guzman_
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,276
- 2,435
Habari za weekend wanaMMU
NI hivi.
Mwaka 2015 nilianza mahusiano na single maza mmoja hapa mkoani. Wakati huo alikuwa anafanya kazi kama mpishi kwenye mgahawa mmoja. Japo alikuwa single maza umri wake ulikuwa bado sana (22). Na ifahamike kuwa nilikuwa nimeshaoa na mke alikuwa akiishi mkoa tofauti. Nilikuwa muwazi kwake na aliheshimu hilo. 2016 tukapata mtoto wa kiume na nilimwachisha kazi na nikamsaidia kujenga nyumba kwenye kiwanja chake na kumpa mtaji wa kuuza nafaka. Kweli alionyesha ukomavu sana kwenye biashara mtaji ulikuwa na ikafika kipindi akawa na 10m kwenye akaunti yake.
2017 mwanzoni akabadilika akaanza maneno ya shombo na kusema hawezi endelea kudate na mme wa mtu. Nikasema sawa ila anipe ruhusa ya kwenda kumwangalia kijana wangu pale nikiwa nahitaji akakubali. Baada kama ya miezi 4 nikaenda kwake kumcheki mtoto kweli nilimkuta pale anacheza nje nikamchukua nikataka kwenda nae ndani sebureni kuingia naona akipigana denda na kijana mmoja sharobaro.
Nikavunga nikamwomba aje nje akanifokea sana kwa nini naenda bila taarifa. Nilichofanya nika chomoa laki 2 nikampa nikamwambia amfanyie shopping mtoto akagoma nikang'oa nanga.
Nikafanya upelelezi kumbe kale kajamaa kalikuwa graduate wa chuo na yule mchepuko wangu ndio alikuwa shuga mammy wake. Nikapiga moyo konde niliumia sana ila nikasema wacha iwe. Yule kijana alianza biashara na yule mama, kijana anaenda huko mikoani kutafuta nafaka yeye anauza. Baadaye nilisikia kijana alipewa kama 15m akatokomea nazo mwanza huko. Mama mtaji ukakata akaenda benki kukopa wakauza nyumba yake. Akahamia chumba kimoja kupanga.
Nilibadili lini so alikuwa hana uwezo wakunipata na niliondoka ule mkoa. Last week nilipata safari ya huko ndo nikaenda kumtafuta. Alikuwa kachoka sana na kijana wangu alikuwa ndo kama hajala siku mbili. Sikutaka kuongea nae nikampa business card nikampa laki 2 nikasepa.
Jioni yake akanipigia nikamwambia aje Hotel flani akaja nikapiga nae story mpaka saa 7 usiku nikamtafutia tax akaondoka.
Inshort ni kuwa hana kazi mtaji ulikata na aliuziwa nyumba hana ramani na ametokea familia duni sana.
Kabla nilimwomba kama ataniruhusu kumwoa mke wa pili alikubali ila baadaye baada ya kupata huyo kijana ndo akakengeuka. Sasa ivi ananiomba huku analia nimsamehe na yuko tayari kuolewa tumlee mtoto wote.
Ila mimi nataka nifanye utaratibu wa kumchukua kijana nikae nae yeye aendelee na shughuli zake. Shughuli ipo kwenye kumweleza bibi mkubwa aweze kumpokea huyu bwana mdogo. Najua kuna watu walishapitia haya nipeni ushauri namna ya kukabiliana na hili.
Asanteni Sana.