Ushauri wa bure kwa Nape Nnauye

Ushauri wa bure kwa Nape Nnauye

magiri

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
40
Reaction score
21
Nimeona nitumie nafasi hii kumshauri kidogo mdogo wangu Nape. Nasema mdogo wangu si kwa maana ya madaraka bali umri kati yangu na yeye. ukimfanyia analysis Nape, kweli unaweza kugundua kwamba ni mwanasiasa mwenye kipawa(charisma) cha kufanya siasa. Na kweli kwa maana ya uenezi, ccm walikuwa wameramba dume maana ana kipawa cha kuongea na hivyo kufanya publicity sawasawa. kuna mambo machache ambayo naona nape anapungukiwa.

1) Nape anapungikiwa heshima. kwa wale wanaomsikiliza nape mara kadhaa wanaweza kukubaliana nami kwamba huyu bwana hasa anapokuwa ana jibu mapigo fulani yaliyoelekezwa kwake au chama chake, hugeuka mbogo na mara nyingi hufikia hatua ya kutukana hata watu ambao kibinadamu waliopaswa kuwa confronted sawa lakjni basi kwa hekima. Nape akianza kumsema dr. slaa utadhani ni mtu wa umri wake au mtu fulani hopeless hivi. kijamii haipendezi kabisa kuongea au kumtukana mtu anayekuzidi umri na hata binadamu mwenzako regardless ya umri ,madaraka , chama, cheo nk.

Najua nia yake ya kufanya hivyo inaweza kuwa kwa maana ya kufanya kinachoitwa kujenga chama chake, lakini akumbuke hao hao anaodhani anawajenga kuna siku watamuita mkosa adabu siku atakapowapinga, let it be kutafuta uongozi ndani ya chama au vyovyote. kumbuka wanaokushangilia na kukuita mfalme leo, kesho watakupiga mawe. jitahidi kuwa na mahusiano ambayo ni cross cutting kwa maana ya kuheshimu watu kwa utu na ubinadamu wao. Nani ajuaye? mtumwa wa leo anaweza kuwa mtawala kesho. kama ulimheshimu, kumbuka natumia kumheshimu na siyo kutomkosoa, atakuheshimu pia.

2) lingine ninalomshauri nape ni kupunguza kujiamini kuliko pitiliza. Kuna upande napendezwa na ujasiri wake but he is many times over confident. nimesema many times kwa sababu kweli mara chache sana nape huongea politely. Na kwa kujua hilo ebu ona wakati katibu mkuu wa ccm anapohutubia na awepo nape pia. unaweza dhani Nape ndiyo senior kwa katibu mkuu. yeye lazima atishe, na kutoa matamko makali makali dhidi ya wapinzani wao, kana kwamba yeye pale ndo final authority. Ni sawa inawezekana kuongea kwa mamlaka ndilo personality yake kulinganisha na personality ya kinana ambaye ni mpole kitabia, lakini akumbuke kuna siku wakubwa watamwambia hawakumtuma aseme hivyo.

Na namshauri tu kwamba siyo afya kiprotokali kuonekana wewe ndo mtoa matamko ya kimamlaka wakati kuna anayekuzidi cheo, vinginevyo niamini tu kwamba huwa anaambiwa na mamlaka aseme hivyo. lakini hata kama ni hivyo naye ajifunze kuchanganya na zake ili asionekane yeye ndo yeye, maana mwisho wa siku kama nilivyosema watu watamrudi yeye.

Najua anaweza kujiamini hivyo kwa sababu ana back up ya watawala na majeshi, lakini akumbuke madaraka yanaharibu na ni hatari. ktk uongozi moja ya mambo unayopaswa kujua kuhandle ni madaraka au nguvu. usipojua, hayo madaraka yatakuharibu wewe. (Absolute power corrupts absolutely). Nilishangazwa sana nilipomsikia Nape kwenye kampeni za chalinze. kweli jinsi alivyotamka kwamba ccm itajibu mapigo kama watachokozwa kweli unaweza ona ujasiri uliopitiliza.

Hivi mimi huwa najiuliza, vipi kama wengine nao wakianza kuona hawana pa kwenda kupata msaada na waamue kujibu? kwa viongozi wanaotawala sasa, zNape akiwemo siyo mfano mzuri kutamba hivyo. vinginevyo ni kuwafanya wengine waone hawana mtetezi na wajenge kiburi na kujilinda. other wise, namyakia Nape siasa njema. Ana kipawa na uwezo na matumaini mbeleni kama atakuwa disciple wa mawazo yangu machache hapo juu.
 
