muuza ubuyu,
Hongera mkuu. Usiwe na hofu kuagiza gari mwenyewe. Ni bei rahisi sana kuliko kununua toka kwenye yard. Kuhusu malipo, account ya BEFORWARD inafahamika dunia nzima. Nimekuwekea kama screenshot kwenye attachment.
Kuhusu status ya hiyo ODO METER angalia hapo hapo kwenye website yao ukisha click gari huonesha kama odometer has been changed. Ila kwa gari hiyo kama ingekuwa imeshabadilishwa isingekuwa imeshasoma hadi laki na zaidi. Hatua inayofuata ni wewe kwenda bank kufanya malipo kwa ku print hiyo Proforma Invoice na sales agreements.
Ukishalipia uta scan hiyo TT application form uwatumie kama bank hawatakupa TT hapo kwa hapo. Wakishapata hiyo, wao watasubiria uwatumie TT ukishaichukua bank na baada ya hapo watabadilisha status ya hilo gari kwakuandika Under offer. Malipo yakishawafikia itasomeka has been sold na watakutumia Export Certificate kwa njia ya email.
Hiyo itakuhakikishia kama odometer imeshabadilishwa au laa na pia kama gari ilishakuwa na owners wangapi maana itaonesha umbali ambao kila mmiliki alioanzia kutembelea na mwaka. Ipo kwa kijapani lakini inaeleweka upande wa chini kushoto.
Wakati huo utakuwa na Car Progress (CAP) page ambayo ni link watakayokuwa wamekutumia kwa email na uki click itafungua hiyo cap page yako ambayo ndo itakuwa sehemu salama ya kukupa maendelea ya kila hatua. Wakati huohuo utakuwa umeshatafuta clearing agent ambaye utamkabidhi hiyo Final Invoice na ata play part yake hadi gari ifanyiwe inspection.
Gari ikipita kwenye inspection watatuma report na watahitaji uhakiki contacts zako (physical address) ambayo baadae gari ikishapakiwa kwenye meli wataitumia kukutumia Bill of Landing, Original Export Certificate, Insurance coverage letter na zawadi yako). Kupitia cap page yako utajua gari inaletwa na meli gani na inatarajia kuondoka tarehe ngapi na kufika tarehe ngapi.
Muda wa kufika meli unatofautiana kulingana na kampuni. Mfano kampuni ya Hoegh Brasilia brake ya kwanza ikifika Africa ni Durban, Maputo, Dar es salaam kisha Mombasa na kwa wastani huchukua siku 29 kufika Dar. Ambazo zinakuja Dar mojakwa moja huwahi kufika. Unawezaku track meli kwakutumia marine vessel ttaffic na utajua ilipo na hii itakusaidia kujipanga. Kama kuna lolote uliza mkuu.