Ushauri wa Anko.

Ushauri wa Anko.

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,928
*Dear Anko,*
Naomba msaada wako nifanye nini? Mimi ni mke wa mtu, na mume wangu tunapendana sana. Juzi niliondoka kwenda kazini nikamuacha mume wangu ana angalia TV. Sikufika mbali gari ghafla likazima, nikalazimika kutembea kwa miguu kurudi nyumbani nikamwambie mume wangu anisaidie. Nilipofika nyumbani sikuamini macho yangu baada kumkuta mume wangu na binti wa jirani yetu. Nilimkabili mume wangu na kwa bahati nzuri kakubali makosa kuwa uhusiano wao una mwaka sasa, lakini cha ajabu akasema atalazimika kumuacha huyo binti polepole ili asimchanganye kisaikolojia kwa kuwa bado mdogo anasoma college. Je hii ni sawa? Nifanye nini? Naomba
ushauri Mzee wangu.
Mimi,
Fransiska wa Mwenge.

*JIBU*
Binti yangu Fransiska,
Nimesoma kwa makini ujumbe wako, kitu ambacho nimekiona mara moja ni hili tatizo la gari kuzimika ghafla. Kwanini uendeshe gari na baada ya muda mfupi lizimike? Hapa kuna matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kuwa chanzo. Inawezekana plug mbovu au uchafu umeingia kwenye mrija unaopeleka mafuta kwenye injini. Au pengine ni tatizo la umeme, au fuel pump, ulicheki kama petroli ipo? Ikiwezekana waone mafundi hapo karibu warekebishe hivyo nilivyovitaja. Gari ikiharibika tena usiiache peke yake barabarani kuna vibaka sana.
Natumaini ushauri huo utakusaidia mwanangu.
Mimi Anko.
 
Hahahahaaaaa anko kiboko.
Kesi ya mbwa mwitu unaipeleka iamuliwe ma fisi
 
Pole Fransisca wa mwenge, unajua kuna tatizo jengine la huyo mwanafunzi, usichana unamsumbua hasa katika umri huo wa college. Mvumilie huyo mwanafunzi akikuwa mkubwa kama wewe ataacha kabisa hizo tabia.

Mwanafunzi ataathirika kisaikolojia na hata mitihani anaweza kufeli chuoni.

From: Your anco supermaket
 
Hahhaaaa huyu anko atakuwa anko nani sijui tu niseme

Back
Top Bottom