Ushauri wa bure kwa viongozi wa UKAWA

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,577
Reaction score
2,227
Wanajamii,

Mimi ni mmoja na wana mapinduzi na mfuasi wa mageuzi au niseme mabadiliko katika nchi yangu. Sote sisi watanzania tunafahamu na kujua ni kwa jinsi gani RUSHWA NA UFISADI unavonyima haki na usawa katika jamii zetu.

Hivi juzi Raisi Magufuli alianza kwa kazi na spidi kubwa kuijenga nchi yetu kwa upya kabisa. Ni mengi na tumeshangazwa kwa yale yaliyojificha lakni tukae kujiuliza je,kuna mengi yapi ambayo hatuyajui?

CCM ni chama kilichokosa dira.Ni chama cha wanyan'gan'ganyi.Watanzania walimchagua magufuli pamoja wengi wetu hatukukubaliana na ushindi huu,lakni niseme tu,kuwa ni bora MAGUFULI alipita kuliko angechukua LOWASSA.

Watanzania,muda sasa umefika kila mtu ajenge nchi na kuvuna kile alichopanda kwa haki.Hawa watu au viongozi tunawapa ridhaa kutuongoza ila ndio watu wa kwanza kuibia nchi na kujitajirisha wao na familia zao nathani hii ifike kikomo.

Rai yangu kwa wana ukawa na wale wanaotaka mageuzi katika nchi yetu naomba tumpe support Raisi magufuli.
hata kama TISS haitamlinda sisi watz tutamlinda maana anapigania maslahi mapana ya nchi na sio kabila wala mtu mmoja mmoja.

Tanzania mpya inakuja na tumwombe Mungu atufikishe huko tunapokwenda.Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana. Watu wanasema hazina hakuna kitu lakini hawakumbuki kwamba nchi ina deni kubwa kuliko miaka yote ile.
Tumwombee sana Rais Magufuli kwenye hili .


Tanzania Nakupenda.
 
Kama umeandika point hivii...wacha nirudi kulala nkiamka ntasoma tenaa
 
Kaa ukijua Mh Rais J P M ni MwanaCcm. Hakugombea kupitia TLP wala Nn.
 
Kaa ukijua Mh Rais J P M ni MwanaCcm. Hakugombea kupitia TLP wala Nn.

Angekuwa Mwana CCM asingepuuzwa na viongozi wa CCM mikoa/wilaya wakati wa zoezi la kusaka saini za wadhamini,Dr Magufi hakuwa chaguo la Wana CCM kwakuwa hakuwa na sifa zile za kuitwa Mwana CCM,kinachowapata sasa hivi ndicho hasa walichokuwa wanajaribu kukikwepa.
 

Ckulijuwa hilo . So kumbe Mzee Mwinyi,Mkapa,Warioba,Kikwete nk. Walimfanyia kampeni kwa shinikizo tu la hakuna namna.
 
Ukweli ni kwamba chaguo la magufuli lilikuwa linatufaa wanyonge na syo mafisad wa sisiem ndyo maana kwa mda wote wa kampen maguful alisema kuna watu anajua hawatak na niwanafik na ndyo maana akaomba watanzania wampeleke ikulu akawafanyie KAZI, kwa namna moja au nyngne nimshkr lowasa kwan ndyo chachu kubwa ya haya tunayoyaona sashv, bila pilika pilika za lowasa ccm wangetuletea membe unategemea nn tungekuwa watu wakunung'unika na kudharauliwa hadi tunaenda makabulin.
 

Ubongo wako ni matope,hivi unataka kusema mwana ccm alieko tukuyu kule ni fisadi? Kulikua na mijizi michache inachafua chama,imekimbilia ukawa na mingine inaendelea kuminywa.mpaka 2020 ccm itakuwa chama kimbilio la wanyonge.ndio maana kwenye kampeni zetu tulikua tunasema ukitaka kuua kunguni usichome nyumba,choma godoro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…