Ushauri: Utumishi wa umma uwe wa mkataba

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,705
Naamini wapo watakao niunga mkono na wapo watakao nipinga.Kutoka na utendaji usioridhisha katika ofisi nyingi za Serikali kwa Watumishi wa Umma nashauri ni vema Serikali ikaanzisha Utumishi wa Mikataba kwa watumishi wake kwa kupangiana Malengo ya kila Miezi 4 kama mwaka wa Serikali ulivyo.

Mtumishi anaposhindwa kuyatimiza atakuwa hastahiri kuendelea na Utumishi.Pia nashauri Mkataba uwe wa miaka 5 kwa vipindi viwili kwa maana ya miaka 10 analipwa Mafao yake yote.Utendaji wa Ofisi na Mashirika yasiyo ya Serikali unakuwa na Mafanikio kutokana Mtumishi kujua nipo kwa mkataba nisipofanya vizuri mkataba unasitishwa lakini Serikali watumishi wanafanyia kazi kwa mazoea na wanasubiri miaka 55 au 60 wastaafu.

Faida ya Mikataba ni kuwa Watumishi watakuwa wanapishana ktk ajira ndani ya miaka 5 au 10 kuliko sasa mpaka miaka 55 au 60.
 
hii haitakuwa na ufanisi na serikali itakuwa inatumia budget kubwa katika kuajiri kila mda, kuoneane kazini na majungu kwamba boss anaweza kukunyima mkataba kisa tu hakukubali au mmekwazana, waajhiriwa watatumia mda mwingi kutengeneza maisha yao maana hawatakuwa na uhakika wa kuwa kazini katika mkataba ujao kazi za ofisi zitazoroteka.

suluhisho nbi serikali iwalipe wafanyakazi wake maslahi mazuri then isismamie nidhamu makazini atakezingua unamchomoa
 
Msihangaike sana si lazima sote tuajiriwe serikalini, si lazima wote tuwe na maisha mazuri, hii dunia haijawahi kuwa na usawa na siku ikiwa na usawa naamini inaweza kuwa sehemu hatari kwa wanadamu na viumbe wote. Wengine tuko huku kwetu vijijini tunashika jembe tunalima na maisha yanasongo, waliojariwa wataamini wewe haujaajiriwa hivyo unawaonea wivu kumbe ni kweli au si kweli......
 
Ili utumishi wa umma uweze kuleta tija licha ya kua wa miaka i.e. 3-5 tena kwa mikataba inabidi hata mishahara iongezwe maana haiwezekani unawaajiri watu kwa miaka 3-5 halafu unawalipa gross 500,000-960,000 hapo mtu hawezi fanya jambo lolote lile la maana
 
Huo Ni wivu tu,hicho kitu hakipo duniani kote,nipo ulaya huu ni mwaka wa tatu sijawahi ona sembuse Tanzânia? Utakuwa una wivu na watumishi wa umma si bure.
Fanya kazi kwa bidii acha fitna,pia hujui kuwa serikali nayo ina changamoto zake? Huonagi Watumishi wanalalamika kuhusu kupandshwa mishahara,madaraja nk? Kwann unaangalia upande mmoja?
 
naunga mkono hoja ,uwe wa mkataba na mtumishi apimwe utumishi wake ndani ya kipindi cha mkataba na akishindwa kutimiza malengo kusudiwa aondoke apishe wengine
 
Mkuu msamehe tu.Anajiita great thinker kwa kutoa uharo humu jamvini.Tumpigie makofi kwa pointless zake zisizotekelezeka!!!

