Ushauri wa Rais Magufuli kwa Rais Museveni kuhusu Bomba la Mafuta

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
1.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Mei, 2016 amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni kwa kuapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa kipindi kingine cha miaka 5 na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi Uhusiano, ushirikiano na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.

Viongozi hao pia wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania, Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandalasi mmoja.

"Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.

"Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu" Amesema Rais Magufuli.


Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo, na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu"Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.

Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania.

"Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo" Amesema Rais Museveni.

Katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Museveni iliyofanyika kabla ya mazungumzo hayo, pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
Kampala
 
Kwenye mradi huu Watanzania tunapaswa kuungana kama tulivyoungana kuhakikisha mradi huu unapita nchini badala ya Kenya.Let's keep on supporting the project without making our EAC Partner Kenya feel offended

Hata hivyo Serikali sasa iwaandae wananchi Vizuri hasa kule ambako Mradi utapita isijekutokea tena Suddent eviction ikaleta violation of human rights

Wananchi wa Pande zote waandaliwe vizuri kuwa friendly kwa project hii
 
Museveni hajajibu hilo la kutumia makandarasi wengi kufupisha muda wa ujenzi.....nadhani ni wazo zuri! Wameshajua kuwa tuna pressure sana na mradi huo! Tuna pressure kuliko Uganda wenyewe!! Anataka mapato zaidi aweze kuwekeza kwenye ahadi maana anajua ahadi zake zinahitaji vyanzo vya uhakika vya mapato! Viwanda kila kanda...meli zile kila ziwa reli barabara hadi mikoani kote etc!
 
Back
Top Bottom