Samahani wadau kwa thread nyingi ninazoleta. Ni kutokana na kuwa na wengi ninaofahamiana nao wanapohitaji ushauri.
Story iko hivi:-
Baba mmoja ameshitakiwa na mkewe, kesi ipo mahakamani tangu mwaka jana mwezi January. Kesi halisi iliyyoandikwa mimi sijaisikia, ila yule mama ananiambia kuwa kule mahakamani yeye anadai talaka kwa sababu huyu baba amekuwa haihudumii familia kwalolote ila anahudumia familia ya hawala yake.
Mama amekuwa akisomesha watoto kwa shida sana.
Kibaya zaidi akirudi usiku anapopigiwa simu na huo michepuko anaongea kile alichokuwa akifanya na michepuko simu ikiwa na loud speaker, nyumba haina sealing board, watoto wanasikia kila kitu.
Kila baada ya siku kadhaa baba anafumaniwa. Sasa mama amechoka anataka talaka.
Baba akiitwa mahakamani haendi anataka wayamalize nyumbani, tukimbembeleza mama anakubali kusamehe baba ila kwa sharti kwamba baba aachane na michepuko na ahudumie familia na watoto. Jibu analotoa ni kuwa hana pesa ya kununua chakula wala kusomesha watoto, ila anasomesha watoto wa michepuko na huduma zote anatao huko.
Kuhusu mahusiano ya ndoa anataka mke ampe ila kuacha kuchepuka hakubali.
Sasa kwa hali kama hii naomba maoni yenu ili nimshauri huyo mama. Na pia kama kuna watu wanaoweza kumpa msaada wa kisheria nitampa mawasiliano.