Wakuu nimewasoma!nashukuru sana kwa waliosaidia kujibu!yaani namaanisha nataka iwe ya kubeba abiria labda kwa mfano kutoka dar kwenda morogoro,au kutoka dar kwenda Tanga n.k.nilikua namaanisha hivyo wakuu manake kufanya ipige route za hapa dar utakufa na stress kabla ya mda si wako. Kuhusu huyu bwana Katabazi hapo juu ni kuwa kwa sasa naishi Dar Es Salaam na mkopo umebakia kidogo sana ambao naweza kumalizia kuulipa kwa biashara zingine tuu sio lazima nitegemeee hiyo gari.
Pili kuhusu mapato kwa ujumla wake hata kwa hivi sasa tunavyofanya za kukodisha kama tour ni kuwa at least kwa siku gari inatakiwa ilaze 80,000 ukikosa sana 70,000 baada ya kutoa operating expenses like posho ya dereva na mafuta kama utapata kazi ya kilometa isiozidi 1200 yaani 600 kwenda na 600 kurudi,kama kilometa zitazidi hapo inakuwa ni kati ya 150,000-200,000 per day.
Sasa nije why nataka kuachana na tours. Huku bongo bizz ni ngumu sana,madalali wameharibu kazi,mtu anakuja anataka kulalia kwa vile anajua kuwa gari haina kazi, kwa hiyo ukitaka hela nzuri ndio hivo unakata miezi hujapata kazi.Kwa mfano kwa ujio huu wa WEF(World Economic Forum) kilikua ni kipindi kizuri sana cha mapato,sasa jamaa waliokamata kazi wanakodisha gari kwa Tshs 150,000,dalali anashika kazi anakupiga na 80,000 per day mafuta ni juu yako. ni biashara kichaa ni bora uwe unajua wazi kuwa gari ina route ya Dar- Tanga kwa mfano mnapakia vichwa vyenu hesabu inaingia.
Ndio hivo wakuu nilikua naomba ushauri wenu.