Siamini kama atakusikia, he counts himself second from the president not from Kinana
 
Nape hata kwa Imani aliyonayo tu haimruhusu kuropoka ovyo kiasi hicho vinginevyo labda awe amegeuka na kuwa muasi wa Injili.

Ushauri uliop ni wa maana sana Laiti autilie maanani na kuufanyie kazi siku zaidi ya hapo akidharau leo mausia hayo siku yaja Atajuta hapo CCM itakapomtelekeza hataamini yatakayompata.
 
Mkuu umemshauri kiungwana sana.Nami namuomba asikie ushauri wako.
Nasikitika kuwa siwezi kukufanya mshauri binafsi kwa sababu sitaweza kukulipa ila Mungu akubariki
 
Ahsante mr, Ngwanga kwa pongezi na kutambua mchango wa wengine. nadhani kwa kuwa wote hapa jf, tutaendelea kushauriana na kuelimishana maana wewe na mimi wote tuna namna ya kusaidiana na hasa kusaidia nchi yetu.
 
Kama Nape Msemaji wa CCM na Katibu wa Uenezi wa chama tawala hajamwelewa Jaji Mstaafu Joseph Sinde Waryoba ujue sasa Nchi iko rehani. Wala msimlaumu Nape maana yeye ni kama spika tu, anasema na kutoa sauti kutoka kwenye chanzo fulani. Hata ukimwangalia anapoongea unatambua kwamba anasema kitu amacho hata yeye mwenyewe haikielewi anachokisema.

Nadhani Mzee Mnawie angekuwa Hai ndo angemsaidia kuchambua mambo. Huwezi kabisa kulinganisha Hekima iliyoshushwa na Mzee Joseph Waryoba na mtu kama Nape ambaye hata umri wake ndani ya Chama, Uzoefu wake, Hekima yake hata shule yake na uwezo wa mitikasi ndani ya CCM hawezi hata kumfikia Mzee Waryoba hata kwa asilimia 2%.

Tunamshukuru Mungukwa kutuwezesha kuwaweka hai wazee wetu kama Mzee Joseph Sinde Waryoba, Jaji Agostino Ramadhani, Mzee Salim Ahamed Salimu, Mzee Joseph Butibu na wazalendo wa Ukweli akina Huphrey Polepole, na akina Prof. wa ukweli Baregu
 
Nape ana laana kila sehemu ya mwili wake kumbuka alishawahi kusema wazee walioko ccm wanasubiri kufa.
 
