambulisha hata kwa ndugu zangu(dada). Lakini baadaye alikuja kunigeuka bila kunieleza sababu ya kufanya hivyo. Alinitumia tu msg kunitaarifu kwamba anaolewa na mtu mwingine baada ya muda mrefu wa kukaa kimya bila mawasiliano kwani alikuwa mbali nami. Iliniumiza sana kwani nilimpenda na sikutegemea kufanyiwa hivyo na yeye. Huyo ni wa pili baada ya wa kwanza kuniambia nina muda mrefu na shule hivyo hawezi kunisubiri. Imepita kama miaka saba kati ya hivi visa viwili na kati niliwahi kuwa na mtu mwingine ila niliachana naye baada ya kutofautiana msimamo. Toka huyo dada wa tukio la karibuni kunifanyia hivyo nimejikuta nakuwa tofauti na nilivyokuwa mwanzo kwani nimepoteza kabisa interest na wanawake na hata kufikia kuwatukana ovyo. Hata wale niliozoeana nao kabla siku hizi wananiogopa hata kunitania. Yaani nimekuwa mtu ambaye kila mtu ananishangaa. Hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata dada zangu natofautiana nao kauli bila sababu na kuanza kuwafokea. Wengine wameanza kukesha kwenye maombi kuniombea. Nimejitahidi kupambana na hii hali lakini dah, hali ngumu na siipendi kwa kweli. Naombeni ushauri nifanyaje ili nirudi kawaida?
Endelea tu kujiweka mbali na wanawake na ujiweke karibu zaidi na MASOMO yako, matokeo utayaona baadaye. Mapenzi siku hizi ni ubabaishaji tu, wekeza ktk elimu yako ndugu yangu.
Bro Nyalotsi...if symptoms persist pale Muhimbili kuna dokta mmoja anaitwa Dr. Hogan..mtafute ubonge naye! Atakusikiliza vyema...
nenda kwa madaktari wa magonjwa ya akili au wanasaikolojia wakakupe ushauri nasaha!!!!!!!!!!!!
Dada kaunga nashukuru kwa ushauri, nitaucheki huo uzi. Lakini mi nitammiss nani?
mkuu, teh!! Yule mama ataona namtania kwani ni mwalimu wangu. Ndo maana nikasema nimepigana sana mpaka sasa bado sijapelekwa kupewa haloperidol. Lakini nitacheki hali itakavyokuwa. Nashukuru kwa ushauri
Mkuu umeua lolz..kwa madaktari wa magonjwa ya akili tena.. Hiyo balaaa!
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Wait a minute.
Nina cases tatu za wahskaji waliosoma medicine halafu issue za breakup au kukataliwa na demu zikawazingua sana. Could there be something? mmoja wapo nakumbuka ilikuwa so serious mpaka akalazwa na dokta wake ndo alikuwa huyo mama Horgan.
Usiogope if u think u getting worse wahenga husema, "Mficha maradhi...kifo humuumbua."
asante kwa ushauri,
Wait a minute.
Nina cases tatu za wahskaji waliosoma medicine halafu issue za breakup au kukataliwa na demu zikawazingua sana. Could there be something? mmoja wapo nakumbuka ilikuwa so serious mpaka akalazwa na dokta wake ndo alikuwa huyo mama Horgan.
Usiogope if u think u getting worse wahenga husema, "Mficha maradhi...kifo humuumbua."
hakikisha unauzingatia ,kwasababu ni wa kweli na utakuokoa kuelekea kubaya zaidi........ nipo serious japo kuna watu wanaweza wakahisi ninajoke.
mkuu niko kazini hayo masomo nilishamaliza muda. Au unanishauri nianze tena kusoma.? Maisha yangu yatakuwa shule tu? Ujue kuna social life ambalo naona niko withdrawn nalo. Am a man, nahitaji kuwa na maisha ya kama wengine.