Ushauri wa wengi humu ukiachwa unambiwa tafuta hela

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,520
Habari za asubuhi wakuu,

Tumaini langu mmeamka salama salmini na wale wenye matatizo ya afya, au mambo mbali mbali ya kimaisha basi mola jalali awape takhfifu na afya njema.

Nimefatilia nyuzi mbali mbali za watu ambao wanaomba ushauri hasa wanaume wanapoachwa ,Ushauri wa wengi ni kuwa watafute hela,Maana wakiwa na hela kila kitu katika mapenzi kitakuwa sawa.

Swali la kujiuliza je ni kweli wenye hela wote kila kitu katika mahusiano kinawaendea sana inamana ndoa zao ziko salam kwa ajili ya pesa?

Pili na je masikini ndoa zao hazina raha au amani kwa sababu hawana pesa?

Jambo hili binafsi nalikataa kwa nguvu zangu zote.

Sio kwamba suluhisho la kukataliwa na watoto wa kike basi ni kukosa pesa, inamana kila mwanamke katika dunia hii kipaumbele chake ni pesa? Hapana hili si sahihihi kabisa wakati mwingine ebu turudisheni uwanaume wetu jaman tuache kujificha katika kichaka cha pesa kwa kuficha madhaifu mengi tulio nayo.

Wakati mwingine tunakataliwa kwa madhaifu mbali mbali tuliokuwa nayo,hasa mionekano yetu na wakati mwingine hata kutokujijali wenyewe kimuonekano hata kimavadhi na pia hata kutokuwa na kauli tamu na laini juu ya hawa watoto wa kike..

Mwanaume kuamini pesa ina'ngoa mtoto wa kike huu ni udhaifu wa kiume na kutokujiamini kama mwanaume na badala yake kuamini pesa kuliko uwanaume, huku ni kufeli kabisa kuwa mtoto wa kiume.

Wengi Hatujawajua wanawake vizuri na Hakuna mpaka leo anayewajuwa,nini Hasa wanataka wanataka, kwanza kuna vitu vingi wanatifautiana sana na kuna vitu vingi wanafanana sana ambavyo hivyo lazima kila mwanamke anavyo na hipo vingi wanatofautina sana na ndomana, ukinipa mwanamke wako mimi siwezi ishi naye na Nikikupa wangu huwezi ishi naye,kutokana na utofauti walo kuwa nao.

Pia hakuna anayeweza mtimizia mwanamke, kila anachotaka, sana sana tu aridhike basi yeye mwenyewe, akiridhika atakwambia napata kila kitu na ukitaka ujuwe kuwa huwa hawatosheki bali wanaridhika pale mtapogombana ndo ataanika mapungufu yako yote. Ila mwanzo wakati mko kwenye mahaba niuwe alionyesha kila kitu kiko sawa.

Wanawake wanasiri kubwa na Mungu amewapa uvumilivu mkubwa sana na ndani yao wameficha sumu kubwa sana na kama siku atamuwa kuitema huwa inaleta maafa makubwa sana, huwa wanasiri nyingi sana wanazo na uvumilivu mwingi na mkubwa sana walopewa na Mungu.

Huwa nasisitiza sana
1.omba sana mwanamke akupende
2. na epuka sana mwanamke akuchukie

Akikupenda huwa anaridhika na akikuchukia basi atakudhalilisha sana

1.Vipi mwanamke anaweza kuridhika?

Mwanamke akikupenda, moja kwa moja ataridhika na ww kwa kila hali,uwe na kibamia uwe huna hela yaani vyovyote vile basi yuko radhi.

Usidhani wanawake wote walokuwa na mahusiano basi ni kweli wanapata kila wanachohitaji kutoka kwa wanaume zao, kuna vitu vingi wanamiss ila wameridhika kuvimiss sababu waliokuwa nao wamewapenda na wameamuwa kuridhika tu.

Kuridhika kwa mwanamke huwa ni chaguo ambalo huja automatic baada ya kumpenda mwanaume ,au huja kwa maamuzi fulani.