Magiri,
NAKUSHUKURU SANA SANA KWA USHAURI WAKO. NAKUAHIDI KUUFANYIA KAZI USHAURI WAKO! Kama wengi jukwaani hapa wangetumia style yako hii ya kushauri kwa lugha ya kiungwana sana jukwaa hili lingekuwa uwanja mzuri sana wa kuzungumza mambo makubwa!
Narudia kukushukuru sana!
Nimeona nitumie nafasi hii kumshauri kidogo mdogo wangu Nape. Nasema mdogo wangu si kwa maana ya madaraka bali umri kati yangu na yeye. ukimfanyia analysis Nape, kweli unaweza kugundua kwamba ni mwanasiasa mwenye kipawa(charisma) cha kufanya siasa. Na kweli kwa maana ya uenezi, ccm walikuwa wameramba dume maana ana kipawa cha kuongea na hivyo kufanya publicity sawasawa. kuna mambo machache ambayo naona nape anapungukiwa. 1) Nape anapungikiwa heshima. kwa wale wanaomsikiliza nape mara kadhaa wanaweza kukubaliana nami kwamba huyu bwana hasa anapokuwa ana jibu mapigo fulani yaliyoelekezwa kwake au chama chake, hugeuka mbogo na mara nyingi hufikia hatua ya kutukana hata watu ambao kibinadamu waliopaswa kuwa confronted sawa lakjni basi kwa hekima. Nape akianza kumsema dr. slaa utadhani ni mtu wa umri wake au mtu fulani hopeless hivi. kijamii haipendezi kabisa kuongea au kumtukana mtu anayekuzidi umri na hata binadamu mwenzako regardless ya umri ,madaraka , chama, cheo nk. Najua nia yake ya kufanya hivyo inaweza kuwa kwa maana ya kufanya kinachoitwa kujenga chama chake, lakini akumbuke hao hao anaodhani anawajenga kuna siku watamuita mkosa adabu siku atakapowapinga, let it be kutafuta uongozi ndani ya chama au vyovyote. kumbuka wanaokushangilia na kukuita mfalme leo, kesho watakupiga mawe. jitahidi kuwa na mahusiano ambayo ni cross cutting kwa maana ya kuheshimu watu kwa utu na ubinadamu wao. Nani ajuaye? mtumwa wa leo anaweza kuwa mtawala kesho. kama ulimheshimu, kumbuka natumia kumheshimu na siyo kutomkosoa, atakuheshimu pia. 2) lingine ninalomshauri nape ni kupunguza kujiamini kuliko pitiliza. Kuna upande napendezwa na ujasiri wake but he is many times over confident. nimesema many times kwa sababu kweli mara chache sana nape huongea politely. Na kwa kujua hilo ebu ona wakati katibu mkuu wa ccm anapohutubia na awepo nape pia. unaweza dhani Nape ndiyo senior kwa katibu mkuu. yeye lazima atishe, na kutoa matamko makali makali dhidi ya wapinzani wao, kana kwamba yeye pale ndo final authority. Ni sawa inawezekana kuongea kwa mamlaka ndilo personality yake kulinganisha na personality ya kinana ambaye ni mpole kitabia, lakini akumbuke kuna siku wakubwa watamwambia hawakumtuma aseme hivyo. Na namshauri tu kwamba siyo afya kiprotokali kuonekana wewe ndo mtoa matamko ya kimamlaka wakati kuna anayekuzidi cheo, vinginevyo niamini tu kwamba huwa anaambiwa na mamlaka aseme hivyo. lakini hata kama ni hivyo naye ajifunze kuchanganya na zake ili asionekane yeye ndo yeye, maana mwisho wa siku kama nilivyosema watu watamrudi yeye. Najua anaweza kujiamini hivyo kwa sababu ana back up ya watawala na majeshi, lakini akumbuke madaraka yanaharibu na ni hatari. ktk uongozi moja ya mambo unayopaswa kujua kuhandle ni madaraka au nguvu. usipojua, hayo madaraka yatakuharibu wewe. (Absolute power corrupts absolutely). Nilishangazwa sana nilipomsikia Nape kwenye kampeni za chalinze. kweli jinsi alivyotamka kwamba ccm itajibu mapigo kama watachokozwa kweli unaweza ona ujasiri uliopitiliza. Hivi mimi huwa najiuliza, vipi kama wengine nao wakianza kuona hawana pa kwenda kupata msaada na waamue kujibu? kwa viongozi wanaotawala sasa, zNape akiwemo siyo mfano mzuri kutamba hivyo. vinginevyo ni kuwafanya wengine waone hawana mtetezi na wajenge kiburi na kujilinda. other wise, namyakia Nape siasa njema. Ana kipawa na uwezo na matumaini mbeleni kama atakuwa disciple wa mawazo yangu machache hapo juu.
 
Ahsante sana Nape, you look gentleman. kama nilivyosema hapo nyuma sina wasi wasi na kipawa chako na uwezo wa kuongoza. Ahsante kwa kuelewa nia ya ushauri wangu na kuupokea positively. Thanks na kazi njema.
 
Ahsante mr, Ngwanga kwa pongezi na kutambua mchango wa wengine. nadhani kwa kuwa wote hapa jf, tutaendelea kushauriana na kuelimishana maana wewe na mimi wote tuna namna ya kusaidiana na hasa kusaidia nchi yetu.

Magiri,
NAKUSHUKURU SANA SANA KWA USHAURI WAKO. NAKUAHIDI KUUFANYIA KAZI USHAURI WAKO! Kama wengi jukwaani hapa wangetumia style yako hii ya kushauri kwa lugha ya kiungwana sana jukwaa hili lingekuwa uwanja mzuri sana wa kuzungumza mambo makubwa!
Narudia kukushukuru sana!

Mwacheni Nape awe mbabe !Hata mwili wake ni wa Kibabe .Namfananisha na rafiki yake wa Zamani ,Lowassa .HATA SURA WANAFANANA NA UMAHIRI MAJUKWAANI.Tofauti yao ni tuhuma.
Vyama vyote vina wababe:
CHADEMA -Lema na Rwakatare
CCM -Nape na Mwigulu
CUF-Mtatiro
Mambo yamenalansi.Alimradi wasipande majukwaani na silaha.
 
