Ushauri wa bure kwa bunge la tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa bure kwa bunge la tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jul 3, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Imekuwa ni desturi yetu kujipendekeza kwa boss hata mahali ambapo hapastahili.Sishangai leo hii bunge letu kusahau majukumu yake ya kuisimamia serikali na kuishauri na kugeuka mtetezi wa serikali kwa kujibu hoja za wabunge wengine kwa kuwa tu wanatoka upinzani.Kasi hii ya hoja za serikali kujibiwa na wabunge zimepelekea mawaziri kubweteka na kusahau wajibu wao kwa kuwa tu kuna wabunge ambao ni mabingwa wa kujibu hoja za wapinzani hata kama matatizo yanayosemwa na wapinzani hao yapo pia kwenye jimbo la watetezi hao(wabunge wa CCM)

  Hali kama hii imepelekea bunge letu kupoteza sifa ya kuwa bunge la wananchi na kugeuka sehemu ya kuponda hoja za msingi zinazo tolewa na upande ambao hausiani na chama tawala.Bunge hili limekuwa halina mvuto na kupoteza kiwango chake kwa kuwa tu viongozi waandamizi wa mhimili huu wa bunge wamegeuka kuwa washangiliaji wa upande mmoja na kusahau kuwa bunge linatakiwa kuongozwa kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizowekwa katika kuliendesha bunge.

  Hali kama hii inahitajika kufanyike mabadiliko makubwa katika mchakato wa katiba mpya kwa Spika wa bunge kutokutokana na vyama vya siasa,yaani asiwe na itikadi ya upande wowote ili kuhakikisha haki ikitendeka.


  Mapungufu makubwa yanayo jitokeza leo kwa bunge letu ni aibu kubwa na upungufu wa uadilifu kwa Spika na wasaidizi wake kwa kushindwa kuliendesha bunge kwa viwango na speed inayotakiwa.Kwa mapungufu haya inajidhihirisha kwa bunge kuridhia matukio ya ufisadi yaliyoshamiri nchini.

  Bunge limekuwa la upande mmoja,na maamuzi yamekuwa ya upande mmoja hali inayoweza sababisha ukumbi wa bunge siku moja kuwa uwanja wa mapambano.Kutokana na ushabiki uliokithiri inaonekana dhahiri bunge limekaa kimkakati kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi za kuwakilisha hoja zao.Hali hii imejidhihirisha pale wabunge wa upinzani walipotaka mwongozo wa Spika kuhusiana na hoaja ya madaktari inayo tishia usalama wa afya ya wananchi.Hoja zao zimekuwa zikipuuzwa na Spika kwa kusaidiana na wasaidizi wake huku akishangiliwa na wabunge waliotoka chama chake,hali ambayo ni hatari sana kama ikiachiwa iendelee.


  Ifike mahali wabunge wajitambue na kuyarudia majukumu yao ya kibunge kwa kuisimamia serikali dhaifu inayotokana na chama dhaifu kitendo kinacho sababisha wabunge toka chama tawala kugeuka watetezi wa serikali ili kukinusuru chama.Rais anapotoshwa,lakini kupotoshwa kwake hakumsaidi bali ni mbinu ya kukimaliza chama chake kwa staili ya samaki hujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe.

  Mihimili ya dola ipo mitatu,kila mhimili unajitegemea bila kuingiliwa na mhimili mwingine.Mbona hata siku mmoja hatujasikia mhimili serikali ukitetea mhimili bunge katika kujenga hoja na jinsi ya kukabiliana na wananchi wake.Tumeona mara nyingi bajeti ya serikali inapokosa tija mawaziri wa serikali huambatana na wabunge wa chama tawala kuinadi kwa wananchi ilihali kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.

  Mwisho napenda nichukue furs hii kuliasa bunge kama chombo cha utetezi wa wananchi ikiwa pamoja na mihimili mingine iachwe itekeleze majukumu yake kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano,na huo ndiyo ile dhana ya mgawanyo wa madaraka inapokuwa na mashiko.
   
Loading...