Na hakuna jambo zuri kwenye maisha kama mtoto wa kike akuridhie, maana ukweli katika dunia hii hakuna mtu ambaye mungu alimpa vyote na hakuna ambaye mtu mungu alimnyima vyote.

Ukijua kuna vitu mungu kakupa basi kubali vipo vingine navyo mungu atakunyima ,Dunia hii mungu ameweka katika uwiano.

Usifikiri wenye pesa wanakila kitu yaani Mungu akupe pesa na akupe na kila kitu wanawake wanachotaka, hili hapana atakupa pesa ila kuna vingine ataunyima.

Kwahiyo pale mtoto wa kiume anapodhani kuwa na pesa kuna mridhisha mtoto wa kike au kuweza kummiliki kila mtoto wa kike, hili ni jambo la uwongo.

Wengi wanasema na kutoa mfano kuna jamaa labda ana hela mademu wanamshobokea kisa ana hela na anawagonga kweli.

Ni hivi wapo mademu ambao wao wenyewe wameamuwa kujirahisisha kwa ajili ya hela tu na kipa umbele chao ni pesa.

Na wapo wanawake wenye misimamo yao na wana jielewa na wanajua nini wanafanya hawa huwa hawababaiki na pesa za mtu na hata akiamuwa kukupenda basi hampendi mtu kisa kwa pesa zake.

Kukataliwa huwa kuna mambo mengi na si kila anayekataliwa ni pesa tu.

Wakati mwingine tunakosa ushawishi, au kukosa mikakati mizuri au njia tunazotumia kutomshawishi yule mtoto wa kike, au kukosa mabalozi wazuri sehemu husika.

Tuwe tunamtindo wa kujitathmini kwanza. Hii itachangia kuongeza ufanisi kwetu
 
Ndefu mno imebidi nisome tu kichwa cha habari, huo ndio juwa ushauri wao(haswa wanaume) ila ukiwazungumzia masuala ya pesa wanageuka kuwa mbogo balaa,wanakimbia vivuli vyao.
Nimeandika ndevu kutokana na unyeti wa jambo lenyewe jaribu tu kuipitia
 
Pesa ndo kila kitu usijidanganye. Ukiwa na pesa huwezi kuachwa hata kidogo.

Mwanamke hata kama ana mapenzi na wewe lakini kama hapati mahitaji muhimu mwisho wa siku atakuchukia tu.

Pia linapokuja swala la pesa, ujue kuna levels za maisha. Inategemea na levels zenu. Kuna level ambayo akipata laki kwa mwezi yaani inamtosha na anajisikia vizuri sana. Kuna level ambazo laki moja ni lunch moja tu.

Cha muhimu ni kuhakikisha unatafuta within your level.
 
Shukran wala hilo sijali maana sio wote watakukubali ila penye ukweli lazima usemwe
Mi sikatai ulichokisema hpo juu ila ndg yng tunaishi hku mitaani tunaona mahusiano mengi yanayovunjika ni machache sana huvunjika kwa sababu km ulevi,gubu,ugomvi nk cna takwimu sahihi ila nna hakika haivuki 10% na 90% zilizobaki zote tatzo pesa aidha kijana umemaliza chuo ajira ngumu demu anaamua kuolewa ama ulikuwa na kazi nzuri ukasimamishwa unaachwa, ulikuwa na biashara ikafa unaachwa, hatimiziwi mahitaji yke sawasawa unaachwaa,umeaumwa muda mrefu huingizi tena pesa unaachwa yaani tuache kubishana kwenye hili vtu vpo wazi c tunaona mitaani? watoto wa kike kwenye hela achana nao kabisa mi ctaki hata kuwaskia ni wachache sana huridhika na upendo wa kweli kudekezwa na kujaliwa!
 