Mwacheni Nape awe mbabe !Hata mwili wake ni wa Kibabe .Namfananisha na rafiki yake wa Zamani ,Lowassa .HATA SURA WANAFANANA NA UMAHIRI MAJUKWAANI.Tofauti yao ni tuhuma. Vyama vyote vina wababe: CHADEMA -Lema na Rwakatare CCM -Nape na Mwigulu CUF-Mtatiro Mambo yamenalansi.Alimradi wasipande majukwaani na silaha.
Mkuu sentensi ya mwisho unamaanisha mwenyekiti wa Simba Sports Club?
 
Nimefurahiaa Nape ameelewaa ushaurii huu mzuri na makini. Binafsi Nape nakubali umejaliwaa kipawa cha kisiasa na si vyema ukakipoteza bure. Fuata kwa umakini ushauri huo. Hongera Nape kwa kuchukua jiko Rasmi.
 
Magiri,
NAKUSHUKURU SANA SANA KWA USHAURI WAKO. NAKUAHIDI KUUFANYIA KAZI USHAURI WAKO! Kama wengi jukwaani hapa wangetumia style yako hii ya kushauri kwa lugha ya kiungwana sana jukwaa hili lingekuwa uwanja mzuri sana wa kuzungumza mambo makubwa!
Narudia kukushukuru sana!

Nape ni mtu mzuri sana tatizo ni wanaompa ajenda!
 
Nimeona nitumie nafasi hii kumshauri kidogo mdogo wangu Nape. Nasema mdogo wangu si kwa maana ya madaraka bali umri kati yangu na yeye. ukimfanyia analysis Nape, kweli unaweza kugundua kwamba ni mwanasiasa mwenye kipawa(charisma) cha kufanya siasa. Na kweli kwa maana ya uenezi, ccm walikuwa wameramba dume maana ana kipawa cha kuongea na hivyo kufanya publicity sawasawa. kuna mambo machache ambayo naona nape anapungukiwa.

1) Nape anapungikiwa heshima. kwa wale wanaomsikiliza nape mara kadhaa wanaweza kukubaliana nami kwamba huyu bwana hasa anapokuwa ana jibu mapigo fulani yaliyoelekezwa kwake au chama chake, hugeuka mbogo na mara nyingi hufikia hatua ya kutukana hata watu ambao kibinadamu waliopaswa kuwa confronted sawa lakjni basi kwa hekima. Nape akianza kumsema dr. slaa utadhani ni mtu wa umri wake au mtu fulani hopeless hivi. kijamii haipendezi kabisa kuongea au kumtukana mtu anayekuzidi umri na hata binadamu mwenzako regardless ya umri ,madaraka , chama, cheo nk.

Najua nia yake ya kufanya hivyo inaweza kuwa kwa maana ya kufanya kinachoitwa kujenga chama chake, lakini akumbuke hao hao anaodhani anawajenga kuna siku watamuita mkosa adabu siku atakapowapinga, let it be kutafuta uongozi ndani ya chama au vyovyote. kumbuka wanaokushangilia na kukuita mfalme leo, kesho watakupiga mawe. jitahidi kuwa na mahusiano ambayo ni cross cutting kwa maana ya kuheshimu watu kwa utu na ubinadamu wao. Nani ajuaye? mtumwa wa leo anaweza kuwa mtawala kesho. kama ulimheshimu, kumbuka natumia kumheshimu na siyo kutomkosoa, atakuheshimu pia.

2) lingine ninalomshauri nape ni kupunguza kujiamini kuliko pitiliza. Kuna upande napendezwa na ujasiri wake but he is many times over confident. nimesema many times kwa sababu kweli mara chache sana nape huongea politely. Na kwa kujua hilo ebu ona wakati katibu mkuu wa ccm anapohutubia na awepo nape pia. unaweza dhani Nape ndiyo senior kwa katibu mkuu. yeye lazima atishe, na kutoa matamko makali makali dhidi ya wapinzani wao, kana kwamba yeye pale ndo final authority. Ni sawa inawezekana kuongea kwa mamlaka ndilo personality yake kulinganisha na personality ya kinana ambaye ni mpole kitabia, lakini akumbuke kuna siku wakubwa watamwambia hawakumtuma aseme hivyo.

Na namshauri tu kwamba siyo afya kiprotokali kuonekana wewe ndo mtoa matamko ya kimamlaka wakati kuna anayekuzidi cheo, vinginevyo niamini tu kwamba huwa anaambiwa na mamlaka aseme hivyo. lakini hata kama ni hivyo naye ajifunze kuchanganya na zake ili asionekane yeye ndo yeye, maana mwisho wa siku kama nilivyosema watu watamrudi yeye.

