Ushauri wa mahusiano bila malipo

Ushauri wa mahusiano bila malipo

KarugendoTz

Member
Joined
Mar 7, 2025
Posts
34
Reaction score
58
Wana JF, uenda hampendi ushauri niutoao – ushauri wa mapenzi, mahusiano na maisha ya ndoa. Lakini nawambia machache tu, kwamba mimi kama mimi, ushauri na maelekezo natoa bila malipo, wala haina haja ya kuudhika kwa ushauri wangu na uonyaji wangu. Wengine wanatuita eti ni Wasukuma, lakini wewe unayeona kama vile mimi nimelenga pesa unakosea.

Tangu mwaka 2021, natoa ushauri huko Facebook, WhatsApp, na YouTube, na wala hata sijawahi kuomba pesa ya mtu. Lengo ni kuokoa ndoa zinazovunjika kwa mambo ya kipuuzi. Kama hujui, fanya uchunguzi uone watu wanavyovunja ndoa kwa mambo yasiyoeleweka.

Basi kama wewe unaona huwezi kuingilia suala la kushauri wanandoa au wachumba, huo ni uelewa wako. Sisi tunapenda ndoa ziendelee, lakini kama hutupendi sisi watoa ushauri, usitutusi, jipitie zako tu. Anayependa kubadilika kwenye ndoa yake atatusikia na kufanya maamuzi atakayoamua.

Asanteni wana JF, kikubwa tusitukanane ndugu zangu.
 
Tag Account yako ya youtube tafadhali
 
Naomba uwashauri KATAA NDOA wote wa JF tafadhali...

Alisikika mchungaji wa JF akiongea...
 
Back
Top Bottom