Ndefu mno imebidi nisome tu kichwa cha habari, huo ndio huwa ushauri wao(haswa wanaume) ila ukiwazungumzia masuala ya pesa wanageuka kuwa mbogo balaa,wanakimbia vivuli vyao.
Utanifafanulia baadae shemeji, maana leo umewahi siti yangu
 
mkuu watu wengi wanaoachwa ukifuatilia malalamiko yao hutupa lawama kwa mwanamke bila ya kujielezea wao walikosea wapi? sasa unajiuliza huyu mwanaume kama alikuwa anampenda, anamjali anamsikiliza, ana mjali in general japoa hana pesa.. sasa hapo unaona kabisa kilichokosekeana ni pesa, na kama anapesa basi mchoyo si mtoaji...

ndiyo maana tunasema tafuta pesa tutakuganda hata uweje..

back to matajiri wanachangamoto nyingi tu kwenye mahusianokwa picha ya watu wa nje wakiona kila siku unatoka na gari nyumba kubwa wanadhani kila siku wewe unapesa la hasha . kuna siku tajiri anakosa pesa unakuta zote zipo kwenye mzunguko au mamabo hayaendi vyema so wanapitia changamoto tena nyingi tu
 
Mi sikatai ulichokisema hpo juu ila ndg yng tunaishi hku mitaani tunaona mahusiano mengi yanayovunjika ni machache sana huvunjika kwa sababu km ulevi,gubu,ugomvi nk cna takwimu sahihi ila nna hakika haivuki 10% na 90% zilizobaki zote tatzo pesa aidha kijana umemaliza chuo ajira ngumu demu anaamua kuolewa ama ulikuwa na kazi nzuri ukasimamishwa unaachwa, ulikuwa na biashara ikafa unaachwa, hatimiziwi mahitaji yke sawasawa unaachwaa,umeaumwa muda mrefu huingizi tena pesa unaachwa yaani tuache kubishana kwenye hili vtu vpo wazi c tunaona mitaani? watoto wa kike kwenye hela achana nao kabisa mi ctaki hata kuwaskia ni wachache sana huridhika na upendo wa kweli kudekezwa na kujaliwa!
mkuu inategemea na mwanamke uliye amuwa kuishi naye si kila mwanamke anaweza kuwa mke ,hata hilo unalosema mimi sikatae ila tunakosea sana kwenye kuchagua

wengi tunaowa wanawake sababu tunawapenda hii ndo shida
 
mkuu watu wengi wanaoachwa ukifuatilia malalamiko yao hutupa lawama kwa mwanamke bila ya kujielezea wao walikosea wapi? sasa unajiuliza huyu mwanaume kama alikuwa anampenda, anamjali anamsikiliza, ana mjali in general japoa hana pesa.. sasa hapo unaona kabisa kilichokosekeana ni pesa, na kama anapesa basi mchoyo si mtoaji...

ndiyo maana tunasema tafuta pesa tutakuganda hata uweje..

back to matajiri wanachangamoto nyingi tu kwenye mahusianokwa picha ya watu wa nje wakiona kila siku unatoka na gari nyumba kubwa wanadhani kila siku wewe unapesa la hasha . kuna siku tajiri anakosa pesa unakuta zote zipo kwenye mzunguko au mamabo hayaendi vyema so wanapitia changamoto tena nyingi tu
miss chagga umezungumza kitu kizuri kuna wakat tuulizane tatizo ni nini ,maana sio kila mahusiano yanavunjika kisa mwanaume huna pesa
 
miss chagga umezungumza kitu kizuri kuna wakat tuulizane tatizo ni nini ,maana sio kila mahusiano yanavunjika kisa mwanaume huna pesa
sasa wengi hawataki kuwa wazi mkuu.. wakisema tatizo in detail bila kuwa bias utaweza toa ushauri unao eleweka .. sas wanatuwekea upande mmoja tu , upande wa pili hatujui
 
mkuu inategemea na mwanamke uliye amuwa kuishi naye si kila mwanamke anaweza kuwa mke ,hata hilo unalosema mimi sikatae ila tunakosea sana kwenye kuchagua

wengi tunaowa wanawake sababu tunawapenda hii ndo shida
Umesema tusioe kwa sababu tunawapenda tu naomba npe ss sababu za msingi tofauti na hyo!
 
Back
Top Bottom