Najua anaweza kujiamini hivyo kwa sababu ana back up ya watawala na majeshi, lakini akumbuke madaraka yanaharibu na ni hatari. ktk uongozi moja ya mambo unayopaswa kujua kuhandle ni madaraka au nguvu. usipojua, hayo madaraka yatakuharibu wewe. (Absolute power corrupts absolutely). Nilishangazwa sana nilipomsikia Nape kwenye kampeni za chalinze. kweli jinsi alivyotamka kwamba ccm itajibu mapigo kama watachokozwa kweli unaweza ona ujasiri uliopitiliza.

Hivi mimi huwa najiuliza, vipi kama wengine nao wakianza kuona hawana pa kwenda kupata msaada na waamue kujibu? kwa viongozi wanaotawala sasa, zNape akiwemo siyo mfano mzuri kutamba hivyo. vinginevyo ni kuwafanya wengine waone hawana mtetezi na wajenge kiburi na kujilinda. other wise, namyakia Nape siasa njema. Ana kipawa na uwezo na matumaini mbeleni kama atakuwa disciple wa mawazo yangu machache hapo juu.
Ni kweli hana adabu maana kuna wakati alitaka kufanya mdahalo na Dr Slaa wakati yeye ni katibu mwenezi na mwenzake ni Katib Mkuu
 
CCM inapenda kuburuta watu kama hao halafu wakishindwa hoja waanze kulia lia kama Ole Sendeka., mwacheni apige kelele nadhan akija akisikia hotuba ya JK leo huenda akanywa sumu akajuta kwa nini mila za ccm amezitia pafuni
 
Wana JF,

Sidhani kama ushauri huu kwa Nnape unaweza kumsaidia na kumbadilisha. Sidhani. Wahenga walisema TABIA huzaliwa ,haina DAWA wala haitengenezwi. Nnape Nauye amezaliwa na tabia hii ya ubabe na ujeuri. Ni hulka,ni kitu kiko ndani ya nafsi au roho ya Bwana Nnape Nauye!

Huwezi kubadili hiyo hali labda Mungu tu ambadilishe huyu jamaa kwa kupitia WOKOVU! Nje ya hapo Nnape atabakia hivohivo mpaka siku yake ya mwisho. Kwa watu wasio na IMANI wanasema Nnape amerogwa na aliyemroga alishakufa siku nyingi kwa hiyo hata swala la kumpeleka kwa mganga/mchawi huyo ili amrudishe katika tabia za kiutu haliwezekani.

Kujua kuwa Nnape ni sawa na mtu aliyerogwa au mwenye mapepo jaribu kusikiliza kauli zake ambazo aghalabu huwa tete na zenye kuacha maswali mengi kuliko majibu siku zote. Kauli zilizojaa jazba, majigambo na upitilizo wa kujiamini! Mfano wa karibu kabisa ni huu wa juzi baada ya Hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji mstaafu J.S.Warioba kwamba swala la Serikali tatu haliepukiki kulingana na maoni ya Watanzania zaidi ya 60% na kulingana na sababu tena za msingi kabisa alizoziainisha Mwenyekiti, bado Nnape amekurupuka kama vile ametoka usingizini na KUNG'ANG'ANA NA SERIKALI MBILI kuwa ndiyo mwafaka wa Muungano!!!
Kwa mtu makini na aliyeenda shule anaweza kumjaji Nnape kuwa ni kama CHIZI ambaye huongea maneno bila kujijua anaongea kitu gani!!!!Mtu anapayuka tu kama Vuvuzela na bila hata kutoa hoja au sababu inayomfanya kutetea hizo serikali mbili. Ukimsikiliza huyu jamaa unaweza kubaini kuwa yeye ni kama wale ndege KASUKU ambao hukariri maneno ya lugha za Bin-adamu ilhali hawajui hata maana yake! Nnape hana tofauti na Kasuku!

Hivi Nnape na CCM yake hawawezi kujiuliuza kwa mfano; kwamba CCM walikuwa wapi wakti Zanzibar inavunja Katiba ya JMT kwa kuanzisha nchi yao yenye Mamlaka kamili? Kwamba sasa tuna SERIKALI 2 NA NCHI 2 badala ya SERIKALI 2 na NCHI 1. Kama CCM waliruhusu Wazanzibara wakavunja Katiba tena bila kuihusisha Serikali ya JMT kwa kufanya marekebisho kwenye Katiba basi waache sasa SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA ICHUKUE MKONDO KWA KUUNDWA KWA SERIKALI YA TANGANYIKA ili kuimarisha Muungano zaidi kuliko ilivo sasa.
 
Back
Top Bottom