Maisha haya hayana mwenyewe,
Nilikuwa mtu mwenye kujiheshimu sana, kuwashauri watu juu ya matendo mema, niliishi nakujitahidi kuwa mfano wa kuigwa lakini sasa mambo yamegeuka.
Tangu utoto na ujana umenifikia sijawahi kuwaza na kunywa pombe ila sasa nakunywa tena kunywa kweli usiku hadi nilewe ndo nilale! sometimes naenda kwenye kuwasilisha ripoti za kazi kwenye kadamnasi maboss wakiwepo ila nakunywa ili nisipate mawazo katikati ya kazi(kama kitwanga alivyofanya)
Nisipokunywa nakuwa very aggressive kwa watu akinikosea kidogo nitampandishia hadi jioni nikirudi mwenyewe naona aibu machozi yananitoka
Nimekuwa mtu wa ajabu sivyo nilivyokuwa zamani natamani siku zirudi nyuma kichwa kinaniumaaa!
Katika kukua kwangu wazazi wangu walinichukia sana hasa mama! nilisoma kwa shida hawakuwahi kunipa moyo! kila nililofanya ni baya natukanwa na naambiwa lazima ntafeli! shuleni nafanya vizuri najitahidi kufanya kazi kwa bidii nyumbani ili mama anipende ila wapii! mama yangu mkubwa& shangazi ndio walinipa moyo sana wakiniambia ni majaribu nitashinda! nilimaliza kidato cha sita bado bikra ila mama akishirikiana na mashoga zake wananiita malaya nilikuwa naumia niliahidi kutorudi nyumbani baada ya kupangiwa form five, ila imani ya dini iliniingia nikawasamehe nakuwapenda tena sana.
Sikuwahi kujivunia upendo wa wazazi japo ndugu na majirani walinipenda nankunisaidia sana mawazo n.k baadae nikaja kujua ni rafiki wa mama yangu alikuwa anamjaza umbea mama ili nisisonge mbele!
Nikiwa chuo mwaka wa tatu nikaona si vyema nikawa na mpenzi! hapa kidonda cha mfadhaiko wa kukosa upendo nyumbani kilitoneshwa, tulikuwa wapenzi bila kufanya chochote tukamaliza chuo ile nimepangiwa kazi tukawa wilaya moja hapo sasa pombe ikatiwa maji tumeweka mipango ya kuoana bado miezi 2 tukavunja amri ya 6 na mimba juu kwakweli huu msumari wa moto nilijichoma,
Bwana yule alikuwa na wanawake 3 kawazalisha (bado anakumbushia kwa 2) kawaahidi kuwaoa, sijakaa vizuri mara ananiambia tukanunue uganga akomeshe watu wanaomloga kidogo nizimie! hapo movie ilinoga na tukaachana nimebaki na mtoto wangu ila najikuta nna msongo wa mawazo wa tangu niko primary sasa hivi hata mambo madogo siwezi vumilia kitu kidogo kinaniumiza
Hatimaye nakunywaaa ndugu wala marafiki hawajui ulevi huu sinaga marafiki wa karibu yangu kila mtu namuona mbaya.
=====
Tazama thread hii na maoni yake yakisomwa ktk Jamii Leo