Hahahaha
Huo Ni wivu tu,hicho kitu hakipo duniani kote,nipo ulaya huu ni mwaka wa tatu sijawahi ona sembuse Tanzânia? Utakuwa una wivu na watumishi wa umma si bure.
Fanya kazi kwa bidii acha fitna,pia hujui kuwa serikali nayo ina changamoto zake? Huonagi Watumishi wanalalamika kuhusu kupandshwa mishahara,madaraja nk? Kwann unaangalia upande mmoja?
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia mia
Na kwa kuongezea,kua na kamati maalumu ya kuwapima na kuwafuatilia.Iwe kamati ya uchunguzi na usiri mkubwa sana.watafanya kazi hawa mabwanyenye wa kutumia kodi zetu vibaya na kuletea jeuri wananchi
 
Nakaribia kuanza kuamini ugali hudumaza akili
Naamini wapo watakao niunga mkono na wapo watakao nipinga.Kutoka na utendaji usioridhisha katika ofisi nyingi za Serikali kwa Watumishi wa Umma nashauri ni vema Serikali ikaanzisha Utumishi wa Mikataba kwa watumishi wake kwa kupangiana Malengo ya kila Miezi 4 kama mwaka wa Serikali ulivyo.

Mtumishi anaposhindwa kuyatimiza atakuwa hastahiri kuendelea na Utumishi.Pia nashauri Mkataba uwe wa miaka 5 kwa vipindi viwili kwa maana ya miaka 10 analipwa Mafao yake yote.Utendaji wa Ofisi na Mashirika yasiyo ya Serikali unakuwa na Mafanikio kutokana Mtumishi kujua nipo kwa mkataba nisipofanya vizuri mkataba unasitishwa lakini Serikali watumishi wanafanyia kazi kwa mazoea na wanasubiri miaka 55 au 60 wastaafu.

Faida ya Mikataba ni kuwa Watumishi watakuwa wanapishana ktk ajira ndani ya miaka 5 au 10 kuliko sasa mpaka miaka 55 au 60.
 
Ndoto za alinacha.Majungu,uonevu,wivu,uonevu nk vitatamalaki maofusini/makazini.We hujui wabongo kwa figisu maofisini/makazini au unaishi Iceland??
Naunga mkono hoja kwa asilimia mia
Na kwa kuongezea,kua na kamati maalumu ya kuwapima na kuwafuatilia.Iwe kamati ya uchunguzi na usiri mkubwa sana.watafanya kazi hawa mabwanyenye wa kutumia kodi zetu vibaya na kuletea jeuri wananchi
 
Wananchi wanachuki kubwa sana na hawa watumishi pengine kuliko viongozu wa serkali kutokana na matendo yao.

Watumishi ni wazembe,majeuri,wanadharau,Hawajui mambo mengi,kazi kupiga soga za umbea tu na Kula kodi za wananchi bure huku wakishindwa kuwahudumia ipasavyo.
Yani wanajifichiaga ktk mgongo wa CCM na kuipakazia ubaya wote wa serkali.Kumbe wao ndo tatzo ndani ya nchi hiii.

Hawa ni kuwafupishia mikataba tu,Hope Rais wetu atayafanyia kazi haya ili kurudisha nidhamu ya utumishi nchini
 
Mimi nipo shamba napambana na kilimo.Karibu tuanze kuandaa mashamba.

We naye boya kweli.Wafanyakazi,Wakulima na Wafanyabiashara wanategemeana.

Hakuna sekta ambayo ni independent, bali dependent.
Mlienda kusomea ujinga shuleni( in faiza foxy voice).
Fanyeni kazi na muwahudumie wananchi wapuuzi nyinyi,ndo mana JPM akija anawapeleka peleka sana maana wazembewazembe sana
 
Mimi nipo shamba napambana na kilimo.Karibu tuanze kuandaa mashamba.

We naye boya kweli.Wafanyakazi,Wakulima na Wafanyabiashara wanategemeana.

Hakuna sekta ambayo ni independent, bali dependent.
Mlienda kusomea ujinga shuleni( in faiza foxy voice).
Kuna aliyekwambia ifutwe au mikataba ibadilishwe kuongeza tija.

Nyi ndo walewale msoelewa content husika
 
Fasiliteta wa ku-facilitate mawazo mfu!!!

JPM amekata mirija yenu hasira mnazuhamishia kwa watumishi.

Nyambafu sana nyie.Mpaka muitike abeeee!!!

Back
Top Bottom